Salam kwako,
Uliyekuwa mwenyekiti wa tume ya kukusanya maoni ya katiba.
Kwa uelewa wangu na wengine wengi, historia inatufundisha kuwa umewahi shika nafasi mbali mbali za kiuongozi katika taifa letu hili pendwa.
Si jambo jepesi na inatokea kwa watu wachache mno kuweza pata nafasi tofauti za uongozi wa juu katika nchi tena kwa vipindi tofauti, hili pekee linatosha kuonyesha kwamba wewe ni mtu mweledi na mchapa kazi, sifa mbayo watawala waliona ni vyema kukitumia kipaji chako katika kulisaidia taifa hili, tunashukuru sana.
Taifa kwa sasa lipo katika mchakato wa kupata katiba mpya ambayo wewe na wenzako wachache mliteuliwa na Rais wetu, na kukabidhiwa jukumu la kukusanya maoni yetu ili baade, mawazo yetu na matarajio yetu yawe kauli moja kama taifa , kazi ambayo mliifanya vizuri, na tunawapongeza sana kwa hilo.
Hatua ya sasa ambayo ni muhimu ni kwa pendekezo la katiba lililohakikiwa na bunge, kama mhimili mwingine wa dola , kupelekwa kwa wananchi ambao ndio wenye maamuzi ya mwisho kama wanakubali mapendekezo hayo au la.
Wananchi wanahitaji kuelimishwa kuhusiana na yaliyomo katika mapendekezo hayo, ili muda unapofika wa kufanya hivyo wafanye maamuzi sahihi.
Watu, taasisi na vyama vimechukua jukumu hilo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wananchi wanafanya maamuzi sahihi, ni jambo la heri kwa ustawi wa taifa letu.
Hivi majuzi tumesikia na kuona yale yaliyotokea pale ubungo, jambo ambalo sitaki nilizungumzie sana kwani limeshazungumziwa na wengi na sihitaji kurudia rudia kwani nitakua nawachosha wengine. Yaliyotokea yametokea, na binafsi nakupa pole na mikiki mikiki uliyopata.
Vitabu vya dini vinatuhusia neno moja, kuhusiana ana amri aliyoitoa mwenyenzi Mungu ya kuheshimu wazazi, jambo hilo ni kuwa " wazazi tusiwachokoze watoto" neno hili linamaana kubwa mno, kwamba ili amri ile ya kuheshimu itimie vyema basi uchokozi unatakiwa usiwepo.
Mzee wangu, umri niliopo mimi pamoja na wenzangu wengi ni umri ambao bado tunakuza watoto wanaokwenda shule, watoto hao wanahitaji kuishi katika Tanzania yenye misingi tuliyoikuta sisi na kubwa zaidi ni amani.
Kwa umri wako wewe , na kwa nafasi yako, ni jambo lisilo pingika kuwa " you have achieved it all" that means " you have nothing to lose" , hivyo basi hata kama yakitokea yatakayotokea kwako wewe hakuna cha kupoteza.
Kumbuka kwamba bado kuna vijana wadogo, ambao hawajatimiza ndoto zao, lakini wanatumaini kuzitimiza kama wewe, hivyo kuwaondolea amani ni dhambi.
Sote tunahitaji amani na ustahimilivu kwa manufaa ya ustawi wa taifa bora, si lazima kila kitu kifanyike sasa, imani yangu inanituma katika kusubiri , hapo ndio siri ya ustawi ilipo, mataifa yote makubwa yamekuwa hapo ya lipo kwa kuvumiliana na kupitia nyakati mbali mbali na zenye kutikisa nchi lakini wamefanikiwa kuwa na mataifa bora yenye uchumi imara kwa kuwa na subira.
Hivyo basi si lazima serikali tatu ziwe sasa, ukifika muda wake muafaka, hizo tatu hata kumi zitapatikana, lakini kama kwa kipindi hiki hizo tatu hazielekei kupatikana, basi ni maombi yangu kwamba tuache kulazimisha mambo at the expense of our country's peace and security.
Natumai, haya yamekufikia vyema,
Wako mjoli,
Stroke.