Salamu toka Mabwepande | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salamu toka Mabwepande

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by zezeta, Mar 8, 2012.

 1. z

  zezeta Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SALAMU TOKA MABWEPANDE.

  Kwa wale wote mnaokumbuka yaliotukuta miezi kazaa iliyopita huku mitaa ya JANGWANI nafahamu mtakua mna fahamu mkasa nlio uandika kuhusu yaliyo nikuta na familia yangu.

  LEO napenda kuwasalimu toka makao mapya tuliyozawadiwa na SERIKALI YETU TUKUFU. Kwenye makala yangu iliyokuwa na kichwa cha SIDHANI KAMA BADO NAIPENDA NCHI YANGU, nilitoa masikitiko yangu ya kupotelewa na mke wangu pamoja na mali zangu zote na kuwa kwenye mazingira ya nusu kifo bila msaada wowote. Napenda kutoa shukrani zangu kwa ndugu na jamaa wote mliojitokeza kunisaidia kwa hali na mali pamoja na serikali YA NCHI hii ambayo SIDHANI KAMA NAIPENDA TENA.
  MWENZENU KWA SASA NIKO MABWEPANDE, NAISHI KWENYE HEMA LA FUTI NANE MIMI PAMOJA NA WATOTO, TUNATUMIA VYOO VYA MUDA AMBAVYO KWA SASA VIPO KWENYE HALI ISIYORIDHISHA KWANI VIMESHA JAA. Na andika haya sio kujidhalilisha kwa kuwaonesha umasikini ulio nikumba la hasha, ila natamani mtafakari pamoja nami kuhusu ukuu wa MUNGU KWANGU NA KWENU PIA.

  HEBU TAFAKARI.
  1. UMEMPANINI MUNGU WEWE ULALAYE KWENYE CHUMBA SAFI , MAZINGIRA MAZURI YENYE PRIVACY YA KUTOSHA.

  2. JE! ULIMPANINI MUNGU HATA AMEKUWEKA MPAKA LEO UKIWA NA AFYA NA MATUMAINI YA MAISHA BORA.

  3. NAKUMBUKA NAMI NILIKUA NA LONG TERM AND SHORT TERM VISIONS AMBAZO KWA SASA KIDOGO ZIMEYUMBA NA KUFIFIA LAKINI WEWE BADO ZAKO ZINACHANUA.

  WAPENDWA NAISHI MABWEPANDE AMBAKO KWANGU NDIO MAISHA YANA ANZA MOJA.
  NA TUMEAMBIWA TUANZE UJENZI KWA KUA MAHEMA NI YA MUDA MFUPI , NIPO NAJIULIZA UJENZI HUO NA UANZIA WAPI ILHALI SINA KITU NA HUKU WANANGU WAPENDWA WANATAKA KUSOMA, KULA , KUVAA NA MAHITAJI MBALIMBALI.

  MIMI SITAKI KUMUULIZA MUNGU KWANINI ALIYARUHUSU HAYA YANIKUTE NA KUNISONONESHA KIASI HIKI.. ILA NATAMANI UJIULIZE WEWE AMBAYE NI MTARAJIWA.

  HUWEZI JUA NINI LITATOKEA,...

  KAMA SIO POWER PLANT YA UBUNGO KULIPUKA BASI MAGOROFA MAREFU YA UDSM AU PENGINE POPOTE YAWEZA KUANGUKA. SI HAYO TU TUNA MADARAJA YALIYOJENGWA KWA UZEMBE MANGAPI?, MIOTO INAYOWAKA BILA SABABU MINGAPI??, MVUA NA MAFURIKO, RADI ZA MASIKA NA MICHAFUKO YA BAHARI. YOTE HAYO NI MAMBO YA KUMUOMBA MUNGU ATUNUSURU NA SERIKALI YA NCHI HII KUYAFANYIA KAZI YALE YALIYO CHINI YA UWEZO WAO

  POLENI SANA NDUGU ZANGU MLIOKUMBWA NA ADHA YA MGOMO WA MADAKTRI.
  MIMI NAWASALIMU.
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mbona kama vile milaana kibao unatupatia? Sijui magorofa gani yatuangukie... sijui madaraja gani hayajajengwa kwa ustadi ndo yatuangamize... ujue hatukupenda yaliyowapata..... Usiiombee nchi yetu mabaya.... yakitokea tupambane tutakavyoweza....basi
  Nakubaliana nawe kuwa kuishi kwenye mahema ni maisha magumu, sijui yakoje maana kwa kweli sijajaribu, lakini maisha yasiyo na privacy ni magumu. Pole kwa kufiwa na laazizi mke wako.
  Lakini kuhusu maisha ya kusonga mbele, nakushauri, kwa vile umeshafahamu kuwa hii serikali haikusaidii chochote, usisubiri kuchimbiwa hadi choo. Kwa vile umeshatambua udhaifu wa serikali yako iliyowekwa madarakani kwa miaka mitano ijayo, usisubiri ikufanyie chochote, kwani haitafanya kitu, bali utaambulia usanii tuu. Tafuta pa kuishi kwa jinsi unavyoweza, we ni mwanaume. Omba msaada kwa marafiki, hata waJF, natumaini hutakataliwa na wote. Achana na serikali. Achana na kuishi kwenye mahema, acha kusubiri choo ijae serikali ije kukuchimbia nyingine. Anza maisha yenye akili upya. Sahau yaliyopita, yaani usipoteze muda mwingi kufikiria uliyokuwa nayo. USHAURI WA BURE, USIOE HARAKA. Ukikiuka hili utalijutia. Subiri wanao wakue kidogo, kisha uoe ukitaka. Pole sana tena. Mungu akubariki.
   
 3. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,178
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka jinsi makamba alivo sisitiza watu wa hame mabondeni, ajabu ni kwamba hata baada ya ninyi kupelekwa mabwe pande naona wenine wamehamia mlipotoka na wanatizamwa tu
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Baniani mbaya kiatu chake dawa!!! NAMKUMBUKA KOMREDI MAKAMBA SAKATA LA JANGWANI!!! ANGESIKILIZWA VIFO KARIBIA VYOTE NA UPOTEVU WA MALI USINGETOKEA!!!! VIVA MAKAMBA!!!
   
 5. z

  zezeta Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu ahsanteni sana kwa faraja mlizo nipa na ahsanteni pia kwa ushauri. Nakubaliana nanyi kabisa kuhusu MAKAMBA KUKIMBIZA WATU JANGWANI, Lakini siku zote GODORO USILO LILALIA HUJUI KIASI CHA CHAWA WALIOMO. JAMANI sio kama tulikua hatutaki kutoka jangwani ila ni hali za maisha ndg zanguni ndio zilichangia sisi kujipa moyo na kubakia kule. NAOMBA NIWAKUMBUSHE KUA pale jangwani sio tu kua tuna kaa shagala bagala la hasha. Tuna hati za serikali kabisa za viwanja na kama kweli serikali / makamba angelikua na nia ya dhati tangu mwanzo wasingelikubali sisi kukatiwa viwanja pale wangeli tusukuma huku mabwepande mapema kabla hatuja kutwa na maafa.

  ACHANA na hilo kuna siku palitokea mlipuko wa transformer pale UBUNGO POWER PLANT TULIKIMBIZANA KWELI BILA MSAADA WOWOTE, NILILITOLEA Mfano hilo kama kuwa weka tahadhari, sio kua serikali haifahamu kua yale mazingira pale ni ya hatari na pana nuka mioto mitupu kila upande. sidhani kama hawapendi kuyaondoa yale ma kuni ya kuzalisha umeme pale la hasha ila ni hali ya maisha na mfumo wa ki TANZANIA wa kutojali mpaka maafa yatokee.

  mfano wangu wa pili ni YALE magorofa yaliyo expire ya UDSM, SIO swala la kuficha kua yale magorofa yana beba mzigo mkubwa kuliko uwezo wake ilhali yakiwa yamechakaa. UNADHANI UONGOZI WA CHUO NA SERIKALI HAWALIFAHAMU HILO?. YOTE YANAFAHAMIKA NI MFUMO TU NDIO UNATUONGOZA NA MPAKA KESHO MA ELFU YA WATAALAMU WATARAJIWA WA NCHI YETU WANAZIDI KUJAZWA NA KUISHI MLE. SIOMBEI ILA KWA MFANO MOJAWAPO YA YALE MA HALL YAKIANGUKA NA KUMEZA WANAZUONI WETU TUTASEMAJE? JE NI UZEMBE WAO AU WA WATAWALA WAO? HIYO NA MINGINE MINGI YAWEZA KUTUPA PICHA YA UHALISIA WA MAISHA YETU YA KITANZANIA.

  NAWASHUKURU WADAU ILA NADHANI NTAKUA NIMEWAFUNGULIA MLANGO MWINGINE WA KUWAZA UHALISIA WA MAISHA NA JINSI YA KUPAMBANA NA MAJANGA.

  LEO NAWAPA POLE WOTE WALIOFIWA NA NDG ZAO KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI WAZALENDO WA KITANZANIA. NALO HILO NI JANGA PIA.
   
 6. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Kumbuka serikali ya tz inatumia feedback system yaani inyeshewe na mvua kwanza ndiyo ikumbuke muamvuli wakati nchi nyingine zinatumia feedforward unajua mvua itanyesha hivyo unatoka na mwamvuli. kwa upumbumbavu huu wa feedback ndio imesababisha leo kuwe na mgomo wa madaktari.

  Lakini ni wewe wa Jangwani mliyeipa kura ccm kwani ilala ilijinyakulia kura za kutosha na tulitahadharishwa kuwa kukichagua ni kuleta maafa ila hatukuelewa sasa maafa ndiyo hayo ngoja magonjwa yalipuke ulipo huku madr. wamegoma unganeni mchimbe vyookuepusha balaa serikali yenu haina haja nanyi itawakumbuka kipindi cha uchaguzi ukifika
   
Loading...