Salamu kwa wanaoleft whatsap

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,310
4,538
SALAMU KWA WANAOLEFT(WHATSAP).

1)salamu ziwafikie,enyi wakimbia kundi.
Kulefti mkumbatie,ndo mana mwakua bundi.
Muadiwe mkimbie,huo wala si ufundi.
Salamu kwa waleftiji,acheni tabia hiyo.

2)hata kundi la maana,nyinyi mwaliacha kando.
Tupendi kujibizana,yenu tabia uvundo.
Tena inachukizana,bora tuwapige nyundo.
Salamu kwa waleftiji,acheni tabia hiyo.

3)tabia hiyo utoto,anzeni badilikeni.
Nyinyi kama viroboto,lakini kama kunguni.
Hivi mwapenda uroto,ama mwakunywa pomoni.
Salamu kwa waleftiji,acheni tabia hiyo.

4)adimini kukuadi,si ulitaka mwenyewe.
Leo wapandwa midadi,watoroka kama mwewe.
Acha itimu ahadi,kundili lina wenyewe.
Salamu kwa waleftiji,acheni tabia hiyo.

5)na mlefti kwa amani,tena msirejeeni.
Mkija tuwapasheni,muwe kama piritoni.
Wadogo kama sahani,i pilau ya sokoni.
Salamu kwa waleftiji,acheni tabia hiyo.

6)adimini wakirudi,nasi twite tuwapashe.
Wakome na ukaidi,kundi mbali walipishe.
Wabaki wanofaidi,kwa faida tujipashe.
Liacheni kundi letu,la wasapi linawiri.

Shairi:SALAMU KWA WANAOLEFTI (WHATSAP)
Mtunzi:IDD NINGA WA TENGERU ARUSHA.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Lugha inakuwa lakini pia inazingatia muktadha. Kwa whatsapp mtu analeft
Ila tukizingatia usahihi wa lugha, si sahihi kusema "kuleft". Left ni past tense (muda uliopita) ya neno "leave". Kwenye WhatsApp, mtu akiondoka kwenye group, iinaoneshwa kwamba, k.m John left- (John aliondoka) kuashiria muda uliopita.
 
Ila tukizingatia usahihi wa lugha, si sahihi kusema "kuleft". Left ni past tense (muda uliopita) ya neno "leave". Kwenye WhatsApp, mtu akiondoka kwenye group, iinaoneshwa kwamba, k.m John left- (John aliondoka) kuashiria muda uliopita.
Kwenye grammar upo sahihi. Lakini kama nilivyosema awali matumizi ya lugha hutegemea pia context. Ndiyo maana nikasema kwa context ya WhatsApp ni sawa kusema mtu ameleft group
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom