Salamu kwa wanaoleft whatsap

SALAMU KWA WANAOLEFT(WHATSAP).

1)salamu ziwafikie,enyi wakimbia kundi.
Kulefti mkumbatie,ndo mana mwakua bundi.
Muadiwe mkimbie,huo wala si ufundi.
Salamu kwa waleftiji,acheni tabia hiyo.

2)hata kundi la maana,nyinyi mwaliacha kando.
Tupendi kujibizana,yenu tabia uvundo.
Tena inachukizana,bora tuwapige nyundo.
Salamu kwa waleftiji,acheni tabia hiyo.

3)tabia hiyo utoto,anzeni badilikeni.
Nyinyi kama viroboto,lakini kama kunguni.
Hivi mwapenda uroto,ama mwakunywa pomoni.
Salamu kwa waleftiji,acheni tabia hiyo.

4)adimini kukuadi,si ulitaka mwenyewe.
Leo wapandwa midadi,watoroka kama mwewe.
Acha itimu ahadi,kundili lina wenyewe.
Salamu kwa waleftiji,acheni tabia hiyo.

5)na mlefti kwa amani,tena msirejeeni.
Mkija tuwapasheni,muwe kama piritoni.
Wadogo kama sahani,i pilau ya sokoni.
Salamu kwa waleftiji,acheni tabia hiyo.

6)adimini wakirudi,nasi twite tuwapashe.
Wakome na ukaidi,kundi mbali walipishe.
Wabaki wanofaidi,kwa faida tujipashe.
Liacheni kundi letu,la wasapi linawiri.

Shairi:SALAMU KWA WANAOLEFTI (WHATSAP)
Mtunzi:IDD NINGA WA TENGERU ARUSHA.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Umeshindwa kujua neno la Kiswahili la hiyo 'wanaoleft'? Mnaharibu lugha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom