Kuwa offline kwa miezi sita

Kuwa offline kwa miezi sita

Poise

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2016
Posts
7,660
Reaction score
7,948
Habari wana jamvi humu JF platform.

Nijipambanue kabisa kuwa Poise, siyo mfuasi wa chama chochote cha siasa hapo Tanzania wala mahala popote pale duniani na katu haitakaa itokee Mimi kuwa mwananchama wa chama cha siasa.
Hivyo basi, ninayoyaandika hapa ni kwa maslahi ya Taifa letu la Tanzania.

Mwaka wa 2018 ni mwaka ulioanza kwa tukio kubwa mno la Poise kumkubali na kuwa mfuasi wa Yesu Kristo hapo mnamo tarehe 01/01/2018.

Maisha yalikuwa mazuri sana kwa mwezi wa kwanza kiimani na mambo mengine ya kila siku.

Tukiwa katika mwezi wa pili tarehe ya 16/02/2018 mambo yakabadilika ghafla mno. Ni siku ya jumamosi ambayo Binti , kitoto kidogo cha chuo kikuu hapo jijini Dar es Salaam aliposababishiwa umauti kwa sababu ya waouvu wachache walio kwenye mifumo yetu ya utendaji wa Serikali na chama kizee sana zaidi ya nyani mzee cha CCM wakiongozwa na management ya NEC na DED wa Kinondoni.

Kwa kupitia, mifumo hiyo tajwa yenye vilaza wachache walipofanya njama na mbinu zote za uovu za kugawa barua na fomu za wasimamizi wa uchaguzi kwa mafungu, ubaguzi na uonevu.
Kwani waliwapatia wasimamizi wa CCM, CUF n ACT-Wazalendo fomu na hizo barua bila ubaguzi ila walipofikia kwa CDM wakawanyima haijulikani malengo yake ni yapi hadi leo ya kufanya ubaguzi ule.

Hivyo, uongozi wa CDM wakaamua kwenda moja kwa moja ofisi ya DED kufatilia barua na fomu za wasimamizi wao.

Hapo ndipo mateso, vipigo na mauaji yaliyoamriwa na baadhi ya watendaji uchwara mbuzi na kuwaagiza polisi wakawazuie viongozi wa CDM na baadhi ya wafuasi wao kwenda ofisi ya DED wa Kinondoni matokeo yake yakasababisha hayo madhila kwa wafuasi wa CDM na wananchi wasio kuwa waandamanaji.

Kwa mfano, mwananchi mmoja wapo tena ni mwanachama wa CCM naye alipata kipigo cha kufa mtu ila badae sana alijieleza kuwa yeye ni mfuasi wa CCM na alikuwa kwenye safari zake tu ghafla ndiyo wakawekwa kati na polisi waliojipa amri au waliopewa amri toka juu ya kuwadunda watu bila huruma wala utu.

Wananchi wengi, wamejeruhiwa, wengine wamepigwa risasi na zaidi ya hapo, Binti yetu, Akwilina A. B alikatishwa maisha yake ili hali siyo mwanachama wa chama cha siasa na hakuwa kwenye kundi la waandamanaji ila alikuwa na uelekeo tofauti na hao waandamanaji. Maana, kwa taarifa rasmi za wanafunzi wenzake wa chuo cha NIT na familia yake zinaonesha kuwa alikuwa kwenye daladala akitoka chuoni, maeneo ya Mabibo kilipo chuo cha NIT akielekea kituo cha daladala cha Makumbusho ili kupata usafiri tayari kuelekea Bagamoyo ili akakabidhi barua yake ya maombi ya field attachment (mazoezi kwa vitendo).

Katika harakati zake hizo, basi mauti hiyo ya kikatili, kiuonevu ikampata akiwa eneo la Mkwajuni, Kinondoni kabla hata ya kufika makumbusho baada ya risasi moja wapo kati ya nyingi zilizofyatuliwa ovyoovyo na polisi kumpasua kichwa pwaaaaah na kuumwaga ubongo wake kwenye daladala na juu ya wasafiri wenzake walio kuwa kwenye daladala kama vile maji yanavyomwagika baada ya bomba laDAWASCO kupasuka.

Mchezo huo, mchafu ukaendelea kwa kuwaswaga wananchi wanapita eneo hilo kama ng'ombe , na kuwapanga barabarani na kisha kuwarukisha kichura-chura, kuwapiga na kuwapandisha kwenye vikarandinga vidogo vya polisi (a.k.a. mbavu za mbwa) wananchi hao wakiwa wameswagwa haswa huku wakichuruzika damu kama nyama zilizo ning'inizwa buchani tayari kuuzwa.

Nimeandika mengi lakini, nirudi upande mwingine, nchi yetu ina hitaji amani, kuendelea kuheshimu watu wetu, sheria na taratibu za nchi ni hilo ni jambo la muhimu na la kila kiongozi kufata.

Vyombo vyetu vya dola hasa, polisi wasitumiwe vibaya kuumiza wananchi ambao ao hao ndiyo chanzo cha watu wanaofanya kazi kwenye vyombo vyetu vya ulinzi.

Polisi, tumieni weredi , hekima na utu mnapopewa majukumu na siyo kufanya pasipo kutathimini madhara ya matendo yenu kwa wananchi ambao nanyi ni sehemu ya wananchi na jiangalieni na ninyi baada ya hizo kazi na maisha ya familia zenu wenyewe leo mpo kwenye vyeo na nafasi hizo ila kesho hamtakuwepo kwenye vyeo hivyo.
Je, mtaishije kwenye jamii mnayoitesa?

Tena, watoto wenu na familia zenu zinaishi na wananchi ao hao mnao watesa kwa hiyo, jitathiminini kuhusu wananchi wanavyokuoneni ninyi baada ya kuua au kutesa jamaa zao wasio na hatia.

Viongozi wa juu , nanyi acheni utendaji feki wa kuacha kutoa pole kwa njia sahihi za mawasiliano yanayotambulikana kiserikali na kitaifa.
Toeni pole na salamu za rambirambi kwa njia ya barua zilizo na anuwani za ofisi zenu husika za Serikali, redio , gazette au luninga ili hadi Babu na Bibi zetu walioko huko Najilinji, kishumundu, Busega , Tosamaganga na Nyakatoke wote wasikie taarifa na siyo kujiandikieni vimaneno vyenu vitano tu tena kwenye mitandao ya kijamii ambako wazee hao hawapati hizo pole na salamu zenu za rambirambi.

Mfano, viongozi leo hii mnatumia FB, LinkedIn, Instagram na nyingine ile maarufu siikumbuki jina ila naona hata Trump anaitumia kule USA.
Kwa hiyo, tuacheni hizo tabia za kihunihuni na ujanjaujanja wa kitoto wa kutoa salamu za pole na rambirambi kwa wananchi walio kwenye mateso , uchungu, huzuni na majonzi kwa kupotelewa na jamaa zao tena kwa vifo vya kikatili na vya aibu kwa mfano, huyo Binti Akwilina A. B alivyouliwa kikatili hapo Kinondoni Dar Es Salaam.

Tanzania, iangalie na kujifunza kwa wale tuliokopeshwa kutoka kwao huu mfumo ya vyama vingi vya siasa , watu waelimishwe na zaidi Katiba itenganishe rasmi utendaji wa chama kwenye Serikali kuu na utendaji wa chama kinachokuwa madarakani. Kwa mfano, kwa sasa hivi, nchi yetu ya Tanzania inavyoendeshwa ni kana kwamba, CCM kama chama ndiyo Serikali na wanachama ndiyo watendaji wa Serikali ili hali wao wametoa Rais tu na siyo kuwa ndiyo wamepewa hati miliki ya nchi.

Jambo, lingine na la muhimu mno mno kwa Taifa letu , la kuangaliwa kwa umakini na watu wote (wananchi na vyombo vyetu vya ulinzi hasa JWTZ na TISS) hakikishine kuwa huu mfumo wa kiongozi yeyote kujichagulia marafiki, washirika na washauri lisimamiwe kwa ukaribu mno mno na hasa mambo wanayoyazungumza na wanayoyapanga kwa sababu, tusipokuwa makini katika eneo hilo hakika kuna siku viongozi wenye vichwa Nazi watauza nchi au kuitumbukiza kwenye vita kwa sababu ya aina ya marafiki na washauri wanao wapata huko nje ya nchi.

Mfano , USA huwa vyombo vyao vya ulinzi na usalama hawana hayo mahaba au imani na marafiki wa viongozi wao wa nchi hasa katika kujichagulia marafiki au washauri au kufanya mazungumzo ya siri na mtu yeyote wao mambo yote hufanywa mbele ya walinzi na washauri wa Serikali/ Rais na siyo vinginevyo.

Ulinzi wa nchi yetu na watu wanaoleta kutokuelewana kwetu hasa wanaotoka nje ya nchi.
Hili nalo ni muhimu, kuzingatiwa mno mno hapo Tanzania wakati Poise, nikiwa kijana mdogo wa umri wa miaka 15+ nchi yetu ililindwa nasi vijana, na wananchi kwa ujumla huku vyombo vya ulinzi vikifanya oparesheni kubwa na zinazohitaji nguvu zaidi, vifaa na weredi wa medani za kivita, kiulinzi na usalama.

Hapa, mtu atajiuliza hivi Poise, anataka kuandika jambo gani?
Hapa nataka kuandika kuwa; Tanzania ya kuanzia miaka ya 2000s wananchi wamejiondoa katika kulinda nchi na vyombo vya ulinzi tu ndiyo vinafanya hicho kitu.
Hii siyo nzuri mno kwa Taifa letu. Mfano, niende kwenye shambulizi la huyu mtoto anaitwa, TA. Lisu huko Dodoma mwaka jana, kama wananchi wangekuwa makini kama nyakati zetu zile tukiwa vijana wadogo mno hakika huko mitaani wale wasiojulikana ilikuwa wajulikane pale pale kwenye eneo la tukio huko mkoani Dodoma.

Sasa hivi, Tanzania ina haribiwa sana na Rwanda kupitia Mr. Slima a.k.a Ngongoti Kagame, huyu ni tatizo hapo Tanzania kwa sasa.
Rais, Mstaafu Mhe. Dr. Kikwete hilo alilijua vizuri ndiyo maana humu ndani alichekacheka nasi na kutuachia tu ila ilipokuja jambo la Rwanda na Kagame na ulinzi wa Taifa letu Dr. Kikwete hakuwa na mzaha wala kuchekacheka au urafiki na watu wanafiki kama Kagame.

Hivyo, Tanzania kuweni makini sana na huu urafiki na ujio wa kila baada ya wiki mbili wa Mr. Slim hapo nchini Tanzania.
Daima nyoka huwa hafunguliwi mlango ili aingie ndani tupate kumuua bali tunafunga milango na kumsaka akiwa uko huko nje ili tupate kumuua.

Mfano mzuri ni namna sasa wakati huo nikiwa kijana na mkakamavu wa Kati wa umri wa miaka 30 tulivyo funga milango na kisha tukamtumbua nduri IDD Amini Dada huko Uganda.

Hapo Poise, namaanisha kuwa Mr. Slim anatakiwa afungiwe nje japo ushirikiano na biashara ziendelee na siyo iendelee kama ilivyo awamu ya ngumi hii kuwa kila siku yuko ikulu au huko Tanzania akimshauri kiongozi wenu.
"Kagame must be stopped visiting Tanzania or die in Tanzania.

Hivyo watanzania wenzentu wote tuwe makini, tusimame kidete kupinga , kutaaa na kukemea na hata kuwaondoa watu au kundi la watu waouvu wanaotaka kuivuruga Tanzania.

Inawezekana kundi hilo au waovu hao wachache wanafanya wayafanyayo kwa kuelewa au kutokuelewa lakini kwa namna yoyote ile ni lazima wakemewe, wapingwe na hata kuondolewa katika nyadhifa hizo walizo nazo ili Taifa liendele kusitawi.

Naipenda nchi yangu mno mno ila , yaliyotokea na kusababisha maumivu, chuki, hasira , huzuni, majonzi kwa kila mtanzania mwenye utu, akili, hekima na maarifa na kila anayeitakia Tanzania mema anapaswa kuyakemea, kuyapinga na kuyazomea na kuwazomea wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuwa kikundi hicho kiovu na cha wauaji kiache hiyo tabia, waache matendo hayo maovu na zaidi watubu na kumrudia huyo Mwenyezi Mungu wanaye muomba kwa imani zao.

Mwisho, Poise niandike kuwa nitakuwa naandika kwa muda tu kisha naandaa mizigo yangu hapa tayari kwa safari maana nimehamishwa kituo cha kazi kutoka Wellington New Zealand na kwenda Middle East, Regional Office kwa kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi kesho wa March 5, 2018 hadi October 4, 2018.

Hivyo, kwa kipindi hicho cha miezi sita sitaweza kuwa online wala kuchangia humu jamvini JF platform.

Nipende kushukurun wote na zaidi , niwape pole jamaa, na wananchi wote walioguswa na madhila yote yaliyotokea katika nchi yetu hasa yanayosikitisha na kuhuzunisha.

Nihitimishe kwa sala fupi-

My prayers: Get well soon, TA.Lisu

R.I.P Binti yetu, Akwilina A. B.
R.I.P wote waliouawa kwa uonevu wa watu wachache wanaotaka wao tu kuishi na kuendeleza uovu wao.

Ndoto zenu zote zimezimwa kama vile mshumaa uzimwavyo.
Daima tutawakumbuka , Kristo Yesu awaangazie mwangaza wake wa milele. Amina.

Tukutane Middle East ila kwa hapa JF platform hadi October 4, 2018.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika ,
Mungu nibariki mno mno Poise.
 
Daah siamini kabisa,huyu jamaa alikuwa muislam wa itikadi kali leo hii ameokoka..aisee
kipindi ukileta thread ya kikristo au dini wakija watu hawa na huyu mleta thread lazima thread ichafuke Poise faiza foxy Gavana @kahataan big show watu hao lazima upate ban.
Leo umetoka uislam umeokoka umewakimbia akina faiza foxy na @khataan watakumiss kweli
 
unaandika yote hayo unadhani tuna time za kusoma..unazingua

inamankusweke ,
Mkuu
Ufupisho:
Poise siyo mwanachama wa chama chochote siasa hapo Tanzania.

Tuilinde Tanzania yetu, waovu wote wakemewe, wapingwe na waondolewe.
Mfano, wauji, watesaji wa wananchi wote waondolewe bila huruma.
Pia, Kagame ni tatizo kwa ustawi wa Tanzania. Tufanye naye biashara na ushirikiano ili asiwe mshauri na Waziri kwenye Serikali yenu hapo Tanzania.

Vyombo vyetu vya ulinzi visitumike kuwaonea wananchi kwa mlengo wowote ule bali vifate na kutii sheria ya nchi.

Poise, nimehamishwa ofisi hivyo nitakuwa offline hapa jf platform kwa muda wa miezi sita kuanzia March hadi October 2018.

Sala fupi:
My prayers: Get well soon, Hon.TA. Lisu,

R.I.P Binti yetu, Akwilina A. B
R.I.P , watanzania wenzentu wote waliouawa kwa ukatili na waouvu tuliowapa madaraka.
Ndoto zenu zote zimezimwa kama vile mshumaa uzimwavyo.

Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu nibariki mno mno Poise .
 
18/26/4 uchungulie humu uone kinachojiri

Gyole,
Mkuu.
Asante mno japo kwa majukumu kwenye ofisi mpya itakuwa ngumu na ukizingatia Middle East siyo salama kwa Binadamu.
 
Daah siamini kabisa,huyu jamaa alikuwa muislam wa itikadi kali leo hii ameokoka..aisee
kipindi ukileta thread ya kikristo au dini wakija watu hawa na huyu mleta thread lazima thread ichafuke Poise faiza foxy Gavana @kahataan big show watu hao lazima upate ban.
Leo umetoka uislam umeokoka umewakimbia akina faiza foxy na @khataan watakumiss kweli
Unasema kweli mkuu?asijekuwa ana-act hapa!ngoja nikasome post zake za zamani ila alichokiandika hapa kina point sana aisee.
 
Habari wana jamvi humu JF platform.

Nijipambanue kabisa kuwa Poise, siyo mfuasi wa chama chochote cha siasa hapo Tanzania wala mahala popote pale duniani na katu haitakaa itokee Mimi kuwa mwananchama wa chama cha siasa.
Hivyo basi, ninayoyaandika hapa ni kwa maslahi ya Taifa letu la Tanzania.

Mwaka wa 2018 ni mwaka ulioanza kwa tukio kubwa mno la Poise kumkubali na kuwa mfuasi wa Yesu Kristo hapo mnamo tarehe 01/01/2018.

Maisha yalikuwa mazuri sana kwa mwezi wa kwanza kiimani na mambo mengine ya kila siku.

Tukiwa katika mwezi wa pili tarehe ya 16/02/2018 mambo yakabadilika ghafla mno. Ni siku ya jumamosi ambayo Binti , kitoto kidogo cha chuo kikuu hapo jijini Dar es Salaam aliposababishiwa umauti kwa sababu ya waouvu wachache walio kwenye mifumo yetu ya utendaji wa Serikali na chama kizee sana zaidi ya nyani mzee cha CCM wakiongozwa na management ya NEC na DED wa Kinondoni.

Kwa kupitia, mifumo hiyo tajwa yenye vilaza wachache walipofanya njama na mbinu zote za uovu za kugawa barua na fomu za wasimamizi wa uchaguzi kwa mafungu, ubaguzi na uonevu.
Kwani waliwapatia wasimamizi wa CCM, CUF n ACT-Wazalendo fomu na hizo barua bila ubaguzi ila walipofikia kwa CDM wakawanyima haijulikani malengo yake ni yapi hadi leo ya kufanya ubaguzi ule.

Hivyo, uongozi wa CDM wakaamua kwenda moja kwa moja ofisi ya DED kufatilia barua na fomu za wasimamizi wao.

Hapo ndipo mateso, vipigo na mauaji yaliyoamriwa na baadhi ya watendaji uchwara mbuzi na kuwaagiza polisi wakawazuie viongozi wa CDM na baadhi ya wafuasi wao kwenda ofisi ya DED wa Kinondoni matokeo yake yakasababisha hayo madhila kwa wafuasi wa CDM na wananchi wasio kuwa waandamanaji.

Kwa mfano, mwananchi mmoja wapo tena ni mwanachama wa CCM naye alipata kipigo cha kufa mtu ila badae sana alijieleza kuwa yeye ni mfuasi wa CCM na alikuwa kwenye safari zake tu ghafla ndiyo wakawekwa kati na polisi waliojipa amri au waliopewa amri toka juu ya kuwadunda watu bila huruma wala utu.

Wananchi wengi, wamejeruhiwa, wengine wamepigwa risasi na zaidi ya hapo, Binti yetu, Akwilina A. B alikatishwa maisha yake ili hali siyo mwanachama wa chama cha siasa na hakuwa kwenye kundi la waandamanaji ila alikuwa na uelekeo tofauti na hao waandamanaji. Maana, kwa taarifa rasmi za wanafunzi wenzake wa chuo cha NIT na familia yake zinaonesha kuwa alikuwa kwenye daladala akitoka chuoni, maeneo ya Mabibo kilipo chuo cha NIT akielekea kituo cha daladala cha Makumbusho ili kupata usafiri tayari kuelekea Bagamoyo ili akakabidhi barua yake ya maombi ya field attachment (mazoezi kwa vitendo).

Katika harakati zake hizo, basi mauti hiyo ya kikatili, kiuonevu ikampata akiwa eneo la Mkwajuni, Kinondoni kabla hata ya kufika makumbusho baada ya risasi moja wapo kati ya nyingi zilizofyatuliwa ovyoovyo na polisi kumpasua kichwa pwaaaaah na kuumwaga ubongo wake kwenye daladala na juu ya wasafiri wenzake walio kuwa kwenye daladala kama vile maji yanavyomwagika baada ya bomba laDAWASCO kupasuka.

Mchezo huo, mchafu ukaendelea kwa kuwaswaga wananchi wanapita eneo hilo kama ng'ombe , na kuwapanga barabarani na kisha kuwarukisha kichura-chura, kuwapiga na kuwapandisha kwenye vikarandinga vidogo vya polisi (a.k.a. mbavu za mbwa) wananchi hao wakiwa wameswagwa haswa huku wakichuruzika damu kama nyama zilizo ning'inizwa buchani tayari kuuzwa.

Nimeandika mengi lakini, nirudi upande mwingine, nchi yetu ina hitaji amani, kuendelea kuheshimu watu wetu, sheria na taratibu za nchi ni hilo ni jambo la muhimu na la kila kiongozi kufata.

Vyombo vyetu vya dola hasa, polisi wasitumiwe vibaya kuumiza wananchi ambao ao hao ndiyo chanzo cha watu wanaofanya kazi kwenye vyombo vyetu vya ulinzi.

Polisi, tumieni weredi , hekima na utu mnapopewa majukumu na siyo kufanya pasipo kutathimini madhara ya matendo yenu kwa wananchi ambao nanyi ni sehemu ya wananchi na jiangalieni na ninyi baada ya hizo kazi na maisha ya familia zenu wenyewe leo mpo kwenye vyeo na nafasi hizo ila kesho hamtakuwepo kwenye vyeo hivyo.
Je, mtaishije kwenye jamii mnayoitesa?

Tena, watoto wenu na familia zenu zinaishi na wananchi ao hao mnao watesa kwa hiyo, jitathiminini kuhusu wananchi wanavyokuoneni ninyi baada ya kuua au kutesa jamaa zao wasio na hatia.

Viongozi wa juu , nanyi acheni utendaji feki wa kuacha kutoa pole kwa njia sahihi za mawasiliano yanayotambulikana kiserikali na kitaifa.
Toeni pole na salamu za rambirambi kwa njia ya barua zilizo na anuwani za ofisi zenu husika za Serikali, redio , gazette au luninga ili hadi Babu na Bibi zetu walioko huko Najilinji, kishumundu, Busega , Tosamaganga na Nyakatoke wote wasikie taarifa na siyo kujiandikieni vimaneno vyenu vitano tu tena kwenye mitandao ya kijamii ambako wazee hao hawapati hizo pole na salamu zenu za rambirambi.

Mfano, viongozi leo hii mnatumia FB, LinkedIn, Instagram na nyingine ile maarufu siikumbuki jina ila naona hata Trump anaitumia kule USA.
Kwa hiyo, tuacheni hizo tabia za kihunihuni na ujanjaujanja wa kitoto wa kutoa salamu za pole na rambirambi kwa wananchi walio kwenye mateso , uchungu, huzuni na majonzi kwa kupotelewa na jamaa zao tena kwa vifo vya kikatili na vya aibu kwa mfano, huyo Binti Akwilina A. B alivyouliwa kikatili hapo Kinondoni Dar Es Salaam.

Tanzania, iangalie na kujifunza kwa wale tuliokopeshwa kutoka kwao huu mfumo ya vyama vingi vya siasa , watu waelimishwe na zaidi Katiba itenganishe rasmi utendaji wa chama kwenye Serikali kuu na utendaji wa chama kinachokuwa madarakani. Kwa mfano, kwa sasa hivi, nchi yetu ya Tanzania inavyoendeshwa ni kana kwamba, CCM kama chama ndiyo Serikali na wanachama ndiyo watendaji wa Serikali ili hali wao wametoa Rais tu na siyo kuwa ndiyo wamepewa hati miliki ya nchi.

Jambo, lingine na la muhimu mno mno kwa Taifa letu , la kuangaliwa kwa umakini na watu wote (wananchi na vyombo vyetu vya ulinzi hasa JWTZ na TISS) hakikishine kuwa huu mfumo wa kiongozi yeyote kujichagulia marafiki, washirika na washauri lisimamiwe kwa ukaribu mno mno na hasa mambo wanayoyazungumza na wanayoyapanga kwa sababu, tusipokuwa makini katika eneo hilo hakika kuna siku viongozi wenye vichwa Nazi watauza nchi au kuitumbukiza kwenye vita kwa sababu ya aina ya marafiki na washauri wanao wapata huko nje ya nchi.

Mfano , USA huwa vyombo vyao vya ulinzi na usalama hawana hayo mahaba au imani na marafiki wa viongozi wao wa nchi hasa katika kujichagulia marafiki au washauri au kufanya mazungumzo ya siri na mtu yeyote wao mambo yote hufanywa mbele ya walinzi na washauri wa Serikali/ Rais na siyo vinginevyo.

Ulinzi wa nchi yetu na watu wanaoleta kutokuelewana kwetu hasa wanaotoka nje ya nchi.
Hili nalo ni muhimu, kuzingatiwa mno mno hapo Tanzania wakati Poise, nikiwa kijana mdogo wa umri wa miaka 15+ nchi yetu ililindwa nasi vijana, na wananchi kwa ujumla huku vyombo vya ulinzi vikifanya oparesheni kubwa na zinazohitaji nguvu zaidi, vifaa na weredi wa medani za kivita, kiulinzi na usalama.

Hapa, mtu atajiuliza hivi Poise, anataka kuandika jambo gani?
Hapa nataka kuandika kuwa; Tanzania ya kuanzia miaka ya 2000s wananchi wamejiondoa katika kulinda nchi na vyombo vya ulinzi tu ndiyo vinafanya hicho kitu.
Hii siyo nzuri mno kwa Taifa letu. Mfano, niende kwenye shambulizi la huyu mtoto anaitwa, TA. Lisu huko Dodoma mwaka jana, kama wananchi wangekuwa makini kama nyakati zetu zile tukiwa vijana wadogo mno hakika huko mitaani wale wasiojulikana ilikuwa wajulikane pale pale kwenye eneo la tukio huko mkoani Dodoma.

Sasa hivi, Tanzania ina haribiwa sana na Rwanda kupitia Mr. Slima a.k.a Ngongoti Kagame, huyu ni tatizo hapo Tanzania kwa sasa.
Rais, Mstaafu Mhe. Dr. Kikwete hilo alilijua vizuri ndiyo maana humu ndani alichekacheka nasi na kutuachia tu ila ilipokuja jambo la Rwanda na Kagame na ulinzi wa Taifa letu Dr. Kikwete hakuwa na mzaha wala kuchekacheka au urafiki na watu wanafiki kama Kagame.

Hivyo, Tanzania kuweni makini sana na huu urafiki na ujio wa kila baada ya wiki mbili wa Mr. Slim hapo nchini Tanzania.
Daima nyoka huwa hafunguliwi mlango ili aingie ndani tupate kumuua bali tunafunga milango na kumsaka akiwa uko huko nje ili tupate kumuua.

Mfano mzuri ni namna sasa wakati huo nikiwa kijana na mkakamavu wa Kati wa umri wa miaka 30 tulivyo funga milango na kisha tukamtumbua nduri IDD Amini Dada huko Uganda.

Hapo Poise, namaanisha kuwa Mr. Slim anatakiwa afungiwe nje japo ushirikiano na biashara ziendelee na siyo iendelee kama ilivyo awamu ya ngumi hii kuwa kila siku yuko ikulu au huko Tanzania akimshauri kiongozi wenu.
"Kagame must be stopped visiting Tanzania or die in Tanzania.

Hivyo watanzania wenzentu wote tuwe makini, tusimame kidete kupinga , kutaaa na kukemea na hata kuwaondoa watu au kundi la watu waouvu wanaotaka kuivuruga Tanzania.

Inawezekana kundi hilo au waovu hao wachache wanafanya wayafanyayo kwa kuelewa au kutokuelewa lakini kwa namna yoyote ile ni lazima wakemewe, wapingwe na hata kuondolewa katika nyadhifa hizo walizo nazo ili Taifa liendele kusitawi.

Naipenda nchi yangu mno mno ila , yaliyotokea na kusababisha maumivu, chuki, hasira , huzuni, majonzi kwa kila mtanzania mwenye utu, akili, hekima na maarifa na kila anayeitakia Tanzania mema anapaswa kuyakemea, kuyapinga na kuyazomea na kuwazomea wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuwa kikundi hicho kiovu na cha wauaji kiache hiyo tabia, waache matendo hayo maovu na zaidi watubu na kumrudia huyo Mwenyezi Mungu wanaye muomba kwa imani zao.

Mwisho, Poise niandike kuwa nitakuwa naandika kwa muda tu kisha naandaa mizigo yangu hapa tayari kwa safari maana nimehamishwa kituo cha kazi kutoka Wellington New Zealand na kwenda Middle East, Regional Office kwa kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi kesho wa March 5, 2018 hadi October 4, 2018.

Hivyo, kwa kipindi hicho cha miezi sita sitaweza kuwa online wala kuchangia humu jamvini JF platform.

Nipende kushukurun wote na zaidi , niwape pole jamaa, na wananchi wote walioguswa na madhila yote yaliyotokea katika nchi yetu hasa yanayosikitisha na kuhuzunisha.

Nihitimishe kwa sala fupi-

My prayers: Get well soon, TA.Lisu

R.I.P Binti yetu, Akwilina A. B.
R.I.P wote waliouawa kwa uonevu wa watu wachache wanaotaka wao tu kuishi na kuendeleza uovu wao.

Ndoto zenu zote zimezimwa kama vile mshumaa uzimwavyo.
Daima tutawakumbuka , Kristo Yesu awaangazie mwangaza wake wa milele. Amina.

Tukutane Middle East ila kwa hapa JF platform hadi October 4, 2018.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika ,
Mungu nibariki mno mno Poise.
Mkuu una ujumbe Mzuri ila ndefu sana.
Fanya kuuweka basi japo kama voice Note
 
Wanajamvi humu JF platform, sasa nakwea pipa kutoka Wellington tayari kuanza safari ya kuelekea ofisi zingine za kanda hapo Middle East.

Tutawasiliana tena kwa JF platform hapo October 4, 2018.
 
Umepotea kwelii asee ni mwaka sasa

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom