Salamu kwa wamiliki wa mabasi popote mlipo

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,749
21,202
Moja kwa moja kwenye mada.

Kwa mtindo huu wanaotumia madereva wenu hakika utadumu ila hautaweza kuhimili soko.

Dereva anataka kuwahi kufika Arusha au Mwanza saa 1700hrs, uko njiani ni fujo na hasara anayokuingizia ipo hivi; njiani kuna matuta makubwa (humps) na zile rasta (rumbles) anachofanya dereva ni kuyapita kwa speed kama zote ili basi la nyuma lisimpite.

Nashuhudia kwa basi za Mwanza -Arusha kama Capricorn, Asante Rabi nk, ni sawa kuwahi ila wanawapa hasara kubwa kwenye uhai na matengenezo ya hizo basi zenu

Bus (made in Tanzania or Kenya) ndiyo hasa yanye hizo ligi za kijinga, ndani ya basi ni kelele za staff carrier na madirisha kuelegea, abilia wanaokaa viti vya mwisho ndiyo wanapaswa kuelezea kwa ustadi kadhia hii ila wanaogopa sababu wakisema dereva anapanick na kuamua kupunguza mwendo na hatimaye Arusha au Mwanza mnaingia saa 2100hrs.

Wenye mabasi (luxury) ya kichina hawadumu lakini wanahimili soko, hii ndiyo akili ya biashara kuhimili soko huku unabadiri kitendea kazi kipya na siyo unadumu sokoni lakini hakuna mabadiriko.
 
Ma bus mengine bana..et una panda bus linaitwa KIAZI KITAMU sijui MASALU mala ASANTE RABI duuh .na yana endana na uhalisia wa gari lenyewe
 
Mabus ya Co. Ya Kilimanjaro naona yenyewe hua ni mwendo wa mdogomdogo tu mpk yanafika,ma-bus ya wastaarabu.
 
Kwa mtindo huo sioni wanachofanya kwa mustakabali wa uhai wa chombo, labda kama basi nyingine ndizo zinalipa kwa basi hizo za Ars-Mwz.
Asante Rabi na Kaprikoni wamewekewa muda na maboss wao,,kabla ya saa 17:30 anatakiwa awe Arusha/Mwanza
 
yapo mabasi yanaofata utaritibu mzuri hasa hii moud baba lao ya tanga,mwendo wao ni mzuri,yani kuanzia bus,dereva na staff wake huduma zao ziko poa mpaka hotel moja ambako wanaingia kuchimba dawa na kupata chakula na vinywaji pale msata ni yenye huduma nzuri na vyoo visafi mpaka ujutii kuichagua baba lao kwa safari za dar na tanga kupitia bagamoyo
 
Hayo ma Bus yakiwahi kufika wanapata faida sana kuliko yakichelewa au nini faida ya kukimbizana kuwahi kufika huko waendako?!

Nimewahi kusafiri kwa Bus kutoka Dar via Nairobi to Musoma na kurudi, huwa naomba Mungu nisitumie usafiri huo tena ikiwezekana.
 
Back
Top Bottom