Salama ya ndoa ni mke amuheshimu mume

Salama ya ndoa ni mke amuheshimu mume

Ofcoz yes
Si kweli maana heshima linatofautiana toka kwa mtu na mtu,unachoona ww ni heshima mwenzako anaweza ona si heshima,kuna mtu akiongea na ww ukakaa kimya kwa heshima anakuona umemdharau na una kiburi,
Kikubwa ni kufuata alichoamrisha Mungu juu ya ndoa tu,
Mwanaume mpende mke
Mke MTII mume,
Full stop
Acheni kujifanya wajuzi zaidi ya muumba
Yy anajua kwa nn kaamrisha wajibu huo kulingana na anavyojua alivyoumba
 
Usalama upo kwenye heshima tu... utampenda umuheshimuye na kumuheshimu umpendaye.
 
Kuheshimiana na kupendana na kuvumiliana pia
Acheni kutunga ya kwenu
Kanuni zilishawekwa na aliyeumba
Mke mtii mume
Mume mpende mke
Tatizo mnaona Mungu eti alipendelea wanaume kufanya ninyi muwatii,zama hizi mnageuza,mnataka utii na upendo mfanyiwe vyote ninyi,
Mafisadi wakubwa
 
Salama ya ndoa ni kufikishana juu ya mlima Kilimanjaro, kama mmoja asipofika ukafika pekeyako ni majaribu makubwa.

Kila mtu atimize wajibu wake, tuache mambo ya kutunzana na kutii au kuheshimu. Unaniheshimu au kunitii lakini uroda wangu unaliwa kwa siri, siku nikijua nakutwanga talaka na utiifu wako
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nadhani Mume anapaswa kumpenda mkewe, na kisha kumtunza na kumsikiliza pamoja na kumjali.
Mke anapaswa kumtii Mume wake, pamoja na kuhakikisha anampea tendo la ndoa.
Tendo lipo kwa wote.. mara nyingi ndoa hufarakana kwa sababu tendo linaoneka ni kwa mume tu. Jmn wake pia game wanapenda na kuhitaji. Huondoa upweke na hurudisha hata hiyo heshima kwa mume. Inawaweka wawekaribu hence heshima mapenzi mpenzi heshimu
 
Ukute mwanamke anakipato chake, basi mume anaonekana kama takataka, me mwanamke wa hivyo kwangu hana nafasi kabisa
 
Mwanamke anayetunzwa 100% ni yule aliye tayari kukaa nyumbani kulea watoto, kama wote tunatoka asubuhi kutafuta fedha then sababu gani inafanya yeye atunzwe na hali wote tunatafuta?? Safari za kikazi anaenda na huna ubavu wa kumzuia na hata ukimzuia hawezi kutii! Nimtunze kwa lipi???

Nafikiri suala sio kumtunza mke, swala ni ndoa ijengwe katika msingi mkuu wa upendo na uchamungu! Ikikosa msingi huu, mke hata umpe nn shida lazima itakuwwpo ktk hyo nyumba. Na hata mume pia anaweza kuwa chanzo cha matatizo ktk ndoa kama hana upendo na uchamungu.

Matatizo ya ndoa chanzo kikuu ni kuoana pasipokuwa na misingi mikuu ya upendo na uchamungu. Mtu unataka kuoa au kuolewa then unaweka kipaumbele ni hela au sura au muonekano wa umbo unategemea kuna ndoa hapo?? Obvious hapo itakuwa ni matamanio tu na yakiisha au yakitoshelezwa ndoa lazima itasumbua tu. Mke unaingia kwenye ndoa huku matarajio yako ni kutunzwa na sio kuwajibika ktk ndoa unategemea nn hapo??
Binafsi nilishagoma kuoa km ntakosa mwanamke wa kufanya majukumu yake nyumbani,lkn hawa wa unaamka SAA 11 asbh unatoka na yy anasafiri mm hapana,
Maana najijua hata Mali nipate mm ni yetu na familia maana kazi anayofanya mke ya kunitunzia nyumba ni kubwa km nnayofanya mm ya kutafuta pesa,najijua siwezi mdhurumu kiuchumi wala kudharau wajibu wake,siwezi mdharau wala kutompenda,
Hawa wa kuzurula oweni nyie,
Nikikosa ambae naona atatimiza takwa la kubeba jukumu la kukaa na familia basi sioi ntakaa na wanangu tu,maana kwa kuoa anaejitwisha jukumu langu ntakuwa sijaoa mke Bali mwanaume mwenye uke,
Ntakuwa nimeoa migogoro,
 
Tendo lipo kwa wote.. mara nyingi ndoa hufarakana kwa sababu tendo linaoneka ni kwa mume tu. Jmn wake pia game wanapenda na kuhitaji. Huondoa upweke na hurudisha hata hiyo heshima kwa mume. Inawaweka wawekaribu hence heshima mapenzi mpenzi heshimu
Kwenye hitaji kuu la mke, tendo halija tajwa mkuu.
Mke anahitaji kupendwa na Mume, na baada ya Mume kumpenda mke hapo ndipo mke hupata hamu ya tendo. Kumbuka kwamba pia mke huweza ingiliwa na Mume hata kama hajawa na utayari na likaitwa tendo, ilhali kiuhalisia mke akiwa amebakwa na Mume wake.
Lakini kinyume chake, Mume hata aweje, jogoo kuwika ni jambo la kawaida na hivyo hali hiyo hupelekea sasa uhalisia kwamba tendo ni one of the basic needs of mwanaume.
 
Hivi hii kauli mlojiwekea ya haki sawa majukumu kwa wote mlikuwa mnamaanisha nini,
Maana ikiguswa mishahara yenu kutumika sawasawa na ya mume mnakataa,lkn ikifika mahali pa kugawana hela ya mume na Mali mnasema haki sawa majukumu kwa wote,
Mmegeuka kupe
[emoji23] [emoji28]
 
Hivi hii kauli mlojiwekea ya haki sawa majukumu kwa wote mlikuwa mnamaanisha nini,
Maana ikiguswa mishahara yenu kutumika sawasawa na ya mume mnakataa,lkn ikifika mahali pa kugawana hela ya mume na Mali mnasema haki sawa majukumu kwa wote,
Mmegeuka kupe
[emoji23] [emoji28]
 
Acheni kutunga ya kwenu
Kanuni zilishawekwa na aliyeumba
Mke mtii mume
Mume mpende mke
Tatizo mnaona Mungu eti alipendelea wanaume kufanya ninyi muwatii,zama hizi mnageuza,mnataka utii na upendo mfanyiwe vyote ninyi,
Mafisadi wakubwa
Povu
 
Nafikiri ungeiweka kwa wanandoa tu ingependeza zaidi, maana ambae hayupo ndani ya ndoa kujadili ndoa ni sawa na kujadili tamthilia ambayo bado hujaiona, ndoa sio boyfriend na girlfriend, ndoa sio mpenzi na mpenzi na wala ndoa sio mchumba na mchumba, hizi zote ni hatua za kudanganyana tu, ndani ya ndoa mambo ni tofauti kbs na fikra za makundi haya matatu.
Ndani ya ndoa ndipo mnajuana tabia halisi zilizofichika kwa jinsia zote mbili kwa kipindi kirefu kila mnapisonga mbele na maisha, huko ndani ndio mtajuana nani alitaka kutimiza lengo na kwa msukumo gani, je kuna aliekimbili/alielazimisha kwakuwa umuri ulimtupa mkono!? Kuna aliefuata pesa/mali, kuna aliekwepa hali ngumu ya kimaisha au manyanyaso fulani, yani kila mkipata mtoto lazima yashuhudiwe mabadiliko mmoja kati yenu, huko hakuna majina ya kipuuzi sijui sweetie, honey, baby nk na kama yatakuwepo basi ni kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa iliyovunjika upande wa pili, it means muda wowote inaweza kukujeruhi.
Huku tuachiwe tuliokwisha yavulia nguo maji basi.
 
Hili nilishindwa kulipanga kwa maelezo ila mkuu umegonga pentagon kabisa. Wanawake tunaotakiwa kuwahudumia 100% ni wale housewives other than that tutatoa basic needs tu za nyumbani maana wao pia wana kipato cha kufanya mambo yao binafsi and it does make a huge sense to me.

Kama unataka nikupe support ya mahitaji 100% basi acha kazi mbaya zaidi hakuna mwanamke atakaelikubali hili kirahisi, mtalumbana sana yani.

Cha mwisho kuwa submissive ni hulka ya mwanamke tu alielelewa katika misingi imara ya kinidhamu. Mwanamke msikivu toka kwao hata anapoelezwa jambo na mume huwa mnyenyekevu na sio mbishi wa kupaza sauti juu ya mumewe. Hatajali anafanya kazi gani ama ana mchango kiasi gani kwa familia kisha atumie hio kama kipimo cha aidha kumuheshimu mume au kutomuheshimu. Mwanamke wa hivi hujenga familia yenye amani na furaha tokana na busara zake.
Well said mkuu. Naunga mkono hoja.
 
Siyo hawataki
Mnataka mtunzwe zaidi ya uwezo wa mume,
Unakuta mumeo mponda kokoto unataka akupe mahitaji sawasawa na anayopewa mke wa Mengi,
Na unamtolea mfano kabisa,
Eti mbona mke wa mengi kazawadiwa Benz na mumewe siku ya birthday yake,
La muhimu msiwe mnaolewa na watu ambao hamuwezi vumilia hali zao za kiuchumi,subirini wazaliwe matajiri watakuja kuwaoa,
well said.
 
Nafikiri ungeiweka kwa wanandoa tu ingependeza zaidi, maana ambae hayupo ndani ya ndoa kujadili ndoa ni sawa na kujadili tamthilia ambayo bado hujaiona, ndoa sio boyfriend na girlfriend, ndoa sio mpenzi na mpenzi na wala ndoa sio mchumba na mchumba, hizi zote ni hatua za kudanganyana tu, ndani ya ndoa mambo ni tofauti kbs na fikra za makundi haya matatu.
Ndani ya ndoa ndipo mnajuana tabia halisi zilizofichika kwa jinsia zote mbili kwa kipindi kirefu kila mnapisonga mbele na maisha, huko ndani ndio mtajuana nani alitaka kutimiza lengo na kwa msukumo gani, je kuna aliekimbili/alielazimisha kwakuwa umuri ulimtupa mkono!? Kuna aliefuata pesa/mali, kuna aliekwepa hali ngumu ya kimaisha au manyanyaso fulani, yani kila mkipata mtoto lazima yashuhudiwe mabadiliko mmoja kati yenu, huko hakuna majina ya kipuuzi sijui sweetie, honey, baby nk na kama yatakuwepo basi ni kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa iliyovunjika upande wa pili, it means muda wowote inaweza kukujeruhi.
Huku tuachiwe tuliokwisha yavulia nguo maji basi.
We jamaa umetisha! Ndoa ni kitu kingine, honey na sweetie hupungua kadiri ya muda unavokwenda. Kadri mnavojaaliwa watoto na mali mambo hubadilika pia. Si rahisi sana mtu kuisemea ndoa kama hujatimiza miaka 5 ndani ya ndoa. Siri ya kufa aijuaye maiti.
 
Back
Top Bottom