Salam zao Apson na Mboma

Status
Not open for further replies.
Mjomba kapata nauli, vibaka wamejipanga wampore asije town_
ndo wanachofanya huko kwa wana wa zenji.
 
Mkulu behu niweke wazi kweli hilo maana kuhusu APSON kila mtu anajua alivyo haribu kwa kuweka TISS kuwa kama chaka la ma incopetents lakini hili la R.O sijakuelewa hebu niweke wazi mkulu

GT nakushukuru kwa kujitokeza dhahili na kuweka hiyo website ya sie waislamu tunaotaka kuoa au kuolewa!!!
 
Ukweli utakuja kujulikana tu, kwa sasa wanatapatapa!! siku zao zitakuja kuhesabika....
 
siku zinahesabika, nchi inaanza kuwa ndogo, watakimbilia wapi na aibu zao?
 
Is there a possibility that somewhere out there an MOU between BWM and JMK exists? This would explain so much especially taking into account the date the MOU could have been signed. Could it be possible that in that MOU an offer was made - an offer that could not be refused ? - something like, I know what you did last summer ? An offer that highlighted the need for the two to stick together ?

I am always a little concerned of alliances of the unlike, they tend to make two completely opposite charaters be ready to die for each other or both perish. They will go to any length to garner and preserve loyalty among their most trusted lieutenants - former and present. Presently there is a very dangerous scenario that is emerging, and we have every reason to be wary of our very own axis of evil.

There is one glimmer of hope nevertheless and it involves fighting back by exposing the truth. Until the truth comes out we are but like some caged animal and only truth can set us free. Truth is like a lamp, you dont light a lamp and then try to hide it - you light it so it chases away darkness. We have just lit the lamp, let it shine so it shows us the dangers in our otherwise dangerous path to freedom.
We shall overcome !
 
kwa kweli unajua mtu mkabila ni mkabila tu; sasa mtu ukifanya ufisadi kwa misingi ya ukabila unategemea watu wa kabila lako kukutetea au kuwa upande wako; sasa unajikuta unashangazwa inakuwaje mtu wa nyumbani hakuungi mkono? Vivyo masuala ya udini. Tumefika mahali tunataka kuangalia fisadi kwa kuangalia ni mtu wa dini yetu au la (zile seti). Sasa mafisadi na wenyewe wameshakuwa wataalamu wa hili.

Wanatuchezea katika vitu hivi vya udini na ukabila. Na sisi katika fikra zetu tunaangalia kama fisadi ni 'mwenzetu' au la. Matokeo yake asipokuwa mwenzetu tutapiga kelele sana lakini tukigundua kuwa ni mwenzetu tunapita kama vile hatumwoni.

Ndiyo kwa sababu hiyo ninakataa katika vita hii dhidi ya ufisadi kuwa na ushirika, udugu, urafiki, ujamaa, umoja na kuremburiana macho kwa aina yoyote na mtu ambaye ana chembe za ufisadi. Kwangu mimi usiposimama kutetea raslimali za nchi yetu, usiposimama kupiga vita uporaji wa utajiri wetu na kugawana kama wawindaji wezi wa mali zetu wewe ni fisadi per excellence!

Na mtu anaposimama kwa namna yoyote kama adui wa jamhuri yetu huyo ni Kigogo wa ufisadi! Haijalishi anatoka kijiji kimoja na babu yangu au walisoma shule moja na mjomba! Nimesema hapo nyuma katika uovu hakuna udugu wala urafiki!
 
Nilidhani hili lilitegemewa na wengi ndio litakuwa toleo la tatu la ripoti ya meremeta, thanks god im still living to witness this prophecy.

hivi meremeta ndio ilihusishwa na jeshi sio ama nakosea? Mwisho wa Ubaya ni Aibuuuu. yangu macho
 
Last edited:
kwa kweli unajua mtu mkabila ni mkabila tu; sasa mtu ukifanya ufisadi kwa misingi ya ukabila unategemea watu wa kabila lako kukutetea au kuwa upande wako; sasa unajikuta unashangazwa inakuwaje mtu wa nyumbani hakuungi mkono? Vivyo masuala ya udini. Tumefika mahali tunataka kuangalia fisadi kwa kuangalia ni mtu wa dini yetu au la (zile seti). Sasa mafisadi na wenyewe wameshakuwa wataalamu wa hili.

Wa kwanza kuingizwa mkenge ni mume wa Anne Kilango, anajifanya anapinga ufisadi kumbe anapalilia. Sisi sio wajinga tena. Tanzania hakuna udini wala ukabila.
 
Last edited:
Wa kwanza kuingizwa mkenge ni mume wa Anne Kilango, anajifanya anapinga ufisadi kumbe anapalilia. Sisi sio wajinga tena. Tanzania hakuna udini wala ukabila.

Navyojua mimi Mzee John Samwel Malechela alikua na share pale Mwadui Diamond Mining wakati akiwa waziri mkuu, sijui anajitoaje kwenye ufisadi.
 
Navyojua mimi Mzee John Samwel Malechela alikua na share pale Mwadui Diamond Mining wakati akiwa waziri mkuu, sijui anajitoaje kwenye ufisadi.

If you wanna rock Malecela investigate dubious deals between him and Mzindakaya when he was RC in Kigoma. Ya kwanza iko kwenye matank ya rami yaliyouzwa Burundi na kusababisha Wa-KGM kukosa barabara ya Rami hadi leo. Pili ukipekua ma-file ya Bodi ya Korosho utamkuta Malecela akiwa Balozi US akishirikiana na Wahindi kuhujumu Bodi, kitu ambacho kiliishia Bodi kutokopesheka na kufilisika japo sasa inafufuka. Lakini pamoja na haya, kwangu yaliyopita si ndwele, kama anajutia, anatubu makosa na kukanya wakengeufu wapya ni mzuri kuliko ambaye anaendelea tu bila kutubu. Hata EL akifanya hivyo nina hakika wengi tutamsamehe.

Bwa bwa bwa! mayowe ya kichanga
 
pole Mwanawane, najua vita hii kubwa, Nimejaribu kusoma mistari ila bado natafakari.
 
Baada ya salamu nina ujumbe kwenu: Stand down. Makuwadi na vikaragosi vyenu viambieni virudi nyuma. Miti mingine haikwewi na milima mingine inatosha kuiangalia kwa mbali tu. Mlifanyalo lifanyeni haraka kwani kiza kimeingia.

NB: Salam kwa RO... if you act now you (kwa kumhamisha kuwadi wao) you might change my mind (probably others too) but if you don't nitaamini umesanction the stealth move.

Otherwise; 2010 ni mwisho wao. So like that stupid commercial here in the US "do you want it to hurt now or later".. ?

Vitoto vya Nzi navyo havilali!

MKJJ, huko kijijini mnasikiliza taarab sana siku hizi nini? Maana mistari hii imekaa ki East african melody lol.
 
Stand down. Makuwadi na vikaragosi vyenu viambieni virudi nyuma. Miti mingine haikwewi na milima mingine inatosha kuiangalia kwa mbali tu. Mlifanyalo lifanyeni haraka kwani kiza kimeingia.

Kwani wanataka kutoa roho ya mtu? Mungu akulinde. Halafu nilikuwa na wasiwasi juu ya kufahamika kwako, zile namba za simu ulizotoa kuchangia ripoti ya Meremeta, si zinaweza kukufanya ukafahamika mzee na hao vikaragosi wakapata kazi ya kufanya?
 
Kufahamika mbona nafahamika vizuri tu; kinachonisumbua ni hili kundi ambalo linaamini kabisa kuwa nchi hii ni ya kwao kabisa na sisi wengine ni wapangaji na tunahitaji kuomba kibali kwao ili tuwe.
 
Kufahamika mbona nafahamika vizuri tu; kinachonisumbua ni hili kundi ambalo linaamini kabisa kuwa nchi hii ni ya kwao kabisa na sisi wengine ni wapangaji na tunahitaji kuomba kibali kwao ili tuwe.
Na huu ndo uongo mkubwa ambao baadhi yetu tumeuingiza rohoni na kuulinda kama mboni ya jicho.Ni makosa makubwa kufikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote hata kama ni ovu kiasi gani, pasipo kupata madhara yoyote.Kama hizi kelele zinazopigwa hazitawabadili nia, naam, kuna nguvu nyingine zitakazoweza kufanya hivyo. Mbona Sani Abacha naye himaya yake ilifika ukingoni?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom