Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 309
Mheshimiwa Rais, mimi ni mpiga kura wako ambaye nimekuwa sifurahishwi na maneno yanayoanza kuzoeleka sasa kama misamiati sahihi ya kuwapa matumaini yasiyokuwepo ama kwa sababu hamna utashi wa kisiasa ama hamna uwezo (ninyi kama wanasiasa) kuyatekeleza na badala yake inakuwa kana vile siye ni midoli yenu ya kujiburudisha nayo.
Naongelea maneno ambayo wewe na wanasiasa wenzako mnapenda kuyatumia kama haya hapa:
Naongelea maneno ambayo wewe na wanasiasa wenzako mnapenda kuyatumia kama haya hapa:
- Tutawapatia wanafunzi wote wa Tanzania Komputa
- Tutajenga barabara za kupita juu kwenye mji wa Dar es Salaam
- Tutaboresha masilahi ya wafanyakazi
- Tutapeleka maji ya ziwa Viktoria hadi Tabora
- Tutaunganisha kila makao makuu ya mkoa kwa njia ya rami