Salaam kwa Ismail Aden Rage - Tabora Mjini; Jiandae...

Salaam kwa Ismail Aden Rage - Tabora Mjini; Jiandae...

Mheshimiwa Kiongozi Wetu,

Kwa masikitiko makubwa napenda kukutumia salaam za kukuamsha na kukutaka sasa uwatumikie wakazi wa Tabora Mjini kama ambavyo uliahidi katika kampeni zako mwaka 2010. Sasa hakuna mzaha tena...

Mkoa wa Tabora umekuwa ni mkoa wa mwisho kabisa kimaendeleo japo kwa hakika ulitakiwa uongozwe na watu makini ili uwe kileleleni kabisa kwa kuwa kuna kila opportunity na resources za kufanya hilo, na sio kuongizwa na nyie wenye kupenda michezo zaidi kuliko kuugua kwa tabu za wananchi wenu. Wewe na viongozi wetu waheshimiwa waliopita mnaona kama Tabora sio yenu. Ni sawa nakubaliana na wewe, na hilo wazo lenu, Tabora sio yenu maana hata asili zenu zinaonyesha nyie sio wenyeji wa Tabora, lau hili ndio linawapa uvivu wa kuuendeleza mkoa huo maskini kabisa.

Wewe toka umechaguliwa kuwa mbunge wa Tabora mjini umejikita zaidi kwenye michezo, basi potelea mbali ingekuwa hata michezo huko jimboni kwako, wewe umekazania Simba simba simba hata umesahau majukumu yako kama mbunge, na mimi sasa ni wajibu wangu na ni wajibu wa kila mwenye kufikiri sawasawa kukukumbusha ili usije sema hukuambiwa. Tabora imebakia hata timu ya mkoa ile ya Milambo ya daraja la kwanza sasa haziko vichwani mwenu nyie wapenda kucheza, sasa hivi kwako wewe mheshimiwa kipi ni bora, nyumba yako iteketee huku ukiiacha na kwenda kuokoa ya jirani, ama uokoe yako kwanza na kisha ya jirani yako? Jibu kiukweli bila unafki!

Tuangalie elimu huko Tabora. Suala la elimu wewe kwako sasa ni kitendawili mheshimiwa, ni karibu tu na mjini kabisa huko kata ya Malolo, ama huko Ntalikwa, hebu tupa jicho kwa shule zetu za msingi na zahanati huko kiloleni. Hebu ona huruma kwa akina mama wa Ng'ambo wanavyohaha kugombania maji visimani, hivi wewe huoni usalama wa raia wako ulivyo rehani huko Chemchem, ama ndio sababu nasikia siku hizi unabeba na bastola kujilinda? Ona miundombinu ilivyo hovyo, halafu unaishia kupoteza muda na Simba, sasa nakuomba chagua moja kati ya Simba ama Siasa.

Maana inafikia wakati sasa wapiga kura wako wanakutafuta wakueleze shida zao na hawakupati, wanashida na mbunge wao lakini wanaambulia patupu.

Imefika wakati sasa uondoke, vuguvugu na wimbi la mabadiliko sasa linapiga hodi Tabora mjini na sisi tunao vijana wazuri tena wenyeji wa hukohuko wenye huzuni na hasira na umwinyi wenu wa kupenda ukubwa hali hamfanyi lolote kwa watu wenu. Hawa sasa tunawapika kuanzia sasa hadi mwaka 2015 ili tuone kati ya vijana wa mabadiliko na wazee wa umwinyi ni wepi hasa watakaoleta mabadiliko na maendeleo hapo Tabora mjini. Hili ni lazima liwe jambo ambalo wewe kama mteuliwa na sauti ya wananchi unatakiwa sasa kuanza kufikiri kama uache wewe mwenyewe kwa hiari yako ama uache baada ya kupoteza mapesa mengi muda na aibu tupu.

Ni sawa kwamba Tabora mjini haijawahi kupata wagombea vijana makini zaidi ya Mr Zambia kwa kipindi chote, lakini sana haijapata mgombea mwenye ushawishi kwa vijana kwa kipindi hicho na mwisho wagombea hao wamekuwa hawana uwezo kifedha na hivyo kazi ya kuyafikia maeneo yote ya jimbo inakuwa ngumu. Sasa tunaanza rasmi mwaka ujao, tutaeleza uozo wako kwa wapiga kura wako na tutaandaa vijana wetu kwa mabadiliko na maendeleo yao kupitia jukwaa la siasa. Tutawaonyesha wana Tabora matumaini yaliyopotea na tutaimba wimbo wa mabadiliko hadi wewe na vibaraka wako muusikie na mfungashe vilivyokuwa vyenu.

Haingii akilini kabisa wakazi wa Cheyo kukosa kituo cha polisi kwa kipindi chote, hakuna mtu anayekuelewa kama soko la pale National, kule Tambukareli, na Rufita, na hata Ipuli, yanavyosuasua na sasa ushuru wa manispaa unalegalega bila mpangilio na wewe upo na unatazama haya bila kusema lolote. Haileti picha njema kuona wafanya biashara wadogowadogo wamachinga ukishindwa kuwatafutia eneo maalum, wewe kazi simba tu simba tu, hivi nikuulize hili, hao Simba ndio walikutuma uwe mbunge wa Tabora mjini mheshimiwa?

Huko Kwihara, pale Kipalapala, pale si ndio yule Mzungu, Dr Livingstone aliacha Tembe lake ambalo ni eneo zuri sana la utalii mkoani Tabora? Pale ndio nyumba ya Chief Abdallah Fundikira aliacha nyumba yake, na pana jiwe kubwa, jabali, mahali ambapo wachawi walikuwa wanauawa? Wewe huoni kama hiyo ni sawa na utalii? Basi wewe labda sema vipaumbele vyako ni vipi hasa mheshimiwa! Maana hatukuelewi kabisa.

Hebu ona wananchi wa Mbungani wanavyohaha na magonjwa ya kuhara kwa sababu mitaro ni hadi milangoni kwao, wewe uko na hamsini zako tu, ama hawakuambii? Hata polisi sasa wanaishi kwenye vibanda vya chuma kama wakimbizi wewe kwako heko tu, labda kwa sababu wanawashikaga wakati wa kampeni.

Tabora mjini sasa ni lazima iwe zaidi ya Wilaya ya Nzega, ni lazima sasa ufike wakati, wanatabora waone kweli mbunge wao na nchi yao inawatendea haki na wote kwa pamoja wanafaidi matunda ya uhuru wao. Kama hayo huyawezi, basi sie akina PANGU PAKAVU TIA MCHUZI, tuko nyuma yako unyayo baada ya mwingine kuhakikisha unaondoka haraka kwenye umwinyi na kuacha ya Tabora kwa wana Tabora.

Hizi na ziwe salaam zako za Krismas na Mwaka Mpya.

Ni Mimi Pangu Pakavu,
Nakusalimia.

Hossam,mungu akubariki sana kuleta hii thread hapa,sijua kama wewe ni mwana TABORA au ni uchungu wa either U-TABORA au UTANZANIA.Sijawahi kuwa mfuatiriaji sana wa siasa za Tabora japo mimi ni haswa ''UNYANORA''born and breed,japo baadae ''NILIHASI''na kwenda kutafuta maisha nje ya''NORA''
Kama nilivyosema kuwa sina sana history ya siasa za Tabora lakini nasikitishwa sana na maendeleo ya Tabora kwa ujumla,unajua watu wa nje ya Tabora wanatusema kwamba sisi wanyamwezi ni YANIYANI,maana yake kwamba tunaridhika na siku inavyokuja kwamba tukipata ugali na NSASA leo siku imepita tunasubiri kesho mungu atatuletea nini,ndivyo watu wanaotujua wasemavyo,wakati sio kweli.Najua wanyamwezi ni very Hardworking people,tuna rasilimali nyingi tu za kutufanya mkoa wa Tabora uwe juu kimaendeleo lakini tumebakia kuwa mikoa masikini na watu masikini wa kutupwa.Bado najiuliza mpaka leo sipati jibu.Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 80 wakati mdogo nilikuwa nakuja Tabora kumtembelea mjombaangu kule Sikonge,yeye alikuwa mkulima,mfugaji na mlina asali.Mwaka huo ulikuwa mwaka wa neema sana kwake kwani alivuna mavuno mazuri sana na akapata pipa 30 za asali na nta kilo 400 ambazo by then alipata kama Tsh 12 million,yes 12 million miaka ile ya 80 na alikua mwanachama wa kile chama cha walina asali cha Kipalapala.Sasa kama mtu just mkulima aliweza kupata pesa yote hiyo na hakuwa pekee kwa nini mkoa bado masikini japo huwezi kusema kwa kuchukua sample moja kama hiyo basi umefikia jawabu kwamba umasikini utakuwa umetoka hapana huo ni mfano tu.
Maelezo yangu hapo juu nilitaka kutoa picha na siasa za Tabora kwa sasa,kwamba kweli wana Tabora tulikosa mtu kabisa tuliefikiria mbadala ambaye angetuletea maendeleo mpaka tumchague Rage kuwa Mbunge wetu?je tulimpima kwa vigezo gani kuona kwamba anatufaa au ni kwa sababu alitupa kofia na kanga na pilau za bure ndio tukamchagua?sijui.
Guys,it is high time tufanya mabadiliko mkoani kwetu.Tutafute mtu mwenye uchungu na Tabora yetu,ikiwezekana atoke hapo hapo Tabora anaye jua matatizo ya Tabora kindanidani.Na wala tusiangalie chama,tuangalie mtu mwenye uwezo wa kutuletea maendeleo na mabadiliko ya kweli,kwa sababu Tabora kuna potential na opputunities nyingi za kuubadili umasikini wetu.

Wakati wa mabadiliko kuelekea 2015 ni sasa na sio kesho na Wana Tabora wenzangu mlio nje ya Tabora na Tanzania twendeni tukatie changamoto ya kuundeleza NORA yetu.Naweza kuwa nimewachosha kwa kuandika ''upupu'' lakini naamini Tabora ni changamoto kwetu wana Tabora na Watanzania kwa ujumla.Mungu ibariki Tabora,mungu ibariki Tanzania
 
mbunge wetu.jpg

samahani,
je ndiye huyo hapo juu.
 
Mimi nina ushahidi aden rage alikuwa ni mmoja wa wanamgambo wa al shabaab na alitoroka kwenye bandari ya lamu kismayu akakimbilia tz akiwa amedandia lori

Baba baba chonde chonde, mwaga mboga baba nimalizie ugali, tumalize mzozo, una proof mkuu??
 
Kashindwa kuwasaidia ndugu zake huko Somalia, af ndo aje awasaidie nyie watu baki wa Tabora!!
 
Na uzipate kweli salaam hizi MJOMBA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
SISI ndo wa ukweli na TABORA HUYU jamaa mnajua kama alikuja kwa lori la fusooooooooo! nawashangaa hata waliompa kura hizo CCM nyinyi mnauza nchi kinyemela mara wahindi mara wasomali ndiyo maana hawana uzalendo hawa. sasa nasema uzawa kwanza ubaguzi baadae msipo elewa mtajua nini maana ya neno MIRAMBO.
 
Halafu nilikuwa sijaona ile pichaaaaaaaaaaaaaa. JAMANI Kweli huyu Ndiye anae tafutwa na jeshi la kenya!!!!!!!!!!!.......... LI-BASTOLA LA NINI MKUTANONI? kanyoli ba'gosha.
 
Vipi kwani watu mbadala hawapo? hebu mjipange 2015 Tanzania inahitaji kuandika historia mpya kabisa
 
Jitieni Nira yenu mkajifunze KWETU.......................
 
Poleni

Mnaonaje mkajaribu upinzani?
Huoni mtaletewa maendeleo ya haraka
Msomali na ubunge wapi na wapi poleni saana
 
Hossam,mungu akubariki sana kuleta hii thread hapa,sijua kama wewe ni mwana TABORA au ni uchungu wa either U-TABORA au UTANZANIA.Sijawahi kuwa mfuatiriaji sana wa siasa za Tabora japo mimi ni haswa ''UNYANORA''born and breed,japo baadae ''NILIHASI''na kwenda kutafuta maisha nje ya''NORA''
Kama nilivyosema kuwa sina sana history ya siasa za Tabora lakini nasikitishwa sana na maendeleo ya Tabora kwa ujumla,unajua watu wa nje ya Tabora wanatusema kwamba sisi wanyamwezi ni YANIYANI,maana yake kwamba tunaridhika na siku inavyokuja kwamba tukipata ugali na NSASA leo siku imepita tunasubiri kesho mungu atatuletea nini,ndivyo watu wanaotujua wasemavyo,wakati sio kweli.Najua wanyamwezi ni very Hardworking people,tuna rasilimali nyingi tu za kutufanya mkoa wa Tabora uwe juu kimaendeleo lakini tumebakia kuwa mikoa masikini na watu masikini wa kutupwa.Bado najiuliza mpaka leo sipati jibu.Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 80 wakati mdogo nilikuwa nakuja Tabora kumtembelea mjombaangu kule Sikonge,yeye alikuwa mkulima,mfugaji na mlina asali.Mwaka huo ulikuwa mwaka wa neema sana kwake kwani alivuna mavuno mazuri sana na akapata pipa 30 za asali na nta kilo 400 ambazo by then alipata kama Tsh 12 million,yes 12 million miaka ile ya 80 na alikua mwanachama wa kile chama cha walina asali cha Kipalapala.Sasa kama mtu just mkulima aliweza kupata pesa yote hiyo na hakuwa pekee kwa nini mkoa bado masikini japo huwezi kusema kwa kuchukua sample moja kama hiyo basi umefikia jawabu kwamba umasikini utakuwa umetoka hapana huo ni mfano tu.
Maelezo yangu hapo juu nilitaka kutoa picha na siasa za Tabora kwa sasa,kwamba kweli wana Tabora tulikosa mtu kabisa tuliefikiria mbadala ambaye angetuletea maendeleo mpaka tumchague Rage kuwa Mbunge wetu?je tulimpima kwa vigezo gani kuona kwamba anatufaa au ni kwa sababu alitupa kofia na kanga na pilau za bure ndio tukamchagua?sijui.
Guys,it is high time tufanya mabadiliko mkoani kwetu.Tutafute mtu mwenye uchungu na Tabora yetu,ikiwezekana atoke hapo hapo Tabora anaye jua matatizo ya Tabora kindanidani.Na wala tusiangalie chama,tuangalie mtu mwenye uwezo wa kutuletea maendeleo na mabadiliko ya kweli,kwa sababu Tabora kuna potential na opputunities nyingi za kuubadili umasikini wetu.

Wakati wa mabadiliko kuelekea 2015 ni sasa na sio kesho na Wana Tabora wenzangu mlio nje ya Tabora na Tanzania twendeni tukatie changamoto ya kuundeleza NORA yetu.Naweza kuwa nimewachosha kwa kuandika ''upupu'' lakini naamini Tabora ni changamoto kwetu wana Tabora na Watanzania kwa ujumla.Mungu ibariki Tabora,mungu ibariki Tanzania

Baba huandiki upupu hata kidogo, umenigusa palepale mkuu wangu, moja kati ya vitu vinavyouma sana ni namna ambavyo Rage anashindwa hata kuipa nguvu jumuiya ya Nyuki pale barabara ya airport. Hawa jumuiya wangepewa fedha kidogo tu za working capital na kupata mizinga ya nyuki ya kisasa wangepanua sana urinaji wa asali Tabora, vijana wengi wangepata ajira indirectly, kwa mfano angepigania hata kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengenezea mishumaa ya bei rahisi. Kwa kufanya hilo Rage angeleta ajira, nishati (taa yaani usalama) na pia angezidi kuitangaza Tabora kama sehemu pekee ya kupata asali safi Tanzania.

Leo hii kule Pemba wanauza asali, wanasema ni ya mikarafuu, na ina soko hata huko Dar na Tanga, sasa ni kwa nini huyu bwana anakazania Simba tu simba tu utadhani yeye ni mbunge wa Simba, wenzake wanatembelea hata majimbo yake baada ya mikutano ya bunge, yeye sidhani hata at this point in time kama atakuwa Tabora, kweli inauma sana Rage.

Mimi kaka hujasema baya, ipo siku ntakutumia msg provately, hapo ntaivua ID yangu ili tufahamiane mkuu.

Ni mimi,
Pangu Pakavu.
 
Haya sasa, tulisema Al-Shabaab wengine wakabisha!Aden Rage kwishny siku nyingi kwa U-AlShaababu wake.

Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuvumilia sura za aina ile hata kidogo. Kitendo cha Aden Rage kujitokeza hadharani na kujitutumua na
BASTOLA mbele ya umma pale Igunga (U-Al-Shabaab usiosameheka tena bila maendeleo yoyote Tabora) ni kwamba kikohozi cha kule Kismayu kilimbana hata akashindwa kukificha hata tone.

Cha msingi, Wana-Tabora Mjini anzeni kumtafuta mapema Kijana mwenzetu mwenye uzalendo wa kweli ili akaanze mapema kupiga jaramba kwenda kupokonya kete toka kwa huyu Al-Shabaab-Mbunge-wa-Posho ili na nyie huko mpate maendeleo kuanzia 2015.

Mimi nina ushahidi aden rage alikuwa ni mmoja wa wanamgambo wa al shabaab na alitoroka kwenye bandari ya lamu kismayu akakimbilia tz akiwa amedandia lori
 
Mnaongozwa na Kilaza!

This is not true. You can not call this guy Kilaza! Can you stand against him anywhere ( at a political rally, court. e.c.tc). Sema tu kawasahau watu wake kwa ajili ya kukaa sana mjini na mengine. Lakini jamaa ni Kilaza? The answer is NO! Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
 
Baba huandiki upupu hata kidogo, umenigusa palepale mkuu wangu, moja kati ya vitu vinavyouma sana ni namna ambavyo Rage anashindwa hata kuipa nguvu jumuiya ya Nyuki pale barabara ya airport. Hawa jumuiya wangepewa fedha kidogo tu za working capital na kupata mizinga ya nyuki ya kisasa wangepanua sana urinaji wa asali Tabora, vijana wengi wangepata ajira indirectly, kwa mfano angepigania hata kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengenezea mishumaa ya bei rahisi. Kwa kufanya hilo Rage angeleta ajira, nishati (taa yaani usalama) na pia angezidi kuitangaza Tabora kama sehemu pekee ya kupata asali safi Tanzania.

Leo hii kule Pemba wanauza asali, wanasema ni ya mikarafuu, na ina soko hata huko Dar na Tanga, sasa ni kwa nini huyu bwana anakazania Simba tu simba tu utadhani yeye ni mbunge wa Simba, wenzake wanatembelea hata majimbo yake baada ya mikutano ya bunge, yeye sidhani hata at this point in time kama atakuwa Tabora, kweli inauma sana Rage.

Mimi kaka hujasema baya, ipo siku ntakutumia msg provately, hapo ntaivua ID yangu ili tufahamiane mkuu.

Ni mimi,
Pangu Pakavu.

Mate,just PM me,am out and about.Will give my contact and start from there,Tabora belongs to us and outsiders will do nothing to develop our less than underdeveloped Tabora.Be and stay blessed
 
Mkoa mzima wa Tabora una matatizo nadhani kwa sasa ni mkoa pekee ambao haujaunganishwa na lami angalau wilaya moja na nyingine ukiachilia Igunga to Nzega ile njia kuu ya Dar to Mwanza.Kweli wenyeji wa Tabora inatuuma sana lakini chanzo ni sisi wenyewe,sasa hv vijana wote tumeukimbia mkoa tumeacha wazee na ndiyo maana Magamba wamechukua 100% nafasi za ubunge na zaidi ya 95% udiwani.Ni kweli jamani vijana wa Tabora tujipange tukafanye mageuzi pale,Lakini wazee wetu mliopo Tabora mimi siwezi acha walaumu nyie hivi kweli hata kama mnaipenda ccm ndiyo mnamchagua huyu msomali kweli?
 
Ni vema umeujuza ulimwengu hayo yanayotokea huko tabora. lakini kama unaweza, siku moja nenda kwenye mkutano wake wa hadhara umweleze moja kwa moja

We humtakii mema mwenzako, hujui kama yule jamaa anatembeaga na mguu wa kuku.
 
ADEN sio al shabab ila ana mkono katika shughuli za uharamia zinazoendelea kila kukicha kwenye bahari ya hindi upande wa somalia,wapo wengi mbona,Hata Lowassa anatajwa kama mmoja wa wafadhiri na wanaonufaika na shughuli za uharamia wa utekaji meli na kudai mabilioni kwa wamiliki,kushamiri kwa maghorofa yanyojengwa na wasomali kariakoo pamoja na biashara zao chanzo chake pia ni pesa za uharamia.Kuna mtandao mkubwa sana wa shughuli hii ambayo wafadhili wake wako kenya,dar es salaam na wengine dubai,na pesa hizo zimekua zikizunguka kwenye miji hiyo tajwa.
 
This is very serious and to my surprise, most of us are anaware of what is going on.
 
With all due respect kwa wana Tabora hivi mlimchagua Rage kwa sifa zipi za uongozi/utendaji alizokuwa nazo? Hivi Tabora hakuna viongozi wa maana wa kuwachagua mpaka mnamchagua Rage of all people?. Hivi ukweli kuwa alikuwa ametoka jela kwa msamaha wa rais muda mfupi kabla ya uchaguzi haukutosha kuwaonesha ni mtu wa aina gani? Watanzania taaaabu kwelikweli!!!.
 
Back
Top Bottom