Salaam kwa Ismail Aden Rage - Tabora Mjini; Jiandae... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salaam kwa Ismail Aden Rage - Tabora Mjini; Jiandae...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hossam, Dec 19, 2011.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa Kiongozi Wetu,

  Kwa masikitiko makubwa napenda kukutumia salaam za kukuamsha na kukutaka sasa uwatumikie wakazi wa Tabora Mjini kama ambavyo uliahidi katika kampeni zako mwaka 2010. Sasa hakuna mzaha tena...

  Mkoa wa Tabora umekuwa ni mkoa wa mwisho kabisa kimaendeleo japo kwa hakika ulitakiwa uongozwe na watu makini ili uwe kileleleni kabisa kwa kuwa kuna kila opportunity na resources za kufanya hilo, na sio kuongizwa na nyie wenye kupenda michezo zaidi kuliko kuugua kwa tabu za wananchi wenu. Wewe na viongozi wetu waheshimiwa waliopita mnaona kama Tabora sio yenu. Ni sawa nakubaliana na wewe, na hilo wazo lenu, Tabora sio yenu maana hata asili zenu zinaonyesha nyie sio wenyeji wa Tabora, lau hili ndio linawapa uvivu wa kuuendeleza mkoa huo maskini kabisa.

  Wewe toka umechaguliwa kuwa mbunge wa Tabora mjini umejikita zaidi kwenye michezo, basi potelea mbali ingekuwa hata michezo huko jimboni kwako, wewe umekazania Simba simba simba hata umesahau majukumu yako kama mbunge, na mimi sasa ni wajibu wangu na ni wajibu wa kila mwenye kufikiri sawasawa kukukumbusha ili usije sema hukuambiwa. Tabora imebakia hata timu ya mkoa ile ya Milambo ya daraja la kwanza sasa haziko vichwani mwenu nyie wapenda kucheza, sasa hivi kwako wewe mheshimiwa kipi ni bora, nyumba yako iteketee huku ukiiacha na kwenda kuokoa ya jirani, ama uokoe yako kwanza na kisha ya jirani yako? Jibu kiukweli bila unafki!

  Tuangalie elimu huko Tabora. Suala la elimu wewe kwako sasa ni kitendawili mheshimiwa, ni karibu tu na mjini kabisa huko kata ya Malolo, ama huko Ntalikwa, hebu tupa jicho kwa shule zetu za msingi na zahanati huko kiloleni. Hebu ona huruma kwa akina mama wa Ng'ambo wanavyohaha kugombania maji visimani, hivi wewe huoni usalama wa raia wako ulivyo rehani huko Chemchem, ama ndio sababu nasikia siku hizi unabeba na bastola kujilinda? Ona miundombinu ilivyo hovyo, halafu unaishia kupoteza muda na Simba, sasa nakuomba chagua moja kati ya Simba ama Siasa.

  Maana inafikia wakati sasa wapiga kura wako wanakutafuta wakueleze shida zao na hawakupati, wanashida na mbunge wao lakini wanaambulia patupu.

  Imefika wakati sasa uondoke, vuguvugu na wimbi la mabadiliko sasa linapiga hodi Tabora mjini na sisi tunao vijana wazuri tena wenyeji wa hukohuko wenye huzuni na hasira na umwinyi wenu wa kupenda ukubwa hali hamfanyi lolote kwa watu wenu. Hawa sasa tunawapika kuanzia sasa hadi mwaka 2015 ili tuone kati ya vijana wa mabadiliko na wazee wa umwinyi ni wepi hasa watakaoleta mabadiliko na maendeleo hapo Tabora mjini. Hili ni lazima liwe jambo ambalo wewe kama mteuliwa na sauti ya wananchi unatakiwa sasa kuanza kufikiri kama uache wewe mwenyewe kwa hiari yako ama uache baada ya kupoteza mapesa mengi muda na aibu tupu.


  Ni sawa kwamba Tabora mjini haijawahi kupata wagombea vijana makini zaidi ya Mr Zambia kwa kipindi chote, lakini sana haijapata mgombea mwenye ushawishi kwa vijana kwa kipindi hicho na mwisho wagombea hao wamekuwa hawana uwezo kifedha na hivyo kazi ya kuyafikia maeneo yote ya jimbo inakuwa ngumu. Sasa tunaanza rasmi mwaka ujao, tutaeleza uozo wako kwa wapiga kura wako na tutaandaa vijana wetu kwa mabadiliko na maendeleo yao kupitia jukwaa la siasa. Tutawaonyesha wana Tabora matumaini yaliyopotea na tutaimba wimbo wa mabadiliko hadi wewe na vibaraka wako muusikie na mfungashe vilivyokuwa vyenu.


  Haingii akilini kabisa wakazi wa Cheyo kukosa kituo cha polisi kwa kipindi chote, hakuna mtu anayekuelewa kama soko la pale National, kule Tambukareli, na Rufita, na hata Ipuli, yanavyosuasua na sasa ushuru wa manispaa unalegalega bila mpangilio na wewe upo na unatazama haya bila kusema lolote. Haileti picha njema kuona wafanya biashara wadogowadogo wamachinga ukishindwa kuwatafutia eneo maalum, wewe kazi simba tu simba tu, hivi nikuulize hili, hao Simba ndio walikutuma uwe mbunge wa Tabora mjini mheshimiwa?

  Huko Kwihara, pale Kipalapala, pale si ndio yule Mzungu, Dr Livingstone aliacha Tembe lake ambalo ni eneo zuri sana la utalii mkoani Tabora? Pale ndio nyumba ya Chief Abdallah Fundikira aliacha nyumba yake, na pana jiwe kubwa, jabali, mahali ambapo wachawi walikuwa wanauawa? Wewe huoni kama hiyo ni sawa na utalii? Basi wewe labda sema vipaumbele vyako ni vipi hasa mheshimiwa! Maana hatukuelewi kabisa.


  Hebu ona wananchi wa Mbungani wanavyohaha na magonjwa ya kuhara kwa sababu mitaro ni hadi milangoni kwao, wewe uko na hamsini zako tu, ama hawakuambii? Hata polisi sasa wanaishi kwenye vibanda vya chuma kama wakimbizi wewe kwako heko tu, labda kwa sababu wanawashikaga wakati wa kampeni.

  Tabora mjini sasa ni lazima iwe zaidi ya Wilaya ya Nzega, ni lazima sasa ufike wakati, wanatabora waone kweli mbunge wao na nchi yao inawatendea haki na wote kwa pamoja wanafaidi matunda ya uhuru wao. Kama hayo huyawezi, basi sie akina PANGU PAKAVU TIA MCHUZI, tuko nyuma yako unyayo baada ya mwingine kuhakikisha unaondoka haraka kwenye umwinyi na kuacha ya Tabora kwa wana Tabora.

  Hizi na ziwe salaam zako za Krismas na Mwaka Mpya.

  Ni Mimi Pangu Pakavu,
  Nakusalimia.
   
 2. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Muamshe kaka, hawa bila kuamshwa wanalewa na usingizi. muamshe
   
 3. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Mnaongozwa na Kilaza!
   
 4. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Angalia asije toka na bastola huyo,huyu kama askari wa al-sha- okoslok kipermekunjugere.

  Ni mwenyekiti wa chama cha cimba na katibu wa kile chama cha watu kule wapi vile!! nimesahau sorry.tetee
   
 5. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanalewa usingizi na posho mlima!
   
 6. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  hahaha kaka huyo kamanda wa al....u utamuweza? mwenzio anatembea na bunduki
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni vema umeujuza ulimwengu hayo yanayotokea huko tabora. lakini kama unaweza, siku moja nenda kwenye mkutano wake wa hadhara umweleze moja kwa moja
   
 8. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa hilo jimbo ni term moja tu kwa siku hizi. Kama akishinda next term atakuwa wa kwanza.
  Bora umemstua umwinyi na koo ndio tatizo pia viking'olewa tabora itasonga. Kufa kwa railway ndio kumeua tabora kabisa
   
 9. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Yuko busy anawasaidia ndugu zake wa Al shaabab
   
 10. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nyie si mnachagua viongozi posho sasa,kilaza kama rage hana hata vision !
   
 11. I

  Ismaily JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyie simmeamua kuichagu CCM na kupenda kupewa kanga,kofia,chupi za CCM na sh,2000,2000,sasa hayo ndiyo matatizo yake,mtaendelea kuwa maskini wa maisha na hatari zaidi nyie na maskini wa fikra! Endeleani na upumbavu wenu wa kuichagua CCM.
   
 12. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  simba yenyewe imemshinda kila siku anafungwa na yanga,
   
 13. MBURE JASHA

  MBURE JASHA JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tuseme unatangaza nia au! tuelewashane vizuri Kiongozi! by the way hayo ndio majitu(mazimwi) ya CCM. yanaangalia "kibubu" kipo levo gani . Uchaguzi kwao ni kuhonga tu ndo maana hayajali
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  lakini hii pia inaonyesha kuna haja ya kuwa na sheria ambayo itawapa nguvu wapiga kura kuwawajibisha wabunge wao pale wanapoona kuwa hawatendi vile wanavyopaswa kuitenda katika kutekeleza majukumu yao
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,655
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Na nyie kwa nini mlichagua kuongozwa na gaidi la kisomali?Nyie watani zangu mnachekesha sana mara muongozwe na muajemi mara msomali kwa nini lakini?
   
 16. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jitambueni, jitoeni mikononi mwa wapenda madaraka kuliko kupenda kuwatumikia wananchi
   
 17. l

  luckman JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  pangu pakavu, ah ha ha haaaaaaaaa, sio hossam???haya bwana nadhani kasikia, yupo pale kkoo round about!
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Muda si mrefu Rufita Street itakuwa hivi

  [​IMG]
   
 19. m

  mpiganaji86 Senior Member

  #19
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nina ushahidi aden rage alikuwa ni mmoja wa wanamgambo wa al shabaab na alitoroka kwenye bandari ya lamu kismayu akakimbilia tz akiwa amedandia lori
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Ismaili-jamii ya waislamu
  Aden-Bandari ya Yemen
  Rage-Hasira
   
Loading...