Salaam kutoka Ngara kwa Waziri wa Nishati

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
718
703
Ndugu waziri nakuletea salaam zangu kutoka nakatunga wilaya ya Ngara, ambazo kwa hakika zimebeba mtazamo wa wilaya yote.

Ndugu waziri, wanaomkumbuka Kalemani hadharani na moyoni sio kwamba wachuki na wewe, bali wanaangalia utendaji wako ukilinganisha na kalemani.
Hapa Rusumo kuna mradi wa ujenzi wa umeme kutokana na maporomoko ya maji kutoka nchi tatu, Tanzania, Burundi na Rwanda.

Kalemani alikuwa akifanya ziara za mara kwa mara, kukagua maendeleo ya mradi huu wa kuzalisha megawati 90. Ndugu waziri, tangu umechukua nafasi hiyo hujafika kukagua na hatuna taarifa utakamilika lini, ibgawa kwa kalemani tuliambiwa utakamilka April hii.

Ndugu waziri, hapa Ngara umeme ni anasa! Hauwaki siku mbili bila taarifa na ukipatikana huwezi kutumia mashine ya kunyoa nywele. Umeme mdogo.

Ndugu waziri, matokeo yake huduma za msingi hakuna nawe upo ofisini, mbaya zaidi hatuelezwi tatizo ni nini na litaisha lini, ingawa za chini chini tunaambiwa kuna nguzo imeanguka wilsyani biharamulo.

Ndugu waziri, sababu hii inayoungwa mkono na tanesco wilaya haiingii akilini. Nguzo ianguke tatizo lidumu zaidi ya miezi miwili?

Ndugu waziri juzi umeme ulikatwa saa 10 jioni , hakuna taarifa. Msemajj wa Tanesco mkoa hapokei simu, namba ya meneja ni sawa na nyara za serikali, nikamtafuta Naibu waziri kwa namba..., hapokei, nikatuma sms hakuna majibu hata sasa!

Ndugu waziri, nimesema huduma zimekosa sitanii, mashine za kusukuma maji hazifanyi kazi, pale hospitali ya rulenge ambayo ndio pekee wilaya hii yenye huduma za x-ray, huduma haziwezi kufanyika na hali ilikuwa mbaya zaidi siku nne nyuma pale mafuta yalipofichwa.

Ndugu waziri, nisikuchoshe kwa ujumbe mrefu lakini toka ofisini, njoo huku kwetu kama alivyofanya mtangulizi wako, kuiga kitu kizuri sio ujinga.

Wasalaam.
 
Huku kibaha umeme umekata anzia saa saba usiku hadi dakika hii.

Tena inasemekana mama anakuja huku leo.

Tubebe bango la maji au umeme au bidhaa kupanda.

Hii nchi huko juu ni kama wameamua kutukomoa

Magu though uliniumiza ila nimekumisi.
 
Kwahiyo unahisi Kalemani alikuwa Waziri kutoka chama gani na Makamba anatoka wapi?
Itikadi zao ni tofauti? Yani unajisumbua tu pale kila mtu anapata ulaji kwa muda wake
 
Huku kibaha umeme umekata anzia saa saba usiku hadi dakika hii.

Tena inasemekana mama anakuja huku leo.

Tubebe bango la maji au umeme au bidhaa kupanda.

Hii nchi huko juu ni kama wameamua kutukomoa

Magu though uliniumiza ila nimekumisi.
walioko juu wanatutazama sisi wengine kama wanaoweza kutufanyia chochote na hatuwezi kubadili hali iliyopo. Swali ni je, Hatuwezi kubadili hii hali?
 
Wewe kwa akili yako kabisa unadhani kuna waziri pale..hao genge zima liliorudi limerudi kwaajili ya upigaji sio kwaajili ya mtanganyika.

Wamekuja kuweka madili ya kupiga pesa ndio mana hawahangaiki na vitu visivyo na maslahi kwao.

#MaendeleoHayanaChama
 
kwa nini Tanesco hawawashi hayo magenerator ya hapo nakatunga kwenu au yalishakufa

Huko kwenu mafuta yalifichwa na nani mkuu wakati sheli zinamilikiwa na mtu mmoja(meddy)

by the way msalimie tajiri Asa mwenye ligodown la cement hapo Nakatunga

halafu yule mbunge wenu kijana wa tajiri wa kahawa katerere si nasikia ni msomi sana anashindwaje kutatua tatizo la nguzo moja kuanguka au ndio anataka 2025 mumreplace na aliekuwepo(kashaza) ama jambaz mstaafu Sama
 
Mkuu, Jeneretor hizo zilipelekwa bila shaka nyumbani kwao makamu, huku kwa sababu hatuna mjomba tumeachwa hivyo hivyo.
 
Hawa jamaa Mungu anawaona, wakatulaghai tukaachana na "Solar" zetu sasa wanakuja kutupiga upya na Majenereta.
Tanesco walisema wamehitimisha maboresho tarehe 10/02/2022 kama ilivyotangazwa na Waziri Makamba, lakini tarehe 27/03 tukaambiwa kwamba umeme utaendelea kupatikana kwa shida mpaka matengenezo na maboresho mbali mbali yatakapoisha, Sema jamaa alikuwa anatafuta shida ya umeme kwa ulazima, alianza maji kupungua, mara kufanya maboresho...kuna kitu anakaitafuta


 
Huku kibaha umeme umekata anzia saa saba usiku hadi dakika hii.

Tena inasemekana mama anakuja huku leo.

Tubebe bango la maji au umeme au bidhaa kupanda.

Hii nchi huko juu ni kama wameamua kutukomoa

Magu though uliniumiza ila nimekumisi.
Maushungi ameniweka pale junction ya Mbezi masaa 2½ kisa anapita kumbe ilikuwa safari ya Kibaha.
 
Hapo kwenye "shell" mtu mmoja ana miliki biashara ya mafuta na taarifa za sasa hivi mafuta hasa Petrol hakuna, maeneo kama Mugoma Leo hii asubuhi wachuuzi yanayuzwa lita moja Tsh 3,500.
 
Hapo kwenye "shell" mtu mmoja ana miliki biashara ya mafuta na taarifa za sasa hivi mafuta hasa Petrol hakuna, maeneo kama Mugoma Leo hii asubuhi wachuuzi yanayuzwa lita moja Tsh 3,500.
vipi Burundi bei sh ngapi mkuu halafu nauli ya kutoka ngara mjini mpaka Rulenge ni ngapi sasa hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…