HATIMAE "BAVICHA" WAMEFANIKIWA KWA HATUA YA KWANZA.
Nikiwa huku mafichoni kusiko julikana na viongozi wenzangu wakiwa gerezani kwa kosa lakuipigania haki na demokrasia huru ya nchi hii nimepata faraja kubwa kuona kwa hatua za awali Polisi na Serikali wamenyanyua mikono na kuruhusu mikutano ya ndani.
Ni jambo jema kwetu kwakuwa tulijitoa kwa hali na mali kuhakikisha tunafanikiwa kwa kile tunacho kiamini kwa maslahi ya chama chetu na Baraza letu.
Viongozi wenu tupo salama huku tulipo,na hatuna hofu kwakuwa tumejitoa kulipigania taifa letu dhidi ya mfumo kandamizi wa Demokrasia na utawala bora.
M/kiti na Katibu mkuu wanawasalimia sana,na wameomba msirudi nyuma kupaza sauti zenu kuililia demokrasia inayonyongwa na watawala kila kukicha.
M/kiti BAVICHA Taifa, George Tito wao wamehamishiwa gereza la Chamwino na Katibu mkuu amebaki Dodoma mjini,tunafikiri kesho lazima itakuwa ni Mahakamani hivyo nawaomba Viongozi na wanachama wote mfike Mahakamani kwaajili ya kuwapa moyo viongozi wetu.
Imetolewa July 10
Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa