Salaam kutoka Gerezani Dodoma: BAVICHA yatangaza ushindi

safi sana bavicha...mmecheza propaganda nzuri sana...good...tumeona Matunda..ila bado
Ushindi gani? Kwani mlizuiwa kuingia ofisini? Au kulipana mishahara? Kazi za kila siku rukhsa siku zote. Kilichokataliwa ni naadamano na mikutani kumtukana Rais au Dr Tulia au Bajeti - hayo ni ya bungeni.
 
Hiyo siku ya tarehe 23 bavicha watajuta kwenda Dodoma kwani POLISI hawahitaji msaada wa vyama kufanya kazi zao
 
Ni lini polisi ilikataza mikutano hiyo ya ndani ya kisiasa?

Yaani mlijitengenezea sanamu ya polisi halafu mkaanza kupambana nayo halafu mnataka mjisifu??

Aliyepotosha tangazo la polisi na Magufuli ni ninyi wenyewe...jana limefafanuliwa mnakuja kujidai washindi haha ha kweli hii ndio bavicha uchwara ....Tarehe 23 mngevunjika miguu haswa....sasa wapeni nauli wale waliojiandikisha kuja kusaidiana na polisi warudi makwao ...halafu sijui makamanda mtamsikiliza nani kati ya lowassa au Mbowe katika aina ya siasa mnazotaka kuzifanya.
Ya CHASO ilikuwa ni kuzuia bendera au sio?.Acha hizo bana usijitoe ufahamu ukweli haki na demokrasia ndo misingi ya siasa safi mambo ya vijipropaganda uchwara na usanii ulaghai hayatatufikisha popote.
 
HATIMAE "BAVICHA" WAMEFANIKIWA KWA HATUA YA KWANZA.

Nikiwa huku mafichoni kusiko julikana na viongozi wenzangu wakiwa gerezani kwa kosa lakuipigania haki na demokrasia huru ya nchi hii nimepata faraja kubwa kuona kwa hatua za awali Polisi na Serikali wamenyanyua mikono na kuruhusu mikutano ya ndani.

Ni jambo jema kwetu kwakuwa tulijitoa kwa hali na mali kuhakikisha tunafanikiwa kwa kile tunacho kiamini kwa maslahi ya chama chetu na Baraza letu.

Viongozi wenu tupo salama huku tulipo,na hatuna hofu kwakuwa tumejitoa kulipigania taifa letu dhidi ya mfumo kandamizi wa Demokrasia na utawala bora.

M/kiti na Katibu mkuu wanawasalimia sana,na wameomba msirudi nyuma kupaza sauti zenu kuililia demokrasia inayonyongwa na watawala kila kukicha.

M/kiti BAVICHA Taifa, George Tito wao wamehamishiwa gereza la Chamwino na Katibu mkuu amebaki Dodoma mjini,tunafikiri kesho lazima itakuwa ni Mahakamani hivyo nawaomba Viongozi na wanachama wote mfike Mahakamani kwaajili ya kuwapa moyo viongozi wetu.

Imetolewa July 10

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa

Sijui unachoshangilia maana mikutano ya ndani ilikuwa inaendelea Kama kawaida ndio maana lowassa yuko Arusha Na mameya Na wenyeviti WA halamashauri za chadema. Punguza ushabiki basi khaaa!!
 
Ya CHASO ilikuwa ni kuzuia bendera au sio?.Acha hizo bana usijitoe ufahamu ukweli haki na demokrasia ndo misingi ya siasa safi mambo ya vijipropaganda uchwara na usanii ulaghai hayatatufikisha popote.
Usikirupuke kupost kabla ya kusoma thread yote.....
 
eti kupigania democrasia!!!!! hahahaaaaa!!!ndani ya chama chenu democrasia haipo!!! ukimpinga Mwenyekiti unaitwa msaliti!! unajiunga chama Leo kesho mgombea urais!!!! tafuteni democrasia ndani ya chama chenu kwanza!! unamtoaji boriti wakati ndani ya jicho lako kuna kibanzi!!?????
 
Safi sana BAVICHA hakuna kurudi nyuma daima hayo manyanyaso yana mwisho hakuna haki inayopatikana bila kupigania.Muda wa ukombozi umeshakaribia

TIME WILL TELL.
 
Mbona
eti kupigania democrasia!!!!! hahahaaaaa!!!ndani ya chama chenu democrasia haipo!!! ukimpinga Mwenyekiti unaitwa msaliti!! unajiunga chama Leo kesho mgombea urais!!!! tafuteni democrasia ndani ya chama chenu kwanza!! unamtoaji boriti wakati ndani ya jicho lako kuna kibanzi!!?????
Mbona unaweweseka sana kaanzisha mada kuhusu hilo tutakukujibu turudi kwenye mada
 
Wewe hujitambui kabisa ndo umeandika nini?
Akili zenu mbovu tu. Wote wenye akili walijua mikutano ya ndani ruksa na mikutano ya mbunge au diwani na wananchi wake ruksa. Huenda wahusika wanawenza wao magereza
 
Usikirupuke kupost kabla ya kusoma thread yote.....
Ulichotaka nisome ni kipi kwamba polisi walizuia maandamano na mikutano ya wazi tu au?Na unachotaka nikuelewe ni kipi kwamba chadema kuna mgogoro wa kimisimamo kati ya lowassa na mbowe au?:(
 
Acha tabia za umbea na unafiki huo mkutano ulifanyika uwanja gani?
Ukweli ni kuwa hata hao BAVICHA walilielewa vizuri sana katizo la Polisi na hata la Rais Magufuli. Hata CHADEMA kwa ujumla wao walielewa vizuri sana ila kwa lengo la kutafuta kick wakaanza kupoteza umma kwa makusudi. Juzi hata kabla hao polisi hawajatoa ufafanuzi kule Arusha ulifanyika mkutano mkutano wa CHADEMA ukiwahusu viongozi wa halmashauri zinazoongozwa na chama chao. Mh Lowassa na katibu mkuu wa CHADEMA walihudhuria na walikuwa wawezeshaji katika huo mkutanao Eaulizeni CHADEMA na BAVICHA kama kulikuwa na katazo kama wanavyotaka kuwaaminisha Watanzania, ilikuwaje wao wakaandaa huo mkutano? Na mbona polisi hawakuwakataza kama walikuwa wamezuia kila aina ya mkutano wa vyama vya siasa?
 
Back
Top Bottom