Sakata ya ugaidi dhidi ya CHADEMA: Shibuda, Sofia Simba watajwa

Indume Yene

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
2,968
Reaction score
727
Katika ile sakata ya kesi ya ugadi dhidi ya makada wa CHADEMA iliyofutwa hivi karibuni mkoani Tabora, mbunge wa CHADEMA Maswa Magharibi atajwa hadharani. Kwa habari kamili soma hapa chini.

Mapya yaibuka

• Makachero wahaha kuwaingiza Dk. Slaa, Mbowe matatani, wakwama

Na Mwandishi wetu

IMEBAINIKA kuwa baadhi ya maofisa wa polisi na makachero wao wamekuwa wanatumia vibaya majina ya viongozi wakuu wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama kisingizio cha kupika kesi za ugaidi dhidi ya viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika tukio la hivi karibuni, makada wa CHADEMA waliokuwa rumande wakikabiliwa na mashitaka ya ugaidi, ambayo hatimaye yalifutwa na mahakama, wametoboa siri kuwa miongoni mwa majina yaliyotumiwa na baadhi ya polisi na makachero waliowatesa ni ya Rais Jakaya Kikwete; na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wiki hii, makada hao - Evodius Justinian, Oscar Kaijage, Rajabu Kihawa, Seif Magesa na Henry Kileo, wamesema pia kuwa njama hizo za polisi na makachero wao, zililenga kuwalazimisha vijana hao wawahusishe viongozi wakuu wa CHADEMA (hasa Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa) na ugaidi na utesaji watu ambao umekuwa unaendelea.

Wengine ambao polisi walitaka watajwe ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.

Hata hivyo, vijana hao wanasema waligoma kuwahusisha, hata baada ya kuteswa kikatili.

Makada hao wanadai kwamba mateso waliyopata yaliratibiwa na viongozi wa Jeshi la Polisi, Advocate Nyombi na afande Pasua.

Mmoja wa makada hao, Kihawa, aliyekamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Dodoma, anadai kuwa alipokuwa anahojiwa, alilazimishwa aseme kuwa viongozi wa CHADEMA ndio wanahusika na utekaji na tindikali.

Akiendelea kusimulia mkasa huo, Kihawa alisema kuwa baada ya kauli hiyo, aliingizwa katika chumba namba 114, ghorofa ya pili, chenye kamera nyingi katika moja ya hoteli maarufu Mjini Dodoma (jina tunalihifadhi kwa sasa) akavuliwa nguo zote, akakalishwa kwenye chupa ya soda kisha akapigwa sana.

"Nilipoteza fahamu lakini nilipozinduka nilikuta nimevalishwa nguo, na nimekalishwa kwenye kiti na kuwekewa chakula karibu," anasema, na kuongeza kuwa hakula chakula hicho, lakini alipotoka nje ya chumba hicho, kwenye ukumbi wa hoteli, aliwakuta vijana waliofukuzwa CHADEMA, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba na Habib Mchange wakinywa na kula.

"Walinikejeli sana, wakasema wanashangilia ushindi," alisema.

Kutoka pale nilichukuliwa na Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, akaniingiza chumbani akadai anampigia simu Waziri Simba, akamwambia, "mama, huyu kijana ninaye hapa. Ungeongea naye ili akubali kulegeza msimamo, au umpigie mwanao Jakaya anipigie, pengine atabadili msimamo wake kama tulivyokuwa tumekubaliana awali."

Kihawa anadai kuwa mtu huyo aliyedaiwa kuwa Waziri Simba alimjibu Shibuda kuwa asingeweza kuzungumza yeye kwa kuwa alikuwa hajisikii vema, ila kwa suala la kuongea na Rais Kikwete, atafutwe Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana au Naibu Katibu Mkuu Bara, Mwigulu Nchemba, ili awaunganishe Shibuda na rais.

Kwa mujibu wa Kihawa, baada ya kupewa ushauri huo, Shibuda alijibu: "Mwigulu ni mropokaji, hawezi kuingizwa katika mkakati huu; na Kinana ni mgumu kuingilika katika suala hili."

Anasema alisikia mazungumzo yao kwenye loud speaker ya simu ya Shibuda, na baada ya kukata simu Shibuda alimwambia kuwa alikuwa anazungumza na Simba, ambaye alidai ni ‘mama mdogo wa Kikwete.'

Kihawa anasema wakati anahojiwa hayo hapo hotelini, maofisa wa polisi walisimama kwa mbali wakimsubiri.

Wengine waliokuwapo wakishuhudia mahojiano hayo ni Meya wa Ilemela, Henry Matata na aliyekuwa Diwani wa Igoma, Adam Chagulani. Matata na Chagulani walishavuliwa uanachama na CHADEMA.

Wahusika walipohojiwa na Tanzania Daima jana, kila mmoja alikuwa na kauli yake kama ifuatavyo:

Tanzania Daima Jumapili: Afande Nyombi, vijana waliokuwa wametuhumiwa kwa kesi ya ugaidi kule Tabora, wamekutaja wewe kuwa ulishiriki kuwatesa ukiwalazimisha wawataje viongozi wakuu wa CHADEMA kuwa walishiriki kutenda ugaidi na utekaji. Unatoa ufafanuzi gani?

Advocate Nyombi: Mimi si msemaji wa Jeshi la Polisi, siwezi kusema chochote.

Tanzania Daima Jumapili: Msemaji atajuaje kama mliwatesa watu wakati wa mahojiano? Mbona huku ni kumwonea msemaji wa Jeshi la Polisi kusemea kila kitu hata mambo ambayo askari fulani ametenda kwa utashi wake?

Advocate Nyombi: Nimekwambia mtafute, msemaji katika hayo yote. Mimi siwezi kuongelea suala hilo, nakutakia Idd Mubaraka njema.

Tanzania Daima Jumapili: Afande Pasua, vijana waliotuhumiwa katika kesi ya ugaidi kule Tabora wamekutaja wewe kuwa ulishiriki kuwatesa, ukiwalazimisha wataje viongozi wa CHADEMA kuwa walishiriki kutenda ugaidi na utekaji. Unatoa ufafanuzi gani?

Afande Pasua: Kwani wewe uko wapi?

Tanzania Daima Jumapili: Nipo Dar es Salaam, hapa ofisini.

Afande Pasua: Njoo ofisini tuongee tuyaweke sawa unayouliza. Umesema unatoka gazeti gani?

Tanzania Daima Jumapili: Nimekwambia Tanzania Daima.

Afande Pasua: Mashtaka hayo kwanza yalikuwa ya serikali, mimi sifanyi kazi ya kubahatisha, mpigie msemaji wa Jeshi la Polisi mimi si msemaji. Alikata simu.

Henry Matata

Tanzania Daima Jumapili: Mstahiki Meya, vijana waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wanadai walihojiwa mbele yako Dodoma. Je, unafahamu nini kuhusu suala hili?

Matata: Kijana Rajab Kihawa ndio namfahamu. Huyu alikuwa mfanyakazi wangu, ila tangu aache kufanya kazi hapa sijaonana naye. Lakini mimi nina ugomvi na wafanyakazi wote wa gazeti lenu na gazeti lenu. Nisingependa kuongea na nyie. Tangu nifukuzwe CHADEMA gazeti lenu linaongeza chumvi habari zinazonihusu. Mimi si meya kwa kura za CHADEMA. CHADEMA walinifukuza, CCM wakaona nafaa, wakanipa kura nikawa meya.

Tanzania Daima Jumapili: Ulikutana na Rajab Dodoma hotelini?

Matata: Nimekwambia sitaki kuongea na gazeti lenu.

bi Mheshimiwa, vijana waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wamekutaja kuwa ulikuwepo wakati wanahojiwa Dodoma. Je, una kauli gani kwa yao hii?

Chagulani: Mimi nilikuwa Dodoma mwezi wa nne lakini nilikuwa Kondoa kwa ajili ya uhamisho wa mke wangu. Hayo unayonieleza siyajui.

Waziri Simba hakupokea simu, na alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu hakujibu lolote.

Msemaji wa jeshi la Polisi, Advera Senso, alipoulizwa kama jeshi ndilo linawatuma polisi kutesa watu wakati linawahoji, alisema: "Mhalifu asitafute huruma ya jamii kwa kuzushia jeshi kwa uhalifu alioutenda yeye, na endapo ikibainika anasingizia uongo na hilo ni kosa pia, kwani Jeshi la Polisi linafuata taratibu za sheria."

Shibuda alipoulizwa jinsi alivyohusika katika sakata hilo alisema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza chochote kwa kuwa alikuwa Agha Khan Hospitali akihangaikia mgonjwa wake.

"Niacheni kwa sasa kwa kuwa nahitaji utulivu wa akili niweze kushughulikia afya ya mgonjwa wangu. Nadhani hata kama ni wewe sijui katika mazingira kama haya ungeweza kweli kuongea?" alisema.

Msemaji wa Ikulu, Salva Rweyemamu, alipopigiwa simu kuulizwa ikiwa wanayo taarifa ya watu wanaotumia vibaya jina la rais katika matukio ya kihalifu aliomba jambo lolote linalohusiana na kazi, lisubiri kwa kuwa alikuwa katika mapumziko ya sikukuu.

"Ndugu yangu, unajua leo ni sikukuu na ni usiku, nitafute wakati mwingine, maana siwezi kuzungumzia mambo ya watu wa CHADEMA muda huu. Niache nipumzike kidogo halafu tuwasiliane siku ya kazi," alisema.

Source: Tanzania Daima
 
asante kwa taarifa , tumewafahamu wahusika wote , CC KICHEERE NYARONYO .
 
kwakweli tunaelekea kubaya,hizi kesi za ugaidi zimeiacha uchi serikali na baadhi ya polis ni sawa tu na mashetani.
 
Hivi huyu afande pasua ana cheo gani ndani ya police force? Au ndie wale watesaji wanaotegemewa na jeshi hili?
 
Kwa kweli sasa ccm inabidi ipumzishwe
nimeshtushwa sana na hii habari na imani yangu imekwisha
sasa nitamwamini nani katika nchi yangu
Nimepatwa na butwaa
 
Mapya yaibuka
• Makachero wahaha kuwaingiza Dk. Slaa, Mbowe matatani, wakwama

na Mwandishi wetu
IMEBAINIKA kuwa baadhi ya maofisa wa polisi na makachero wao wamekuwa wanatumia vibaya majina ya viongozi wakuu wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama kisingizio cha kupika kesi za ugaidi dhidi ya viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Katika tukio la hivi karibuni, makada wa CHADEMA waliokuwa rumande wakikabiliwa na mashitaka ya ugaidi, ambayo hatimaye yalifutwa na mahakama, wametoboa siri kuwa miongoni mwa majina yaliyotumiwa na baadhi ya polisi na makachero waliowatesa ni ya Rais Jakaya Kikwete; na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wiki hii, makada hao - Evodius Justinian, Oscar Kaijage, Rajabu Kihawa, Seif Magesa na Henry Kileo, wamesema pia kuwa njama hizo za polisi na makachero wao, zililenga kuwalazimisha vijana hao wawahusishe viongozi wakuu wa CHADEMA (hasa Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa) na ugaidi na utesaji watu ambao umekuwa unaendelea.
Wengine ambao polisi walitaka watajwe ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Hata hivyo, vijana hao wanasema waligoma kuwahusisha, hata baada ya kuteswa kikatili.
Makada hao wanadai kwamba mateso waliyopata yaliratibiwa na viongozi wa Jeshi la Polisi, Advocate Nyombi na afande Pasua.
Mmoja wa makada hao, Kihawa, aliyekamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Dodoma, anadai kuwa alipokuwa anahojiwa, alilazimishwa aseme kuwa viongozi wa CHADEMA ndio wanahusika na utekaji na tindikali.
Akiendelea kusimulia mkasa huo, Kihawa alisema kuwa baada ya kauli hiyo, aliingizwa katika chumba namba 114, ghorofa ya pili, chenye kamera nyingi katika moja ya hoteli maarufu Mjini Dodoma (jina tunalihifadhi kwa sasa) akavuliwa nguo zote, akakalishwa kwenye chupa ya soda kisha akapigwa sana.
"Nilipoteza fahamu lakini nilipozinduka nilikuta nimevalishwa nguo, na nimekalishwa kwenye kiti na kuwekewa chakula karibu," anasema, na kuongeza kuwa hakula chakula hicho, lakini alipotoka nje ya chumba hicho, kwenye ukumbi wa hoteli, aliwakuta vijana waliofukuzwa CHADEMA, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba na Habib Mchange wakinywa na kula.
"Walinikejeli sana, wakasema wanashangilia ushindi," alisema.
Kutoka pale nilichukuliwa na Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, akaniingiza chumbani akadai anampigia simu Waziri Simba, akamwambia, "mama, huyu kijana ninaye hapa. Ungeongea naye ili akubali kulegeza msimamo, au umpigie mwanao Jakaya anipigie, pengine atabadili msimamo wake kama tulivyokuwa tumekubaliana awali."
Kihawa anadai kuwa mtu huyo aliyedaiwa kuwa Waziri Simba alimjibu Shibuda kuwa asingeweza kuzungumza yeye kwa kuwa alikuwa hajisikii vema, ila kwa suala la kuongea na Rais Kikwete, atafutwe Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana au Naibu Katibu Mkuu Bara, Mwigulu Nchemba, ili awaunganishe Shibuda na rais.
Kwa mujibu wa Kihawa, baada ya kupewa ushauri huo, Shibuda alijibu: "Mwigulu ni mropokaji, hawezi kuingizwa katika mkakati huu; na Kinana ni mgumu kuingilika katika suala hili."
Anasema alisikia mazungumzo yao kwenye loud speaker ya simu ya Shibuda, na baada ya kukata simu Shibuda alimwambia kuwa alikuwa anazungumza na Simba, ambaye alidai ni ‘mama mdogo wa Kikwete.'
Kihawa anasema wakati anahojiwa hayo hapo hotelini, maofisa wa polisi walisimama kwa mbali wakimsubiri.
Wengine waliokuwapo wakishuhudia mahojiano hayo ni Meya wa Ilemela, Henry Matata na aliyekuwa Diwani wa Igoma, Adam Chagulani. Matata na Chagulani walishavuliwa uanachama na CHADEMA.
Wahusika walipohojiwa na Tanzania Daima jana, kila mmoja alikuwa na kauli yake kama ifuatavyo:
Tanzania Daima Jumapili: Afande Nyombi, vijana waliokuwa wametuhumiwa kwa kesi ya ugaidi kule Tabora, wamekutaja wewe kuwa ulishiriki kuwatesa ukiwalazimisha wawataje viongozi wakuu wa CHADEMA kuwa walishiriki kutenda ugaidi na utekaji. Unatoa ufafanuzi gani?
Advocate Nyombi: Mimi si msemaji wa Jeshi la Polisi, siwezi kusema chochote.
Tanzania Daima Jumapili: Msemaji atajuaje kama mliwatesa watu wakati wa mahojiano? Mbona huku ni kumwonea msemaji wa Jeshi la Polisi kusemea kila kitu hata mambo ambayo askari fulani ametenda kwa utashi wake?
Advocate Nyombi: Nimekwambia mtafute, msemaji katika hayo yote. Mimi siwezi kuongelea suala hilo, nakutakia Idd Mubaraka njema.
Tanzania Daima Jumapili: Afande Pasua, vijana waliotuhumiwa katika kesi ya ugaidi kule Tabora wamekutaja wewe kuwa ulishiriki kuwatesa, ukiwalazimisha wataje viongozi wa CHADEMA kuwa walishiriki kutenda ugaidi na utekaji. Unatoa ufafanuzi gani?
Afande Pasua: Kwani wewe uko wapi?
Tanzania Daima Jumapili: Nipo Dar es Salaam, hapa ofisini.
Afande Pasua: Njoo ofisini tuongee tuyaweke sawa unayouliza. Umesema unatoka gazeti gani?
Tanzania Daima Jumapili: Nimekwambia Tanzania Daima.
Afande Pasua: Mashtaka hayo kwanza yalikuwa ya serikali, mimi sifanyi kazi ya kubahatisha, mpigie msemaji wa Jeshi la Polisi mimi si msemaji. Alikata simu.
Henry Matata
Tanzania Daima Jumapili: Mstahiki Meya, vijana waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wanadai walihojiwa mbele yako Dodoma. Je, unafahamu nini kuhusu suala hili?
Matata: Kijana Rajab Kihawa ndio namfahamu. Huyu alikuwa mfanyakazi wangu, ila tangu aache kufanya kazi hapa sijaonana naye. Lakini mimi nina ugomvi na wafanyakazi wote wa gazeti lenu na gazeti lenu. Nisingependa kuongea na nyie. Tangu nifukuzwe CHADEMA gazeti lenu linaongeza chumvi habari zinazonihusu. Mimi si meya kwa kura za CHADEMA. CHADEMA walinifukuza, CCM wakaona nafaa, wakanipa kura nikawa meya.
Tanzania Daima Jumapili: Ulikutana na Rajab Dodoma hotelini?
Matata: Nimekwambia sitaki kuongea na gazeti lenu.
bi Mheshimiwa, vijana waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wamekutaja kuwa ulikuwepo wakati wanahojiwa Dodoma. Je, una kauli gani kwa yao hii?
Chagulani: Mimi nilikuwa Dodoma mwezi wa nne lakini nilikuwa Kondoa kwa ajili ya uhamisho wa mke wangu. Hayo unayonieleza siyajui.
Waziri Simba hakupokea simu, na alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu hakujibu lolote.
Msemaji wa jeshi la Polisi, Advera Senso, alipoulizwa kama jeshi ndilo linawatuma polisi kutesa watu wakati linawahoji, alisema: "Mhalifu asitafute huruma ya jamii kwa kuzushia jeshi kwa uhalifu alioutenda yeye, na endapo ikibainika anasingizia uongo na hilo ni kosa pia, kwani Jeshi la Polisi linafuata taratibu za sheria."
Shibuda alipoulizwa jinsi alivyohusika katika sakata hilo alisema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza chochote kwa kuwa alikuwa Agha Khan Hospitali akihangaikia mgonjwa wake.
"Niacheni kwa sasa kwa kuwa nahitaji utulivu wa akili niweze kushughulikia afya ya mgonjwa wangu. Nadhani hata kama ni wewe sijui katika mazingira kama haya ungeweza kweli kuongea?" alisema.
Msemaji wa Ikulu, Salva Rweyemamu, alipopigiwa simu kuulizwa ikiwa wanayo taarifa ya watu wanaotumia vibaya jina la rais katika matukio ya kihalifu aliomba jambo lolote linalohusiana na kazi, lisubiri kwa kuwa alikuwa katika mapumziko ya sikukuu.
"Ndugu yangu, unajua leo ni sikukuu na ni usiku, nitafute wakati mwingine, maana siwezi kuzungumzia mambo ya watu wa CHADEMA muda huu. Niache nipumzike kidogo halafu tuwasiliane siku ya kazi," alisema. SOURCE- TANZANIA DAIMA
 
Udaku mwengine Bwana! Kwani huyu Shibuda hana akili hivi kiasi cha kuwa mbunge wa Chama makini?
 
Hatimae Shibuda taulo limemdondoka Mwee,mwenyewe kwelii!!!"MWISHO WA UBAYA NI AIBU".
 
Inaumiza sana, Ikulu ifafanue jambo hili. Hatutaki Ikulu yetu itumike kubambikiza kesi watu. Waliotumia vibaya jina la Rais wa Jamhuri yetu kutisha watuhumiwa watafutwe na waeleze ukweli wa jambo lile
 
Mi nimependa ya Shibuda....
" Mwigulu Nchemba ni mropokaji na Kinana haingiliki"..
Sasa hapa swali ni je...
  1. Nani kawatuma polisi kuihusisha CDM na ugaidi?
  2. Shibuda ameingiaje kwenye kwenye hili sakata linalohusisha polisi?
 
Last edited by a moderator:
We have chosen dishonesty as a way of life. We are truly addicted to lying. It's almost an automatic reflex. It seem telling the truth, being moral and good is near to impossible because we are not brave enough for that.

By living and dying dishonestly ,the politician are taking advantage of it.

Hii story ukiisoma kwa macho matatu utagundua kama ukweli umechanganywa na uongo mwingi kwa faida ya kibinafsi na kisiasa lakini wanasahau kama njia ya muongo ni FUPI.

Taifa la wananchi waongo hata serikali nayo itakuwa niya kiongo kiongo kwa vile serikali inatokana na wananchi hao hao waongo waongo. Kama wananchi hawabadiriki, hata serikali kutoka kuzimu au mbinguni ikiingia madarakani haiwezi kuepuka kazi za uwongo uwongo.

Wametengeneza story na Rajabu Kihawa ya ukweli na uwongo mwingi ili kuhakikisha Mh. Shibuda anafutika katika siasa za CHADEMA. Walikosa kwa muda mrefu sehemu ya kumpata kwa sababu ameamua kwa muda mrefu kuwa kimya kisiasa. Wanatafuta negative reaction zake ili wapate sehemu ya kuanzia kumsindikiza atoke nje ya mlango wa CHADEMA.

This is truly more than gutter politics.
 
Napatwa na wasiwasi mkubwa kwa akili za wafuasi wa chadema kila walishwalo wanakula banti na viroba si mchezo..mhariri tanzania daima km kweli gazet lako limeandika utumbo huu napatwa na wasiwasi huu ya utashi wako bt ni gazet la chama chenu cha wazee wakudanganya watu.hadith ya kitoto na kipuudhi kwamwenye akil timamu amepima vijana wenu wamedhiirisha ni wafupi wa akil wameanin hiyo habar na kuichangia seriously tena poor chadema low thinking capacity walio nayo watu wenu ndo maana wanaamin mkishika madaraka vitu vitashuka bei ndan ya miez 6.na vijana wote watapata ajira..wakomboz Feli na vilaza..
 
Back
Top Bottom