Taarifa hizi zilipatikana kipindi cha kama mwezi mmoja hivi na juhudi za kutaka kuthibitishwa zinaendelea. Tetesi zinadokeza kuwa Kutokana na hali ya nchi ilivyo maamuzi magumu yanahitajika na tayari yamewagawa wana CCM na baadhi ya watendaji wa serikali zote mbili za SMZ na SMT.
Suala la Zanzibar, (uchaguzi wa 2015) na kufutwa kwake na Jecha kumeacha sintofahamu baina ya wahisani na serikali ya JMT na kutaka suala hili lipatiwe ufumbuzi. Jumuiya ya Kimataifa na wadau wa maendeleo hasa Ulaya na Marekani wametowa masharti mazito kuhusu suala la Zanzibar kupatiwa ufumbuzi kiasi cha kuathiri mwenendo wa bajeti kwa JMT. Taarifa zinadokeza kuwa kuna changamoito kubwa sana ya utengenezaji wa bajeti kwa mwaka 2017/2018 ikiwa Tanzania haitakubali masharti yaliyowekwa na jumuiya za Kimataifa kuhusu suala la Zanzibar.
Hali hiyo inartipotiwa kuwagawa wana CCM na watendaji wengine wa serikali zote mbili wengine wakitaka masharti yatekelezwe ili kuinusuri nchi na hatua kali zinazoweza kuchukuliwa na wengine wakipinga.
Imeripotiwa kuwa kuna viongozi waandamizi wa SMZ wakiongozwa na kiongozi mkubwa wanapinga hatua yoyote ya kukubali mabadiliko Zanzibar kama miongoni mwa masharti ya wahisani na jitihada za chini chini za kujenga misimamo kwa wanachama zinaendelea kufanywa na kundi hili kwa upande wa Zanzibar.
Kundi linalounga mkono kutii masharti inaelezwa kuwa linaegemea zaidi katika maslahi ya Taifa na kuangalia zaidi mkwamo unaoweza kulikumba Taifa na kupoteza haiba a yake kimataifa. Tayari kunaripotiwa uwezekano wa kugawika wana CCM wa Tanzania Bara ambao inaripotiwa kuguswa zaidi na athari inazozipata Tanzania ambayo kwa mara ya kwanza imeonja uchungu wa moja kwa moja wa kunnyimwa baadhi ya misaada na nchi wahisani kwa suala la Zanzibar na wale wa Zanzibar hasa Wahafidhina ambao hawataki kusikia neno lolote la mabadilko.
Tunaomba wenye taarifa za uhakika waziweke hapa kwa maslahi ya Taifa.
Kwa hisani ya msamaria mwema.
Kishada.