QUALITY
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 853
- 115
Wiki chacha zilizopita nilianzisha uzi hapa JF wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa kijiji cha Mwanzo Mgumu, kata ya Msimbu wilayani kisarawe Mkoa wa Pwani ( Nyumbani kwa Baba Riz 1) kutokana na 'mabaunsa' wasiofahamika kuvamia chumba cha kuhesabia kura na kutokamea masanduku yote yaliyohesabiwa kura na yasiyohesabiwa kura. Vile vile nikasema kuwa wakati huo Chadema walikuwa na zaidi ya kura 100 zilizohesabiwa huku CCM ikiwa na kura zaidi ya 20. Nikasema kuwa Uongozi wa wilaya haukuweza kumchukulia hatua mtu yo yote pamoja na wananchi kuwataja wahusika siku chache baada ya tukio hilo...
Naona CD ya ccm ya Ukabila imepotea, ya Ukanda imepoteza wateja na sasa ya udini nayo imeanza kuchuja (Mwanzo mgumu Msimbu wakristo 5%).. Je, ni CD gani sasa itazinduliwa na ccm? ya Chama cha vurugu? Kazi kwao. Mimi sipo.
Chadema will always win. CCM mchujo wake ni mkali sana.