SAKATA LA WANA-CCM, KANISA KATOLIKI: Mapadri nao kutengwa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,648
2,000
SAKATA LA WANA-CCM, KANISA KATOLIKI: Mapadri nao kutengwa

Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga; Tarehe: 11th December 2010 @ 23:59

UPEPO sasa unaelekea kuwageukia baadhi ya mapadri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga ambao nao wanadaiwa kuwa ‘wasaliti’ kwa kukaidi maagizo ya kanisa hilo kwa kushindwa kuwaadhibu waumini wanaodaiwa kuisaliti imani yao katika Uchaguzi Mkuu wa Octoba mwaka huu.

Uamuzi huo utakuwa mwendelezo wa adhabu za kanisa, baada ya wiki iliyopita gazeti hili kuripoti juu ya kutengwa na kanisa hilo waumini ambao ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zaidi ya 400 kutokana na ushabiki wa waziwazi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya kanisa hilo, Jumapili hii, Kanisa Katoliki Parokia ya Familia Takatifu linakusudia kuyatangaza majina ya waumini 20 zaidi wa Parokia hiyo ambao wameisaliti imani yao na hivyo watapewa adhabu ya kutengwa na Kanisa hilo hadi hapo watakapotubu.

Taarifa zaidi iliyopatikana kutoka ndani ya Kanisa hilo inaeleza kuwa kwa sasa wameorodhesha majina ya baadhi ya mapadri wa kanisa hilo jimboni hapa ambao
wanashutumiwa kukaidi maagizo ya Kanisa hilo ambapo mapadri wote walikubaliana kuwatambua na kuwaadhibu kwa kuwasimamisha, kuwatenga na kuwafukuza waumini wote wanaodaiwa kuisaliti imani ya Kanisa wakati wa kampeni na hatimaye uchaguzi wa mwaka
huu.

Inadaiwa kuwa, katika orodha ya majina ya mapadri hao ‘wasaliti’ wapo ambao wataonywa na kuendelea na uongozi wa kiroho, lakini pia wapo ambao wataadhibiwa kwa kutengwa hadi hapo watakapokuwa tayari kutubu.

Majina hayo yatatangazwa hadharani hivi karibuni.

Uchunguzi uliofanywa na HABARILEO Jumapili umebainisha kuwa Mhashamu Baba Askofu Damian Kyaruzi Jimbo la Sumbawanga, amebariki hatua nzima ya kufukuzwa kwa waumini wanaodaiwa kuisaliti imani yao kuhudhuria Ibada za Misa Takatifu na kufungiwa Sakramenti zote kwa kile anachodai kuyathamini maamuzi ya wengi hata hivyo hayuko tayari kulizungumzia jambo hili hadharani.

Mwandishi wa habari hizi, licha ya kuomba miadi kwa takribani wiki nzima na baadaye kukubaliwa, siku ya miadi (juzi) alishindwa kuonana na kiongozi huyo wa kiroho jimboni humo ili kuzungumzia suala hili, ikidaiwa kuwa ana orodha ndefu ya watu anaopaswa kuonana nao ambapo wengi wao walikuwa ni mapadri wake.

Mgongano huo wa kiimani unaolihusisha Kanisa hilo na baadhi ya waumini wao ambao wengi wao ni wana CCM ambao wanakadiriwa kuwa zaidi ya 400, umechochewa na kile Kanisa hilo kinachoeleza kauli za kufuru dhidi ya Utatu Mtakatifu pale ambapo Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeish Hilaly wa CCM katika moja ya mikutano yake ya kugombea nafasi hiyo anadaiwa kuikufuru imani ya Kanisa hilo kwa kujifananisha na Yesu Kristo mwana wa Mungu katika dhana zima ya mafiga matatu.

Mgongano huo wa kiimani ulioanza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni za CCM na kuendelea baada ya hapo, ndipo kwa mara ya kwanza baadhi ya makatekista kadhaa walipovuliwa na Kanisa nyadhifa zao hizo wakituhumiwa kuishabikia CCM hususani mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM ambaye ni Muislamu.

Mmoja wa makatekista hao akizungumza kwa njia ya simu na kujitambulisha kwa jina la Deusdeus Mwakalunde ambaye alikuwa katekista wa Parokia ya Familia Takatifu lililopo Isesa alikiri kuvuliwa wadhifa wake huo akishutumiwa kuisaliti imani yake kwa
kuishabikia CCM wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu .

“Nasema hivi ni kweli mimi ni mmoja wa makatekista wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga tuliovuliwa nyadhifa zetu hizo tuko wengi idadi kamili siikumbuki kwa sasa hata hivyo kwa sasa kanisa hilo halina tena mpango wa kuturudisha …. Kwanza mie ni Katibu wa CCM Kata ya Mollo imekuwa ni vigumu kwangu, “ alisema.

Kwa mujibu wa katekista huyo ‘msaliti’ waumini wa Parokia hiyo kupitia katekista wao ambaye jina lake limehifadhiwa wameshataarifiwa kuwa waumini wa parokia hiyo ambao ni wana CCM wapatao 20 majina yao yatatangazwa kwenye Misa Takatifu ya Jumapili (leo) kuwa watengwe na kufukuzwa kwa usaliti.

Hali ikiwa tete hivyo, baadhi ya waumini waliohojiwa na gazeti hili baadhi yao wameunga mkono kuadhibiwa kwa baadhi ya mapadri “wasaliti’ hao wakidai kuwa nao pia wanastahili adhabu kama walizopewa baadhi ya waumini wenzao ambapo baadhi yao wanalilaumu Kanisa hilo kuwaadhibu waumini wenzao bila hata kuwapatia fursa ya kujitetea kwenye Mahakama ya Kanisa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei wa Kanisa Kuu mjini hapa, Kanoni Kanyengele alilieleza gazeti hili kuwa kama kweli kuna mapadri waliosaliti imani basi wanastahili adhabu na wanapaswa kutubu.

“ Sheria ni Msumeno haibagui wadhifa wa muumini au kiongozi wa kiroho, “ alisisitiza. Lakini baadhi ya waumini waliotengwa na Kanisa wanadai kuwa waliwasiliana na Mbunge Aeshy Hilaly na kumweleza masahibu yaliyowapata kwa kumshabikia na kwamba walitaka awasaidie kumaliza dhahama hii.

“Ndipo alipotueleza kuwa kama tumetengwa, basi tutafute kiwanja mjini hapa na akatuahidi kuwa atatujengea kanisa kwenye kiwanja hicho,” alisema mmoja wao.

Hata hivyo mwanasiasa huyo alitakiwa na gazeti hili aeleze kama kiwanja hicho kimepatikana alikana kuwa hajawahi kukutana na wana CCM hao waliotengwa na kusema. “Hizi ni mbinu za kunichafua kisiasa siwezi kutoa ahadi kama hiyo. “

Hata hivyo kabla ya hapo akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana alikana kuikufuru imani ya Kanisa Katoliki kwa kujifananisha na Yesu Kristo Mwana wa Mungu.

”Nilichowaeleza wapiga kura wangu ni dhana nzima ya mafiga matatu … labda ulimi
uliniponza ila nilisema kuwa hata Serikali ya Mungu mbinguni inaongozwa kwa mfumo wa mafiga matatu basi nikaishia hapo kwa kuwa CCM ilikuwa inaamini kuhusu mafiga matatu kuwa lazima achaguliwe rais, mbunge na diwani kutoka CCM na si vinginevyo.”

Mbunge huyo alisema kutokana na sakata hilo sasa yuko tayari kuonana na Baba Askofu Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga na Uongozi wa juu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ili kueleza ukweli wa suala hilo.

"Niliwasisitizia wapiga kura wangu ambao wengi wao ni Wakatoliki ambao ni asilimia 95 ya wapiga kura wote jimboni umuhimu wa mafiga matatu ambapo nilisema kuwa hata Serikali yaMungu mbinguni inaongozwa kwa misingi ya mafiga matatu... ndiyo nilivyosema, " alisisitiza.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo jimboni humo wamekuwa wakimtuhumu gombea huyo wa CCM kwamba alifananisha mafiga matatu na Utatu Mtakatifu kwa kumfananisha mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kama Mungu Baba, yeye mgombea ubunge kama Yesu Kristo mwana wa Mungu na wagombea udiwani sawa na Roho Mtakatifu.

Mbunge huyo alisema ana imani kuwa Mhashamu Baba Askofu Kyaruzi na hata Baraza la Maaskofu wamedanganywa kwamba ni wana CCM 10 waliotengwa na Kanisa wakati ukweli ni kwamba ni wengi wanazidi hata ile idadi iliyoripotiwa hivi karibuni ya wana CCM 400.

“Nimestushwa na habari iliyochapishwa hivi karibuni kwenye moja ya gazeti linalochapishwa kila siku, si HABARILEO kwamba msemaji wa Baraza hilo la Maaskofu Tanzania aliponukuliwa akisema kuwa ni wana CCM 10 tu ndio waliotengwa au kufukuzwa makanisani.

Akifafanua alisema kwamba hadi sasa wanachama wa vikundi vya burudani zaidi ya 40 ambavyo ni vya CCM , wanachama wake ambao wengi wao ni waumini wa Kanisa hilo wamesimamishwa na baadhi ya matekista nao pia wamevuliwa nyadhifa zao.

Wakati huo huo baadhi ya waumini waliotengwa wanakusudia kutubu makanisani ambapo baadhi yao bado wanashikilia misimamo yao ya kutokuwa na utayari huo wa kutubu na kufuatia hali hiyo hivi karibuni kilifanyika kikao cha ndani kilichowakutanisha waumini waliotengwa na Kanisa hilo ili kujadili mustakabali wao.

Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa CCM Viwanja vya Sabasaba mjini hapa ambapo kilihudhuriwa na wana CCM anakadiriwa kuwa zaidi ya 40 ambao wengi wao walikuwa wamevalia fulana za chama chao.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Rukwa, Hipolitus Matete, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Charles Kabanga, Katibu wa CCM Mkoa, Fratern Kiwango na Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini.

Hata hivyo kikao hicho kililazimika kusimama kwa muda pale Katibu wa CCM Mkoa, Kiwango alipobaini kuwepo kwa mwandishi wa habari hizi ukumbini humo na mara moja aliwambia wajumbe: "Naomba tutambuane wale wote ambao hawakualikwa hawastahili kuhudhuria na miongoni mwetu yupo huyu mwandishi naye atoke nje,” alisisitiza.

Kauli hiyo ilileta taharuki miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho ambao mmoja wao aliomba aoneshwe huyo mwandishi ili amtoe kwa nguvu ndipo alipojitokeza Mbunge Aeish na kutuliza tafrani hiyo pale alipofanikiwa kumtoa nje mwandishi huyo kwa ustaarabu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Daniel Ole Njoolay aliliambia gazeti hili leo ofisini kwake kwa kukiri kuwa mgogoro huu umewagawanya hata hivyo alisisitiza kuwa anaamini kuwa mgogoro huu si wa kudumu wakati ukifika utaisha wenyewe.

"Hapa ni suala la muda ni kama kimbunga muda ukifika kitatulia chenyewe lakini nasema ipo haja na waumini wenyewe wawe watiifu kwa viongozi wao wa Kanisa pale
wanapopewa maagizo ni kuyatekeleza na si vingnevyo,” alisisitiza.
 
kayumba

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
653
195
Au huu ndiyo udini tunasikia wana siasa wakiongelea kila kukicha! Hivi ni haki kulaumiwa na dini yako kwa kukishabikia chama fulani au hapa kuna maelezo ambayo mwandishi hajayaweka sawa? Tunavyolijua kanisa Katoliki kila kitu kinaamriwa tokea juu(Rome), Je huu ndiyo msimamo wa Kanisa hilo? Kosa la hawa waumini linalosemwa ni usaliti, usaliti gani huo au nao waliwekeana makubaliano ya siri?

Ningependa kupata majibu ya maswali haya kutoka kwa yeyote anayejua ukweli wa kinachoendelea!
 
Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,325
2,000
Hii inawezekana kabisa kwa mgombea Ubunge kuikashifu Imani ya Kanisa. Naona ilikuwa ni agenda ambayo CCM walikuwa wamekubaliana kuwa wao ni "UTATU MTAKATIFU" maana hata kule Shinyanga kuna mgombea udiwani ambaye pia ni Katibu mwenezi wa CCM (M) alitumia maneno hayo hayo wakati akimnadi mgombea ubunge wao. Tena yeye alitamka wazi wazi kwenye mkutano kuwa Mkwere ni Mungu Baba, Mbunge ni Mungu Mwana na yeye mgombea udiwani ni Roho Mtakatifu.

Pumbavu zao hawana adabu! Na kwa bahati mbaya au nzuri huyo jamaa naye ni muumini wa dini fulani. Sasa jamani kukashifu imani za watu wengine ni vizuri? Mimi nashangaa kwa nini hawa wa Sumbawanga hawajampiga chini huyu zoba, sisi kule tulimbwaga huyo jamaa wa CCM aliyejifananisha na Roho Mtakatifu. Na mbaya zaidi ndo alikuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga. Sawa kabisa Watengwe hao!!!!!
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,952
2,000
Alichofanya Mbunge huyo wa CCM ni kosa kubwa kwa kanisa Katoliki labda haielewi imani hiyo. Yeye ni muislam, afikirie kuwa kama kungekuwa na mgombea yeyote yule wakati wa Kampeni angejifananisha na Mtume Muhamad, mashekhe na maimam wangekaa kimya?

Huyu mbunge wa CCM ni muislam, yawezekana asijue uzito na ubaya wa kauli ambayo alikuwa akiitumia lakini hao wakatoliki kushabikia kauli hiyo walifanya kosa kubwa sana kuukufuru utatu Mtakatifu ambao kadiri ya imani ya Kanisa Katoliki Utatu huu ndiyo Mungu Mwenyewe, na mtu yeyote kujifananisha na nafsi yeyote katika utatu mtakatifu maana yake alijifananisha na Mungu, ambayo ni kufuru. Kwa mujibu ya kanuni ya Kanisa Katoliki hawa wanastahili kufanya toba maalum na baadaye kuikiri imani yao upya, na kutambua kuwa utatu Mtakatifu ni Mungu, na hakuna chochote iwe katika nchi au juu mbinguni cha kufananishwa nao.

Kiimani walifanya kosa kubwa sana, na kanisa halijafanya kosa. Hao waliofungiwa, kama bado wanayakubali mafundisho ya Kanisa Katoliki, wanachotakiwa kufanya ni kutubu na kuomba msamaha wa dhambi. Mungu ni mwenye huruma.
 
ifolako

Member
Nov 8, 2010
98
0
UDINI,UDINI,UDINI!Tatizo la kupokea kila uambiwacho na mapadri kuwa ni kweli bila ya kuuliza maswali(dogmaship) ndio hilo.Wana ccm wamejua ni upuuzi kumpigia kura mtu hasiyefaa hata ukatibu kata ukampa cheo kikubwa,sasa wanaanza kulimana wenyewe kama CDM!
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,952
2,000
Au huu ndiyo udini tunasikia wana siasa wakiongelea kila kukicha! Hivi ni haki kulaumiwa na dini yako kwa kukishabikia chama fulani au hapa kuna maelezo ambayo mwandishi hajayaweka sawa? Tunavyolijua kanisa Katoliki kila kitu kinaamriwa tokea juu(Rome), Je huu ndiyo msimamo wa Kanisa hilo? Kosa la hawa waumini linalosemwa ni usaliti, usaliti gani huo au nao waliwekeana makubaliano ya siri?

Ningependa kupata majibu ya maswali haya kutoka kwa yeyote anayejua ukweli wa kinachoendelea!

Kayumba, mwandishi hajaweka vizuri maneno yake labda pengine alitaka kuuficha ushabiki wake wa kisiasa. Hawa wamesimamishwa siyo kwa sababu ya kuwa mashabiki au wana CCM balli kwa sababu ya kumfananisha mwanadamu na Mungu. Kwa wakatoliki Utatu Mtakatifu ni Mungu. Na Utatu Mtakatifu ni Mungu Baba, Mungu Mwana (Yesu Kristo) na Mungu Roho Mtakatifu. Hawa wakatoliki walikuwa wakiwanandi wagombea wa CCM kuwa JK ni Mungu Baba, Mbunge ni Mungu Mwana (Yesu Kristo) na Diwani ni Mungu Roho Mtakatifu. Kwa hiyo wawachague wagombea wa CCM maana wakiwachagua wote watatu ndiyo Umungu wao utakamiliki. Hiyo katika kanisa Katolki ni kufuru - kosa kubwa kuliko mengine yote, kumfananisha mwanadamu yeyote na Mungu.
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,874
2,000
Au huu ndiyo udini tunasikia wana siasa wakiongelea kila kukicha! Hivi ni haki kulaumiwa na dini yako kwa kukishabikia chama fulani au hapa kuna maelezo ambayo mwandishi hajayaweka sawa? Tunavyolijua kanisa Katoliki kila kitu kinaamriwa tokea juu(Rome), Je huu ndiyo msimamo wa Kanisa hilo? Kosa la hawa waumini linalosemwa ni usaliti, usaliti gani huo au nao waliwekeana makubaliano ya siri?

Ningependa kupata majibu ya maswali haya kutoka kwa yeyote anayejua ukweli wa kinachoendelea!

mbona kila kitu kiko wazi, kakashifu utatu mtakatifu which is a key belief ktk kanisa, na waumini wakashabikia na afterall wakaonywa na hawakutaka kujifunza. Katu kanisa lisivumilie mienendo kama hiyo.
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,952
2,000
Hawa wakatoliki watakuwa wanapoteza muda wao kufikiria kwamba tatizo lao linaweza kumalizwa kwa mtazamo wa kisiasa. Hili ni suala la kiimani, wakitaka liishe ni lazima wapitie katika taratibu za imani ya Kanisa Katoliki. Kanisa Katoliki halina utaratibu kabisa, maamuzi yake kuathiriwa na wanasiasa. Kwao kiongozi kama ni mkatoliki ni kama mkristo wa kawaida ndiyo maana huwezi kusikia hata siku moja kiongozi wa serikali akapewa hata nafasi ndogo kabisa ya kuhutubia hadhara ya Kanisa Katoliki kama kiongozi.

Kama wanadhani wameonewa, mahali pekee wanaweza kwenda ni kwenye Church Tribunal Court. Kadinali Pengo hawezi kubadilisha uamuzi wa Askofu wa Jimbo la Sumbawanga. Askofu wa Jimbo la Sumbawanga hayupo chini ya Pengo bali yupo chini ya Papa. Ni papa au mahakama ya kanisa pekee ndiyo inayoweza kubadili maamuzi ya Askofu wa Sumbawanga. Huyo Mbunge anayesema anataka kwenda kumwona Pengo nadhani ni mbumbumbu wa mfumo wa uongozi wa kanisa. Yeye hawezi kuwaombea msamaha hao waumini, inabidi wao wenyewe watubu kwa nafsi zao, toba ya kiimani.
 
Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
1,500
SAKATA LA WANA-CCM, KANISA KATOLIKI: Mapadri nao kutengwa

Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga; Tarehe: 11th December 2010 @ 23:59

UPEPO sasa unaelekea kuwageukia baadhi ya mapadri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga ambao nao wanadaiwa kuwa ‘wasaliti' kwa kukaidi maagizo ya kanisa hilo kwa kushindwa kuwaadhibu waumini wanaodaiwa kuisaliti imani yao katika Uchaguzi Mkuu wa Octoba mwaka huu.

Uamuzi huo utakuwa mwendelezo wa adhabu za kanisa, baada ya wiki iliyopita gazeti hili kuripoti juu ya kutengwa na kanisa hilo waumini ambao ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zaidi ya 400 kutokana na ushabiki wa waziwazi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya kanisa hilo, Jumapili hii, Kanisa Katoliki Parokia ya Familia Takatifu linakusudia kuyatangaza majina ya waumini 20 zaidi wa Parokia hiyo ambao wameisaliti imani yao na hivyo watapewa adhabu ya kutengwa na Kanisa hilo hadi hapo watakapotubu.

Taarifa zaidi iliyopatikana kutoka ndani ya Kanisa hilo inaeleza kuwa kwa sasa wameorodhesha majina ya baadhi ya mapadri wa kanisa hilo jimboni hapa ambao
wanashutumiwa kukaidi maagizo ya Kanisa hilo ambapo mapadri wote walikubaliana kuwatambua na kuwaadhibu kwa kuwasimamisha, kuwatenga na kuwafukuza waumini wote wanaodaiwa kuisaliti imani ya Kanisa wakati wa kampeni na hatimaye uchaguzi wa mwaka
huu.

Inadaiwa kuwa, katika orodha ya majina ya mapadri hao ‘wasaliti' wapo ambao wataonywa na kuendelea na uongozi wa kiroho, lakini pia wapo ambao wataadhibiwa kwa kutengwa hadi hapo watakapokuwa tayari kutubu.

Majina hayo yatatangazwa hadharani hivi karibuni.

Uchunguzi uliofanywa na HABARILEO Jumapili umebainisha kuwa Mhashamu Baba Askofu Damian Kyaruzi Jimbo la Sumbawanga, amebariki hatua nzima ya kufukuzwa kwa waumini wanaodaiwa kuisaliti imani yao kuhudhuria Ibada za Misa Takatifu na kufungiwa Sakramenti zote kwa kile anachodai kuyathamini maamuzi ya wengi hata hivyo hayuko tayari kulizungumzia jambo hili hadharani.

Mwandishi wa habari hizi, licha ya kuomba miadi kwa takribani wiki nzima na baadaye kukubaliwa, siku ya miadi (juzi) alishindwa kuonana na kiongozi huyo wa kiroho jimboni humo ili kuzungumzia suala hili, ikidaiwa kuwa ana orodha ndefu ya watu anaopaswa kuonana nao ambapo wengi wao walikuwa ni mapadri wake.

Mgongano huo wa kiimani unaolihusisha Kanisa hilo na baadhi ya waumini wao ambao wengi wao ni wana CCM ambao wanakadiriwa kuwa zaidi ya 400, umechochewa na kile Kanisa hilo kinachoeleza kauli za kufuru dhidi ya Utatu Mtakatifu pale ambapo Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeish Hilaly wa CCM katika moja ya mikutano yake ya kugombea nafasi hiyo anadaiwa kuikufuru imani ya Kanisa hilo kwa kujifananisha na Yesu Kristo mwana wa Mungu katika dhana zima ya mafiga matatu.

Mgongano huo wa kiimani ulioanza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni za CCM na kuendelea baada ya hapo, ndipo kwa mara ya kwanza baadhi ya makatekista kadhaa walipovuliwa na Kanisa nyadhifa zao hizo wakituhumiwa kuishabikia CCM hususani mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM ambaye ni Muislamu.

Mmoja wa makatekista hao akizungumza kwa njia ya simu na kujitambulisha kwa jina la Deusdeus Mwakalunde ambaye alikuwa katekista wa Parokia ya Familia Takatifu lililopo Isesa alikiri kuvuliwa wadhifa wake huo akishutumiwa kuisaliti imani yake kwa
kuishabikia CCM wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu .

"Nasema hivi ni kweli mimi ni mmoja wa makatekista wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga tuliovuliwa nyadhifa zetu hizo tuko wengi idadi kamili siikumbuki kwa sasa hata hivyo kwa sasa kanisa hilo halina tena mpango wa kuturudisha …. Kwanza mie ni Katibu wa CCM Kata ya Mollo imekuwa ni vigumu kwangu, " alisema.

Kwa mujibu wa katekista huyo ‘msaliti' waumini wa Parokia hiyo kupitia katekista wao ambaye jina lake limehifadhiwa wameshataarifiwa kuwa waumini wa parokia hiyo ambao ni wana CCM wapatao 20 majina yao yatatangazwa kwenye Misa Takatifu ya Jumapili (leo) kuwa watengwe na kufukuzwa kwa usaliti.

Hali ikiwa tete hivyo, baadhi ya waumini waliohojiwa na gazeti hili baadhi yao wameunga mkono kuadhibiwa kwa baadhi ya mapadri "wasaliti' hao wakidai kuwa nao pia wanastahili adhabu kama walizopewa baadhi ya waumini wenzao ambapo baadhi yao wanalilaumu Kanisa hilo kuwaadhibu waumini wenzao bila hata kuwapatia fursa ya kujitetea kwenye Mahakama ya Kanisa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei wa Kanisa Kuu mjini hapa, Kanoni Kanyengele alilieleza gazeti hili kuwa kama kweli kuna mapadri waliosaliti imani basi wanastahili adhabu na wanapaswa kutubu.

" Sheria ni Msumeno haibagui wadhifa wa muumini au kiongozi wa kiroho, " alisisitiza. Lakini baadhi ya waumini waliotengwa na Kanisa wanadai kuwa waliwasiliana na Mbunge Aeshy Hilaly na kumweleza masahibu yaliyowapata kwa kumshabikia na kwamba walitaka awasaidie kumaliza dhahama hii.

"Ndipo alipotueleza kuwa kama tumetengwa, basi tutafute kiwanja mjini hapa na akatuahidi kuwa atatujengea kanisa kwenye kiwanja hicho," alisema mmoja wao.

Hata hivyo mwanasiasa huyo alitakiwa na gazeti hili aeleze kama kiwanja hicho kimepatikana alikana kuwa hajawahi kukutana na wana CCM hao waliotengwa na kusema. "Hizi ni mbinu za kunichafua kisiasa siwezi kutoa ahadi kama hiyo. "

Hata hivyo kabla ya hapo akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana alikana kuikufuru imani ya Kanisa Katoliki kwa kujifananisha na Yesu Kristo Mwana wa Mungu.

"Nilichowaeleza wapiga kura wangu ni dhana nzima ya mafiga matatu … labda ulimi
uliniponza ila nilisema kuwa hata Serikali ya Mungu mbinguni inaongozwa kwa mfumo wa mafiga matatu basi nikaishia hapo kwa kuwa CCM ilikuwa inaamini kuhusu mafiga matatu kuwa lazima achaguliwe rais, mbunge na diwani kutoka CCM na si vinginevyo."

Mbunge huyo alisema kutokana na sakata hilo sasa yuko tayari kuonana na Baba Askofu Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga na Uongozi wa juu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ili kueleza ukweli wa suala hilo.

"Niliwasisitizia wapiga kura wangu ambao wengi wao ni Wakatoliki ambao ni asilimia 95 ya wapiga kura wote jimboni umuhimu wa mafiga matatu ambapo nilisema kuwa hata Serikali yaMungu mbinguni inaongozwa kwa misingi ya mafiga matatu... ndiyo nilivyosema, " alisisitiza.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo jimboni humo wamekuwa wakimtuhumu gombea huyo wa CCM kwamba alifananisha mafiga matatu na Utatu Mtakatifu kwa kumfananisha mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kama Mungu Baba, yeye mgombea ubunge kama Yesu Kristo mwana wa Mungu na wagombea udiwani sawa na Roho Mtakatifu.

Mbunge huyo alisema ana imani kuwa Mhashamu Baba Askofu Kyaruzi na hata Baraza la Maaskofu wamedanganywa kwamba ni wana CCM 10 waliotengwa na Kanisa wakati ukweli ni kwamba ni wengi wanazidi hata ile idadi iliyoripotiwa hivi karibuni ya wana CCM 400.

"Nimestushwa na habari iliyochapishwa hivi karibuni kwenye moja ya gazeti linalochapishwa kila siku, si HABARILEO kwamba msemaji wa Baraza hilo la Maaskofu Tanzania aliponukuliwa akisema kuwa ni wana CCM 10 tu ndio waliotengwa au kufukuzwa makanisani.

Akifafanua alisema kwamba hadi sasa wanachama wa vikundi vya burudani zaidi ya 40 ambavyo ni vya CCM , wanachama wake ambao wengi wao ni waumini wa Kanisa hilo wamesimamishwa na baadhi ya matekista nao pia wamevuliwa nyadhifa zao.

Wakati huo huo baadhi ya waumini waliotengwa wanakusudia kutubu makanisani ambapo baadhi yao bado wanashikilia misimamo yao ya kutokuwa na utayari huo wa kutubu na kufuatia hali hiyo hivi karibuni kilifanyika kikao cha ndani kilichowakutanisha waumini waliotengwa na Kanisa hilo ili kujadili mustakabali wao.

Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa CCM Viwanja vya Sabasaba mjini hapa ambapo kilihudhuriwa na wana CCM anakadiriwa kuwa zaidi ya 40 ambao wengi wao walikuwa wamevalia fulana za chama chao.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Rukwa, Hipolitus Matete, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Charles Kabanga, Katibu wa CCM Mkoa, Fratern Kiwango na Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini.

Hata hivyo kikao hicho kililazimika kusimama kwa muda pale Katibu wa CCM Mkoa, Kiwango alipobaini kuwepo kwa mwandishi wa habari hizi ukumbini humo na mara moja aliwambia wajumbe: "Naomba tutambuane wale wote ambao hawakualikwa hawastahili kuhudhuria na miongoni mwetu yupo huyu mwandishi naye atoke nje," alisisitiza.

Kauli hiyo ilileta taharuki miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho ambao mmoja wao aliomba aoneshwe huyo mwandishi ili amtoe kwa nguvu ndipo alipojitokeza Mbunge Aeish na kutuliza tafrani hiyo pale alipofanikiwa kumtoa nje mwandishi huyo kwa ustaarabu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Daniel Ole Njoolay aliliambia gazeti hili leo ofisini kwake kwa kukiri kuwa mgogoro huu umewagawanya hata hivyo alisisitiza kuwa anaamini kuwa mgogoro huu si wa kudumu wakati ukifika utaisha wenyewe.

"Hapa ni suala la muda ni kama kimbunga muda ukifika kitatulia chenyewe lakini nasema ipo haja na waumini wenyewe wawe watiifu kwa viongozi wao wa Kanisa pale
wanapopewa maagizo ni kuyatekeleza na si vingnevyo," alisisitiza.

"HAKUNA WA KUFANANA NA YESU"

Kwa Mujibu wa imani ya Kikristo ambayo wakristo huwa wanabatizwa nayo ni kuwa hakuna kitu chochote kinachoweza kulinganishwa na uungu wa Mungu ambao unajifunua kwetu katika Nafsi tatu. Huo ndio msingi mkuu wa imani ya kikristo. Hakuna wa kufanana na Mungu Baba, wala Mungu mwana wala Mungu Roho Mtakatifu.

Kitendo cha mtu yeyote kujaribu kujifananisha na nafsi mojawapo ya Mungu, ni kuikashfu imani ya Kikristo si kwa kanisa katoliki tu bali kwa makanisa yote ya kikristo. Kitendo cha muumini yeyote wa kikristo kumshabikia mtu aliyekashfu ukristo, ni sawa na kuikana imani ambayo alibatizwa kwayo. Hivyo kwa taratibu za kikanisa unastahili kutengwa mpaka utakapotambua kosa lako utubu mbele ya kanisa na mbele ya Mungu na utasamehewa.

Kwa muumini yeyote ambaye haoni kuwa kumshabikia mtu aliyeikashifu imani ya kikristo ni makosa. Basi hajui alitendalo na wala hajui msingi wa mkristo. Huyo hata kama ni mhudhuriaji kanisani, basi anaenda tu kwa mazoea na wala hayasikilizi maandiko vizuri. Biblia inatuambia, Imani pasipo matendo kwa bwana haifai kitu, imekufa. Huyo ni mkristo mfu. Kama unajiona uko karibu na CCM kuliko Mungu aliyekuumba, fanya uamuzi kama Kingunge uwe muumini wa CCM na uachane na imani ya Kikristo.

Msimamo wa Askofu Kyaruzi ni wa msingi na ni muhimu wakristo waliosimamishwa watambue kuwa uhusiano wao na Mungu ni wa kibinsfsi na kwamba kila mtu atasimama mbele ya Mungu pekee yake. Kila mtu aitafakari imani yake na kama roho mtakatifu atamwonyesha kuwa alifanya kosa, awe tayari kuungama. Kama roho mtakafujo (roho wa ibilisi) atamwongoza kuanzisha malumbano na askofu, basi na afanye hivyo ila ajue hukumu inamngoja. Nasikitika kusikia kuwa kuna mapadre na makatechsta ambao tayari wanaongozwa na roho mtakafujo na wanataka kuanza kulumbana.

Makanisa mengine yote yanatakiwa kuwa na huo msimamo. Kuacha mambo madogomadogo yaendelee ndani ya kanisa ndo kunasababisha mpaka mnajikuta mnaingiza ushoga ndani ya kanisa.
 
Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
1,500
Hawa wakatoliki watakuwa wanapoteza muda wao kufikiria kwamba tatizo lao linaweza kumalizwa kwa mtazamo wa kisiasa. Hili ni suala la kiimani, wakitaka liishe ni lazima wapitie katika taratibu za imani ya Kanisa Katoliki. Kanisa Katoliki halina utaratibu kabisa, maamuzi yake kuathiriwa na wanasiasa. Kwao kiongozi kama ni mkatoliki ni kama mkristo wa kawaida ndiyo maana huwezi kusikia hata siku moja kiongozi wa serikali akapewa hata nafasi ndogo kabisa ya kuhutubia hadhara ya Kanisa Katoliki kama kiongozi.

Kama wanadhani wameonewa, mahali pekee wanaweza kwenda ni kwenye Church Tribunal Court. Kadinali Pengo hawezi kubadilisha uamuzi wa Askofu wa Jimbo la Sumbawanga. Askofu wa Jimbo la Sumbawanga hayupo chini ya Pengo bali yupo chini ya Papa. Ni papa au mahakama ya kanisa pekee ndiyo inayoweza kubadili maamuzi ya Askofu wa Sumbawanga. Huyo Mbunge anayesema anataka kwenda kumwona Pengo nadhani ni mbumbumbu wa mfumo wa uongozi wa kanisa. Yeye hawezi kuwaombea msamaha hao waumini, inabidi wao wenyewe watubu kwa nafsi zao, toba ya kiimani.

Mkuu sioni pa kukugongea thanks. Hapa umenena.

Nawashangaa hao jamaa ambao ni wakristo wanaongozwa na mtu ambaye si mkristo kufikia maamuzi. Mwenyewe kesha sema ulimi uliteleza. Naona hapa ni sawa na chongo kuongozwa na kipofu.
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
15,304
2,000

Huyo mbunge alikuwa anaropoka bila ya kujali kuwa hiyo ni imani ya wenzake ambayo haijui, sasa naye atalijua jiji. Jamaa huyu ni mbumbumbu si wa mambo ya kawaida tu, hata darasani alikuwa mbumbumbu hadi alipofukuzwa shule akiwa Form Two, na hivi sasa ni mwenye elimu ya darasa la saba tu. Mbaya zaidi aligombea ubunge CCM huku headmaster wake aliyemfukuza akigombea CDM, na ilikuwa dhahiri kuwa CHADEMA walishinda kwa tofauti ndogo ya kama kura 100, lakini Pinda akamzuia msimamizi wa uchaguzi kumtangaza headmaster mshindi!
 
Profesa

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
905
1,000
Huo ni wehu kuweka kicha cha habari kama hiki... Hali haiko kama inavyoandikwa humu... Alieandika habari hizi hana nia njema... Kiongozi anapokuwa hana nidhamu unadhani ni nani wanaomfahamu? Sasa inakuwaje bila aibu analindwa(ambayo ndio desturi ya baadhi ya makundi ya siasa) kwani hakuna shuguli nyingine za kufanya lazima awe kiongozi....

Ninashawishika kusema kuna kundi fulanila kisiasa linajinufaisha na hali hiyo... Ndo mana bila aisbu leo hii.. Na sijui kama ni vijana wa intelijensia ndo wanaowapa viongozi wetu hizi vegue feedbacks... Eti kuna mpasuko wa kidini... Vurugu za tandale inakuwaje zitangazwe kuwa zilitokea nchi nzima?

Epukeni hili ni hatari sana
 
Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,766
2,000
HABARI LEO: Hawa jamaa wana ajenda zao za siri ktk mradi wa ccm-udini. Ni uwongo mtupu ulioandikwa hapa ukweli ni kwamba waliotengwa hawazidi hata 10 sasa sijui hizo figure 400 zimetoka wapi na bado wanaendelea kuupotosha uma, kanisa lilifanya uamuzi huu ndani ya kanisa kwa usiri na hapakuwa na lengo la vyombo vya habari kulijua ila kuna baadhi ya waandishi ambao pia ni waumini walipata mtaji kwa manufaa ya sera ya udini ya mkwele.

gazeti la mwananchi liliandika taarifa hii vizuri sana
 
Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,891
1,225
HUWEZI UKAJIFANANISHA NA YESU HARAFU UKAISHI ?? AISHE KHALFANI hILAY ANADIWA KUMUPA MIMBA MWANAFUNZI WA ST. AITWAYE MARY LUISI NA KESI IPO MBIONI PIA ANATAJWA KUMUTEKA MUHINDI AITWAYE RAHIMU NA KUMULAWITI KWA ZAMU HUKU AKIMUTISHIA KWA BASTOLA
 
Chizi Fureshi

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,718
1,500
Kinga halali inaweza kuwa siyo haki tu, bali wajibu mkubwa kwa yule aliye na madaraka kwa ajili ya uhai wa wengine. Kinga ya mema ya jumla kwa wote, inadai kwamba adui asiye na haki azuiwe asilete madhara. Kwa sababu hii, wale walio na mamlaka halali wana pia haki ya kutumia silaha kuwafukuza adui dhidi ya raia ambao wameaminishwa chini ya madaraka yao. Juhudi za serikalikuzuia kuenea kwa tabia yenye madhara kwa haki za watu na sheria za msingi za raia zinalingana na haja ya kulinda mema ya jumuiya. Mamlaka halali yana haki na wajibu wa kutoa adhabu inayolingana na uzito wa kosa. Lengo la kwanza la adhabu ni kurekebisha vurugu iliyoletwa na kosa. Inapotokea kwa hiariya upande wenye hatia, inakuwa na thamani ya fidia. Hapo adhabu zaidi, zaidi ya kutetea taratibu za jamii, na kulinda usalama wa watu, inakuwa na lengo la kuwa dawa. Kadiri inavyowezekana lazima kurekebisha upande ulio na hatia."KATEKISIMU YA KANISA KATOLIKI".
 
Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
2,000
Au huu ndiyo udini tunasikia wana siasa wakiongelea kila kukicha! Hivi ni haki kulaumiwa na dini yako kwa kukishabikia chama fulani au hapa kuna maelezo ambayo mwandishi hajayaweka sawa? Tunavyolijua kanisa Katoliki kila kitu kinaamriwa tokea juu(Rome), Je huu ndiyo msimamo wa Kanisa hilo? Kosa la hawa waumini linalosemwa ni usaliti, usaliti gani huo au nao waliwekeana makubaliano ya siri?

Ningependa kupata majibu ya maswali haya kutoka kwa yeyote anayejua ukweli wa kinachoendelea!
ukiamka leo ukamkashufu mtume Muhamad S.A.W utatafutwa mahali popote duniani uadhibiwe kwa kumkashifu mtume wetu. hali kadhalika kwa kanisa katoliki dhambi zote zinasameheka kasoro kumkashifu Roho mtakatifu. wao walisema na wakatangaza kwenye kampeni kuwa KIKWETE NI MUNGU BABA, HUYU MBUNGE WAO NI YESU KRISTU NA KUWA DIWANI NI ROHO MTAKATIFU.YAANI WAKAUKASHIFU UTATU MTAKATIFU, kwa hiyo kwa vyovyote vile kanisa lilipaswa kuwafukuza na wala siyo kuwa tenga , kwa kuwa kanisa halina mamlaka ya kusamehe dhambi ya kumkashifu ROHO MTAKATIFU
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom