Sakata la viroba: Mselia wa Dodoma ajipiga risasi na kufa

INAWEZEKANA KWELI SERIKALI INAWEZA ISIWE NA SABABU YA KULAUMIWA, LAKINI BUSARA NI YA MUHIMU KATIKA KUCHUKUA HATUA YOYOTE ILE. KABLA YA KATAZO LA SERIKALI KUHUSU VIROBA KULIKUWA NA KIBALI CHA SERIKALI CHA KUENDESHA BIASHARA HIYO. KUNA WATU WALICHUKUA MIKOPO ILI KUENDESHA BIASHARA HIYO. WATU HAWA WALIKUWA WANALIPA KODI KWA BIASHARA HIYO, HIVYO NI WATU WA SERIKALI WANAOLIONGEZEA PATO TAIFA KWA KULIPA KODI.
KABLA YA KATAZO SERIKALI ILIPASWA KULIJUA HILI NA KUTOA MUDA WA KUTOSHA HATUA KWA HATUA. HATUA YA KWANZA INGEKUWA KUONDOA KIBALI CHA BIASHARA HIYO NA KUTOA ZUIO LA UAGIZAJI WAKE, HATUA YA PILI NI KUWEKA MUDA MAALUMU WA KUMALIZA KWA STOCK ILIYOKWISHA KUINGIZWA NCHINI.

JAMBO LA BUSARA ZAIDI LILIKUWA NI KUPIGA MARUFUKU BIASHARA HIYO KWA KUWA INAHARIBU AFYA ZA WATU NA KUFANYA UHAKIKI WA BIDHAA ILIYOKO SOKONI NA KWENYE MADUKA AU MAGHALA YA WAFANYABIASHARA NA KISHA KUWAPA RUZUKU/KUWARUDISHIA PESA YAO.





Tafakari...!!
 
Bora aende tu km walivoenda wanywaji wengi tu,tangulia ukatushie nafasi huko.viroba noma zaid ya unga
 
Me huwa sielewi mtu unajiua vip kwa sababu nya mali. Hamna kitu kibaya kama kushikanisha nafsi yako na mali. Tulikuja duniani tukiwa hatuna chochote na hivyo tutaondoka tukiwa watupu.

Tuwe na ushirika na Mungu na jamii inayotuzunguka. Hii ndiyo furaha kamili. Furaha ya kweli si katika mali bali katika kumuabudu Mungu na wapendwa wako katika familia, mke,mume, watoto, wazazi, na hata marafiki.

Tuache kuabudu mali, hii ndo inapelekea watu kuuana, kulogana, kudhulumiana, kufanya ndugu mandondocha n.k. Laiti tungejua yule unayemuua, au kumdhulumu au kumfanya ndondocha ndiyo furaha yako, mtu asingefanya vile.

Nasaha hizi ziwaendee wote washakamanisha nafsi na mali.
Huelewi pengine umejaliwa kuwa na mke au mume mwenye mapenzi ya dhati, pia jamii iliyokuzunguka ni njema,makuzi uliyokulia ni mazingira salama,,, ndugu yangu wengine hatuna hayo yote ni ya kununua sasa swali. Bila pesa na mali tutaishi maisha gani? Acha tu maisha yaende tu ila usilolijua ni sawa na giza. Waliopitia changamoto nzito tunapenda kusema ndugu yetu muda umemfika wa kurudi nyumbani kupumzika na astarehe kwa amani. Amina.
 
Ashusheje hv inszsni hawakushusha?na unazani ni yeye tu mwenye hivyo viti?
Lkn unajua kuwa tangazo la awali kupiga marufuku viroba lilitoka mwaka jana mwezi wa 6 hivi, na liliweka ukomo wa viroba kuwa 1 jan 2017?
muda umepita, na mambo yamebadilika, lkn fikra na tafakari za watu (akiwemo marehemu), zilibaki vile vile, kwenye "kilevi cha mazoea"....
 
Jamani mm viroba sivipendi from the begins na nilitathimini madhara ya gongo na viroba nikaona viroba ni hatari azidi ni pengine vimedhuru watu wengi zaidi kwa tafiti isiyo rasmi, lakini kwa upande mwingine ni investment kubwa sana juzi na had tunaendekea serikali imeshakamata shehena ya azidi ya billion 10 sio mchezo mchezo kwa mfanyabiashara kufilisiwa kwa dakika, amelipa kodi ana mitambo anawafanyakazi, hatujui mtaji kapata wapi, watathmini Wa serikali walikua wapi wakati mchakato Wa kuzalisha viroba, madhara ya kimazingira wanayoyasema ni yapi? Hivi soda zilizofungashwa kwenye plastic zinavyochafua Mimi yetu, Maji, na vitu vingi vinafungashwa kwenye plastics, havichafui mazingira? Nadhani kuna haja ya kufanyia review ya haya matamko sio mambo ya kukurupuka tu, sina ushaidi ya jamaa aliyejiua lakini kwa hasara wanayoipata kuna uwezekano Wa kujiua kama hawezi kujihimili. Mambo ya kukurupuka serikali imeonywa Mara nyingi lakini haielewi tu...unadhani wataalamu wetu na viongozi wetu kichwani ni ubashite mtupu
 
Lkn unajua kuwa tangazo la awali kupiga marufuku viroba lilitoka mwaka jana mwezi wa 6 hivi, na liliweka ukomo wa viroba kuwa 1 jan 2017?
muda umepita, na mambo yamebadilika, lkn fikra na tafakari za watu (akiwemo marehemu), zilibaki vile vile, kwenye "kilevi cha mazoea"....
Ok sawa na mwenye kiwanda je inakuwaje.
 
Lala Salama Mselia, Japo hukufanya vyema kujiondoa uhai.

Lawama zote nazipeleka kwa serikali iliyojaa uonevu.
Acha utaira wew vijana wangapi wanakufa kisa hvyo viroba,,, wengne vinawazidi mpaka wanashindwa udumia ndoa zao,,, vifo vingi vya vijana WA boda boda husababishwa na kukithiri unywaji wa viroba,,,,, Leo mtu kajiua unasingizia serikali onevu je matatzo katka jamii kuhusu vijana wanaotumia vinywaji vya viroba, kwanin usilaumu viwanda na wauzaji wa viroba........ Wakati mwingne msicoment vitu ili mradi uonekane umecoment
 
Mwache ajipige risasi,serikali ilitoa muda wa kutosha alitakiwa atumiwe common sense
Ni kawaida wenye akili ndogo kama hizi zako wapo na wataendelea kuja kuipongeza serikali ya matamko kwa upuuzi huu wanaoufanya. Bora ukae kimya na si kushadadia alicho fanya huyo jamaa kwa maana hujui nini maana ya biashara, endelea kusubiri ugali wa shikamoo.
 
kama alikua na shehena ya viroba ingeua watu wengi zaidi.R.I.P. mseli.
 
Huyu amekufa kwa sababu ya matamko ya serikali ya awamu ya tano.
 
Nilishuhudia tukio lile la shehena za viroba kupakuliwa.....ilisikitisha sana.....ila angevihamisha mapema sijui alibugi vipi!
 
What goes around comes around. Wengi pia wamekufa kwa kunywa viroba. Shetani ametimiza malengo yake kwake.
Wanadamu tunapaswa kumtegemea Mungu na sio mambo ya dunia hii.
 
Back
Top Bottom