SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA AROBAINI NA SABA
“Naomba unisamehe sana Tommy, nimefanya kazi kwenu kwa muda mrefu sana usinifanyie hivi ndugu yangu”
“Kwahiyo muda huu ndo umegunuda kwamba mimi ni ndugu yako baada ya kuona kwamba upo kwenye hali ambayo hauwezi kutoka?”
“Hapana hapana, ilikuwa ni tamaa tu”
“Ulipewa shingapi kukamilisha lile jambo?”
“Milioni miamoja”
“Miliona mia ndiyo imekufanya umuuze baba yangu?”
“Ndiyo, ndiyo”
“Unajua wengi huwa mnakosea wapi Luck?”
“Hapana”
“Pale ambapo unahisi unajua kila kitu ndio muda sahihi wa kukaa na kujifunza kwa sababu unakuwa umewazidi tu baadhi ya watu wenye uelewa mdogo ila kuna mazingira mengine wewe unakuwa ni leaner/lena kabisa ambaye hakuna ulijualo. Hata wewe nina uhakika kwamba ulikuwa unayafanya haya kwa sababu ulijua ndani ya familia hakuna mtu ambaye anaweza kukutafuta kwa kupotea kwako na ukaona kwamba mimi ni kijana ambaye si chochote wala si lolote kwa sababu kama ungenifahamu huenda ungechukua tahadhari ambazo zingenipa mimi ugumu wa kuweza kukupata” mwanaume aliongea huku akimfanya Luck kumweza mate kwa shida sana.
“Jambo ambalo kwa sasa siwezi tena kuliruhusu Luck ni mtu mwingine kufa kwenye familia yangu, hilo kamwe halitatokea tena kuanzia hivi ninavyo ongea na wewe”
“Mimi nipo tayari kufanya lolote unalo lihitaji Tommy ila naomba unipe nafasi ya kuishi, nipe nafasi nyingine ndugu yangu nitabadilika na kuwa mtu wa tofauti kabisa, naahidi nitakuwa mtu wa mfano sana kweye jamii ambapo watu wengi watatamani kuweza kujifunza kutokwa kwangu na sitakuja kujihusisha na haya mambo tena kwenye maisha yangu mpaka nakufa” alikuwa akijitetea huku akiwa anatetemeka kuona kama anaweza kuipata huruma ya mtu huyo na kupewa nafasi nyingine tena ya maisha kwa kusingizia kwamba aliyokuwa ameyafanya zilikuwa ni tamaa tu na kuanzia siku hiyo alikuwa tayari kabisa kubadilika.
“Kwa bahati mbaya sana maisha hayakupi nafasi mbili Luck, maisha yanakupa nafasi moja tu pekee ya kuweza kuiishi kwa usahihi ambapo unatakiwa kujisahihisha kabla ya watu wengine kuja kukusahihisha kwa lazima. Kama ulikuwa na uhitaji wa kubadilika haukutakiwa kusubiri siku ambayo unakuwa hauna namna ya kuyaokoa maisha yako ndipo ufanye hivyo, hilo ni jambo ambalo ulipaswa kulifanyia maamuzi mapema sana lakini wewe umesubiri mpaka leo ndo unaniambia utabadilika? Maisha ukiyachezea mara moja tu huo ndio unakuwa mwisho wako” alimwangalia sana mtu huyo baada ya kumpa somo, kila alipokuwa anamwangalia, hasira zilikuwa zinamkaba sana kwani huyo ndiye ambaye alikuwa amesababisha baba yake kuishia kitandani maana kama angeifanya kazi yake kwa usahihi basi huenda baba yake angepona kabisa kwenye ule mtego.
“Ulikuwa unajua kwamba mdogo wangu angeuawa?”
“Ndiyo Tommy ila nilijua nikiwa sijafanya maamuzi ya kuacha bado kufanya kazi na hao watu ila kwa sasa naapa nimeacha”
“Mimi sijakuuliza kama umeachana nao, kwahiyo hata siku ambayo mdogo wangu anatekwa ulikuwa unajua?” mwanaume huyo alijibu kwa kubabaika sana lakini aliishia kupigwa risasi ya bega ambayo ilimfanya atoe kilio kingine.
“Ndiyo ndiyo, mimi ndiye niliye husika kukamilisha ule mpango kwa sababu nilikuwa najua kila kitu”
“Why Luck?”
“Nisamehe sana Tommy sitarudia tena ndugu yangu”
“Noelia au Sasha unamjua?”
“Ndiyo”
“Anapatikana wapi?”
“Muda mwingine huwa anakuwa pale Sea Cliff Casino”
“Na yule ambaye alikuwa anaigiza kama bibi yake anaitwaje?”
“Norah”
“Ok, Remsi muda huu yuko wapi?”
“Muda mwingi huwa anakuwa kwa baba yake Osterbay ila kwa sasa nadhani yupo kwake Kigamboni ambako ana mjengo wa siri ambao huwa anaenda kwa siri sana pale ambapo anahisi mambo yake hayaendi vizuri”
“Unaweza ukanitajia eneo na namba ya hilo jengo?”
“Ndiyo ndiyo” alijibu kwa pupa sana akiwa anayatoa maelezo hayo kwa umakini sana ambapo baada nya kukamilisha maelezo hayo mwanaume alimmiminia risasi nyingi sana kwenye kichwa chake kisha akakikata kichwa cha mwanaume huyo na kukiweka juu ya sofa. Hakukaa tena hilo eneo bali alitoweka haraka sana kwani alikuwa amempa ahadi Remsi kwamba hataweza kumaliza masaa ishirini na manne akiwa hai na huenda ndiyo sababu kubwa ambayo ilimfanya aweze kukimbilia huko Kigamboni ili kuweza kujificha.
Tommy safari yake usiku huo ilienda kuishia Mji mwema akiwa kwenye mwendo mkali sana. Baada ya kufika eneo ambalo alikuwa amejiridhisha vyema, alishuka kwenye gari yake na kuanza kutembea kwa mguu ili kuweza kuwahi sehemu ambayo bila shaka ndiyo ilimfanya awepo saa hizo.
Alitembea haraka haraka sana mpaka karibu na jengo ambalo lilionekana kuwa kubwa sana lakini mbali kidogo na eneo hilo walionekana wanaume wanne ambapo wawili kati yao walikuwa wajapan, wanaume hao ndio wale ambao walikuwa wamepewa kazi na mr Oscar kuhakikisha kwamba wanaua kila mtu ambaye alikuwa akionekana kuwa karibu sana na mr Mafupa na usiku huo walikuwa wamemtembelea mtoto wa mzee huyo ili kuweza kummaliza kabisa ili baba yake abaki anatapa tapa ambapo atakosa msaada kabisa kitu ambacho kitamfanya awe mtumwa wa mr Oscar kwenye maisha yake yote.
Wanaume hao walikuwa nyuma ya muda kidogo kitu ambacho kilifanya Tommy aweze kuwawahi kufika ndani ya eneo hilo huenda kama wangemuwahi basi wangefanikiwa kumuua kijana huyo kabla ya Tommy. Tommy baada ya kuingia ndani ya jengo hilo alirusha kifaa kimoja ambacho kilikuwa kama bomu lakini kazi yake ilikuwa ni kutoa moshi ambao ulikuwa ni mwingi sana kitu ambacho kilipelekea mtu kutokuwa na uwezo wa kuona kile ambacho kipo mbele yake.
Mwanaume alivaa mask usoni kwake ili asiweze kuzurika na moshi huo ambao ulikuwa mbele yake, aliingia kwa sarakasi safi sana ambapo buti lake moja lilitua chini na lingine likafuatiwa. Hakuwa na maelezo mengi kila ambaye alikuwa anakutana naye mbele alikuwa anamchinja vibaya sana huku akiwa anapandisha ghorofani ndani ya jumba hilo la kifahari. Aliua walinzi wengi sana kupitia huo moshi mpaka pale ambapo ulianza kupungua ndipo alipokuwa amefika kwenye ghorofa ya juu kabisa ambapo kwa mbele aliona kuna lango kubwa likiwa limefunguliwa kuonyesha wazi kwamba ndani yake kulikuwa kuna mtu anamsubiri.
Baada ya Tommy kufika hilo eneo alikutana na mwanaume mmoja ambaye alikuwa kifua wazi akiwa amempa mgongo mithili ya mtu ambaye alikuwa amezama kwenye ibada nzito sana.
“Sikujua kwamba inaweza kuwa rahisi sana kwa mtu wa kawaida kama wewe kuweza kujua kwamba mimi nipo ndani ya hili eneo lakini inaonekana imekuwa rahisi sana kwako hata kuwaua walinzi ambao wapo nje hapo” ni sauti nzito ya mwanaume huyo ambaye alikuwa bado amekaa hapo chini akiwa amempa mgongo Tommy.
Huyo mwanaume ambaye alikuwa amekaa hapo chini ndiye ambaye alikuwa anaitwa R mwenyewe, huyo ndiye ambaye alikuwa amefanya ukatili wote kwenye familia ya Tommy hususani ule wa kuuawa kwa mdogo wake na kumteka dada yake ambapo aliishia kumbaka kwa namna ambayo ilimfaa yeye. Alinyanyuka taratibu baada ya kuona mtu ambaye alikuwa nyuma yake hakuwa akiongea jambo lolote lile, na ndipo alipo igeuza sura yake. Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwenye maisha yao wanaume hao kuweza kuonana uso kwa uso na ndiyo ambayo ilipaswa kuwa siku ya mwisho ya mmoja kati yao.
Mwanaume huyo mwili wake ulikuwa umekatika sana kwani alikuwa kifua wazi lakini chini alikuwa peku akiwa amevaa traki nyeupe pee huku pembeni yake kukiwa na upanga ambao ulikuwa unang’aa sana.
“Una miaka mingapi?” hilo ndilo lilikuwa swali la kwanza la Tommy kwenda kwa mtu huyo.
“Miaka haina umuhimu wowote ule hapa ndugu yangu zaidi tu ya kuyaokoa maisha yako. Nimesikia umeua vijana wengi sana tena kikatili, nasikia unalia lia kwa sababu ya mimi kufanya mapenzi na yule Malaya dada y……” hakumalizia sentensi yake kwani upanga ulirushwa kwa kasi ya ajabu na kumbaraza kwenye shavu lake baada ya kufanikiwa kuukwepa. Alikuwa anavuka mipaka ya kuongea na wanaume wenzake kauli kama hizo, upanga huko ulienda kujichomeka ukutani.
“Hahahaa hahahaha” alicheka kwa sauti kali sana lakini iliyo jaa kejeli, kisha alijivuta na kujizoa mpaka lile eneo ambalo alikuwepo Tommy, mwanaume huyo alizirusha ngumi zake kwa pamoja ambazo zilitua kwenye kifua cha Tommy na kumzoa mpaka nje ambapo alilazimika kuingia upya tena ndani ya chumba hicho.
R hakuwa mnyonge kabisa kwenye suala zima la urushaji wa ngumu hivyo alikuwa anashambulia kwa kasi sana hali ambayo ilionekana kuanza kumpa wakati mgumu Tommy baada ya kupokea teke la shingo ambalo lilimpeleka chini ila kwa kutumia mkono wake mmoja alijinyoosha vizuri na kuzikunja ngumu zake kwa usahihi ambazo ziliitikia vizuri kabisa. R alizunguka chini kwa mitama mikali lakini alimkosa Tommy hivyo akahitaji kujizungusha ili asimame lakini alikutana na ngumi moja nzito mno ya mdomo ambayo iliufanya mdomo huo upasuke na kuanza kutoa damu kwa wingi.
Alisimama huku akiwa anapiga makelele kwa hasira, alitishia kama anapiga kisha akarudi nyuma na kwenda kwa nguvu akihisi kwamba amempoteza mpinzani wake kumbe yeye ndiye ambaye alikuwa amepotezwa, alidakwa mkono wake ambao ulipokea kiganja kizito akatupwa mbali lakini kwa bahati nzuri wakati anarushwa mbali alikuwa amefanikiwa kuzichomoa bastola kwenye mwili wa Tommy. Kabla hajatua chini aliruhusu bastola hizo kuweza kutoa risasi lakini risasi ambayo ilitoka ilikuwa ni moja tu pekee ambayo ilizama kwenye kifua cha Tommy.
Tommy alipokea maumivu makali sana ya kifuani hali ambayo ilimfanya apige goti lake moja chini na mwanaume huyo akaishia kucheka kwa sauti na dharau sana huku yeye mwenyewe akiwa kwenye hali ambayo haikuwa nzuri. Alizitupa bastola hizo ambazo alihisi kwamba huenda mtu huyo alikuwa amezitumia na risasi ambayo ilikuwa imebakia ilikuwa ni moja tu kisha akauchomoa upanga wake pale chini ambapo alikuwa ameuhifadhi vizuri sana.
Akiwa na upanga wake mkononi alijirusha na kuushusha kwenye bega la Tommy, Tommy ni kama alichelewa kufanya maamuzi kwani upanga ulimbaraza kidogo na kumchana, akiwa bado kwenye mshangao mwanaume huyo aliuzamisha upanga huo kidogo kwenye eneo la kifua cha mwanaume huyo. Ni kama Tommy aliweza kuzinduka kutoka kwenye mshangao baada ya kurusha ngumi kali sana saba ambazo zilitua vyema kwenye mbavu za R.
Ukurasa wa 47 unafika tamati.
Wasalaam,
Febiani Babuya.
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app