Sakata la SKOL: Wafuatao pia wachunguzwe

omusimba

JF-Expert Member
Jul 25, 2012
310
77
Natoa pongezi za dhati Wa viongozi wetu RC DSM na mh. Raisi.

Kuna watu wamesababishia hasara katika miradi ya ujenzi jijini DSM hasa Manispaa ya Kinondoni.

Bila kusita vyombo vya usalama viwahoji wafuatao kutokana mahusiano yasiokuwa ya afya na SKOL:
1. Aliyekuwa meya Wa kinondoni. Huyu kafaidi kila hisani toka SKOL. Sitaki kuingia ndani ila wahusika chukueni hatua.
2. Alikuwa mkuu Wa mkoa Wa dsm kabla ya mwaka 2016. Nendeni pale yard ya SKOL Sinza mtapata kila aina ya msaada aliopata mkuu huyu kama hisani.
3. Mwenyekiti wetu Wa CCM Kinondoni; huyu ametumia Sana ma-landcruiser ya SKOL kwa shughuli binafsi na mpaka za chama.

Katika kuthibitisha hili pitieni mifumo ya CCTV camera pale SKOL kuanzia 2012 mpaka 2016 mtapata ushahidi wa kutosha.
 
Kama imehusishwa na Chama....hakuna mashitaka hapo!

JPM ameshajua kuwa hata vikao vya juu vya chama vinaendeshwa na wafanya biashara kwa kilipwa tender kubwa kubwa na favor za kodi!

Ameshajua nchi hii inavyoendeshwa nadhani kuanzia sasa hatashangaa tena! Maana ameona CCM walivyohaha kupata hizo 2Bil za Mkutano Mkuu! Ameona alivyojishusha na kukopa kwa ajili kujazilizia mapato mwezi May.....sasa akili imemjia!

Nchi hii sio tajiri kama alivyokuwa anadhani,!!! Ina changamoto lukuki wafadhili wakisusa weke tu tutachapana! Madawa Chanjo ARV TB etc! Sasa bakuli lazima likatembezwe ili najeti iweze balance! La sivyo aibu!! Hapo hakuna hata kiwanda kimoja.....kinachofikiriwa!!

Ajipange kuwapa favor kubwa wawekezaji na assurance kuwekeza viwanda kila kanda kutokana na study!! Asigombane na wafanya biashara wa ndani......awakumbatie watamsaidia!!!
 
Nasikia huyo Skol kuna barabara nyingi tu kajenga huko jiijini Dar na ziko vyema ila za Halmashauri hakuna kitu.

Niliambiwa kwamba kaongezea barabara ya Nyerere kipande cha airport kwenda Mombasa na ipo vyema
 
SKOL wako vizuri sana. Katika construction industry, performance yao ni outstanding hapa mjini
 
Wale Wahaya ni viburi sana ngoja watumbuliwe tu. Wamekuwa wakisema hakuna mtu anayeweza kuzuia mipango yao hata miovu kuanzia Ikulu hadi barabarani.
 
Kama imehusishwa na Chama....hakuna mashitaka hapo!

JPM ameshajua kuwa hata vikao vya juu vya chama vinaendeshwa na wafanya biashara kwa kilipwa tender kubwa kubwa na favor za kodi!

Ameshajua nchi hii inavyoendeshwa nadhani kuanzia sasa hatashangaa tena! Maana ameona CCM walivyohaha kupata hizo 2Bil za Mkutano Mkuu! Ameona alivyojishusha na kukopa kwa ajili kujazilizia mapato mwezi May.....sasa akili imemjia!

Nchi hii sio tajiri kama alivyokuwa anadhani,!!! Ina changamoto lukuki wafadhili wakisusa weke tu tutachapana! Madawa Chanjo ARV TB etc! Sasa bakuli lazima likatembezwe ili najeti iweze balance! La sivyo aibu!! Hapo hakuna hata kiwanda kimoja.....kinachofikiriwa!!

Ajipange kuwapa favor kubwa wawekezaji na assurance kuwekeza viwanda kila kanda kutokana na study!! Asigombane na wafanya biashara wa ndani......awakumbatie watamsaidia!!!
Ha haha !!!
 
SKOL wako vizuri sana kama kuna barabara wamejenga chini ya kiwango wa kulaumiwa ni Serikali yenyewe pamoja na macolsutant wake, maana wao ndiyo wakaguzi kwa kila process na designer wanotoa specifications ambazo skol anapaswa kuzifuata
 
Barabara nyingi za halimashauri ziko chini ya kiwango, nadhani kuna shida Katika usimamizi wa mikataba au je matumizi ya barabara sio sahihi? Je kama defect realabilty period imeisha baada ya mwaka mmoja barabara inaharibika nani anawajibika? Ni nani anadhibiti malori yenye uzito mkubwa kupita kwenye hizo barabara?
 
Bara bara za halmashauri zilijengwa kwa kuwekwa layer moja ya lami badala ya layer mbili. Ikiwa halmashauri yenyewe ilitaka hivyo ili kupunguza gharama za mradi, then wa kulaumiwa ni wao wenyewe... na sio wakandarasi.
Hapa kuna case to case,kuna ambazo zimejengwa chini ya kiwango mfano ile ya tabata St Mary's ile iliharibika hata kabla ya miezi sita,hapo tatizo sio design.
 
Kuifungia kampuni ya ujenzi sio tatizo, lakini ni nani mwenye mamlaka hayo?
Kama kulikuwepo na ujenzi chini ya kiwango wakina nani hasa walisababisha?
Na ikithibitika pasipo shaka kuwa wanasiasa au yoyote yule kwa nafasi yake alihujumu au kufanya fojali yoyote basi vyombo vinavyohusika (CRB,Takukuru,ERB na Mahakama) wawajibishe wahusika kwa mujibu wa nafasi na viapo vyao.
Ni vyema mleta mada kwa kuanzia uisaidie Polisi katika hatua za awali ili kazi iwe rahisi.
 
SKOL aliingia Dsm na kuanza kazi vixuri.
Tatizo ni kuanza kushirikiana na wanasiasa kupata kazi.
Wanasiasa ni hatari kushitikiana nso kwa karibu sana.
Watasaidia lakini "cha juu" watataka mapema, achilia mbali watendaji waliotoa kazi.
Mwisho wa siku kazi mbovu na hakuna wa kukemea.
Tumpe pole tu Skol , he has learned the hard way.
 
Kuna watu kama huna Mungu unaweza panga mengine yasiyoandikika. Hakuna uchungu na nchi kabisa...anyways i hope wote waliokula haramu wajumlishwe pia...muda wa kuisoma namba ni sasa.
 
Natoa pongezi za dhati Wa viongozi wetu RC DSM na mh. Raisi.

Kuna watu wamesababishia hasara katika miradi ya ujenzi jijini DSM hasa Manispaa ya Kinondoni.

Bila kusita vyombo vya usalama viwahoji wafuatao kutokana mahusiano yasiokuwa ya afya na SKOL:
1. Aliyekuwa meya Wa kinondoni. Huyu kafaidi kila hisani toka SKOL. Sitaki kuingia ndani ila wahusika chukueni hatua.
2. Alikuwa mkuu Wa mkoa Wa dsm kabla ya mwaka 2016. Nendeni pale yard ya SKOL Sinza mtapata kila aina ya msaada aliopata mkuu huyu kama hisani.
3. Mwenyekiti wetu Wa CCM Kinondoni; huyu ametumia Sana ma-landcruiser ya SKOL kwa shughuli binafsi na mpaka za chama.

Katika kuthibitisha hili pitieni mifumo ya CCTV camera pale SKOL kuanzia 2012 mpaka 2016 mtapata ushahidi wa kutosha.
Mkuu unaka Uchunguzi utumie camera za Skol? utapata matokeo gani sasa
 
Wale Wahaya ni viburi sana ngoja watumbuliwe tu. Wamekuwa wakisema hakuna mtu anayeweza kuzuia mipango yao hata miovu kuanzia Ikulu hadi barabarani.
Kusema kweli nakwazika na watu wenye kupenda kutamka maswala ya makabila katika kila maongezi. Unamaanisha mleta uzi hakujua kama hawa ni wahaya ama basi tu kirusi kishaushambulia sana ubongo wako kiasi hiki? yawezekana pia labda kwenu mnafundishwa kuhusu wahaya tu hapa duniani ...hebu tutajie na wewe kabila lako ili tuone kama huko kwenu ni malaika tu.
 
Back
Top Bottom