Sakata la Rushwa ya Askofu.DR.Mokiwa lachukua sura mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Rushwa ya Askofu.DR.Mokiwa lachukua sura mpya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lu-ma-ga, Oct 18, 2010.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Nawaomba taarifa hii muifikishe kwa wote wapenda mabadiliko kwa haraka
  Jana nilipata taarifa kuwa baada ya mpango wa kumpatia Askofu Mokiwa Tshs.11milioni ili asaidie chama Fulani kuwashawishi waumini wake kushindikana, Chama hicho hakijakata tama kuitumia karata hiyo.

  Kuna taarifa kuwa kuna mpango unaendelea kuandaliwa wa kujaribu kuwapatia baadhi ya MAASKOFU wa madhehebu ya kikristu makubwa, mfano RC, KKKT, FGC n.k kiasi kikubwa cha fedha ili katika muda wa wiki mbili kuanzia leo wajaribu kuwashawishi waumini wake ili wakipigie kura chama hicho.

  Taarifa hizi ni za uhakika na tusipoteze muda kuuliza source of information, kwani jaribio la kumhonga askofu tayari lilishafanyika japo halikufanikiwa.Ili kutekeleza mpango huu chama hicho kinatumia kikosi chake cha kampeni kwa kuwatumia wazee wa makanisa hayo ili wapate urahisi wa kuwaingia maaskofu hao.Maeneo ambayo yamewekewa umuhimu ni kanda ya Ziwa, Kanda nyanda za juu kusini ambako kuna madhehebu mengi ya kikristu ambako pia kuna idadi kubwa ya wapiga kura na upepo wa mabadiliko unavuma kwa kasi.

  Mtoa habari alinidokeza kuwa kuna ubishani katika hiyo kamati ya kampeni ni kwamba uwezekano wa kutofanikiwa mbinu hiyo chafu kwani misimamo ya maaskofu imekuwa kinyume sana na rushwa ila wanataka wajaribu Zari kwani mbinu zao nyingi inaonekana zinagonga mwamba.Inaonekana swala la kuiba kura limedhibitiwa sana mwaka huu, na hivyo kwao wanaona linaweza lisisaidie , wanataka kujaribu mbinu nyingi kadri iwezekanavyo.

  Lakini pia alidokeza kuwa inawezekana wajanja ndani ya chama hicho wanaanza kubuni namna ya kuzichukua pesa kwani mwaka huu imekuwa vigumu kuchukua kwa kuwa fungu linadhibitiwa na watu wa karibu wa mgombea.

  Nawaomba mfikishe taarifa hizi kwa chadema na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania na pia maaskofu wapewe taarifa hizi ili wajue nini kinawanyemelea.
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  CCM kubalini yaishe HAMTAKIWI TENA, JK usiingize nchi kwenye uhasama kwa kutaka kwako kutawala kinyume cha ridhaa,mbona ukiondoka kwa amani utabakia kuwa na heshima yako kama ris mstaafu,usitafute makubwa ukaondoka kwa aibu, usiwasikilize wapambe, sikia sauti ya wengi,ambayo ni sauti ya Mungu, wewe umechacha hufai tena kuongoza.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  DHAMBI hiyo!!!
   
 4. Kesa

  Kesa Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninampongeza Askofu Mokiwa kwa ujasiri na kusimamia wito wake wa KITUME kwa Ujasiri na kuonyesha kwamba hata kama alichaguliwa kwa kura kuwa Askofu lakini Yule anaye mtumikia ana mamlaka KUU kuliko mamlaka zote za hapa duniani. Ni heri kufa kuliko kuli aibisha jina la Kristo. Huu ni U Mafia. Hawa watu hawana nia njema kabisa na taifa hili. Ndio maana hata ahadi wanazotoa hazina mantiki wantufanya sisi wote kam watoto wailioko darasa la awali!! Ni walfi, laghai, tapeli, whauni kama alivyozoea kuwaita Baba wa Taifa
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Taarifa hizi ni za uhakika na tusipoteze muda kuuliza source of information,

  KAMA SIO MWITA CHACHA BASI MARWA

  DUH UTAKI WAKUULIZE KABISA HUKU WAKO WENGI NDUGU KILA ANAEANDIKA ANATAKA USHAHDI ....HAYA HABARI NJEMA
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Wacheze na kitu chochote, siyo RC.

  Kwanza kabla hawajafanya huo upuuzi wao, waulize Kwa nini Askofu Kilaini alihamishwa kutoka ST. Joseph na kupelekwa Bukoba? Wakipata jibu la swali hilo kwa ufasaha, hakika hawatathubutu kutoa rushwa kwa Kanisa Katoliki. Wataaibika.
   
 7. M

  Mwanaume Senior Member

  #7
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Naungana na mtoa habari. Wapenda mabadiliko fuatilieni hili jambo. Kuna habari za uhakika kwamba watu hao pia wana mpango wa kuanza ratiba ya kuhonga wapiga kura kuanzia tarehe 27
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kuna mtu jana alinidokeza kuwa kulikuwa na mkutano mkubwa pale Arusha (Burka karibu na TANAPA makao makuu) wa madhehebu yote kuiuombea uchanguzi uwe wa amani pili likuwa ni kupanga na kuunda kamati ya kuelimisha waumini kuhusu upigaji kura (yaani waumini wachangu mtu anae mwogopa mungu, kiongozi ambae siyo fisadi) tatu kuangalia kama wana weza wakafanya misa 2 badala ya nne au zaidi kama wanavyo fanya wiki zingi na wakati huo huo kufupisha angalau watumie saa moja kila misa hasa ikiwa ni kuhakikisha kila mwenye haki ya kupiga kura anapata haki hiyo lakini sikupata nafasi ya kufika kwenye mkutano huo...kwa mikakati hiyo sidhani kama madhebu yatakubali kudanganyika au wamechele mbinu zao hizo chafu....
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  siyo kuanzia tarehe 27...tabia hiyo ipo hapa arusha, ukikutwa na kadi ya kupigia kura unapewa kuazia 5000 mpaka 30000 sijajua wanatumia vigezo gani yaani yupi apewe 5000,10000,15000 ....na wakati kampeni za nyumba kwa nyumba zinazofanywa na CCM wana toa sukali, unga na nk...
   
 10. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Nawashauri wazichukue wakawasaidie wenye uhitaji
   
 11. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 80
  Gooooooooo Dr. Slaa goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
   
Loading...