Wengine huwa hatukurupuki tunapoandika humu. Aliyetoa kauli kwamba pesa zilizokusanywa ni 215 million ni Gambo. Sasa kama huo si ukweli aliyesema uongo ni Gambo. Acha kukurupuka.
RAMBIRAMBI
Katika hatua nyingine, zaidi ya Sh milioni 200 zimepatikana kutoka kwa wadau mbalimbali wanaoendelea kuchangia rambirambi kwa familia za wanafunzi hao wa
Shule ya Lucky Vincent waliopoteza maisha kwenye ajali ya basi iliyotokea wiki iliyopita.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alisema hadi sasa wamepokea kiasi cha Sh milioni 215 kutoka kwa wadau mbalimbali, ikiwamo Bunge la Tanzania.
Gambo aliwataja wadau wengine kuwa ni Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Wizara ya Elimu Zanzibar, mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii pamoja na wadau wengine.
Alisema hadi sasa zaidi ya Sh milioni 190 zimetumika, ikiwamo Sh 3,850,000 kwa familia 32 zilizopoteza watoto wao katika ajali hiyo, gharama za mazishi, ikiwamo magari na usafiri kwa ajili ya maziko yaliyofanyika katika mikoa ya Arusha, Iringa, Tanga, Mbeya na Kilimanjaro.