Sakata la PhD Feki: Dkt. Makongoro Mahanga akamatwa kwa amri ya Mahakama Kuu, afikishwa kortini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Makongoro Mahanga leo amekamatwa na Polisi kwa amri ya Mahakama Kuu Dar na kufikishwa mahakamani.

================================================================

Dar es Salaam. Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani.

Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14 milioni.

Fedha hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”.

Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi.

Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.

Chanzo: Mwananchi
 
Mungu wangu, milioni 14, kwani hicho kitabu chenyewe kiliingiza shilingi ngapi?
Kipindi wanatajwa mafisadi wa elimu tulishangilia kwelikweli ....lakini baada ya wengine kuhamia chama chetu hii issue ikajifia ndio maana hata hatukumbuki kwamba shujaa wetu alishinda kesi ....siasa za Bongo ....tegemea mashabiki waseme Chadema yupo mmoja waliobaki bado wapo CCM ....jibu rahisi tu ..
 
Wote hawa si wanachadema? Msemakweli aonyeshe ukamanda kwa kumsamehe Kamanda mwenzake. Kwa nini wazalilishane wakati wote watoto wa chama kimoja?
 
Back
Top Bottom