Sitashangaa sana kama Nape atapitishwa na NEC, watu wengi ndani ya CCM wameanza kuamka na sidhani kama wataona uvivu kotofautiana na Nchimbi. Ningeomba tutumie hii thread kuwajadili hao waliopitishwa na Nchimbi na team yake, apart from Zainab- who are they?
Nafikiri haya maneno ya Nape, yako very clear au ni mimi peke yangu ninayaona tofauti, kwamba ni NEC peke yake ndiyo wenye huu uamuzi na sio Nchimbi na kamati zake, au?
Kana-Ka-Nsungu, umepatia maana hata hii story imepelekwa na Nchimbi huko Mwananchi kupitia kwa mwandishi mmoja mkubwa ambaye hata hivyo sasa anaondoka hapo Mwananchi, ambaye alimpa kijana wake, aliyeandika.
Hao akina Nchimbi hawana uamuzi wa mwisho lakini ndio wanaoanza kusambaza sumu na wameshaianza kazi hiyo. hapo anatakiwa mtu makini wa kujenga hoja katika vikao vya juu kumuokoa nape, la sivyo, ameshakwenda huyo
Said Mtanda ni kijana wa Jk kabsa..amekulia mikononi mwa JK akiwa bagamoyo...hadi akaingia chuo kikuuu akasomea sociology akiwa intake moja na Ridwani....amekua ndani ya chama sababu anajua lililokuwa linakuja....akagombea Mwenyekiti Vijana bagamoyo then mkoa wa Pwani....akawa mjumbe wa vikao vya UV CCM......alikuwa miongoni wa wapiga dembe wa mjoba wake--JK...mpo??sasa ni msaidizi maalumu wa mzee makamba na yeye ndio mwandishi habari wa
Makamba...anandaliwa kuja kupewa kazi nzito nzito kwa sasa anapikwa...kumbukeni JK alipopitaa nae alikaa sana kwenye chama kama vile hayupo.......
Kazi iliyopo kwa Ridhwani atampigia nani debe?Said Mtanda au Beno?
huwa mara nyingi sana namsikia Makamba akitaka kutishia mtu yeyote huwa anasema"wenye chama hawataki............'"nani mwenye chama????hata Nape nae alimwambia same words....
Makamba always anasikiliza JK anataka nini sio matakwa ya chama....subirini mtaona kabla JK hajatoka....kina Said na wengineo wengi tuu watawekwa sehemu nzuri nzuri....ili kulipa fadhilaa kwa madai wameiva kwenye chama na ni waamini kwa chama.........
Tatizo lipo kwa watu wa ina ya NCHIMBI,watu wanaoaminika walichangia ushindi wa Mkulu,hapa kuna tatizo sababu moja kubwa kama mkuu akiwaaca watamziria nchi na ndiyo maana mkuu wa nchi yuko makini sana.kuna madhara kama Nchimbi akipuuzwa ila atakchofanya ni kutumia wazee kuamua hili ili asionekane yeye anampendekeza nani.
Hapa ndipo ninapoona utawala wa nchi umefikishwa pabaya. Kwa nini uongozi wa nchi unawekwa rehani kiasi hiki? Kwa nini watu binafsi wawe wanashikilia sehemu ya uwezo wa kufanya maamuzi?
Kwani ridwan yeye hagombei uvccm? mbona nilisikia na yeye anagombea? au ameghairi kuwaachia watoto wa wakulima?
Na je, nafaham Ridhwan alitangaza kuwa anamsupport Benno, Je na huyu Said Mtanda ambaye ni Mwenyekiti wake wa Uvccm wilayani kwake bagamoyo, pia ni mjumbe wa baraza kuu la taifa kutoka mkoani kwake, na pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya mkoa wake, atamtosa?
au tuseme ndio aliteleza kuwa kimbele mbele kushabikia asichokijua kitakachotokea? ndio mwisho mbaya anaouchungulia?
Watu juu mnauliza Said Ni nani kwa sababu gani,yaani kugombea lazima uwe flani?
Mpita njia,
Tatizo ni kwamba ,haiwezekani ukatoka bila kuwa na mtu na hii imani imejengeka sana na inaharibu kila kitu.Mkapa aliweza hili ila Jk alikuwa na kundi kubwa sana na kuwalipa wote itachukua muda sana.
Mie nafikiri tupate watu wenye mawazo kama Mzee Mwanakijiji,wenye upeo kama Mchungaji kishoka then tuwapendekeze wagombee uongozi.
kwani wakikusaidia na ukawatosa watakufanya nini?ishu inakuja kuwa kwenye System.Je wataendelea kuwa na wewe?hivi mnamkumbuka John Githongo?we need watu kama huyu
Mzee Mwanakijiji for Tarime 12th October 2008
kaka sera yangu ni jino kwa jino na panga kwa panga...ukiona mahali nimeng"ata basi ujue nami nimetendwa the same......Nape amekwisha siku nyingi niliwaambia hivyo....acheni ndoto za asubuhi hapa.Kamati za vijana ambazo wewe unaziita kwa kejeli kuwa ni kamati za Nchimbi{najua chuki zako kwa Nchimbi}zinapeleka mapendekezo yenye uzito unaostahili kwenye kamati kuu.Na zinatakiwa kupunguza majina mpaka yabaki machache kwa uamuzi wa mwisho....Nakwambia Nape hana ujanja wa kucheza ngoma hii ata kama atapitishwa.Nafikiri haya maneno ya Nape, yako very clear au ni mimi peke yangu ninayaona tofauti, kwamba ni NEC peke yake ndiyo wenye huu uamuzi na sio Nchimbi na kamati zake, au?
Hayo ya Nape tuliyategemea ila wasim-ipyana tu. Nchimbi siku yake inakuja subirini tu.
kama mnataka kumsaidia Nape Mwandosya mmechelewa kwa kuwa Nape hajakatwa na Mtu bali amekatwa na kanuni ambayo imemfikisha kikomo cha umri na umri ni ukuta,sasa kujaribu kudai ni Nchimbi ndio kamkata ni kusingizia kusiko na kikomo kwa kuwa kikao kilicho mkata sicho kilichopitisha hio kanuni,Sitashangaa sana kama Nape atapitishwa na NEC, watu wengi ndani ya CCM wameanza kuamka na sidhani kama wataona uvivu kotofautiana na Nchimbi. Ningeomba tutumie hii thread kuwajadili hao waliopitishwa na Nchimbi na team yake, apart from Zainab- who are they?