Sakata la mitumba: Marekani yaiwekea vikwazo Rwanda. Tanzania, Kenya na Uganda kufuata

Uzuri mmoja najua biashara ya nguo. Mitumba mingi ya Tz inatoka UK. Nguo nyingi ni za Primark,Newlook,H&M,SprtsDirect,GeorgeAsda na Tesco. Hizo nguo nyingi ni £5-15 tena chini zaidi kukiwa na Sale.
Sasa kama nguo inauzwa £5 UK ambapo muuza duka kwa saa analipwa £7 itashindwa kuuzwa Tz kwa 10,000 au chini ya hapo?
Sasa hizi zinazouzwa Kariakoo mnasema za quality ya chini bei ya jumla Kariakoo ni 15,000 hivi Kinondoni na Sinza zinauzwa 20-25k =approx £10. Kuuza nguo quality from China inawezekana tatizo wafanyabiashara wetu hawajanyooka feki wanauza bei ya kawaida tu.

Sijui biashara ya mitumba. Ila pengine kuna sababu wafanyabiashara wanakwepa kununua hizo nguo bora!! Na zaidi ya H&M sijui kama hizo stores zingine zipo China.

Ila chifu, unaongelea nguo za 15,000 hadi 25,000; hizi ni middle class ndiyo wanaweza kuzi-afford. Watu wetu hapa nimaanisha hao peasants walio wengi vijijini. Ambao wanavaa nguo za mitumba za buku buku, au jezi za michezo feki kutoka China, za buku buku pia.
 
Sio dampo man, binafsi mitumba inanioko sana nkiwa na ten navaa juu mpaka chini coz io ten nkigusa shop tu itabidi niongeze ten nyingine kununua shat tu, wakati huohuo sisi viwanda tunavolinda ni vipi manaake sijaona viwanda vya pamba apa bongo zaidi ya vile vinavosokota kanga na matenge, itafika day nchi nzima tunagonga kanga moko tu na shuka la mmasai manaake pamba yenyewe naskia uko kanda ya ziwa wanasuasua kulima
utakuwa hujui tu dar hapa kuna kiwanda kinatengeneza jeans zinauzwa marekani na uingereza
 
90% tumelelewa na mitumba kama unabisha muulize mama yako.unapofungia uwe natakwimu familia ngapi zinazotegemea mitumba,kama haujakuta 79% kwanjia moja au nyingine zinaenda chooni kwakutegemea mitumba
 
Hao Chadema wameisha pewa pesa na Trump watukane Rais wetu sababu ya kukataza mitumba
Vita vya kiuchumi ni vikubwa , Magufuri tukuombee sana maana wataweka vikwazo sababu tumekataza michupi iliyo isha valiwa na hawa majambazi kuletwa kwetu

Faza Chadema wanahusikaje hapa?
 
siyo hoja hata kama ningekuwa nimevaa mtumba lakini si sababu ya mimi kukubaliana na upuuzi huu wa wamarekani. tunahitaji kuwa na viwanda vya nguo kutosheleza soko la ndani na nchi jirani. usione ndoto kuwa na viwanda vya nguo ni kuwa na maamuzi tu na uthubutu. kaza baba magufuli na marais wengine wa east africa
mkataba wa AGOA umekuruhusu kuuza bidhaa US kutoka TZ tena baadhi ya bidhaa hizo hazitotozwa ushuru ila kwa kuwa viongozi wako hawakukupa elimu kuhusu mkataba huo, we unaona viwanda vyetu haviendelei kwa sababu ya mkataba huo., hebu jiulize ni wafugaji wangapi wa nyuki wanaojua chochote kuhusu AGOA?.
 
Sijui biashara ya mitumba. Ila pengine kuna sababu wafanyabiashara wanakwepa kununua hizo nguo bora!! Na zaidi ya H&M sijui kama hizo stores zingine zipo China.

Ila chifu, unaongelea nguo za 15,000 hadi 25,000; hizi ni middle class ndiyo wanaweza kuzi-afford. Watu wetu hapa nimaanisha hao peasants walio wengi vijijini. Ambao wanavaa nguo za mitumba za buku buku, au jezi za michezo feki kutoka China, za buku buku pia.
Maximum profit ndio sababu pekee. Hizo za 15,000/20,000 kukiwa na big retailers zitauzwa hadi 3000-10,000. Itafika hatua tutakuwa na mitumba from within hao wa vijijini watavaa hio mitumba ya humu humu. Ila hio ni gradual process sio kupiga marufuku abraptly. Mfano wangeweka sharti kuwa mitumba ni GRADE ONE coz hata huko US/UK watu wanavaa mitumba.
 
Merekani hawana aibui Basi na sisi tuwe tunawauzia mitumba!! Tukivaa nguo zetu tuwe tunazikusanya zile kukuu tuwauzie ikiwa ni pamoja na soksi!!!!
 
siyo hoja hata kama ningekuwa nimevaa mtumba lakini si sababu ya mimi kukubaliana na upuuzi huu wa wamarekani. tunahitaji kuwa na viwanda vya nguo kutosheleza soko la ndani na nchi jirani. usione ndoto kuwa na viwanda vya nguo ni kuwa na maamuzi tu na uthubutu. kaza baba magufuli na marais wengine wa east africa
Hizo nguo bei yake itakuwa sawa na ya mitumba???
 
Akitukanwa poa tu. Maana tukimtukana sisi mtatupoteza.
Hao Chadema wameisha pewa pesa na Trump watukane Rais wetu sababu ya kukataza mitumba
Vita vya kiuchumi ni vikubwa , Magufuri tukuombee sana maana wataweka vikwazo sababu tumekataza michupi iliyo isha valiwa na hawa majambazi kuletwa kwetu
 
Naongeza kipato kwa biashara ya mitumba,
Let say Tanzania inazuia mitumba ina viwanda vingap vya nguo?Maama Rwanda sijafika.
Au ndo tunamtegemea MCHINA?
 
Kuna watu wanashabikia kuzuiwa kwa mitumba huku nawaona wamevaa mituba kuanzia saa ya mkononi hadi kiatu. Wewe kaa kimya mnufaika wa mitumba. Ngoja ikatazwe hapo ttaheshimia. Nilichokuwa na dhani kingekuwa sihihi ni uvaaji wa nguo za ndani ambazo ni mitumba ndio ungepigwa marufuku
 
000_11l7d2_0.jpg


Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuiwekea vikwazo vya kibiashara na kuondoa msamaha wa kodi kwa nchi ya Rwanda siku chache tu baada ya nchi hiyo kuzuia kuagizwa kwa mitumba kutoka nchini Marekani.

Hata hivyo wawakilishi wa biashara wa Marekani wanasema kuwa nchi za Kenya, Tanzania na Uganda na zenyewe zitakabiliwa na hatua kama hizi baada ya mataifa hayo nayo kutangaza kuzuia uagizwaji wa mitumba.

Vikwazo hivi vya Marekani kwa Rwanda vinatarajiwa kuanza kutekelezwa ndani ya siku 60.

Nchi nyingi za Afrika zilikuwa zimetiliana saini na Marekani chini ya makubaliano ya AGOA ya ubadilishanaji wa bidhaa na huduma na baadhi kutotozwa kodi, lakini hivi karibu nchi za Aftika mashariki zilitangaza kusitisha uingizwaji wa mitumba kutoka Marekani.

Nchi za Afrika Mashariki mwaka 2016 zilidai kuwa zitasitisha uagizwaji wa nguo za mitumba na viatu ifikapo mwaka 2019 ili kulinda viwanda vyao vya ndani.

Hata hivyo mwezi Machi mwaka jana, shirikisho la viwanda nchini Marekani lililalamika kwa Serikali likidai kuwa zuio hili la nchi za Afrika Mashariki litaathiri viwanda vya marekani.

Shirikisho hilo limedai kuwa ajira zaidi ya laki 4 za raia wa Marekani ziko hatarini kutokana na tangazo hilo la nchi za Afrika.

Shirikisho hilo limedai pia kitendo cha nchi za Afrika Mashariki kinaenda kinyume na makubaliano ya mkataba wa AGOA unaolenga kuhamasiaha biashara na nchi za kusini mwa jangwa la Sahara kupitia soko huru la Marekani.

Source: Radio France Internationale - RFI

Duh, ni kiwanda gani cha Marekani kitakachokosa biashara wabongo wakiacha kuvaa mitumba?
 
Viwanda alivyoacha Nyerere mmeua vyote halafu mnasingizia wazungu?
Aisee,acheni masihara
Mawaziri kabisa eti tena wasomi walishindwa kusimamia viwanda vikue wakasimamia vife leo mwasingizie wazungu,kwani mlishikiwa mtutu?
 
Back
Top Bottom