Sakata la Mauaji ya polisi Arusha: Makinda kamdhalilisha waziri mkuu Pinda!!

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema aliingia matatani baada ya kuomba muongozo kwa spika akitaka aelezwa ni hatua zipi zinaweza kuchukuliwa endapo itabainika waziri mkuu analidaganya bunge na taifa? Baada ya kauli hiyo spika wa bunge anna makinda kutokana na ama ubabe wake au uelewa wake mdogo wa hoja akamtaka mh. Lema athibitishe bungeni kauli yake kwamba pinda kadanganya au vinginevo afute kauli yake. Baadaye baada ya kushauriwa na watu makini akaona waziri mkuu atadhalilika endapo lema atawasilisha ushahidi wake bungeni hivyo akamwambia lema apeleke ushahidi wake kwa maandishi. Wengi tulitegemea makinda angetoa hukumu kwa lema kwa kumdhalilisha waziri mkuu au angeuambia umma kwamba ushahidi unaonesha kweli pinda alidanganya.bunge na taifa. Nilisoma baadhi ya ushahidi wa lema kwenye gazeti la raia mwema ambao kwa kiasi kikubwa pinda alidanganya. Kwanza pinda alisema watanzania watatu walipoteza maisha wakati ukweli ni watanzania 2 na mkenya mmoja. Pili pinda anasema mauaji yalitokea takribani mita 500 kutoka kituo cha polisi wakati ushahidi unaonesha wengine waliuawa umbali wa kilomita tatu kutoka kituo cha polisi. Pinda pia alisema chadema wasiweza kushinda uchaguzi wa umeya kwa kua walikua na madiwani 14 na ccm wana madiwani 16. Kwanza kura zinapigwa kwa siri ukizingatia mgawanyiko uliokuwepo ndani ya ccm mkoa wa arusha ni wazi madiwani wengine wangeasi, pili chadema walishinda hai wakati walikua na madiwani wachache kuliko ccm. Hayo ni machache tu mengi anayo lema mwenyewe..
 
Kwanza mengi wanayo wananchi wa arusha wenyewe,lakini kubwa na la msingi pinda amepoteza uhalali wa kuongoza,sio kiongozi na lazima awajibike a
 
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Wataendelea kuumbuana wakati wanaekelekea kwenye anguko kuu..
 
inasikitisha sana kuona ni jinsi gani serikali inashindwa kua makini hasa katika maslahi yanayowagusa wengi, nilishangaa sana baada ya kusuikia kutoka bbc kua serikali imeomba kesi inayo wahusu viongozi wa chadema iharishwe huku wakiendelea kukusanya ushahidi, je ushahidi gani? wakati mambo yapo bayana na watu walichukua video na picha mbalimbali? mi nadhani hapo kuna njama zinafanywa ili kuhujumu ukweli.
 
mnafiki mkubwa huyo mtoto wa mkulima aliegeuka kua fisadi, hana lolote kinachomliza ni ulafi wake wa madaraka.
 
Back
Top Bottom