figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,719
- 55,830
Heshima kwenu Wakuu,
Leo kuna mkutano wa Wandishi wa habari unafanyika magomeni. Kubwa katika yote ni kuelezea Sakata la Mchanga. Nimepata habari ikisema, "baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini ambao ni wamiliki wa makonteina yanayodaiwa kukamatwa bandarini, watakuwa na Press Conference leo Saa 5:30 asubuhi hii Hoteli ya Travatine Magomeni.
Wanaomba waandishi wa Habari na Wapigapicha. Good morning once again"
Ntawaletea kinachojiri kutoka hapa Magomeni. Nshafika sehemu ya Tukio.
Karibuni.
=========
UPDATES:
=========
1130HRS: Wanahabari wameshafika Sehemu ya tukio, ila wahusika bado hawajaonekana
1200HRS: Wahusika wameshawasili eneo la tukio
Wanaanza kujitambulisha kuna Rweyemamu Kente ni msafirishaji na mchimbaji
pia kuna Laurent Matemu mdau katika madini, Salum Nassoro, Mohamed Mkwayu ni mchimbaji paul ndo wameongezana naye
Rweyemamu Kante anaongea:
Sisi ni wachimbaji wadogo, makontena yetu yamezuiwa Mkuba, tumekuja kupaza sauti rais aelewe, ingawa wakubwa wamezuiwa, tunataka ieleweke kwamba na sisi wachimbaji wadogo tumeathirika
Mimi nimeathirika kutokana na zuio sababu Kontena 13 zimezuiliwa Mkuba ICD
Madini yapo sehemu nyingi, mimi ni mchimbaji na msafirishaji, migodi ambayo tupo nayo na vibali tunavyo vya wachimbaji wadogowadogo, migodi yetu sisi ni ya copper sio dhahabu
Tatizo la Tanzania ni kwamba deposit ya copper ni ndogo, migodi yetu sisi ni ya shaba, ukiseme uweke mitambo ya kuyeyusha, hauwezi kwani hatuna madini ya kutosha
Hili zuio lilikuwa linalenga wachimbaji wakubwa lakini watu wa Serikali wametuunganisha na sisi.
Sisi kwa mwezi tunapata Contena tano au sita, sisi ni wamachinga katika sekta ya Madini kama walivyo wa kariakoo, hivyo tunamuomba rais atuwekee mazingira rafiki.
Mohamed Mkwayu mchimbaji wa shaba Mpwapwa. Anasema:
Tunampongeza rais kwa hatua anazozichukua, tatizo la kutokusafirisha mchanga wameunganisha na sisi, sisi tuna kiwanda nchini cha kuongeza thamani. Baada ya hapo ndo tunasafirisha. Hata sisi tumezuiwa
Sisi tulikuwa tunachimba copper, hatupo kwenye dhahabu, hili swala tunaomba watu wa Wizara washughulikie, tulikuwa tunalipia baada ya mchanga wetu kupimwa ndo tunasafirisha
Rais aangalie kwa kina hili swala. Wenzetu wa dhahabu wanaendelea na kuandaa dhahabu yao, lakini sisi tumeshindwa sababu ni wachimbaji wadogo, kikubwa tunampongeza rais, sisi ni wachimbaji wa hapahapa nchini.
Paul kalyembe mchimbaji wa Zinc na Copper anasema:
Sisi tumekata leseni ya kuchimba na kuuza. Sisi hatuhusiki na dhahabu
Hatuna uwezo wa kuchimba na kuweka kiwanda cha kuyeyusha madini, sisi ni machinga.
Kwa kutumia waandishi wa habari, tunaomba mtusaidie kufikishia rais hili swala kwamba atuonee huruma sisi wachimbaji wadogo wadogo ili tuendelee na kazi zetu
Tunachohitaji kutoka kwa rais ni
1. Atuondolee zuio la kusafirisha madini yetu, bado tuna madini ambayo bado yapo kwenye utafiti kama Nickel, mlezi wetu ni stamico, tunafanya kwa uangalizi wake.
2. Sisi tunatozwa storage bandarini japo serikali ndo imezuia Makontena. Kila siku tunatozwa dollar 20 kwa siku pale Mkuba
*Kotena ambazo zimeshikiliwa ni 60 nickel na 7 copper, nikisimamisha mgodi siku moja napata hasara ya millioni nne, toka wametangaza mwezi umeisha. Hivyo unaweza kujua kiasi gani cha hasara tumepata.
Baadhi ya Wachimbaji walioongea na Waandishi ni;
Mohamed Mkwayu - Mcimbaji wa Madini ya aina ya Shaba Mpwapwa, Mmiliki wa Migodi na Msafirishaji wa Mchanga.
King Selemani - Mnunuzi wa Madini ya Metal
Paul Obed Kalyembe - Mchimbaji wa madini ya Shaba.
Thobias weyemamu - Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo wa Madini ya Metalic