Sakata la Makontena: Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally amnyooshea kidole Makonda kwa ubinafsi. Amuonya kutoita wakazi wa Dar "Wananchi wangu"

hahahahahaaaa...wameanza kumtolea uvivu...kumbe wamemvumilia sana
 
Who will stand with him, hasa pale mtukufu alipojiweka mbali nae
 
MUNGU ANISAIDIE!
ila I HAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAATE THIS MTU BASI TU!
 
Kuna mwingine kawaambie wananchi watafute nchi nyingine waende...kuna vituko sana kwa wateule wa Magufuli.
 
Mimi Daudi Albert Bashite mkuu wa mkoa Wa Mzizima ninawaagiza wananchi wangu kwamba:-

1. "Mtu yeyote atakayeingia kwenye mkoa wangu atoe taarifa kwa serikali ya mtaa ama eneo husika, La sivyo atarudi alipotoka. Sitaki wanachi wangu wabughudiwe"

2. "Mgeni akija kwako akae siku mbili arudi kwao, wananchi wangu wana maisha magumu watateseka kukulisha na kukulea. Hili lisitokee kwenye mkoa wangu, labda nikiwa nmetoka madarakani."
 
View attachment 857507

Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally Katika mwendelezo wa mahojiano aliyoyafanya na Raia Mwema, amemnyooshea kidole, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa namna anavyotekeleza majukumu yake ya ukuu wa Mkoa na kudai kuwa kulikuwepo udhaifu katika kushughulikia makontena kutokana na kufanya kazi bila kushirikishana.

Alieleza kuwa, Mkuu wa Mkoa alipaswa kuwashirikisha wenzake tangu hatua za awali, kwa kuwa Serikali ni moja, hakuna cha Waziri wala Mkuu wa Mkoa - wote ni Wateule wa Rais.

Bashiru alimnyooshea kidole Makonda kwa ubinafsi na kukumbushia jinsi ambavyo Mkoa wa Dar es Salaam ni mmojawapo ya Mikoa aliyoitaja hivi karibuni kwa kutotekeleza vyema Ilani ya CCM kutokana kufanya kazi bila ushirikiano.

"Hapa sina maana kwamba ni Mkuu wa Mkoa tu hapana, ni uongozi mzima chini ya Mkuu wa Mkoa na uongozi mzima chini ya Mwenyekiti wa Chama."

Aliongezea kuwa, "Rais hawezi kwenda kuwafundisha uhusiano mwema, wao wenyewe ndio wanatakiwa kujua kwamba uhusiano mwema kikazi unamjenga zaidi kiongozi yeyote..."

Vilevile, Katibu Mkuu alimuonya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam juu ya tabia yake ya kuwaita wakazi wa Dar es Salaam, wananchi (Mkoa) wangu. "Na hii habari ya Dar es Salaam ya Makonda, hakuna Dar es Salaam ya Makonda, ni Dar es Salaam chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda."

Bashiru aliongezea kuwa: "Kuna wakati namsikia anasema wananchi wangu, nani kamwambia anao wananchi wake? Hakuna wananchi wako. Hakuna kiongozi anamiliki wananchi, ni wananchi wenzangu."

View attachment 857506
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akihutubia wananchi eneo la Mnazi Mmoja.

Aidha, Dk. Bashiru alikumbushia jinsi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyowahi kuonya juu ya ubinafsi: .... mkianza kusema mimi - wewe au wao - sisi, hamfiki.

Hivyo, aliwaasa vijana wanaopewa uongozi wawe wanyenyekevu na kuacha papara kwani watapotea kama ambavyo vijana wengi waliowahi kuwa juu walipotea kwa kukosa unyenyekevu.

View attachment 857504
Kosa limefanyika kwa kuwapa waty vyeo kisa kulipa fadhila badala ya kuchukua watu waliopo katika utumishi wa umma au kuwafanyia interview.Chuo cha uongozi kina kazi gani?
 
Anafanya hivyo kutokana na upeo wa elimu yake na aliyemteua na kuendelea kumkumbatia anajua hilo
 
View attachment 857507

Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally Katika mwendelezo wa mahojiano aliyoyafanya na Raia Mwema, amemnyooshea kidole, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa namna anavyotekeleza majukumu yake ya ukuu wa Mkoa na kudai kuwa kulikuwepo udhaifu katika kushughulikia makontena kutokana na kufanya kazi bila kushirikishana.

Alieleza kuwa, Mkuu wa Mkoa alipaswa kuwashirikisha wenzake tangu hatua za awali, kwa kuwa Serikali ni moja, hakuna cha Waziri wala Mkuu wa Mkoa - wote ni Wateule wa Rais.

Bashiru alimnyooshea kidole Makonda kwa ubinafsi na kukumbushia jinsi ambavyo Mkoa wa Dar es Salaam ni mmojawapo ya Mikoa aliyoitaja hivi karibuni kwa kutotekeleza vyema Ilani ya CCM kutokana kufanya kazi bila ushirikiano.

"Hapa sina maana kwamba ni Mkuu wa Mkoa tu hapana, ni uongozi mzima chini ya Mkuu wa Mkoa na uongozi mzima chini ya Mwenyekiti wa Chama."

Aliongezea kuwa, "Rais hawezi kwenda kuwafundisha uhusiano mwema, wao wenyewe ndio wanatakiwa kujua kwamba uhusiano mwema kikazi unamjenga zaidi kiongozi yeyote..."

Vilevile, Katibu Mkuu alimuonya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam juu ya tabia yake ya kuwaita wakazi wa Dar es Salaam, wananchi (Mkoa) wangu. "Na hii habari ya Dar es Salaam ya Makonda, hakuna Dar es Salaam ya Makonda, ni Dar es Salaam chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda."

Bashiru aliongezea kuwa: "Kuna wakati namsikia anasema wananchi wangu, nani kamwambia anao wananchi wake? Hakuna wananchi wako. Hakuna kiongozi anamiliki wananchi, ni wananchi wenzangu."

View attachment 857506
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akihutubia wananchi eneo la Mnazi Mmoja.

Aidha, Dk. Bashiru alikumbushia jinsi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyowahi kuonya juu ya ubinafsi: .... mkianza kusema mimi - wewe au wao - sisi, hamfiki.

Hivyo, aliwaasa vijana wanaopewa uongozi wawe wanyenyekevu na kuacha papara kwani watapotea kama ambavyo vijana wengi waliowahi kuwa juu walipotea kwa kukosa unyenyekevu.

View attachment 857504
Hata saa mbovu kuna wakati inakuwa sahihi.
 
Tehetehe, "wananchi wangu"imekaa vibaya, "wananchi wenzangu"iko vizuri,hata wabunge warekebishwe katika hili
 
Nanukuu

"Na hii habari ya Dar es Salaam ya Makonda, hakuna Dar es Salaam ya Makonda, ni Dar es Salaam chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda."

"Kuna wakati namsikia anasema wananchi wangu, nani kamwambia anao wananchi wake? Hakuna wananchi wako. Hakuna kiongozi anamiliki wananchi, ni wananchi wenzangu."

Mwisho wa kunukuu
 
Pambana na ya kwenu!
Fukara nyinyi walahi!
Unarudia yale yale ambayo katibu mkuu wako kamnukuu mwalimu nyerere hivi nyie mmerithi ukichaa wa mwenyekiti wenu,?

Aidha, Dk. Bashiru alikumbushia jinsi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyowahi kuonya juu ya ubinafsi: .... mkianza kusema mimi - wewe au wao - sisi, hamfiki
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom