Hili tatizo limesababishwa na serikali wenyewe kila siku wanakuja na sheria mpya wanawanyima wafanya biashara kuuza soko wanalotaka wao kwa manufaa ya wakulima. Kuna wakati hakuna kuuza mahindi nje mara uzeni mara tutanunua hata hujui kesho watakuja na sheria zipi bila kujali watu wame invest wewe huchangii katika gharama zao ikifika siku wanataka kufanya biashara wanaingiza pua zao utasema walitoa ruzuku kusaidia kilimo. acha soko huru wauze wanakotaka ili uhitaji uwe mkubwa na bei itapanda wateja wakiwa ni wengi bei itajihukumu yenyewe kama soko huru tuache kuingilia biashara za watu. Ni kama ndege wakiona booking watu wengi bei zinapanda mnaweza kuwa mko wote ndani ya ndege lakini kila mtu kalipa bei tofauti. Usifanye regulation katika bei acha soko lihukumu iwe usafirishaji, wakulima hata real estate. Mwezi wa 6 nilikuwa Dar hotel zote bei juu sababu high season ni sawa lakini sasa ije mfano mwaka mpya wenye magari hakuna kupandisha bei askari wameshajaa mbona hawafanyi kwa biashara zingine. Kama Mahindi waacheni wauze wanakotaka kwenye maslahi kwao serikali kusanya kodo stahiki tu biashara sio jukumu lako.