Sakata la Madiwani: CHADEMA yalegeza masharti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Madiwani: CHADEMA yalegeza masharti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jul 22, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ripoti ya Uchaguzi Chadema

  Ripoti ya Kamati iliyondwa na Chadema kuchunguza maridhiano ya madiwani wake ,CCM na TLP Arusha Mjini, imesema hakuna tuhuma za rushwa katika mchakato huo kama ilivyoeleza na baadhi ya viongozi wa chama hicho akiwemo Lema.

  Dk Slaa awaandikia barua madiwani

  Kamati Kuu ya Chadema imewataka madiwani wake kuomba radhi kama sehemu ya utawala bora. Barua hiyo ya kuwataka waombe radhi madiwani wote inakuja zikiwa ni siku chache tu mara baada ya madiwani wanane kuitunishia misuli Chadema iliyowataka wajiuzulu nyadhifa zao walizozipata katika mwafaka wakidai hawawezi kujiuzulu.

  Kwa mujibu wa taarifa za uhakika zinadai ya kuwa barua za kuwataka madiwani hao waombe radhi zimetua mkoani Arusha, jana mnamo saa 4;30, ambapo zilisambazwa kwa madiwani wote.

  Barua hiyo (Mwananchi ina nakala yake) yenye KUMB c/hq/m/ar/01/157 na kichwa cha habari kisemacho,

  "YAH;KUTAKIWA KUOMBA KWA USHIRIKI WENU KATIKA KURIDHIA MWAFAKA /MARIDHIANO BATILI"

  iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willlibrod Slaa, inawaagiza madiwani hao kuwa ni imani yao watafuata agizo la kuomba radhi kwa kutumia busara zao na utawala bora.

  "Chadema toka mwanzo ilipinga uchaguzi wa meya, jambo lililopelekea "maandamano makubwa tarehe 5 Januari 2011 kutokana na kukiukwa kwa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi kitendo cha maridhiano /mwafaka wa 15,4,2011 na uchaguzi uliofuatia wa naibu meya nao unakiuka sheria ,kanuni na taratibu maradufu kuliko hata uchaguzi wa meya mwenyewe"

  Katibu wa Chadema, Dk Slaa alipoulizwa na gazeti hili alikiri chama chao kuwaandikia barua madiwani hao huku akisisitiza, yeye hataki kujibishana na madiwani hao, lakini watapambana na sheria hadi kufikia leo majira ya saa 7.02 mchana.

  "Mimi sihitaji kujibishana na madiwani wetu, lakini nasubiri hadi kesho (leo) saa 7:02 mchana tujue, wao watapamba na sheria kama kuna mtu anaweza kupambana na sheria tutaona,"alisema Slaa.

  My Take:

  Naomba kufahamishwa iikiwa barua za kutakiwa kujiuzulu nyadhifa zao bado ziko pale pale au zilitolewa kimakosa, au zimeambatana na barua za kuomba Radhi. Kuna mkanganyiko, habari inasema barua za kuomba Radhi zimetumwa baada ta Madiwani kutunisha misuli barua za kujiuzulu.

  http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/13854-ccm-chadema-wavutana-bungeni

  Source: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, bandiko lako la juu hapo ndio ripoti ya CDM ndio wameitoa leo kama alivyosema Dr Slaa?
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Chadema na Slaa hapa wamechemka, ukweli wanaujua ni upi lakini wanashindwa kuuweka wazi, wanashangaza!

  Hivi nani asiejuwa kuwa muafaka ulifikiwa na Mbowe na Pinda? sasa Slaa anashinda na Mbowe? Uchunguzi wa kamati ya Marando uwekwe wazi.

  Naona kinachotakiwa ni Slaa kuwaomba radhi madiwani kwani ni yeye ndio kabla ya uchunguzi alisema kuna rushwa imetembea. Namuonea huruma Slaa, alifikiriuongozi wa chama kitaifa ni sawa na ubunge? ni vitu viwili tofauti na huwa hatakiwi kukurupuka.
   
 4. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Habari za saloon magomeni lhizo lete dokezo la muafaka wa pinda na mbowe hapa short of that weka kichwa chako kwenye drier uendelee kutengeneza nywele.huna mpya
   
 5. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  madiwani watatu walipewa barua mbili , ya kuwataka kujiuzulu na kuomba radhi ambayo pia walipewa madiwani wote , hili la kusema ni baada ya kutunisha msuli ni uzushi wa mwandishi
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Ripoti ya ya Uchaguzi Chadema (gazeti la Mwananchi)

  Hata hivyo, Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Chadema kuchunguza maridhiano ya madiwani wake ,CCM na TLP Arusha Mjini, imesema hakuna tuhuma za rushwa katika mchakato huo kama ilivyoeleza na baadhi ya viongozi wa chama hicho akiwemo Lema.

  Ripoti hiyo ambayo gazeti limefanikiwa kuiona, ilisema licha ya kamati kuwahoji madiwani pamoja na watu mbalimbali mjini Arusha, hakukuwa na dalili zozote za kuhongwa."Kamati ilijitahidi kutafuta ukweli juu ya jambo hili kupitia uchambuzi wa taarifa mbambali za mahojiano na madiwani na viongozi wa chama Wilaya na Mkoa, pamoja na mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ambaye ni moja ya watu waliotoa tuhuma hizi," ilisema sehemu ya ripoti na kuongeza:

  "Kamati haikuweza kupata chembe ya ushahidi unaoweza kuthibitisha angalau, kwa mbali kwamba kuna diwani aliyehongwa ili akubaliane na maridhiano."

  Ripoti hiyo ilifafanua kwamba, "Kwa kuzingatia maelezo ya madiwani na hali halisi mitaani mjini Arusha, madiwani wamechafuka sana kwa tuhuma za rushwa zilizoelekezwa kwao."

  Iliongeza kwamba, madiwani wengi walitaka kwenda mahakamani kwa nia ya kuwashitaki watu waliotoa tuhuma za rushwa dhidi yao ili wajisafishe.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kamati iliweza kuwashawishi madiwani hao na hatimaye kuachana na dhamira yao ya kwenda mahakamani.

  "Kamati haina uwezo wa kukanusha moja kwa moja uwezekano wa kuwapo kwa mazingira ya rushwa katika mchakato wa kupatikana mwafaka/maridhiano. Hata hivyo, ni jukumu la waliotoa tuhuma kuthibitisha hali hii; vinginevyo, ni muhimu hatua na jitihada za kisiasa zikafanyika katika kuwasafisha madiwani wetu," ilisisitiza.

  Ripoti hiyo ilifafanua kwamba, kama hapakuwa na uthibitisho wowote wa maana dhidi ya tuhuma za rushwa, jitahada za kuwasafisha madiwani hao zichukuliwe.

  "Kwa mfano, kwa kufanya mkutano wa hadhara jijini Arusha kwa ajili ya kufafanua na mambo mengine yatakayoamuliwa na Kamati Kuu, juu ya tuhuma za rushwa," ripoti ilieleza na nakuongeza.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, "Hii ni muhimu sana sio katika kuwasafisha madiwani na chama mbele ya wananchi tu, lakini pia kama njia ya kuleta maelewano baina ya mbunge na madiwani."
  Taarifa hiyo iliongeza kwamba, "Kamati haimini kwamba madiwani wetu wataendelea kustahimili kutokuingia kwenye vikao vya Baraza la Halmashauri...hivyo haipendekezi kwamba turudi tulipokuwa kwa maana ya kuendelea kugomea vikao na kudai uchaguzi kurudiwa."Ripoti hiyo ilieleza zaidi pia kwamba, chama taifa kiliingilia jambo hili kwa kuchelewa wakati tayari madiwani walishakubaliana na wenzao.

  Ripoti hiyo inasema, "Hii haikubaliki katika misingi ya kutatua migogoro inayohusisha pande mbili tofauti, na hasa katika mambo ya siasa." Ilieleza sehemu nyingine ya ripoti."Hata hivyo, kamati ilisema , madiwani hawakufuata kikamilifu taratibu za chama katika ushiriki wao katika maridhiano, hasa katika suala la uteuzi wa mgombea Naibu Meya.

  Ilisema pia kwamba, viongozi wa madiwani walikuwa hawawapatii taarifa kamili madiwani wenzao kuhusu maendeleo ya mazungumzo ya maridhiano na yale yaliyokuwa yanaamuliwa katika chama.

  " Kamati inapendekeza kuwa Kamati Kuu iwape onyo kali, viongozi wa madiwani, Estomih Mallah na John Bayo, na kuwataka kuomba radhi kwa kitendo chao hicho," ilisema.

  Mapendekezo zaidi ya kamati ni pamoja na chama kifanye uchaguzi haraka katika ngazi ya wilaya na kuwa na mfumo kamili wa kiutendaji katika ngazi hiyo.

  Ilisema kuna mahusiano dhaifu na ya kimgogoro baina ya madiwani na Mbunge wao wa Arusha Mjini, hali inayohatarisha utekelezaji wa majukumu yao kama wawakilishi wa wananchi na taswira ya chama katika Wilaya na Mkoa."Hali hii isipotatuliwa mapema inaweza kukiathiri chama kisiasa katika chaguzi zijazo."
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  alichokosea jairo na timu yake ni kuandika barua, na ni ushahidi wa kutosha pakachani samaki wote wameoza, ingawa hivyo, tunakujua wewe umejivua akili.
   
 8. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  cdm cdm ushahidi wa rushwa huwa c wa moja kwa moja wkt mwingine hata mazingira tu yanaweza kuthibitisha hilo ,
  Mallah alikuwa akiwafeed wrong information madiwani wenzake mpaka wakaingia kwenye muafaka fake kwa msukumo gani?
   
 9. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Onesha ushahidi wa muafaka huo otherwise haya ni maneno ya bara barani na hayana mashiko. Pengine mwenzetu uliwapelekea vitumbua walipokuwa wakikutana!!
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Akili za kimsukule hizi, unataka kutuaminisha kwamba Dr Slaa kazi ya ukatibu mkuu wa CHADEMA ameianza mwaka huu?
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Nimesoma habari nzima lakini sijaona sehemu yeyote inayoonyesha Chadema kulegeza masharti.
  Nachoomba viongozi wa Chadema ili waendelee kuwa na imani ya wananchi they have to mean what they say
  otherwise people might not take them seriously in future.
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sasa ndio tunaanza kumjua Slaa halisi sio yule aliyejivika ngozi ya kondoo kumbe ni chui. Ni mtu wakujichanganya na asiye na msimamo ndio hali inayojionyesha hapa
   
 13. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Dada angu naona unao tu Pinda na Mbowe mpaka kieleweke. Kila unapoenda lazima uwataje kuhusiana na hii sakata ya arusha
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Kwani kuna kipi kimebadilika Slaa kasema deadline iko pale pale saa 7:02 mchana wadanganye wenzako wakione cha moto

  Chadema hawapeani miezi 6 kama mlivyowapa kina Lowassa eti mtu unaambiwa uangalie kama unafaa mwenyewe uamue

  huo ni uongozi gani sijawahi ona. Hivi kwanza wewe uko kundi gani CCM-Rachel, CCM-Ikulu au CCM-Ccj maana mnatuchanga sasa.
   
 15. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Dada Yangu.
  Ni vizuri ujuwe Mbowe ni share holder wa Chadema na Dr Slaa ni mwajiriwa tu ndani ya Chadema.

  Lakini aliyepotosha yote ni Godbless Lema mbunge wa Arusha mjini kwani yeye ni ndumilakuwili na kwa kujuwa ushari na kutoitakia amani nchi yenu Dr Slaa anakurupuka sana kuhakikisha Arusha hakuna amani.

  Ni vizuri sana Lema na Slaa wajivue magamba hapo.
   
 16. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Kwani hao ni watu wamepumbazwa wamekuwa kama maroboti yaliyosetiwa nafikiri faza fox yeye kasetiwa kidude cha 'Mbowe na Pinda' kuna Muhadhiri yeye wamemseti 'Chadema yapwaya' na Rejao yeye akibonyezwa lazima aseme 'Chadema ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiii' ukiwauliza wachangie zaidi ya hapo labda unatafuta matusi.
   
 17. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  shida ya kuandika kutoka kulia kwenda kushoto
   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ww kweli siasa huzijui, nyie hamkumwambia Zitto wakati ule wa sakata la Magwanda kutoka bungeni kuwa achague anavyoona inafaa ? au hukuwepo nchini mzee. Na ww ni kundi gani la CDM kati ya haya CHADEMA - Katoliki, CHADEMA mseto au CHADEMA - islamu ?
   
 19. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama mpaka sasa hujaweza kumfahamu slaa basi wewe sio mtanzania mzalendo..ila sisi wazalendo tunamfahamu slaa tangu alipoibua kashfa mbalimbali za serikali mpaka sasa watanzani wote tunafahamu richmonduli ni nini..tunafahamu maovu yote kwenye mikataba ya madini nani asiyejua kuwa wananchi walifukiwa huko bulyanhulu? Madiwani arusha unaweza kufananisha na CCJ ya nape, sitta, mwakyembe?
   
 20. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na kweli kwa kulazimisha kamati kuu imlipe kama anavyolipwa mbunge mafao yake yawe makubwa , nakubaliana na ww kabisa kuwa Slaa ni mzalendo
   
Loading...