Sakata la Madiwani: CHADEMA yalegeza masharti

Nasubiri kusikia wameshajiuzulu nyadhifa walizopewa. Hatuna muda wa kusikiliza malumbano. Upuuzi waliofanya walikitia aibu chama na hatuwezi kuendelea kuwavumilia. Tena huo ujinga wanaouendekeza unatuongezea hasira.
 
Chadema na Slaa hapa wamechemka, ukweli wanaujua ni upi lakini wanashindwa kuuweka wazi, wanashangaza!

Hivi nani asiejuwa kuwa muafaka ulifikiwa na Mbowe na Pinda? sasa Slaa anashinda na Mbowe? Uchunguzi wa kamati ya Marando uwekwe wazi.

Naona kinachotakiwa ni Slaa kuwaomba radhi madiwani kwani ni yeye ndio kabla ya uchunguzi alisema kuna rushwa imetembea. Namuonea huruma Slaa, alifikiriuongozi wa chama kitaifa ni sawa na ubunge? ni vitu viwili tofauti na huwa hatakiwi kukurupuka.

Pole Sana FaizaFoxy, najua unajaribu sana kupambana na Dr Slaa, ila hutaweza. Dr alikuwa Makamu mwenyekiti na katibu mkuu wa Chadema wakati akiwa Mbunge. Kwa hiyo ukatibu mkuu sio cheo kipya kwake. Na Dr huwa hakurupuki hata kidogo. Madiwani wamefanya makosa na wanatakiwa kufuata miongozo ya chama. CDM sio CCM ambapo Sita ana CCM-CCJ yake, EL ana CCM-Richmond yake, JK ana CCM-Membe yake, Nape ana CCM-Magamba yake. Kwenye mvurugano huo mnatamani sana kuona CDM inakuwa kama kwenu. Mtasubiri sana.

Arusha kutatulia siasa za Mobutu hamziwezi Tanzania. Jengeni uchumi, washani umeme, waleteeni watanzania ajira, Pambaneni na rushwa. Acheni ugomvi wa uraisi 2015. CDM inasonga mbele kwa kasi ya hali ya juu, kipimo kitakuwa Igunga.
 
Ww kweli siasa huzijui, nyie hamkumwambia Zitto wakati ule wa sakata la Magwanda kutoka bungeni kuwa achague anavyoona inafaa ? au hukuwepo nchini mzee. Na ww ni kundi gani la CDM kati ya haya CHADEMA - Katoliki, CHADEMA mseto au CHADEMA - islamu ?
Usilazimishe kuiga kila kitu vitu vingine havi fit kwanza hujajibu swali upo kundi gani CCM-Rachel, CCM-Ikulu au CCM-Ccj lakini kwa akili zako zilivyo huwezi kuwa CCM-Rachel sanasana CCM-Ccj waropokaji kwa kina nepi.
 
Hivi mnafikiri Chadema wajinga ina watu makini zile barua hazikutaja neno rushwa hata mara moja makosa wanayotuhumiwa si kula rushwa ni kwenda kinyume na katiba na kanuni za chama kutotii maagizo halali ya chama, hayo ya rushwa ni ya kutamkwa pembeni tu tena magazetini, wewe unafikiri Marando na Prof. Safari walipelekwa pale ki makosa wanajua kila kitu. Hilo la rushwa ni kesi nyingine kama Malah anaona amekashifiwa akaifungue kesi lakini barua za kujiuzulu ziko palepale ngoja ifike saa 7:02 uone, halafu sioni kwanini wamewaongezea dk 2 za kazi gani.
Feedback, hamna aliosema CDM wajinga! Namnukuu Dr Slaa "Upungufu mwingine ni kuwepo kwa mianya ya rushwa ya kuwashawishi Madiwani husika kushiriki kwenye maridhiano hayo" mwisho wa kunukuu
 
Ilisema pia kwamba, viongozi wa madiwani walikuwa hawawapatii taarifa kamili madiwani wenzao kuhusu maendeleo ya mazungumzo ya maridhiano na yale yaliyokuwa yanaamuliwa katika chama.

“ Kamati inapendekeza kuwa Kamati Kuu iwape onyo kali, viongozi wa madiwani, Estomih Mallah na John Bayo, na kuwataka kuomba radhi kwa kitendo chao hicho,” ilisema.

..inaelekea madiwani Mallah na Bayo walitumia ujanja-ujanja ktk kuwashawishi wenzao kufikia makubaliano na CCM.

..Kamati Kuu ya CDM imezingatia mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi iliyoongozwa na Mabere Marando.

..sasa kama madiwani Mallah na Bayo watashindwa kuomba radhi kama walivyoelekezwa na Kamati Kuu ya CDM basi hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa dhidi yao.

..sijaona mahali ambapo Dr.Slaa amekwenda kinyume na maelekezo ya Kamati Kuu ya CDM.
 
Feedback, hamna aliosema CDM wajinga! Namnukuu Dr Slaa "Upungufu mwingine ni kuwepo kwa mianya ya rushwa ya kuwashawishi Madiwani husika kushiriki kwenye maridhiano hayo" mwisho wa kunukuu
Hayo hayamo kwenye barua waliyokabidhiwa unayosema ni yale aliyonukuliwa na waandishi hata hivyo kusema kuna mianya ya rushwa sio kuwa ume confirm vitendo vya rushwa.
 
Hayo hayamo kwenye barua waliyokabidhiwa unayosema ni yale aliyonukuliwa na waandishi hata hivyo kusema kuna mianya ya rushwa sio kuwa ume confirm vitendo vya rushwa.
Kwa hiyo hayo maneno Dr Slaa ameropoka?
 
Wewe endelea kuwaponza madiwani mara ooo Slaa karopoka mara rushwa mara..... siku wakitimuliwa wewe utawasaidia nini.
Bora kufa umesimama kuliko kuhishi umepiga magoti, kwani CDM ni kampuni binafsi inaweza kufukuza yoyote atakaenda kinyume na Mbowe na a loser Slaa
 
Chadema na Slaa hapa wamechemka, ukweli wanaujua ni upi lakini wanashindwa kuuweka wazi, wanashangaza!

Hivi nani asiejuwa kuwa muafaka ulifikiwa na Mbowe na Pinda?

Mimi na baadhi ya wengi humu huo muafaka wa Pinda na Mbowe hatuujui. Kwa heshima na taadhima naomba utujulishe huo mwafaka ili tuache mabishano yasiyoelekea mstakabali kwa sababu tu yakutojua kilichojiri.
 
..inaelekea madiwani Mallah na Bayo walitumia ujanja-ujanja ktk kuwashawishi wenzao kufikia makubaliano na CCM.

..Kamati Kuu ya CDM imezingatia mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi iliyoongozwa na Mabere Marando.

..sasa kama madiwani Mallah na Bayo watashindwa kuomba radhi kama walivyoelekezwa na Kamati Kuu ya CDM basi hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa dhidi yao.

..sijaona mahali ambapo Dr.Slaa amekwenda kinyume na maelekezo ya Kamati Kuu ya CDM.
Mbona hajachukua hatua? Au naye yupo bondeni kwenye mnuso.
 
Onesha ushahidi wa muafaka huo otherwise haya ni maneno ya bara barani na hayana mashiko. Pengine mwenzetu uliwapelekea vitumbua walipokuwa wakikutana!!

1) "Taarifa hizo zilieleza kuwa Mwenyekiti Mbowe alikuwa ameshakutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu jinsi ya kutafuta muafaka wa kudumu kuhusu mgogoro huo na walikubaliana kumaliza suala hilo kabla ya Julai mosi mwaka huu."

Source: Raia Mwema
 
Back
Top Bottom