Sakata la Madini: Tundu Lissu ataka J Kikwete ashitakiwe haraka sana

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Tundu Lissu wakati akichangia bajeti amesema Rais mstaafu awamu ya nne Jakaya Kikwete ashitakiwe sababu ndo alisaini Leseni ya Bulyanhulu

Tundu Lissu asema Rais Kikwete naye anapaswa kuwajibishwa kwani ndiye aliyesaini leseni ya mgodi wa Bulyanhulu akiwa waziri.

My Take:

Kumbe ndo maana Kikwete alisema bora anyimwe kura za urais kuliko Tundu Lissu kupewa kura za Ubunge akaingia Bungeni. Alijua atayafumua madudu yake.

======

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ameipa changamoto Serikali kwa kuitaka kumuingiza Jakaya Kikwete katika orodha ya watuhumiwa wa sakata la makinikia.

Akichangia bungeni leo Jumanne, katika hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18, Lissu amesema kuwa wakati wa kusaini mikataba ya madini Kikwete alikuwa ni Waziri wa Maji, Nishati na Madini.

“Katika taarifa hii ya jana wamependekeza watu fulani fulani washtakiwe makamishna, mwanasheria mkuu, Chenge (Mbunge wa Bariadi Andrew), Ngeleja (Wiliam- Sengerema) jamani naombeni niwaambie kitu ili wabunge muwe na maarifa,”amesema na kuongeza:

“Mtu wa kwanza kusaini mikataba na leseni za madini alikuwa ni Meja Jakaya Mrisho Kikwete, Agosti 5 mwaka 1994 alisaini leseni ya Bulyankulu inayopingwa leo hii wakati akiwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini wakati huo hakuwa na kinga ya urais.”

Amesema wakati aliposaini leseni na mikataba hiyo alikuwa hana kinga kwa masuala ambayo aliyafanya.

“Rais (Kikwete) alisaini si ya Bulyankulu pekee ya Nzega, ya Geita hizo leseni zina saini ya Kikwete anaponaje kwa mapendekezo haya? Anaponaje kama kweli mnataka kuwashughulikia watu walioshiriki kwenye mambo haya?”amehoji.

“Mbona mnachagua chagua hizi? Leseni na hizi sheria tangu mwaka 1999 tumesema tatizo kubwa ni sheria.”

Amemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kama anataka kukumbukwa wakati wa uongozi wake basi asikubali kupitisha miswada ya sheria kwa hati ya dharura.

Akijibu swali hilo, Ndugai amesema atairuhusu miswada hiyo ya madini na gesi iingie bungeni kwa hati ya dharura.

“Kwanza wanaoamua siyo mimi tu ni kamati ya uongozi ya Bunge, lakini kama itakuja kwa hati ya dharura hii (madini) itaruhusiwa kwasababu moja tu tunaibiwa sana.” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Hapo lazima mh Ndugai amtafutie kosa ili asimamishwe kuhudhuria vikao.Halafu akija uswazi Mkulu amshughulikie!

Wakati Chenge anadunda mtaani huku akiendelea kuongoza vikao vya Bunge!!Only in Tanzania where the line between law makers and law breakers is almost invisible.
 
MJADALA WA BAJETI:Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu asema Rais Kikwete anapaswa kuwajibishwa kwani ndiye aliyesaini leseni ya mgodi wa Bulyanhulu akiwa waziri.
tmp_13610-IMG_20170613_1830341198750363.jpg
 
Lissu ntakuchoka sasa kwa upuuzi wako,hebu tengeneza hoja zingine hii achana nayo,miccm itaumbuana yenyewe,yapo mambo mengi tu ya kupigia kelele mfano kwenye elimu kuna kila aina ya uozo.
 
Hapo lazima mh Ndugai amtafutie kosa ili asimamishwe kuhudhuria vikao.Halafu akija uswazi Mkulu amshughulikie!

Wakati Chenge anadunda mtaani huku akiendelea kuongoza vikao vya Bunge!!Only in Tanzania where the line between law makers and law breakers is almost invisible.
Watahakikisha siku Mikataba inapelekwa Bungeni lazima akina Lissu watakuwa wametimuliwa mjengoni ili wasichangie.
 
Lissu amekua mropokaji sana,mwanasheria aliesoma sheria anaeifahamu katiba yetu vizuri hawezi ongea upuuzi wa aina yake
 
Back
Top Bottom