Sakata la Madawa JKNIA: Mwakyembe acharuka!

Sakata la Madawa JKNIA: Mwakyembe acharuka!

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,629
Reaction score
6,816
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameionya Kamati ya Nne ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri wa Anga nchini (NCASC) kujiondoa kabla hajaifikia iwapo mzigo wowote wa dawa za kulevya kutoka Tanzania utakamatwa nje ya nchi ukitoka nchini kwa njia ya anga.

Dk Mwakyembe alitoa onyo hilo jana Dar es Salaam wakati akizindua rasmi Kamati hiyo yenye wajumbe 11 na kusisitiza kuwa ina wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama katika viwanja vya ndege unaimarishwa, ili kudhibiti biashara ya dawa za kulevya nchini.

“Mimi sidhani suala la kukamatwa kwa dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ni dogo,” alisema Dk Mwakyembe na kusisitiza kuwa kashfa ya dawa za kulevya kupitishwa katika uwanja huo, inadhalilisha jina la Baba wa Taifa kitaifa na kimataifa.

Alisema kutowajibika kwa mamlaka zinazohusika na ulinzi na usalama katika viwanja vya ndege, kumesababisha kuendelea kwa ugaidi wa kimataifa na kusikitishwa na udhaifu unaofanywa na mamlaka hizo hali inayoliletea Taifa fedheha kubwa.

“Sidhani kama mamlaka hizo zinahitaji sheria ili ziwe na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu,” alisema Waziri na kusisitiza kuwa umefika wakati kwa viongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa ili kuleta tija na maendeleo nchini.

Alisema amekuwa akisikia mijadala kuhusu kukamatwa kwa dawa za kulevya, lakini hakuna anayechukuliwa hatua za kisheria kuhusu kashfa hiyo na kuongeza kuwa viongozi wanakataa kuheshimu sheria, hali ambayo alisema inadhalilisha na kushusha hadhi ya viwanja vya ndege nchini.

Baada ya kuzindua Kamati hiyo, Dk Mwakyembe alizuia zawadi zilizoandaliwa kutolewa kwa Kamati inayomaliza muda wake ikiongozwa na Mwenyekiti, Jafari Mpili na kukataa pia kupiga nayo picha ya pamoja badala yake akaomba akutane na Kamati mpya, jana saa nane mchana kujadili kwa kina majukumu.

Awali, katika hutoba yake kwa mgeni rasmi, Mwenyekiti wa NCASC ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Fadhili Manongi, alitaja changamoto kadhaa za kiusalama katika sekta ya anga nchini.

Changamoto hizo ni pamoja na kuchelewa kuridhiwa na Bunge mikataba ya kimataifa inayohusu na usalama wa usafiri wa anga kama vile mkataba wa Beijing na Itifaki ya Mwaka 2010.

Nyingine ni kutojua taratibu za kiusalama na maneno ya kukatisha tamaa kwa maofisa usalama wa viwanja hasa kutoka kwa viongozi waandamizi wa Serikali kwa kauli zao na kutoelewa kanuni za usalama kwa wadau wengi.

Moja ya malengo ya NCASC ni kushauri TCAA hatua za usalama zinazotakiwa katika viwanja vya ndege ili kudhibiti vitisho na ugaidi dhidi ya usafiri wa anga, viwanja na miundombinu yake.

Doa kwa Taifa Juzi katika taraifa yake, Serikali ilisema biashara ya kusafirisha dawa za kulevya imeanza kutia doa taswira ya Watanzania kimataifa. Ilisema uthibitisho ni kwamba katika baadhi ya nchi, kila Mtanzania anayeingia, hivi sasa anachukuliwa kama mshukiwa wa moja kwa moja wa dawa hizo na hivyo kupekuliwa kwa kina.

Serikali ilisema Watanzania waliokamatwa hivi karibuni wakiwa na dawa hizo wamechangia kwa kiwango kikubwa kutoa doa taswira ya nchi. Wiki iliyopita, Mtanzania Jackline Mollel (35), alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare, Zimbabwe akidaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 72.

Kabla ya tukio hilo, Julai, Watanzania wawili, Agnes Gerald ‘Masogange’ (25) na Melisa Edward (24), walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oliver Tambo, jijini Johannesburg, Afrika Kusini, wakidaiwa kuingiza dawa za kulevya kutoka Tanzania zikiwa na thamani ya mamilioni ya fedha. Walifikishwa mahakamani jijini humo.

HabariLeo
 
Mwakyembe nakuaminia fanya kile ulichofanya bandalini
 
...mwakyembe hutaweza kupambana pekeyako kama magogoni imekaa kimya,mwenzako magufuli pamoja na mikwala yote lakini vimemo vinatangulizwa magari ya wakubwa yaliyozidi uzito yanapita kamakawa...
 
Atawaweza huyu. sio kama wengine. kama bandarini ameondoa miungu watu itakuwa JKNI. Hili ni Jembe. Magufuri yule kelele nyingi kama hujapeleka bahasha
 
Inabidi tuwe tunaipongeza serikali inapofanya jitihada kiasi fulani,najua si kubwa limefanywa ila Kuzuia zawadi walizokuwa wanapewa kamati ya ulizi inyomaliza muda wake na kukataa kupiga nao picha kiasi fulani inaonyesha he mean business not playing ....

I know is not all that could be done but at least not business as usual ...kuwapongeza na ku smile nao kwenye picha ili hali kunatuhuma inayohusu kamati yao.Hongera serikali though you can do more
 
huyu ataweza, walishamwaga mboga,yy anamwaga ugali!
 
Nendeni mkamwambie mwakyembe kuwa acharuke awezavyo ila sisi watanzania tunachotaka si micharuko si makaripio si kuongeza ulinzi airport hatutaki!

Tunataka kusakwa walioshika mpini wa kuuza na kusambaza tunataka majogoo wa hii biashara wawajibishwe hadharani tuwajue tunataka wanaopitisha pale wajulikane hivi nani aliyekagua mizigo ya wale wadada wawili walokamatwa south atafutwe ndo utaratibu tunaoutaka hatutaki siasa zenu.

Kama mmeshindwa kudhibiti majogoo wa madawa ya kulevya ni bora kukaa kimya we fuatilia kwa Siri ibuka na majina mahakamani uwaziri sio fixed position ukigusa pabaya unabadilishwa Jamani madawa ya kulevya yanaharibu nguvukazi yanatupatia Aibu kwa sector nyingi hata ulinzi tutaonekana dhaifu please tuijenge Tanzania yetu kwa mapenzi ya dhati jamani Tubishane siasa ila utaifa mbeleeeeeeee

Mungu Ibariki Tanzania
 
Hizi kamati mnaunda za nini wakati majina mlitumbia mnayo? Au wangesema Chadema wanamajina ya wauza madawa ndo mngekua mnawasumbua na Polisi lakin kwakua alisema Kiongozi wenu mnajifanya hamsikii. Nendeni mkachukue majina kwake kule tena mchukue majina ya mapapa sio vidagaa.

Na hiyo kamati ivunjwe maana ni ufisadi tu huo. Kamati ya nini wakati majina mnayo. Ufisadi mtupu. Wizi mtupu.
 
mwakyembe atafanya kile ambacho tunakitarajia kama ulivyofanya bandarini.
 
...mwakyembe hutaweza kupambana pekeyako kama magogoni imekaa kimya,mwenzako magufuli pamoja na mikwala yote lakini vimemo vinatangulizwa magari ya wakubwa yaliyozidi uzito yanapita kamakawa...

tutajie namba za hayo magari na vimemo vilitumwa lini ili tuweze kukuamini,vinginevyo huu ni umbea na majungu.
 
hii biashara sidhan kama mwakyembe ataiweza ina a lot of money involved nadhan ndo mana amechukua caution approach ya kudeal na kudhibiti airport tu badala ya kudeal na kutafuta waliopitisha... ame act intelluigently maana kuwakamata wahusika kwa kweli sidhan kama ni kitu rahisi ivyo... these people are so connected and powerful.
 
Kwakweli Mwakwembe ni Jembe anaweza sana kama anaweza kushinikiza fisadi Lowa hasaa akangoka haya hayamshindi kwanza kakaa kimya mada mrefu akisoma dira , nadhani ni wakati sahii wa kuwaenyesha, hapo tumebaki na tanga, bagamoyo, magogoni , msasani na zanzibar
[
Nendeni mkamwambie
mwakyembe kuwa acharuke awezavyo ila sisi watanzania tunachotaka si
micharuko si makaripio si kuongeza ulinzi airport hatutaki!

Tunataka kusakwa walioshika mpini wa kuuza na kusambaza tunataka majogoo
wa hii biashara wawajibishwe hadharani tuwajue tunataka wanaopitisha
pale wajulikane hivi nani aliyekagua mizigo ya wale wadada wawili
walokamatwa south atafutwe ndo utaratibu tunaoutaka hatutaki siasa zenu.

Kama mmeshindwa kudhibiti majogoo wa madawa ya kulevya ni bora kukaa
kimya we fuatilia kwa Siri ibuka na majina mahakamani uwaziri sio fixed
position ukigusa pabaya unabadilishwa Jamani madawa ya kulevya
yanaharibu nguvukazi yanatupatia Aibu kwa sector nyingi hata ulinzi
tutaonekana dhaifu please tuijenge Tanzania yetu kwa mapenzi ya dhati
jamani Tubishane siasa ila utaifa mbeleeeeeeee

Mungu Ibariki Tanzania
 
Tunampongeza Mwakyembe kwa kuonyesha nia ya kupambana na hili janga; ila ushirikiano unahitajika kutoka ngazi zote!
 
Kama mwenye kaya kakalia majina ya wauza unga sidhani kama Mwakuembe ataweza
Hawa wengi wao ndo wafadhili wa chama.na sasa hv tunaelekea kwenye uchaguzi
 
Kwenye thread kama hizi zenye manufaa kwa nchi yetu kamwe hutaona comment ya misukule ya ccm ikiongozwa na mfanyabiashara mkubwa kama wafuatao' hatachangia kabisa ila ngoja waone uzi unaomuongelea Dr Slaa,Mbowe na Chadema utafikiri wamekataliwa
Ritz
Hamy-D mke wa bosi
ZeMarcopolo
Habariyamujini
Mafilili
Uncle Deo
Scramble
FaizaFoxy drug muller
Radhia Sweet
Nape
Chama
Chris Lukosi
Chilisosi
Mtela Mwampamba
Juliana Shonza,hawa wawili wa mwisho wamebadili ID wanaingia kwa majina mengine ili wasijulikane

Kwa sababu unagusa maslahi yao na sababu ya wao kukaa mjini hawatachangia make umewatia kidole machoni

WAZINGU WA UNGA NYIE OMBENI CCM ISITOKE MADARAKANI KAMA MAKAMBA JANUARY ALIVYOSEMA,LAAKINI WAKITOKA MTAKOMA MPENDE MSIPENDE
 
Mwakyembe nakuaminia fanya kile ulichofanya bandalini

bandarini ndio pa hovyo pembe zote za tembo zinapita hapo kwa mujibu wa cnn na mizigo ilokamatwa sehemu tofauti duniani
 
Hongera sana Dr. Mwakyembe kwa hatua stahiki hii mambo ya watu kuharibu halafu wanapongezwa na kupatiwa zawadi huwa ni zaidi ya wendawazimu
 
Back
Top Bottom