Elections 2010 Sakata la mabomu mwanza: Polisi wajitetea

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,273
17,096
Friday, 22 October 2010 07:52

Frederick Katulanda, Mwanza

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro amesema jeshi lake liliamua kutumia busara kuepuka kupiga mabomu ya machozi kwa mara nyingine usiku kutuliza wafuasi wa Chadema ambao waliokuwa wakifanya vurugu baada ya kumtano wa mgombea Urais Dk Willibroad Slaa kumalizika.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelezea vurugu ambazo zilitokea tena jana majira ya saa 1:30 usiku ambapo wafuasi wa Chadema walishambulia gari la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Nyamagana, na kupiga kwa mawe ofisi za CCM wilaya hiyo, Kamanda Sirro alisema kuwa alilazimika kutumia busara kwa vile kama jeshi lake lingeamua kupiga mabonu basi maafa yangekuwa makubwa zaidi.

“Ni kweli baada ya mkutano kulikuwa na vurugu, lakini ninafanya kazi kwa busara, kulikuwa na watu wengi sana barabarani na mitaani ambao walikuwa wakirejea makwao kutoka mkutanoni, katika hali kama hiyo nisingeweza kupiga mabomu ya machozi ningeuwa watu wengi sana,” alieleza kamanda Sirro.

Alisema kumalizika kwa mkutano wa Dk Slaa ambao ulikuwa na watu wengi kulisababisha mji wa Mwanza kujaa watu wengi na kusisitiza kuwa kama wangeamua kuwatuliza ama kuwatawanya watu hao kuzuia vurugu za usiku na kupiga mabomu basi watu ambao wangekufa idadi yao ingekuwa kubwa.

“Tulichofanya kwa kutumia askari wetu tuliweza kuwakamata watu waliokuwa wakifanya vurugu hizo na ambao tutawafikisha mahakamani baada ya upelelezi kukamilika kwa kosa la kuharibu ofisi za CCM,” alifafanua.

Akielezea tukio la gari la UVCCM kushambuliwa na wafuasi wa Chadema, kamanda Sirro alisema kuwa gari hilo limeshambuliwa kutokana na kuingia katika msafara wa Dk Slaa baada ya dereva wa gari lake kukikimbia hasira za wananchi kutokana na kusababisha ajali.

Kamanda alieleza kuwa dereva wa gari hilo la UVCCM kabla ya kuingilia msafara huo wa Dk Slaa alikuwa amegonga mwendesha pikipiki Hemilian Sprian (28) na hivyo alikuwa akikimbia kujisalimisha polisi.

“Dereva huyo baada ya kugonga ile pikipiki iling’ang’ania chini ya gari, basi alikuwa akikimbia sasa alipofika eneo hilo la makutano ya barabara ya Pamba na Kenyatta pikipiki ile ilinasuka kutoka uvunguni mwa gari, wakazidi kumkimbiza. Kwa hiyo aliingia barabra ya Kenyatta na kuja ambapo alipofika makutano ya New Mwanza Hoteli na Kenyatta ndipo alipokumbana na msafara wa Slaa,” alieleza kamanda.

Alisema katika hali ile wafuasi wa Chadema nao kwa vile gari waliliona likiwa na picha za mgombea ubunge wa jimbo la Nyamagana basi walidhani lilikuwa limekuja kuvamia msafara wao ndipo wakalishambuliwa, lakini polisi walikuwepo hapo na kuokoa vurugu hizo.

Alisema baada ya kutulizwa wafuasi hao walipofika ofisi za CCM Wilaya ya Nyamagana walianza tena kushambuliwa ofisi hizo kwa mawe ambapo walipeleka kikosi kimoja na kutuliza watu hao ambapo walifanikiwa kukamata wawili.

Source:Mwananchi

Kazi ipo....kikosi kizima kukamata watu wawili wasio na silaha...halafu jamaa anaongelea kuua kama ni kitu cha kawaida kwake....halafu watu wakiwa wengi ni lazima kuwatuliza au kuwatawanya?
 
Nikisema hapa watasema JF wanachukia serikali, kumbe ni mm na mawazo yangu: Hawa MAKAMANDA sielewi wanachaguliwa vp, wengi wana kauli za mtu asiyesoma wala hana busara za mtu mzima, ni waropokaji tu, na wengi wanatumia miguvu zaidi kuliko akili, hili ni tatizo. Kwa maelezo yake tu inaonekana dereva wa hiyo gari alikuwa na makosa, kwanza amegonga na kukimbia, na pili ameenda kufanya fujo kwny msafara wa chama pinzani!!!! ingetokea hvo kwa mtu wa chadema sijui maelezo yangeegemea wapi?!!!! Halafu hebu nijuzeni, kwani kulitangazwa halii ya hatari au watu kutotembea usiku? Kwa nini polisi izuie watu kutembea usiku, inatakiwa kuwalinda na vibaka, au kuna point naikosa? KITAELEWEKA TU, nyie makamanda mjue november mtakuwa na bosi mpya, HANA MCHEZO, inabidi muende shule!:faint:
 
Na hajasema huyo dereva wa CCM kakamatwa au vipi....kwake yeye wakosaji ni CHADEMA tu
 
...of course kama kuna vurugu mahali itatokea, wahusika wakuuu ni polisi, kwa kukamata kila wanayemhisi anafanya vurugu. Hawa jamaa sijajua wanafanya kazi kwa maslahi ya nani, wakati sie WALINDWA ndio waajiri wao. Kumbukeni vizuri ile stori ya mwanafunzi wa shule ya Sekondari Iyunga (Mbeya) aliyeuawa mikononi mwa Polisi, wakimtuhumu kuanzisha mgomo shuleni pale.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom