Sakata la Lovness Tarimo limejaa ukakasi

Sakata la Lovness Tarimo limejaa ukakasi

Hahahaha binti juha kweli huyu.. Kumbe ndivyo wanavyofanya.. Lakini bado kuna ukakasi huyu nyuma yake kuna mtu au watu wanamtumia
Mbona sijaona ukakasi wowote.
Kuna picha alikuwa miss fitness 2019 kama sikosei alikuwa alikuwa ana mwili wa kimazoezi lakini wa kike.

Ametrend kwa jinsi alivyo kiume na si kingine. Watu wanamuhoji na yeye kaamua kutumia fursa.

Siku hizi kila kila kitu ni fursa, ujue tu kuitumia fursa ya umaarufu vizuri.
 
Huyo ni mwanamke ,kumbe hujui watu wavypenda trend kuna yule mwanariadha Semenya hata wenzie walikuwa hawamtaki ila ni mwanamke kabisa.
Ila wanasema Semenya alipimwa alikutwa na korodani mbili Kwa ndani, na sasa hivi ameoa mwanamke mwenzake.
 
Wakati mijadala ikielekea mwishoni kuhusiana na kijana Lovness Tarimo na jinsia yake ambaye kwa mwonekano tuu huwezi kumuweka kwenye jinsia ya like bali ya kiume
Na hata kama ni mwanamke basi ana silika nyingi za kiume kuliko za kike... Lovness ni mwalimu wa mazoezi gym na ana misuli ya kutosha sana
Sakata lake lilizidi kuchukua sura mpya mitandaoni baada ya kuwahakikishia watu kupitia mahojiano mbalimbali kwamba yeye ni mwanamke na ana mchumba na hivi karibuni anatarajia kuolewa
Tukiachana na maswali ya maandishi wetu ya kumuuliza kwamba ni lini aliondolewa ubikira wake na kama anaingia kwenye siku zake kama wanawake wengine, juzi akajitokeza mwanadada aliyedai ni mke halali wa Lovness walikuwa wanaishi Wote Canada na wana mtoto
Mwanadada anadai mme wake Lovness aliondoka Canada wiki mbili zilizopita na kurudi Tanzania na nipo kupitia mitandaoni akasoma habari hizo za aibu za mumewe kujitangaza ni mwanamke

Mdada huyo akiongea kwa uchungu na majonzi huku akijizuia sana asilie kutokana na habari za mumewe huyo aliahidi kufanya lolote ili apate pesa za kumtibia mumewe kwakuwa anaamini kuna kitu Kibaha kimempata mpaka kufikia kufanya aliyofanya

Kitu kilichokuja kumpa mshtuko karibia azirai ni pale mwandishi aliyekuwa anaongea naye kumwambia mchumba wa kiume wa Lovness ni mzungu

Sasa hebu tujiongeze kidogo tusijekuwa tunalishwa matango pori na Hizi bongo muvi zisizoisha
Ni nani alimuibua Lovness Tarimo?
Ni nani aliyehakiki jinsia yake?
Ni nani aliyejaribu kuhoji background yake?
Je huyo mchumba mpya wa Lovness kuna mwandishi alihangaika kumtafuta na kumhoji?
Kwa mwanamama anayedai Lovness ni mumewe wa ndoa na walikuwa wanaishi wote Canada, je kuna ithibati zozote kazitoa hasa nyaraka kuthibitisha madai yake?
Kwa mwandishi aliyemhoji huyo mwanamama imekuwaje ndio huyohuyo alimhoji Lovness!? Je ni coicedence ama?
Hii habari ina ukakasi mwingi, lakini poa kwa wazazi kama ikithibitika Lovness ni mwanaume je ni sahihi kumpa mtoto wa kiume jina ambalo limekaa kike?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wachagga wana matatizo ya jinsia.
 
Back
Top Bottom