Sakata la kuteswa Kibanda, Waziri Membe atajwa!

Sakata la kuteswa Kibanda, Waziri Membe atajwa!

Tatizo tuna serikali dhaifu!

Kwanini asikamatwe!

Ukweli umeanza kujilikana!

Laana inawaandama watu wa CCM ndio maana kila siku mnaumbuka!

Mlianza kuwazushia CHADEMA sasa mnaanza kuumbuana wenyewe kwa wenyewe!

Na hii laana itawatafuna mpaka mtoke madarakani!

Hapo kwenye red sijakusoma mkuu; Kamanda hata wakitoka madarakani hiyo laana itaendelea kuwatafuna wao na vizazi vyao hadi wanaingia kaburini.
 
Bashe aache kukurupuka kuongea mambo asiyona ushahidi nayo, huo unakuwa kama umbea tu na kuwapaka watu matope kwa manufaa ya kundi fulani
 
Bashe aache kukurupuka kuongea mambo asiyona ushahidi nayo, huo unakuwa kama umbea tu na kuwapaka watu matope kwa manufaa ya kundi fulani

Mkuu kati yako na Bashe ni nani anayekurupuka ? Kwani ni nani asiyejua ya kuwa muishiwa Miyembe alisha tangaza ana maadui kumi na moja na waandishi wa habari wakiwamo?
 
Kwa mujibu wa afisa mtendaji mkuu wa New Habari ambao ndio waajiri wa Kibanda ndugu Hussein Bashe, yupo mwanasiasa aliyetangaza vita ya wazi na waandishi wa habari kwa kuwa eti ni kikwazo kwa mipango yake ya kuwania urais 2015.

Bashe hakumtaja huyo mwanasiasa ila naamini kati ya wana jamvi wote yupo au mpo mnaomjua huyu mwanasiasa.

Kwa faida na usalama wa waandishi na taifa kwa ujumla ni bora atajwe ili waandishi wakae chonjo kila wakimwona, wakimsikia au hata kuhisi uwepo wake. Asichoweza shetani ni kumshawishi mungu amsamehe ila yaliyobaki yote yapo ndani ya uwezo wake.

SOURCE: ITV HABARI

Tatizo wadau JF walio wengi hawatunzi kumbukumbu ya matukio au kukumbuka yaliyokwisha jadiliwa hapa. Nijibu kwa uwazi kama ifuatavyo:

Edward Lowasa alipoanza kufumbua kinywa chake baada ya kimya kingi baada ya kupagawa na roho wa Bwana alipoombewa huko West Africa, alirudi na kuitisha vyombo vya habari. Moja ya tamko lake lilikuwa kuwatisha waandishi wa habari na vyombo vya habari kwamba chombo cho chote au mwandishi wa habari akiendelea kumwandama kwa kuandika tuhuma za kashfa zake atafunguliwa mashtaka mahakamani, Alikanusha kwamba tuhuma zote hazimhusu na hakuna ushahidi juu ya tuhuma hizo.
 
Swali hapa je huyu Huseein Bashe ni credible person to listen to?
 
Swali hapa je huyu Huseein Bashe ni credible person to listen to?
Tatizo wadau JF walio wengi hawatunzi kumbukumbu ya matukio au kukumbuka yaliyokwisha jadiliwa hapa. Nijibu kwa uwazi kama ifuatavyo:

Edward Lowasa alipoanza kufumbua kinywa chake baada ya kimya kingi baada ya kupagawa na roho wa Bwana alipoombewa huko West Africa, alirudi na kuitisha vyombo vya habari. Moja ya tamko lake lilikuwa kuwatisha waandishi wa habari na vyombo vya habari kwamba chombo cho chote au mwandishi wa habari akiendelea kumwandama kwa kuandika tuhuma za kashfa zake atafunguliwa mashtaka mahakamani, Alikanusha kwamba tuhuma zote hazimhusu na hakuna ushahidi juu ya tuhuma hizo.
 
Kwa mujibu wa afisa mtendaji mkuu wa New Habari ambao ndio waajiri wa Kibanda ndugu Hussein Bashe, yupo mwanasiasa aliyetangaza vita ya wazi na waandishi wa habari kwa kuwa eti ni kikwazo kwa mipango yake ya kuwania urais 2015.

Bashe hakumtaja huyo mwanasiasa ila naamini kati ya wana jamvi wote yupo au mpo mnaomjua huyu mwanasiasa.

Kwa faida na usalama wa waandishi na taifa kwa ujumla ni bora atajwe ili waandishi wakae chonjo kila wakimwona, wakimsikia au hata kuhisi uwepo wake. Asichoweza shetani ni kumshawishi mungu amsamehe ila yaliyobaki yote yapo ndani ya uwezo wake.

SOURCE: ITV HABARI

bernad camilius membe ritz uncle
 
Last edited by a moderator:
Na alaaniwe.get well soon jembe langu kibanda!

Huyu jamaa ilinipa wasiwasi mkubwa baada ya kusia alikuwa ngome ya lowasa na alisema fisadi huyu ndiye anaetakiwa kuwa rais mwaka 2015 angali anamjua
 
Membe alisema wapo watu 10 atawamaliza.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
*Jina lake latajwa mipango ya matukio ya kigaidi
*Agoma kuzungumza, simu yake yaita bila majibu
*Wadau wa habari kukutana na taasisi za usalama

JINA la Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaitafa, Bernard Membe, limeanza kuhusishwa na tukio la kutekwa na kuteswa kikatili na watu wasiojulikana lililomkuta Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda.

Madai ya kulihusisha jina la Waziri Membe na tukio hilo, yalianza kuzagaa miongoni mwa watu waliofika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumjulia hali Kibanda, muda mfupi baada ya kutendewa unyama huo.
Makundi ya watu waliokuwa hospitalini hapo walilioanisha tukio hilo na kauli iliyopata kutolewa na Waziri Membe katika mahojiano ya kipindi cha Dakika 45, kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, alipoeleza kuwa anao maadui wakubwa 11, wakiwamo waandishi wa habari wawili ambao aliahidi kuwashughulikia.

Ingawa Membe alikutana na shinikizo la watu mbalimbali lililomtaka awataje maadui zake hao 11, wakiwamo waandishi wa habari wawili ambao alikuwa na mpango wa kuwashughulikia, hadi sasa hajapata kufanya hivyo, jambo ambalo linadaiwa na wadadisi wa mambo kuwa ni uamuzi wake wa kuchukua mkondo wa kutekeleza kile alichokisema kwa vitendo.

Tamko lake hilo katika kipindi hicho kilichorushwa hewani Julai 16, 2012, ambalo limeibua hali ya sintofahamu, sasa linaonekana kuchukuliwa kwa uzito zaidi na wanahabari na wamiliki wa vyombo vya habari, baada ya kuwa moja ya mambo mazito yaliyozungumzwa jana katika mkutano wa wamiliki wa vyombo vya habari.

Kwa takribani siku mbili, Membe amekuwa akitafutwa na gazeti hili kwa ajili ya kuzungumzia madai hayo, lakini hata hivyo jitihada za kuzungumza naye hazikufanikiwa, baada ya simu yake kuita wakati wote bila majibu.

Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya kiganjani, hakujibu, licha ya kuonyesha umefika.

Jana katika mkutano huo wa wamiliki wa vyombo vya habari ulioketi Hoteli ya Serena, Dar es Salaam, kujadili kuzorota kwa mazingira ya usalama ya waandishi na wanaharakati wengine, suala hilo la Membe pia lilijadiliwa.

Wakijibu maswali ya waandishi waliotaka kujua namna viongozi wa serikali na watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama wanavyohusishwa na matukio ya aina hii, wamiliki hao walieleza kuwa wapo baadhi ya watendaji waandamizi wa serikali waliokwishalitangazia taifa kuwa wanao maadui 11 hapa nchini, wawili kati ya hao ni waandishi wa habari walioahidi kuwashughulikia.

Akizungumza kwa niaba ya wamiliki wenzake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Hussein Bashe, alisema ni jambo la kushangaza kuona kauli kama hiyo iliyotolewa na kiongozi mwandamizi wa serikali haijafanyiwa kazi na vyombo vya ulinzi na usalama.

"Mfano, mwaka jana, alinukuliwa mwanasiasa na kiongozi wa Serikali kupitia kipindi cha Dakika 45, akisema kuwa ana maadui 11 ambao kati yao, wawili ni waandishi wa habari, hivi kauli hii ambayo ilikuwa ikiruka katika kituo cha luninga haikusikika au adui mwenyewe kati ya waliotajwa ndiyo Kibanda?

"Kama ni hivyo, mbona haitwi ili ahojiwe kuhusu hali hii na vyombo hivi vya ulinzi na usalama vya nchi yetu, tunahitaji kuona kuwa Serikali yetu inafanya kazi na hata kulinda maisha ya watu wake," alidai Bashe.

Sehemu ya kauli ya Waziri Membe katika kipindi hicho kilichokuwa kikiongozwa na mtangazaji Selemani Semunyu, ambayo sasa inaonekana kuwa hatari kwake, alisema: "Lazima watu hao wajue kwamba ukikaa juu ya nyoka, ipo siku atakugonga tu. Hili nawaachia Watanzania waamue, lakini kuna watu 11, wakiwamo waandishi wawili wa habari, nitawatwanga kweupe."

Kutokana na hali ya kuzorota huko kwa usalama, hususan wa wanahabari, wamiliki hao waliazimia kuundwa kwa kamati ya watu 16 ambayo itakutana na vyombo vya usalama nchini kuzungumzia kwa undani wa tukio hilo na usalama wa makundi yanayolengwa na vitendo vya kushambuliwa, kuumizwa na hata kuuawa kwa waandishi.

Maazimio mengine yaliyofikiwa katika mkutano huo ni kuitaka serikali kuunda tume huru ya wapelelezi kuchunguza undani wa sakata hilo, kwa sababu kasi ya upelelezi wa vyombo vya usalama vya hapa nchini hairidhishi na kwamba baadhi ya watendaji ndani ya vyombo hivyo wanahusishwa na matukio haya ya utesaji na utekaji.

Aidha, katika kikao hicho, wanachama wa MOAT ambao walisoma tamko lao kwa waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao chao, walisema pamoja na kuwepo kwa vitendo vya kuwatesa na kuwaua waandishi, bado ukweli utasimama katika jamii.

Wamiliki hao, ambao waliachiana zamu kusoma tamko lao, walisema vyombo vya usalama kudaiwa kuhusika na vitendo vichafu dhidi ya rais ni udhaifu.

Mmoja wa wajumbe hao, Reginald Mengi, akisoma moja ya maazimio ya mkutano huo, alisema kumekuwa na tishio dhidi ya wanahabari, huku akimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kutaja maofisa wa vyombo vya ulinzi waliokwenda nyumbani kwa mwandishi wa habari, Eric Kabendera na kuwatisha wazazi wake.

"Tunajua wazi jambo hili lilipangwa na watu ambao wamekuwa wakitumia fedha hata za ufisadi ili kutishia uhai wa waandishi wa habari, kutokana na matukio haya yaliyojitokeza namuomba Waziri Nchimbi awataje maofisa hao, kama asipofanya hivyo tutawataja kwa majina mchana kweupe.

"Pamoja na hila na vitimbi vinavyofanywa na watumishi hao wa idara za ulinzi na usalama dhidi ya wanahabari, ni vema Serikali ichukue hatua za haraka ili kuondoa hali hii. Hivi sasa Watanzania wamekuwa wakiishi kwa woga na katu huwezi kusema nchi ina amani huku watu wake wakitishwa.

"Ninapenda kusema kuwa kwa matukio haya ya kupigwa na kuteswa kwa Kibanda na hili tukio la wazazi wa Kabendera kuhojiwa kule Bukoba, ni wazi hata wakituua watakaobaki watasema ukweli wa nini kilichopo sasa," alisema Mengi.

Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa MOAT, pia alitumia fursa hiyo kutangaza majina ya kamati itakayokutana na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, kuwa ni pamoja na yeyé mwenyewe ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo, wajumbe ni Hussein Bashe, Tido Mhando, Aga Mbuguni, Abdallah Mrisho, Ansbert Ngurumo, Mikidadi Mahamud, Pili Mtambalike, Godfrida Jola, Tumaini Mwilenge na Deodatus Balile.

Wengine ni Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri nchini, Neville Meena, Samson Kamalamo, Henry Muhanika, Japhet Sanga na Jesse Kwayu.

Alisema wadau hao, mbali na kukutana na Waziri Nchimbi, pia watakutana na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Othuman Rashid na Naibu wake, Jack Zoka pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dk. Edward Hosea.

CHANZO: MTANZANIA JUMATANO
 
Nilichosoma kwenye magazeti alichosema Membe,MAADUI ZAKE WATAAMA NCHI. Ambacho sioni ubaya wowote.
 
si aseme tu kama ni yule alietabiriwa na mnigeria atakuwa rais?
au ni yule aliejenga ofsi ya spika jimboni kwake?
au ni yule anaemiliki hoteli fukweni huko wanakogombania gas
au ni yule tembo wakimwona wanatetemeka sana???
au ni yule alikuwa prefect katika muungano wa nchi za watu weusi??/?
taja Bashe la sivo tutajua ni mikwala yako tu kujijenga kisiasa
nahisi ni yule uliegombana nae na ndio mmiliki wa hotel huko fukweni kwa chamaki nchanga kwenye Maembe mengi

At DENTIST naye anautaka U-RAISI, Duh Kweli umekuwa RAHISI.
 
Mmmhhhhh ...!!!!!!!!!!! Labda rafiki yangu Pasco ukanieleweshe kidogo hapa maana sijaelewa kitu kabisa humu.
 
Sasa itakua ni kipigo endelevu kwakua hawa waandishi wa kibongo wanapenda mshiko na kutumiliwa, hii ndio faida yake usitegemee kama utamuonea mwengine na wewe ukabaki salama iko siku yako tuu.
 
Back
Top Bottom