Sakata la kupandisha madaraja kwa rushwa Moshi: Idara ya utumishi manispaa yapanga mbinu chafu kujiokoa

mtumishihuru

Member
Jan 8, 2020
8
45
Poleni kwa ukimya wa siku kadhaa, tulikuwa na majadiliano na wanasherua kadhaa kupata ushauri wa namna ya kuwa salama iwapo tutaamua kuweka ushahidi ambao unaweza kuambatana na ku-reveal identity. Tuko pazuri! Niwashukuru sana wanajamvi wanaozidi kutuma salamu za pole na wengine kutuma evidence zaidi. Hii ni vita inayogusa vyeo vya watu ambao pia wana viconnections vyao na wanaweza kuvitumia kujiokoa. Hata hivyo kwa nguvu za Allah, dhalimu itashindwa na haki!

Basi wakati tukiwa chimbo hasa baada ya kuanika tabia chafu n* udhalimu wa baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya utumishi Manispaa ya Moshi kupandisha madaraja watumishi kwa rushwa na baada ya Idara hii kujikanganya na kuwashusha madaraja walimu waliopandishwa hivi karibuni ((niseme baadhi kwa sababu si wote...ni wachache tu ndiyo wanaichafua hii idara na tutadeal nao, pia nakala za barua zipo), kwa takribani wiki nzima wamekuwa wakijadili namna ya kujiokoa. Bahati mbaya kabisa Mkuu wa Idara pia amejiingiza katika mtego wa wadhalimu hawa. Katika moja ya vikao vya ndani chini ya mkuu wa idara ambacho audio za mazungumzo yake tunayo ( shukrani sana kwa mzalendo uliyetutumia audio hii), mapendekezo kadhaa yalitolewa kama ifuatavyo:
1.Kuendelea kuwa karibu na walimu walioshushwa daraja ili wasije wakatoa siri ya majadiliano yaliyofanyika kabla hawajashushwa ( kumbuka tulisema kabla ya kushushwa waliitwa wakabembelezwa kuhusu kushushwa). Hofu kubwa ya wadhalimu hawa ni kwamba iwapo walimu hawa walioshushwa wakiitwa na TAKUKURU wanaweza kutumia hasira ya kushushwa na kuwageuka na kusema kweli kwamba walitoa rushwa. Hili likifanyika litakuwa pigo kubwa sana kwa Idara na hadi mkuu wa idara anaweza kupoteza nafasi yake. Inshallah, tuna imani mbinu hii itashindwa!

2.Mbinu ya pili iliyopangwa ni kuwarubuni baadhi ya walimu ili waweze kumtaja mmojawao kama mwandishi wa makala. Hii iitawapa Idara justification ya kumfanyia kitu kibaya ili iwe mfano kwa walimu wengine wasiwe waropokaji. Majina kadhaa ya suspects yalitajwa kutokana na kuunganishaunganisha matukio ya walimu waliokuwa mstari wa kufuatilia madai yao. Ugumu wa hili ulionekana kuwa kuna wasiwasi kama walimu walengwa watakubali kujitoa mhanga ili kuwasingizia wenzao. Hapa Grace akapendekeza itumike mbinu ya kuwarubuni wachache kuwa watapandishwa daraja baada ya miezi kadhaa. Hili lilipita na linasubiri utekelezaji. Majina ya wanaopanga kusingiziwa uandishi wa makala tunayo na tumeanza mawasiliano nao kuona namna bora ya kisheria ya kuwaokoa. Tutaendelea kulifuatilia hili kwa karibu na kuanika ukweli hapa.

3. Mbinu ya tatu ilikuwa ni kwenda polisi kufungua kesi ya matumizi mabaya ya mtandao. Changamoto wakati wa kujadili mbinu hii ilionekana kwamba walishajichanganya wakawashusha madaraja baada ya makala kutoka meaning ni USHAHIDI kuwa tuhuma zilikuwa za kwenye makala zilikuwa za kweli. Hofu kubwa ni kuwa japo lengo ni kushift attention kwenda kwa mwandishi wa makala kama mwenye makosa ili kuwapumbaza watu macho wasiangazie udhalimu uliotajwa katika makala, je akitokea kiongozi mkubwa akafuatilia reaction yao kwenye makala itakuwaje?. Pia kulikuwa na hofu kuwa mwandishi alisema mambo haya yamefika TAKUKURU na fact kwamba wamewashusha wafanyakazi madaraja ni evidence kwamba madai yana ukweli.Pia wakienda polisi wanahitaji kuwa na evidence za wanao wasuspect lakini hawana evidence...na polisi haifanyii kazi hisia. Hata hivyo ilipendekezwa kwamba kwenda Polisi bado ni muhimu ili kuonekana walau walichukua hatua baada ya kutuhumiwa. Kwamba ikitokea kiongozi akahoji watakuwa na uwezo wa kukana kwamba sisi hatuhusiki na suala hili tumeripoti Polisi. Hapa mkuu wa idara na watumishi wengine walisema wanafahamiana na wakubwa wa Polisi Manispaa ya Moshi na kwamba watatafanya mawasiliano ili wapate msaada. Hili nalo tunalifuatilia kwa karibu kuona utekelezaji wake

Hata hivyo Idara imeanza kuwa na hofu iwapo Mkurugenzi atawaunga mkono hadi mwisho. Kumbuka Mkurugenzi ni mtu mpenda haki na inawezekana akawaacha wafe na msalaba wao.

MY TAKE: Idara ya utumishi wamepaniki sana na wanaona mambo yamewakalia vibaya. Badala ya kuadress issue ya msingi- upandishaji madaraja kwa rushwa- sasa wanataka kujinasua kwa gharama yoyote.

Kwa sasa kikundi chetu cha watumishi huru tunawashukuru sana walimu ambao wameendelea kututumia documents zaidi.Sisi mmoja mmoja pia tumepata fursa ya kukusanya ushahidi. Tumefarijika kupata uungwaji mkono mkubwa na Mungu awabariki.

Wajibu wa kikundi chetu sasa ni kuwalinda waalimu ambao wanaweza kuwa wahanga wa mbinu hizi chafu. Documents ziko-organised zote na iwapo hawataachambinu hizi chafu nakala zitaenda TAKUKURU, CWT, kwa mkurugenzi, MKOANi na Tamisemi.

Allah pamoja nasi daima!
 
moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,323
2,000
Mh Jaffo, ebu fatilia jambo hili ili na hatua stahiki zichukuliwe.
 
Lwamadovela

JF-Expert Member
Mar 5, 2019
268
250
Hakuna kitu naumia kuona

Mungu yupo!!
 
NDUKI

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
3,085
2,000
Mh Jaffo, ebu fatilia jambo hili ili na hatua stahiki zichukuliwe.

Kwenye kikao cha kutimia kwa AKIDI watu wamefoji jina hakufatilia wala hatua stahiki hazijachukuliwa itakuwa hili ndugu.
 
Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,529
2,000
Kwani kwa kawaida madaraja uwa yanapandishwa mwezi wa ngapi kwenye hizo halmashauri hadi kupelekea baadhi kuahidiwa kupandishwa miezi michache ijayo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom