Habari wakuu,
Kwanza nianze kwa kuwapongeza wanafunzi wote waliofaulu kwenye matokeo yaliyotangazwa leo ya kidato cha sita, nawapa pole ambao alama zao haziridhishi na wasife moyo pia nawapa pole zaidi wale ambao wamefaulu lakini kulingana na vigezo vipya, alama walizopata hazitotosha kusonga mbele kwenye vyuo vyote nchini.
Kilichonileta leo ni tangazo ambalo limetolewa na tume ya vyuo vikuu kuhusu kutangaza vigezo vipya ili kudahiliwa vyuo vikuu. Humu jamvini tuna mjadala wake pia unaosema TCU yatangaza alama mpya kwa mwanafunzi kuingia Chuo Kikuu. Cha ajabu nafungua gazeti la habari leo la leo, kuna sehemu afisa muandamizi wa TCU anasema tangazo halijatoka kwao. Nikajisumbua kuingia tovuti ya TCU na kulikuta na vigezo ambavyo wanasema hawajavitoa, vipo!
Tukiacha kwamba vigezo kuwa vikubwa hasa kwa wanaotoka stashahada, Najiuliza

- Hivyo vigezo alivitoa nani?
- TCU walivijadili kabla ya kuvitoa kwa umma?
- Coordination ilivyo ndani ya TCU kama taasisi hasa kwa unyeti wake kwani tumeikabidhi jukumu kubwa la kuendesha elimu ya vyuo vikuu nchini
- Mwisho vigezo walivyotoa tumetofautiana na karibu dunia nzima hata kwa nchi ambazo zimetuacha mbali kwa ubora wa elimu.