Sakata la Kibiti: Mwigulu Nchemba ni wakati wa kujitafakari na kujiuzulu ateuliwe Adadi Rajab

Kazi ya Waziri sio kubeba SMG na kupambana na majambazi. Hata IGP hatakiwi kwenda front line kupambana na majambazi/magaidi. Kazi zao ni za kimkakati zaidi. Haihitaji Waziri aliyewahi kuwa polisi-kama tuna akili hiyo basi achukuliwe polisi aliyekuwa mkuu wa opereshen na mafunzo kama Chagonja na Venance Tossi maana hao ndo wana uzoefu na upambanaji na operesheni, sio Adadi Rajabu aliyekuwa mkuu wa upelelezi.

Ktk suala la Pwani, serikali imekwama kwenye intelijensia. Tuombe usalama wa taifa na kitengo cha upelelezi cha polisi waongeze juhudi zao. Mashambuliz ya Pwani yana ajenda flani ya siri kiasi kwamba hakuna mtu yupo tayari kushirikiana na vyombo vya dola. Kwa hiyo tatizo sio nguvu, tatizo ni intelijensia na injelijensia inatokana na taarifa zinazotolewa na wananchi. Diplomasia itumike ili kuwashawishi watu watoe taarifa na sio kuwapa watu vyeo vikubwa kana kwamba wao ndo wanaopeleleza.
 
Naheshimu sana utendaji kazi wa Mh.Mwigulu,Nathamini mchango wake katika ujenzi wa taifa la kizalendo..Nyingi za falsafa anazoziamini kuhusu uwajibikaji/uzalendo zinatumiwa kwa kiasi na Serikali ya awamu ya tano na ktk ilani ya chama dola..

Lakini ili kulinda heshima ya serikali na yake,kesho yake ya kisiasa na kuthamini utaratibu wa uwajibikaji anapaswa kujiuzulu.Nadhani ndani ya CCM kuna utaratibu mzuri wa kujitafakari kutokana na makosa yanayotendwa na walio chini {subordinates}.Kujiuzulu haina maana kakosea yeye bali walio chini yake wakati mwingine mfumo.

Pamoja na hili ipo haja ya Kuunganisha Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Ulinzi ili kuimarisha mbinu,mipango,mikakati na utekelezaji wake mtambuka hivyo Majeshi yote kuwa chini ya Waziri mmoja japo chini ya idara tofauti {JWTZ,Polisi,JKT,Magereza,Zimamoto,etc}.
 
Bado sijaona Hoja ya Msingi ni kwanini mkomalie Mwigulu awajibishwe.

Je kuna sehemu Polisi wamekwamishwa kufanya kazi zao!!

Toeni Hoja ambazo ni very technical in connection to his role. Au tu ni kwavile ni Waziri wa hiyo wizara.

Kwanini isiwe ni RPC wa Pwani na chain yake ya Command hadi kwa commissioner wa Operation. Hoja iwe kama kuna hitaji lolote lakutekeleza kazi yao lilikwamishwa na Mwigulu.

Kwanini isiwe RSO wa Pwani anayehusika ktk kukusanya taarifa nakuzifanyia kazi kisha kutoa taarifa sahihi na kwa wakati zinazoweza kusaidia polisi au vyombo vingine kuchukuwa hatua kuzuia madhara.

Hoja iwe kuwa taarifa hizo zilikusanywa nakuchambuliwa na zilizomuhusu waziri Nchemba hazikuzingatiwa, alipuuza au kuchelewa kuchukuwa hatua.

Kipindi cha vita ya Kagera chukulia Askari wa adui kila kukicha wanapenya nakukamata maeneo yetu. Lakini wakati huohuo askari wetu wanapatiwa logistics zote wanazohitaji ili waweze kukabiliana na adui. Je ikitokea wanazidiwa tena wetu wapo wengi na silaha nzito zaidi mfano kwa uwiano wa 3:1. Je hapo waziri anahusikaje!! Hoja ingekuwa kama waziri alizembea walipohitaji logistics nk.

Tatizo letu huwa tukiona mtu fulani nyota yake inang'aa na anaweza kufanikiwa zaidi mbeleni basi JUHUDI ZINAFANYIKA ZA KUMCHAFUA NAKUTAKA AWAJIBISHWE HATA KWA SUALA AMBALO HALIMUHUSU.

Jicho la tatu lapaswa kutumika ili kuangaza nini hasa kiini cha tatizo..Taifa linakabiliwa na tishio kubwa la kiusalama ikiwa vitendo hivi vyenye athali kijamii,kisiasa na kiuchumi vitaachwa ..lipo tatizo na upo udhaifu katika mifumo yetu ya utendaji,usimamiaji na utekelezaji..Tatizo sio mtu.
 
Kwa akili ya yule jamaa atakuja anasema wengine waliuawa wakati yeye si waziri anaonewa

Umenichekesha sana,japo mambo yanahuzunisha,atahesabu ndani ya muda wake wamekufa wangapi na kabla wamekufa wangapi?
 
aliyoandka mkuu ni kweli kb sio mwigulu nnaemfahamu mm huenda ulikua humfatilii huko nyuma,,kapoa sanaaa,na makamba nae ndo JIIIII
Mkuu ni kweli,Nchemba na Makamba walipaswa kutumbuliwa zamani sana. na nadhani hawa ni muda tu, watatumbuliwa.Ila mimi naona ni kama mawaziri wote pamoja na Waziri Mkuu wao. Waziri Mkuu alikuwa moto mwanzoni lakini naye sasa kimya, Waziri wa elimu naye hivyo hivyo,Maghembe ndiye wala hajawahi kufurukuta,pamoja Mwakyembe na wengine.Ambao tunawasikia sikia ni Umi,Waziri wa Afya,Waziri wa Ardhi na Mbarawa.Sijui kuna nini.
 
Mkuu ni kweli,Nchemba na Makamba walipaswa kutumbuliwa zamani sana. na nadhani hawa ni muda tu, watatumbuliwa.Ila mimi naona ni kama mawaziri wote pamoja na Waziri Mkuu wao. Waziri Mkuu alikuwa moto mwanzoni lakini naye sasa kimya, Waziri wa elimu naye hivyo hivyo,Maghembe ndiye wala hajawahi kufurukuta,pamoja Mwakyembe na wengine.Ambao tunawasikia sikia ni Umi,Waziri wa Afya,Waziri wa Ardhi na Mbarawa.Sijui kuna nini.


ummy anaonekana anafanya kazi kwa woga (nionavyo mimi)yaan km fata kaupepo
 
Halafu wanakuwa vinganganizi ata kama ameshindwa kutekeleza majukumu yake
 
Kwa sababu watu 38 wamepoteza maisha chini ya wizara yake,idad ambayo inaipita ya wanafunzi na dereva waliokufa kwenye ajali ya Lucky Vicent,kama jeshi lililo chini yake limeshindwa kuwalinda watanzania wenzetu baso hana sababu ya kuendelea kuwepo ofisini
Non-sense
Kwani ajali ya Lucky Vicent Mwigulu ndo alisababisha?, hao watu 38 waliokufa kibiti Mwigulu kahusikaje?
Mauaji ya kibiti ni mambo yanayohitaji ushirikiano wa wananchi na jeshi la polisi, sasa waziri kazuia nini hapo.
Je ingekua Tanzania ndo Kenya kwa Alshabab mngesema serikali ijiuzuru?
Watanzani mkikosa hoja mna maneno yasiyokua na maana
 
Watanzania wengi tu tumechoshwa na Mauaji kibiti.

Hii wizara inahitaji wataalam wa mambo ya ulinzi na wabobezi kama Adadi Rajabu. Ushauri wangu Mwigulu sio strategic katika hili yeye ni mchumi , haitaji eleimu ya Chuo kikuu kuona kuwa kakwama 100%; Tunaweza sema tatizo lilikuwa IGP , katolewa IGP bado wembe ni ule ule. niwakati wa Mwigulu kuchukua maamuzi magumu ya kuachia ngazi ; Kama Ally Hassani Mwinyi , kule Shinyanga.
Si wa kwanza . Kaenda mpaka Kibiti kafanya Mikutano , Karusha picha za watuhumiwa na Donge nono . Bado Fail

CC JPM
Why Adadi? Personal interest eee??
 
Back
Top Bottom