Sakata la Kibiti: Mwigulu Nchemba ni wakati wa kujitafakari na kujiuzulu ateuliwe Adadi Rajab

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,541
2,000
Non-sense
Kwani ajali ya Lucky Vicent Mwigulu ndo alisababisha?, hao watu 38 waliokufa kibiti Mwigulu kahusikaje?
Mauaji ya kibiti ni mambo yanayohitaji ushirikiano wa wananchi na jeshi la polisi, sasa waziri kazuia nini hapo.
Je ingekua Tanzania ndo Kenya kwa Alshabab mngesema serikali ijiuzuru?
Watanzani mkikosa hoja mna maneno yasiyokua na maana
Halafu wewe ndio utakuwa wa kwanza kupongeza siku rais akimtumbua mwigulu.
 
Good Father

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
9,309
2,000
Umekunywa maji ya bendera ya kijanai utaacha kushangilia atakaloamua mwenyekiti wako
Sina chama wala haitatokea kuniona nashangilia vyama vya kipuuzi sijui ccm, chadema,act etc
Nyie ndo mna njaa hangaikeni na vyama.
Kazi yangu inanitosha sina haja ya kufanya unafiki
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,643
2,000
Hiyo ni chuki binafsi kwa Mwigulu

Hivi kwann watu hatupendani, akijiuzulu wewe utapata nn kwa mfano...
Kujiuzulu sio solution,solution ni kupanga mikakati yenye tija,kwa kutumia vikosi maalum vya kupambana na magaidi.Na kutumia mitambo na zana za kisasa.
Kama hatuna ombeni msaada kwa nchi zilizobobea kupambana na magaidi.
Magaidi sio wezi wa kuku,ni watu wamejifunza mbinu za medani kwa kiwango kikubwa,na hatujui undani wa watu hao.
 
Feb 15, 2017
8
45
BARUA YA WAZI KWA RAIS MAGUFULI

Kwako Mtukufu Magufuli, Rais wa Wanyonge na Wanafunzi Wasiobeba Mimba, Mtumbua Majipu Mkuu, Msutaji Mkuu, Usiye na Doa (Mr. Clean), Tingatinga, nakadhalika nakadhalika……………………

Salaam!

Ninaandika Waraka Huu kwako ili kukumbusha kuwa “Tanzania kwanza UCCM baadaye”. Kama ilivyokuwa kwa Ali Hassan Mwinyi enzi akiwa waziri wa mambo ya ndani, Baada ya kuharibu na kushindwa kusimamia ulinzi na usalama katika wizara yake, aliwajibika kujiuzulu kiungwana ili kumpisha mtu anayeweza kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Alifanya hivyo bila simile kwani alitambua kuwa UCCM upo endapo watanzania wana amani na uwekevu.

Sasa sisi kama watanzania tunaishi kwa taabu, kwa sababu jeshi la Polisi si walinzi tena bali nao ni wahanga wa upungufu wa usalama nchini yaani (2UC). Mauaji yanayoenda huko Kibiti yanatia dosari nchi yetu na kuhanikiza harufu ya chuki.

Kwa picha hii Ndg. Mwigulu Lameck Madilu Nchemba ameonesha incompetence, udhaifu katika wizara yake. Ni vema ili kulinda heshima yake ajiuzulu mwenyewe na ampishe mtu mwingine ateuliwe kusimamia wizaya ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi.

Hebu tujiulize kidogo kama Mwigulu aliomba urais kupitia CCM, Lakini wizara ndogo kama hii inamshinda je angebahatika kuwa amiri jeshi mkuu si watu wangebakwa bila kujali jinsi zao?

“Siasa nzuri siyo ya kujisifia ujinga bali ni ile inayolenga kuwanufaisha watanzania” (Nyerere 1984).

Mheshimiwa Rais Magufuli pokea waraka huu bila jazba uufanyie kazi.

Na Faru Yohana 1999.
Nanjilinji.
 
mtayeshelwa

JF-Expert Member
Oct 28, 2011
1,168
1,500

Maelezo malefu yaliyojaa pumba tupu..
 
R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,000
Kiatu kikubwa hiki!

editoon3june-jpg.522133
ha ha ha ha ha ha
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
7,302
2,000
Hivi kwann mmemkomalia Mwigulu ajiuzulu?
Kuna muda hata baba nyumbani akiona nyumba imemshinda hutafuta ushauri. Kwa yanayo endelea Kibiti Mwigulu ameshindwa kuongoza Wizara, na kama ana taka heshima anatakiwa ajiuzulu Mh rais aweke hapo mtu mwingine mwenye utaalamu wa kikachero na sio Economy class one
 
YusuJo

JF-Expert Member
Apr 10, 2016
538
500
Watanzania wengi tu tumechoshwa na Mauaji kibiti.

Hii wizara inahitaji wataalam wa mambo ya ulinzi na wabobezi kama Adadi Rajabu. Ushauri wangu Mwigulu sio strategic katika hili yeye ni mchumi , haitaji eleimu ya Chuo kikuu kuona kuwa kakwama 100%; Tunaweza sema tatizo lilikuwa IGP , katolewa IGP bado wembe ni ule ule. niwakati wa Mwigulu kuchukua maamuzi magumu ya kuachia ngazi ; Kama Ally Hassani Mwinyi , kule Shinyanga.
Si wa kwanza . Kaenda mpaka Kibiti kafanya Mikutano , Karusha picha za watuhumiwa na Donge nono . Bado Fail

CC JPM

Sidhani kama hili suala ni la mtu mmoja. Kwa hali ilipofikia, hali hii inahitaji collective efforts za watanzania wote. Mimi naamini serikali imefanya juhudi kubwa, serikali inasikikishwa na mauaji haya. Kuna something extra ordinarykwenye suala hili. Si jambola kusema fulani akiwa waziri atamaliza, au fulani akiwa IGP atalimaliza! Ni suala la watanzania kusimama pamoja kukataa mauaji haya. Naamini lazima kati ya watanzania milioni 40 na zaidi kuna wachache wanaelewa kwa namna moja au nyingine mtandao huu hatari unavyofanya shughuli hii.... na hapo ndipo uzalendo unatakiwa kuanzia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom