Sakata la Kibiti: Mwigulu Nchemba ni wakati wa kujitafakari na kujiuzulu ateuliwe Adadi Rajab

Watanzania wengi tu tumechoshwa na Mauaji kibiti.

Hii wizara inahitaji wataalam wa mambo ya ulinzi na wabobezi kama Adadi Rajabu. Ushauri wangu Mwigulu sio strategic katika hili yeye ni mchumi , haitaji eleimu ya Chuo kikuu kuona kuwa kakwama 100%; Tunaweza sema tatizo lilikuwa IGP , katolewa IGP bado wembe ni ule ule. niwakati wa Mwigulu kuchukua maamuzi magumu ya kuachia ngazi ; Kama Ally Hassani Mwinyi , kule Shinyanga.
Si wa kwanza . Kaenda mpaka Kibiti kafanya Mikutano , Karusha picha za watuhumiwa na Donge nono . Bado Fail

CC JPM

Ebu nisaidie kuelewa, una maana huyu adadi ni Bukhari wa kibiti?
 
Mwiguluuuu Leo yamekugeukia kweli CCM kiboko,

Ndio mazala ya siasa za CCM haya..mmateuana kwa kuangalia ukada leo mnalalamikia mazara..

Waziri wa mambo ya ndani anatakiwa na uzoefu wa maswala ya ulinzi na usalama, wako wazee kibao jeshini huko na usalama wa Taifa.
Waziri wa ulinzi Lazima mkongwe kutoka JWTZ na si vinginevyo.. Ukada usiwe sehemu ya uteuzi.
 
Mwigulu akitolewa mauaji yakiendelea utasema nini??
Hakuna anayesema Mwigulu ndiye anayeua watu. Ila kwa kuwa wizara yake inahusika na ameshindwa kudhibiti, ndo maana anatakiwa aachie ngazi. Huo ni ustaarabu kwa mtu aliyeelimika. Unafurahiaje kufanya kazi ambayo matokeo yake hayaonekani? Ndiyo maana wenzetu walioendelea hata wakituhumiwa tu, hujiuzulu. Lakini njaa za mabara maskini, haziruhusu watu kujiuzulu. Pathetic.
 
Kwa sababu watu 38 wamepoteza maisha chini ya wizara yake,idad ambayo inaipita ya wanafunzi na dereva waliokufa kwenye ajali ya Lucky Vicent,kama jeshi lililo chini yake limeshindwa kuwalinda watanzania wenzetu baso hana sababu ya kuendelea kuwepo ofisini
Hiyo ni chuki binafsi kwa Mwigulu

Hivi kwann watu hatupendani, akijiuzulu wewe utapata nn kwa mfano...
 
Hiyo ni chuki binafsi kwa Mwigulu

Hivi kwann watu hatupendani, akijiuzulu wewe utapata nn kwa mfano...
Kwani MUHONGO ameondoka umepata nini?Mtu asipowajibika anawajibishwa, ambapo leo hii inaitwa KUTUMBUA,unaweza ukawa hupendi ila ndo utaratibu huo,ameshindwa kuwajibika anapisha,kama wewe unatafsiri simpendi Mwigulu basi huenda Magufuli ndo hawapendi anaowateua
 
Hata akitenguliwa Mwigulu maana ni maamuzi ya aliyemteua lakini sishauri uteuzi wa Adadi Rajabu kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwasababu ninazozijua Mimi.

Pamoja na Fani yake ya ukachero lakini kwa Serikali ya Magufuli hapana.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hata akitenguliwa Mwigulu maana ni maamuzi ya aliyemteua lakini sishauri uteuzi wa Adadi Rajabu kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwasababu ninazozijua Mimi.

Pamoja na Fani yake ya ukachero lakini kwa Serikali ya Magufuli hapana.
Upo sahihi,abaki kuwa Mbunge tu
 
Hivi kwani serikali inashindwa kupeleka Jeshi kusafisha huo msitu wanaojivunia hao Magaidi.?
 
Bado sijaona Hoja ya Msingi ni kwanini mkomalie Mwigulu awajibishwe.

Je kuna sehemu Polisi wamekwamishwa kufanya kazi zao!!

Toeni Hoja ambazo ni very technical in connection to his role. Au tu ni kwavile ni Waziri wa hiyo wizara.

Kwanini isiwe ni RPC wa Pwani na chain yake ya Command hadi kwa commissioner wa Operation. Hoja iwe kama kuna hitaji lolote lakutekeleza kazi yao lilikwamishwa na Mwigulu.

Kwanini isiwe RSO wa Pwani anayehusika ktk kukusanya taarifa nakuzifanyia kazi kisha kutoa taarifa sahihi na kwa wakati zinazoweza kusaidia polisi au vyombo vingine kuchukuwa hatua kuzuia madhara.

Hoja iwe kuwa taarifa hizo zilikusanywa nakuchambuliwa na zilizomuhusu waziri Nchemba hazikuzingatiwa, alipuuza au kuchelewa kuchukuwa hatua.

Kipindi cha vita ya Kagera chukulia Askari wa adui kila kukicha wanapenya nakukamata maeneo yetu. Lakini wakati huohuo askari wetu wanapatiwa logistics zote wanazohitaji ili waweze kukabiliana na adui. Je ikitokea wanazidiwa tena wetu wapo wengi na silaha nzito zaidi mfano kwa uwiano wa 3:1. Je hapo waziri anahusikaje!! Hoja ingekuwa kama waziri alizembea walipohitaji logistics nk.

Tatizo letu huwa tukiona mtu fulani nyota yake inang'aa na anaweza kufanikiwa zaidi mbeleni basi JUHUDI ZINAFANYIKA ZA KUMCHAFUA NAKUTAKA AWAJIBISHWE HATA KWA SUALA AMBALO HALIMUHUSU.
 
Mwigulu wa awamu ile sio Mwigulu wa sasahivi
Makamba wa awamu ile sio Makamba wa sasahivi.

Hawa wote hawaonyeshi tena Yale makeke yao kwa hofu ya kuambiwa wanajijenga na kukinyemelea kiti cha Mkuu.
Hivi kweli tumefika hapo, I don't think so.
 
Back
Top Bottom