Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,063
- 744
Jumapili Mar 16, 2008 16.03.2008 1429 EAT
*Sasa wanasheria waanza kumbana Lowassa
*Wahoji usahihi wa kauli zake nje ya Bunge
Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete alidanganywa na wasaidizi wake kuhusu mambo mbalimbali katika mchakato wa kusainiwa kwa mkataba wa Richmond kiasi cha yeye kujikuta akilitangazia Taifa habari zisizo sahihi kutoka kwa wasaidizi wake, Majira Jumapili imethibitisha.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa kina kuanzia katika mwenendo wa jinsi kampuni hiyo ilivyopewa tenda hadi ilivyosababisha vigogo kadhaa kung'oka serikalini, sasa ni dhahiri kuwa katika hatua mbalimbali za watu kuonekana walikuwa tayari kuibeba kampuni hiyo kwa gharama zozote, Rais Kikwete naye alijikuta mara kadhaa akipewa taarifa zilizokosa usahihi na kuzitumia majukwaani kufafanua mambo kwa Taifa.
Majira Jumapili sasa imethibitisha kuwa maelezo ya Rais Kikwete wakati wa mahojiano yake na kituo cha Televisheni ya Taifa (TvT) mwaka jana kuwa kampuni hiyo ya Richmond ilipewa tenda kwa kigezo cha kuwa na bei ya chini kuliko zote, sasa imebainika kuwa Rais alidanganywa na waliompa takwimu na yeye kuzitumia.
Kasoro hiyo ilibainika kufuatia aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO, Bw. Yohanes Hans, kuiambia Kamati ya Bunge iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Dkt. Harrison Mwakyembe, kuwa suala hilo halikuwa sahihi na ilienezwa makusudi kuifanya Richmond ikubalike pamoja na kutokuwa na uwezo.
Katika madai hayo ambayo hata ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nayo iliyashabikia kuwa ndicho kigezo cha msingi cha kuikubali kampuni hiyo, Richmond ilikubali kuuza umeme wake kwa senti 4.99 zilizojengewa uzushi kuwa ni za chini zaidi.
Rais Kikwete naye akitumia kigezo hicho hicho bila kufahamu ajenda pana ya wanamtandao wa Richmond waliohakikisha takwimu hiyo inamfikia na anazitumia, naye alilisisitizia Taifa kuwa TANESCO na hata wizara walikuwa wakitafuta kampuni yenye bei ndogo na hivyo kuipa tenda Richmond.
Lakini tofauti na takwimu alizopewa Rais, Mkurugenzi wa zamani wa TANESCO aliwaumbua walioeneza madai hayo ya Richmond kuwa na bei ndogo kwa kuiambia Kamati ya Mwakyembe kuwa kampuni iliyopeleka bei ndogo kuliko zote wakati wa zabuni, haikuwa Richmond bali Songas iliyokuwa tayari imekubali kuuza umeme wake kwa senti 3.84 za dola kwa uniti tena bila capacity charges (Richmond inalipwa sh. milioni 152 kwa siku za capacity charges).
Sehemu ya maswali kati ya Kamati Teule ya Bunge na Bw. Hans yalikuwa kama ifuatavyo;
Dkt. Harrison Mwakyembe: Tumeambiwa kwamba TANESCO ilijaribu kuwa na makubaliano na kampuni ya Songas wakati huo, lakini vipengele vya makubaliano havikukubaliwa na Wizara ya Serikali kwa kuwa Kampuni ya Songas ilipendekeza bei ya juu. Sijui kama hilo ni kweli au ni maelezo tu yaliyotolewa?
Bw. Yohanes Hans: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unatakiwa kujibu hilo, makubaliano yaliyosainiwa yanafanana na tuliyokuwa tumeafikiana na Songas, kwa hiyo swali hilo ni gumu kulijibu. Kuhusu bei kwa uniti tulijadiliana na Songas bei iwe senti 3.84, nafikiri ya Richmond ilikuwa senti tano.
Mwakyembe: 4.99?
Hans: Senti 4.99. Hiyo ni hoja ya kwanza, hoja ya pili ni kwamba jenereta za Songas zinafanana kabisa na jenereta zilizopo Ubungo ambazo DOWANS (Kampuni iliyonunua mkataba wa Richmond) imenunua. Kwa hiyo hayo uliyoelezwa yalikuwa na sababu zake, kwani tungeweza kununua umeme wa bei rahisi na mashine zilizopo ndizo ambazo Songas walikuwa wazilete. Nadhani hilo ni jibu zuri kwa swali lako.
Sasa wanasheria kadhaa waandamizi wameibuka na kusisitiza kuwa kauli ya hivi karibuni ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, kuwa alipata ushauri wa kisheria asivunje mkataba na Richmond ni mambo yanayoacha maswali magumu bila majibu.
Wanasheria hao wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutoka kampuni kadhaa za uwakili binafsi jijini Dar es Salaam, waliiambia Majira Jumapili kuwa ni vyema Bw. Lowassa akawataja mawakili anaosema walimpa ushauri huo na hilo likaenda hadi kwa Rais, kwa sababu suala hilo linaweza kuidhalilisha taaluma ya sheria.
"Ukiutazama mkataba wa Richmond, jinsi walivyoshindwa kuutekeleza na kisha inakuja kauli ya Lowassa kuwa alitaka kuuvunja mkataba huo lakini wanasheria wakubwa tu, wakamshauri asifanye hivyo, ni suala linaloibua maswali mengi," alisema mhadhiri wa sheria kutoka Kitivo cha Sheria cha chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
"Mtazamo wangu ni kwamba kama kweli wapo waliomshauri hivyo basi tunapaswa kuwajua ili tuupime uadilifu wao kitaaluma na kwa Serikali, kwa sababu ukitazama mambo haya, kisheria kuna maeneo yalikuwa wazi kuwa Richmond ilidanganya," alisema mhadhiri huyo.
"Kusema uongo juu ya uwezo wake ni sababu tosha kwa mujibu wa sheria za mikataba, kuuvunja mkataba," alisema mhadhiri ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu.
"Sisi tunawafundisha vijana wetu hapa kwa miaka mingi tu tena ni katika darasa la awali kabisa la sheria za mikataba kuwa udanganyifu kama ilivyofanya Richmond iliyojieleza kuwa ni kampuni yenye uwezo kumbe hata haipo kisheria, unatosha kuvunja mkataba.
"Ni vyema Lowassa akalisaidia Taifa kuwajua hao waliomwambia tofauti, tunataka kujua kama ni wanafunzi wetu au wametoka wapi, tuupime utaalamu wao?," alihoji mhadhiri huyo na kuomba asiwekwe bayana gazetini kwa sababu ya utumishi wake.
Katika fungu la (ii) B la mkataba kati ya TANESCO na Richmond (nakala tunayo), kampuni hiyo iliyojieleza kutoka Marekani, ilijifunga kimkataba ikijinasibu kuwa na uwezo. Fungu hilo linasema "Mleta mitambo (Richmond), ana vifaa na uwezo wa kifedha na kiufundi wa kujenga, kufunga na kuuendesha mtambo huo (wa megawati 100) kama inavyotakiwa na TANESCO."
Pamoja na ahadi hiyo ya kimkataba, Richmond walishindwa katika maeneo yote waliyoyaahidi kwenye kipengele hicho na bado Lowassa akasema alishauriwa asivunje mkataba huo.
Naye wakili wa kujitegemea ambaye ni mmoja wa mawakili waandamizi nchini ambaye pia aliomba kutowekwa bayana jina lake kwa sababu za kimaslahi, aliunga mkono hoja ya kumtaka Bw. Lowassa kuwataja wanasheria waliomshauri asiuvunje mkataba wa Richmond kwani hata yeye amestaajabishwa na kauli hiyo.
"Nina wasiwasi na wataalamu hao. Kama ulivyoniuliza, jibu langu ni kweli vipo vipengele vya wazi kabisa vya kuuvunja mkataba huo. Kwanza, kuna udanganyifu ambao uliathiri utekelezaji wa mkataba. Pili, kama Serikali ikithibitisha kuna viongozi walikula rushwa, nayo ni sababu ya kuvunja mkataba na tatu uhalali wa kampuni ya Richmond yenyewe kisheria," alisema Wakili huyo.
"Tumesikia kuwa hata Marekani haikusajiliwa na iliyosajiliwa hapa si iliyosaini mkataba. Hapa hao wanasheria wa Lowassa wangefanya vyema utafiti wa kisheria, naamini wasingempa ushauri anaodai kupewa," alisema kama angeulizwa ushauri wake kwa Serikali, angesema mkataba huo uvunjwe, ingawa alionesha wasiwasi iwapo hilo kwa sasa linawezekana kwani mkataba huo umeshatekelezwa na Dowans baada ya Richmond kukimbia.
Hata hivyo, ilibainika pia kuwa kwa mujibu wa kipengele cha fungu la 21.1 la mkataba wa TANESCO na Richmond, linalozungumzia matukio yanayoweza kuvunja mkataba (events of default), Richmond ilijifunga kimkataba kuwa watakuwa wamesababisha kuvunjika kwa mkataba huo.
Iwapo;
"Kauli yoyote au uhakika wowote uliotolewa na mleta mtambo (Richmond) katika mkataba huu vitabainika kuwa si sahihi na itabainika au kuwa hakika kwamba ahadi hiyo ilitolewa na ikawa ni sehemu ya msingi wa mkataba na ahadi au kauli hiyo ikaonekana haikuwa sahihi na kuathiri uwezo wa mleta mitambo kutimiza majukumu yake kimkataba." Wanasheria walipooneshwa kifungu hiki na gazeti hili, walisema kilitosha kuifukuza Richmond iliposhindwa hata kuleta mitambo nchini.
Zaidi gazeti hili limebaini kuwa kwa kipengele cha rushwa kwa mfano, hata Baraza la Kimataifa la Kutatua Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) la London, Uingereza, lililosikiliza kesi ya TANESCO na IPTL, lilisema katika hukumu yake kuwa ushahidi wa IPTL kutumia rushwa katika kupata mkataba ungewasilishwa, TANESCO ingekuwa na nafasi kubwa ya kushinda kesi hiyo.
Nyaraka rasmi za Baraza hilo, zinaonesha kuwa wanasheria kutoka kampuni ya Mkono Advocates na ushauri wa kitaalamu uliotolewa na mmoja wa wasomi waliobobea katika taaluma ya sheria mbalimbali zikiwamo za kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ulionesha kuwa rushwa kwa mujibu wa fungu la 19 la Sheria ya Mikataba ya Tanzania, ni kigezo tosha cha kuvunja mkataba.
Hata hivyo, ushahidi huo wa rushwa haukupelekwa London, ikielezwa ulibaki Dar es Salaam ambako aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa PCB (sasa Mkurugenzi Mtendaji wa TAKUKURU), Bw. Edward Hosea, alikuwa akijiandaa kuutumia katika shauri la jinai lililotarajiwa kufunguliwa ambalo hata hivyo mpaka sasa halijafunguliwa na hakuna sababu rasmi zilizotolewa.
Kwa kushindikana ushahidi huo kupelekwa London, hukumu ya Baraza hilo iliyoibwaga TANESCO na kuilazimu iwalipe IPTL mabilioni ya fedha zikiwemo za capacity charges huku hali ikiwa ni ile ile kama Richmond; IPTL nao, wazalishe, wasizalishe, walitakiwa kulipwa. Hukumu ya London ilitolewa Februari 2, 2001.
Wasomi waliozungumza na gazeti hili na wanaojua vyema mwenendo wa kanuni za uendeshaji mashauri katika Baraza hilo la London, wanaamini kama Serikali ingeamua, ingeuvunja mkataba na Richmond bila kuwajibika, lakini kama ilivyokuwa kwa IPTL ambako ushahidi uliachwa Dar es Salaam, woga ni kwamba hata katika hatua hiyo, huenda wanamtandao wa Richmond wangeweza kuihujumu hata kesi hiyo; tatizo ni uadilifu na kujitoa, si sheria.
Source: Majira Jumapili
Rais yeye ni kudanganywa tu kila kukicha mara kashauriwa vibaya maana kichwani mwake ni hamnazo, OK tutaona mengi.
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=5999
16.03.2008 1429 EAT
Kikwete alidanganywa kuhusu Richmond

Ukiona Raisi anadanganywa hujue hamna kitu hapo, Jiulize hao wanaomdanganya wanapata wapi ujasiri wa kumdanganya, ni kwa sababu wanajua hayuko makini hivyo wanaweza kumrubuni
Rais alidanganywa na wasaidizi wake? Au Alikubali aonekane kuwa anadanganywa?
Anazo 'resources' zote anazoweza kuzitumia kama angekuwa hataki kudanganywa!
Haya ya Richmond Kikwete aliyaelewa thika tokea mwazo wake, waandishi wa habari wasitafute njia za kusafisha uchafu unaoonekana wazi.
Kuna wanasheria gani tena zaidi ya hao wa Mwanyika ambao Lowasa atakuwa anawazungumzia. Mwanyika mwenyewe shasema wao walikuwepo tu katika vikao mbalimbali vya mkataba bila ya kufanya kazi ya kisheria.
Ni dhahiri kwamba baadhi ya yaliyotokea katika Richmond, yamekopwa toka IPTL. Wahusika walidhamiria kutumia 'model' ile ile ya IPTL. Ndio maana Lowasa anaonekana kutumia kesi ya IPTL kule London, ambako serikali ya Tanzania iliamua maksudi kubwagwa, na kuendelea kulipia mabilioni ya walalahoi kwa IPTL hata kama huduma haitolewi.
Hivi hawa viongozi bado kweli wanaamini Tanzania tutaendelea kuwa salama?
Mkuu Babah,
Heshima mbele, vipi hayo maandishi kama yapo yakiwekwa hap JF ili tuyaangalie kwa undani na kutoa hukumu? Mimi sijawahi kuyaona au kuiona hiyo ishu ya TVT mkuu, lakini naaamini kuwa kuna mwenye nayo hapa ayaweke tuchambue, maana sikatai kuwa yapo!