Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Kafulila amefeli kutofautisha Kampuni ya IPTL iliyotokana na Muungano wa kampuni ya Mechmar (Malaysia) Berhard (70%) na VIP(30%), na kampuni ya PAP/IPTL iliyoundwa baada ya kununuliwa kampuni kwa kampuni hizo hapo juu,hivyo kitendo cha kuzungumzia utendaji kazi wa kampuni ya IPTL(CHINI YA PAP) kwa kuihusisha na kampuni ya IPTL chini ya Mechmar na VIP ni kuionea PAP na kuikosea kampuni hii ya PAP/IPTL.KAFULILA AUMBUKA KWA KUSEMA SETH HATAKIWI KENYA
View attachment 186998
mmililki wa IPTL na mwakandege mwanasheria wa IPTL
KAMPUNI ya kufua umeme ya Pan African Power Solution inayoimiliki kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imezidi kungaa katika nchi za jumuia ya Afrika Mashariki katika kusambaza nishati ya umeme.
Hatua hiyo inasababishwa na serikali ya Kenya kuipatia barua kampuni hiyo ya kufanya nao kazi ya usambazaji umeme katika mradi unaohusisha nchi mbili za jumuia hiyo, ambazo ni Tanzania na Kenya.
Barua ya Kenya iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli, Injinia Joseph .K. Njoroge ya tarehe 19, Agosti 2014 kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Sing Sethi.
Taarifa zaidi kuhusiana na barua hiyo, yenye kumbukumbu namba ME&D/CONF/3/2/73A iliyokuwa na kichwa cha habari Expression of interest for IPP for 2000MV power generations and supply to Kenya and Tanzania.
Barua hiyo, ilieleza kuwa inazitaka pande tatu hizo ikiwemo PAP, Tanzania na Kenya kukutana haraka kuona ni namna gani uzalishaji huo utaanza haraka iwezekanavyo.
Akithibitisha barua hiyo, Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/PAP, Joseph Makandege alisema kampuni yao inaendelea kuchapa kazi na haitishiki na kauli za wanasiasa kwa kuwa wao si wanasiasa.
Tunafurahi kuwa tunazidi kuaminiwa na serikali mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Hii inadhirisha ufanisi na ueledi wetu katika tasnia nzima ya nishati,alisema.
Hivyo, alisema anaamini maneno yote yanayoenezwa juu yao kuwa yanatawaliwa na chuki na wivu wa kibiashara kutoka kampuni zingine za usambazaji wa umeme.
Kutolewa kwa barua hiyo kwa IPTL kutaweza kuondoa sintofahamu iliokuwepo, baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR- Mageuzi) kudai kuwa Seth anayeongoza kampuni hiyo amepigwa marufuku kufanya biashara ya aina yoyote Kenya.
Kafulila alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini hapa, kuwa Seth ni fisadi na kwamba Kamati ya Bunge ya nchini Kenya imempiga marufuku kufanya biashara nchini humo.
===================================
Chanzo: habarileo