Sakata la fedha ya EGMA: Lowassa au Kikwete?

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
Ama kweli waswahili walisema mwenye nia njema haumbuki. Wale waliosema kuwa JK ataumbuka na sakata la EGMA wako wapi leo hii..?

Hatimaye ukweli uko hadharani baada ya watuhumiwa wa sakata hilo kufikishwa mahakamani. Watuhumiwa hao ni Henry Kitilya, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA na swahiba wa karibu wa Lowassa, Sioi Sumari, aliyekuwa Afisa wa Benki ya Stanbic na mkwe wa Lowassa na Shose Sinari aliyekuwa mfanyakazi wa Stanbic na mtoto wa Mwanasheria Eva Sinare yule ambaye alihamia UKAWA siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 na akamsafisha Lowassa kwenye mdahalo wa ITV.

Isitoshe na yule Bashir Awale Msomali aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Stanbic anayetajwa katika sakata hili ni rafiki wa karibu wa Lowassa na ndiye aliyekuwa akimpigania apatiwe uraia wa Tanzania na alikuwa katika timu ya kampeni ya Lowassa na mmoja kati ya waliohusika na sakata lile la wale walioshikwa wakipika matokeo katika zile centre za UKAWA.

Je, wale walisoma kuwa JK ataumbuka wako wapi leo..?

Zile hela zilizolipwa EGMA zilikwenda wapi..?

Au ndio hela za kampeni za UKAWA..?

Mjadala umefunguliwa...
 
Wewe funga tu mjadala ila swali kuu hapa ni kuwa unapokuwa rafiki au mkwe wa mtu mnashirikiana ufisadi au ni undugu?
 
CHADEMA wanachuki za ajabu na JK, na wanaumia sana mioyoni wanapoona anazidi kubarikiwa! i dont know kwakweli hizi chuki zao zinatokana na nini, sidhani kama ni siasa tu!
 
We zichi kweli
 
Ama kweli waswahili walisema mwenye nia njema haumbuki. Wale waliosema kuwa JK ataumbuka na sakata la EGMA wako wapi leo hii..?

Hatimaye ukweli uko hadharani baada ya watuhumiwa wa sakata hilo kufikishwa mahakamani. Watuhumiwa hao ni Henry Kitilya, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA na swahiba wa karibu wa Lowassa, Sioi Sumari, aliyekuwa Afisa wa Benki ya Stanbic na mkwe wa Lowassa na Shose Sinari aliyekuwa mfanyakazi wa Stanbic na mtoto wa Mwanasheria Eva Sinare yule ambaye alihamia UKAWA siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 na akamsafisha Lowassa kwenye mdahalo wa ITV.

Isitoshe na yule Bashir Awale Msomali aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Stanbic anayetajwa katika sakata hili ni rafiki wa karibu wa Lowassa na ndiye aliyekuwa akimpigania apatiwe uraia wa Tanzania na alikuwa katika timu ya kampeni ya Lowassa na mmoja kati ya waliohusika na sakata lile la wale walioshikwa wakipika matokeo katika zile centre za UKAWA.

Je, wale walisoma kuwa JK ataumbuka wako wapi leo..?

Zile hela zilizolipwa EGMA zilikwenda wapi..?

Au ndio hela za kampeni za UKAWA..?

Mjadala umefunguliwa...

Kwa ufusadi wote huu ambao serikali ya awamu ya tano inaufumua, swali kubwa ni kuwa serikali ya awamu ya nne ilijua nini? Na serikali hii iliongozwa na JK au EL? Kama si katiba yetu nadhani yungeshuhudia mengi mahakamani safari hii!
 
Mkubwa wewe hujui kuwa lowassa ni rafiki mkubwa wa kikwete pia. Na jk mwenyewe aliwahi kusema hawakukutana barabarani. Unganisha hapo mkubwa
 
Ya EGMA yako above your capabilities kama vile ya February Ma rope,hata mkijadiliana mutakuwa munadanganyana na hakuna lolote litakalotokea pale Kisutu.Aliyefungua mjadala nimuombe aufunge.
 
Back
Top Bottom