Sakata la Dowans lamuibua Nape...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,541
2,000
na Mwandishi wetu

MKUU wa Wilaya ya Masasi, Nape Nnauye, amewashauri Watanzania kuacha itikadi za vyama, kuungana kwa pamoja na kuandamana ili kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro (ICC) dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ya kuilipa kampuni ya Dowans sh bilioni 185.

Nnauye alitoa ushauri huo jana kupitia mtandao wa ‘face book’ ambapo alionyeshwa kukerwa na hukumu hiyo iliyotolewa hivi karibuni na mahakama hiyo.

“Hivi kwa nini Watanzania wasiungane kwa pamoja hata kama ni kwa maandamano kupinga hukumu ya kuwalipa Dowans 185 bilioni , bila kujali itikadi zetu, tulinde pesa za kodi zetu,” alisema Nape kwa njia ya mtandao.

Hukumu hiyo iliyotolewa Novemba 15 mwaka huu, imezua mjadala mkubwa nchini huku baadhi ya wananchi wakisema hali hiyo imesababishwa na viongozi wazembe na wasio na uchungu na nchi.

Katika hukumu hiyo, TANESCO iliamriwa na ICC kuilipa Dowans fidia ya sh bilioni 185 kutokana na kuvunja mkataba wake wa kuzalisha umeme bila ya kufuata taratibu.

Shirika hilo lilitangaza kuvunja mkataba wa Dowans Agosti mosi, 2008 ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya mkataba huo kumalizika.

Awali, serikali kupitia TANESCO mwaka 2006 iliingia mkataba uliodaiwa kuwa na harufu ya rushwa kwa ajili ya kuzalisha megawati 100 za umeme na kampuni ya Richmond Development LLC ili kuiokoa nchi na giza kwa kukosa umeme kulikotokana na ukame.

Mjadala wa mitambo ya Dowans, uliwahi kuligawa taifa kwa kipindi kirefu mwaka 2008 baada ya Kamati Teule ya Bunge chini ya Uenyekiti wa Dk. Harrison Mwakyembe, kutoa taarifa ya kuchunguza uhalali wa kampuni ya Richmond na mkataba baina yake na serikali.

Kutokana na taarifa iliyowasilishwa bungeni Februari mwaka 2008 aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alijiuzulu ikiwa ni ishara ya kuwajibika kama kiongozi mkuu wa ofisi yake iliyodaiwa kushiriki katika kuiwezesha Richmond kushinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura.

Wakati wa mjadala huo, aliyekuwa Mkurugenzi wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, aliishauri serikali kuinunua mitambo hiyo jambo lililoungwa mkono na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Kabwe Zitto (CHADEMA), huku akipingwa vikali na wenzake ndani na nje ya chama chake.

Hata hivyo, Bunge lilikataa kupitisha pendekezo la ununuzi wa mitambo ya Dowans likisema kufanya hivyo ni kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 inayokataza serikali au taasisi zake kununua mitumba.

Uamuzi huo wa ICC ulitolewa na jopo la majaji watatu chini ya uenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Unyantwali na Jonathan Parker.

Jopo hilo liliamuru TANESCO ilipe fidia ya zaidi ya sh bilioni 36 na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya sh bilioni 26 tangu Juni 15 mwaka huu, hadi fidia hiyo itakapolipwa.

Kadhalika, jopo hilo liliamuru malipo ya sh bilioni 60 na riba ya asilimia 7.5 ambayo ni sawa na sh bilioni 55 kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.

Katika uamuzi huo, jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi wa ICC na utawala ni sh bilioni moja zinatakiwa kulipwa na pande zote.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,541
2,000
Kwa maoni yangu Nape is a very cheap politician..............................badala ya kulaumu uongozi wa TANESCO kwa kuzuia mitambo ya DOWANS isivyo halali na kinyume cha sheria ili kuwanufaisha walaji wachache ndani ya shirika hilo na mabosi wao serikalini.................

Nape ameamua kufunika ukweli huo kwa kushauri maandamano...............maamuzi ya kimahakama hayawezi kudhalilishwa na utani utani wa mitaani kama Nape anavyoshauri................................

Jukumu letu ni kuwashughulikia wale wote walioshiriki katika kuzuia mitambo ya DOWANS na watueleze taifa lilinufaika vipi na wao kuvunja sheria.............................
 

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,195
Ndugu wana Jamvi

Nimekuwa nafuatilia kwa karibu Sakata la TANESCO kuangushwa katika kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans katika Mahakama ya Usuluhishi katika Mambo ya Biashara aka ICC.

Katika kesi hiyo Dowans ilikuwa inataka ilipwe na TANESCO kama fidia ya Hasara iliyopatikana kwa TANESCO kuizuia DOWANS kuuza Mitambo yake.

Kuna Swali la Msingi ( Fundamental Question) ambalo naona bado sijapata Jibu lale

Je Ni Kwa nini TANESCO walizuia DOWANS kuondoa na Kuuza Mitambo yao?
 

Mkerio

Member
Mar 12, 2006
35
0
mimi namwona Nape kama kijana mzalendo. Ni kweli kama tukiamua kufanya maandamano ambayo mimi naona ni mazuri kwa ajili ya kuleta changamoto, agenda iwe kuishinikiza serikali iwachukulie hatua waliohusika katika sakata la richmopnd hadi dowans. Bunge lilipiga kelele wachukuliwe hatua serikali ikakataa. Dowans kama kampuni hawana tatizo, tatizo lipo kwa waliosaini mkataba tena na kampuni hewa maana tuliambia richmonduli ilikuwa hata haijasajiliwa.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,541
2,000
Je Ni Kwa nini TANESCO walizuia DOWANS kuondoa na Kuuza Mitambo yao?

Hilo ni swali ambalo hakuna mtu yoyote ndani ya CCM yupo tayari kulijibu...........na jibu lake ni kuwa lengo lilikuwa ni kushinikiza tununue mitambo chakavu na hata JK alisikika akisema kama sheria ya manunuzi ndiyo kikwazo basi ikibadilishwe.....................
 

Diehard

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
448
500
Unajua watanzania wanapenda kuzunguka zunguka kama Sitta ndivyo alivyo Nape hapa ilitakiwa waseme Kamata Lowasa, Rostam, Karamagi, Msabaha, Idrisa Rashid, na wote waliohusika kwenye deal hili feki full stop, tunaona aibu utafikiri tunataka kumtongoza Sister
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,523
2,000
mimi namwona Nape kama kijana mzalendo. Ni kweli kama tukiamua kufanya maandamano ambayo mimi naona ni mazuri kwa ajili ya kuleta changamoto, agenda iwe kuishinikiza serikali iwachukulie hatua waliohusika katika sakata la richmopnd hadi dowans. Bunge lilipiga kelele wachukuliwe hatua serikali ikakataa. Dowans kama kampuni hawana tatizo, tatizo lipo kwa waliosaini mkataba tena na kampuni hewa maana tuliambia richmonduli ilikuwa hata haijasajiliwa.

mzalendo mpumbavu....walikuwa wanafanya mambo kipumbavu sasa inawa cost..ndo shida ya watanzania kushabikia vitu kijinga jinga then baadaye mnaanza kulalamika..DOWANS walipwe tena hata mara 50 ya hiyo ili iwe fundisho
 

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
500
Dowans walipwe, kwa sababu watanzania hawajawa serious na mali zao, hivyo waache mafisadi waendelee kujipakulia until tanzanians will get tired and stop them.
Tunawalaumu el ra ec na wenzao but ni juzi tu watanzania wamewapigia kura kuwa wabunge wao. Let them eat mpaka siku watu watachoka au wataelewa na kuwa serious
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
Tatizo sijui ni hivi vyeo vya promotion inawapa kusema pumba, ama basi tu wanaamua kutafuta umaarufu wa kijinga.

Hatua ya kwanza watanzania tumeivuka, ambayo ilikuwa tukiambiwa maneno ya uongo tunakubali kuwa wanatuambia ukweli.
Sasa tumegundua kuwa wanachotuelezea ni uongo.
Kilichobaki ni wao kugundua kuwa tumeshtukia uongo wao.

Mungu ibariki Tanganyika Mungu ibariki africa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom