Sakata la Dawa Nchini; Waziri Ummy Mwalimu waambie wananchi Ukweli

Wewe lazima ni mganga mkuu sehemu.

Siku wakiacha kuweka siasa kwenye mambo ya msingi ndio tutafika tunakoenda.
 
Sawa mkuu, demand ya dawa nchi nzima ni USD 400M kwa mwaka....
Kwanini wananchi wasisaidiwe kujiunga NHIF badala ya kuendelea kukomaa na bei za dawa ambazo hatutengenezi?
Andika iyo USD 400M kwa hela zetu,acheni kutufanya tuendelee kutoelewa kama ambavyo hatuelewagi kila kitu tunashangilia tuu
 
Umofia kwenu wakuu.

Toka sakata la bei za dawa na kuonesha kuwa kwa kuwa serikali imeamua kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, basi huduma za afya , hasa dawa na vifaa tiba zimepungua kwa kias kikubwa..... nilibaki nimeshika tama kwa mshangao...

Kwakuwa kinachosababisha dawa kupanda bei si wafanyabiashara kuhitaji faida Pekee, bali ni gharama sana kuingiza na kutunza dawa hapa nchini, zaidi sana ikichangiwa na serikali kutokulipa suppliers wake kwa wakati... nikipata muda nitaeleza kwa urefu.

Leo Akiwa Tanga Waziri Ummy anawaagiza wakuu wa wilaya wawashughulikie waganga wa mikoa na wilaya ambao hospitali zao zinakosa Follic Acid (Muhim sana kuzuia mama mja mzito kupata mtoto mwenye kichwa maji).... nimepatwa na butwaa zaidi.. kwa kuwa

1. Waganga wa mikoa/Wilaya hawajui hizo dawa watapata wapi, kwa kuwa kwanza wao si wazalishaji na kwa level waliyopo ni ngumu sana kujua dawa ikiadimika watapata wapi..
Kwa wasiofahamu, Waganga hawa kwa kushirikiana na Mfamasia wa mkoa/Wilaya wanapiga simu MSD, wakikosa wanaenda kwa msambazaji wa karibu, wakikosa wanapiga simu Dar, wakikosa huko hawana ujanja tena.

2. Huko Wilayani na Mikoani hakuna Vendor yupo tayari kuuza huko dawa kwa sababu ya changamoto ya malipo...
Upeleke dawa wilayani .. labda mzigo wa milioni 20, then margin labda ilikuwa 10% uje kulipwa zaidi ya miezi sita au mwaka mzima, inflation rate ya TSH ni 3% kila mwezi, kuna faida au hasara?

3. TFDA walishazuia zamani sana Dawa za Kopo.
Hizo Fefol zilizokuwa zinauzwa huko hospitali za mikoa/Wilaya siku hizi hazipo sokoni.. kuna blister pack ambayo ni ghali .. may be 3000 kutoka kwa wholesaler wa Kariakoo... Hadi kufika huko wilayani itakuwa bei gani?

4. Dawa za kuongeza damu zimeadimika sana nchini
Kampuni kubwa za kutengeneza dawa za kuongeza damu, zinaona kama ni product isiyo na faida, hivyo nyingi hazizalishi kwa wingi kama ilivyokuwa kwa zile za kopo hapo nyuma.. nitafafanua na kutoa mifano ikilazimu

5. Bajeti ya W/Mkoa kununua dawa ni ndogo mno kulinganisha na mahitaji.. hivyo wananchi wataendelea kukosa tu dawa kama hawataambiwa ukweli.



Sasa ukweli ni Upi.

Kwanza bei za dawa na vifaa tiba sio bei rahis kama wananchi wanavyotaka kuaminishwa
Hizo Amoxyclav za elfu nne, zilikuwepo toka zamani.. labda ni hao msd wenyewe kwenye manunuzi yao.... Kwa taarifa tu ni kuwa Amoxycalv zipo za hiyo elf nne had elf 30 kwa molecule hiyo hiyo (Nadhan hizo hata wazri ndizo anazotumia)
Hep B bei ni 11500-20,000 (Pungufu unaongea)
Je wananchi watapata ahueni?
Hapana , gharama za matibabu kwa wananchi wa kawaida hazipo OPD, zipo kwa mgonjwa anapolazwa au anapopata Ajali au Magonjwa Makubwa na ya kudumu kama Kisukari/Figo/Cancer

Kwa faida kidogo tu, ukipata tatizo kwenye figo ukahitaji kusafishwa(Dialysis) si chini ya laki 6 kwa mara moja.. na utahitaji kufanyiwa mara kwa mara.

Dawa ya cancer mfano Avastin Inj si chini ya Mil. na utahitaji kudungwa sindano zaidi ya moja

Kisukari wewe ni maisha yako yote.. na dawa zake si chini ya sh800 kwa kidonge.

Presha nayo vile vile.

Suluhisho.

Kwa wananchi wa kawaida hakuna namna yeyote ya maana zaidi ya kuwa na bima ya Afya.. iwe NHIF/ au private.. CHF ni uchuro... achaneni nayo kwa kuwa mwisho wako wa kutibiwa ni hospitali ya wilaya ambako napo dawa hakuna, na limit ya matibabu ni kubwa sana ukilinganisha na NHIF


Wananchi wanaopiga makofi kama mazuzu kushangilia bei za dawa wasizozalisha/ au wasiojua hata zinatoka wapi na ubora upi.. bima ya Afya ndie mkombozi wao Pekee....

Nilidhani ingekuwa busara, Mh. Ummy, akaelekeza nguvu zake kwenye kuwekeza kwenye bima ya Afya na namna gani bora kuwafikia wananchi walio wengi (Sio ile ya CHF ).. kutoka mili 3 waliopo sasa....
Hata kujiunga kwa lazima kama kweli wanataka mapinduzi ya kweli ya sekta ya Afya hapa nchini

Waziri ana bima yake, wala hatakaa alie shida ya dawa, ila kwa mwenendo wa malipo wa NHIF nae kuna siku atalia, japo kilio cha kwenye V8 hakina machozi.


Nitarejea kuelezea zaidi masoko ya dawa na namna viwanda vinavyotengeneza dawa zenye faida...
Kifupi tu, dawa hizi za level ya wilaya makampuni mengi ya maana yalisha achana nazo maana haziwasaidii kulipa tafiti na kupata faida...
Tutoke huko kama taifa...
Waziri Ummy njoo na mpango mzuri wa bima ya Afya kwa kila nyumba(si CHF) nitashiriki kuuboresha ..... Huo ndio ukweli mchungu unaotakiwa kila mwananchi aujue.
Mungu akubariki sana mkuu .
 
ukiwa unaongea ongea ukiwa na taarifa kamili msikilize Mganga Mkuu wa Tanga akizungumzia upatikanaji wa dawa.
 

Attachments

  • dkt+mahita.mp4
    8.9 MB · Views: 15
Na takribani 40% ya Watanzania ndio wanaotibiwa hosptalini.
Wengi wanatumia mitishamba au wanajinunulia tu dawa pharmacy.
 
Back
Top Bottom