Sakata la Dawa Nchini; Waziri Ummy Mwalimu waambie wananchi Ukweli

Ushamba anao Mwenyekiti wako wa Chama Cha Makinikia?Either sema unachoolewa lakini si kutukana watanzania,boya wewe
Turudi kwenye mada ...ya msingi hayo mengibe kagoogle kwani hakuna muda wa kupeana mafunzo.
 
Guys huwezi kuongelea dawa ya malaria ya 20k eti ni nzuri sana. How many Tzns can afford that?
Babu yangu aliyepo kule Ngudu can not aford that, hata akisaidiwa ni kazi bure coz it won't make any difference na aliyekunywa mseto wa sh 1500/=.

Pumbafu kabisa
 
Mkuu mleta mada nakubaliana na wewe katika hitimisho...kwamba ni lazima waziri apambane kutekeleza Ilani ya CCM yaani Universal coverage ya health Insuarance.Kumbuka kuna ugumu wa kuanza direct na jamii nzima kujiunga na NHIF Vs CHF.

Wakati wa kampeni za uchaguzi niliwahi kuhoji wagombea akiwemo mama Anna Mghwira juu ya uelewa na maoni yao kuhusu compulsory health insuarance ingawa hawakuweza kulijibu(REJEA MJADALA WA TWAWEZA UCHAGUZI 2015)

Kuhusu kushuka kwa dawa hilo halina ubishi kwani hadi bei elekezi zimeshatoka.Unachotaka kukitetea ni lugha ya wafanyabiashara tu...mara ooo gharama za uingizaji na blah blah nyingine...

Katika suluhisho lako ningefurahi kama ungeongelea uwepo na uwekezaji katika viwanda vya dawa na vifaa tiba...hili ni eneo muhimu ambalo litapunguza gharama na ukiritimba wa kupatikana kwa dawa na pia ni eneo lenye ajira na faida ya kutosha.

Ningependa ujiulize kwa nini hadi leo R/L na NS zinatoka Uganda ?Ningependa kusikia maoni yako kwa muktadha huu.

Tatizo letu/lenu wataalamu hamuongelei mada nyeti katika afya na ndio maana wanasiasa wanakosa ya kuongelea kuhusu afya na wanabaki na matusi na dhihaka kuhusu ukosefu wa dawa na vifaa tiba.

Tatizo lenu maDMOs na hata RMOs hamuongei katika vile vikao vyenu mnavyokutana...mkiwa kule mnachat watsapp na kupiga soga.

Leo hii ukiingia Group la watsapp la ninyi DMOs/RMOs au wafamasia huwezi kulitofautisha na kundi la watsapp la wapiga singeli wa Tandale..wote ni mipicha ya wahenga tu.

Kuhusu kauli ya ummy...iko very specific na sioni kama kuna upotoshaji unless muanze kuipotosha na kuwatishia wananchi kama ilivyo kawaida ya barvichaa.

Kama unahisi huwezi kuitekeleza kaa pembeni aingie anayeweza...This is how the new Government runs things...
Naomba nijibu kipengele cha R/L na DNS..
Hiyo ni kati ya biashara muflis kuifanya...
Maji tupu hela hakuna... Nani wa kufanya uwekezaji kwenye biashara kichaa?
Bei ya R/L na DNS si zaidi ya mia nane bei ya jumla....
 
Bei zipi hizo mkuu?
Hivi mnafikiri dawa za binadam ni sawa na sukari au Unga?
Hapa unaongelea dawa tofauti zaidi ya aina elfu 5000 na vifaa tiba elfu moja na mia tano...
Sasa zinashuka vipi wakati sisi hatuzalish dawa wala hatufanyi tafiti za kutengeneza Dawa?
Dawa lazima zipungue bei hii ni kutokana na ukweli kuwa sasa serikali/MSD watanunua moja kwa moja toka kiwandani tofauti na awali ambapo serikali ilikuwa inanunua kupitia wakala/agent. Hivyo haitaji kuwa na digrii kuelewa kuwa kwa mfumo huu mpya lazima bei ipumbue. Lakini ukiona kelele basi jua kuna watu waliozoea 10% wataumia pia mawakala. Heko Waziri Ummy kwa maamuzi haya waache wapige kelele lakini sisi tunaojitambua tunaona juhudi zako za kuhudumia wananchi.
 
Dawa lazima zipungue bei hii ni kutokana na ukweli kuwa sasa serikali/MSD watanunua moja kwa moja toka kiwandani tofauti na awali ambapo serikali ilikuwa inanunua kupitia wakala/agent. Hivyo haitaji kuwa na digrii kuelewa kuwa kwa mfumo huu mpya lazima bei ipumbue. Lakini ukiona kelele basi jua kuna watu waliozoea 10% wataumia pia mawakala. Heko Waziri Ummy kwa maamuzi haya waache wapige kelele lakini sisi tunaojitambua tunaona juhudi zako za kuhudumia wananchi.

Ninaweza kuthibitisha kuwa MSD hawana uwezo hata wa 40%kutosheleza mahitaji ya dawa nchini....
Gharama za matibabu vipi?
 
Umofia kwenu wakuu.

BAADA YA KUPITIA UZI HUU, NILIAMUA KUFANYA UTAFITI WA NDANI NA KINA ILI KUJIRIDHISHA NA KILICHOWASILISHWA HAPA, MAANA MASUALA YA AFYA YA BINADAMU SI JAMBO LA KIMCHEZO MCHEZO

Toka sakata la bei za dawa na kuonesha kuwa kwa kuwa serikali imeamua kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, basi huduma za afya , hasa dawa na vifaa tiba zimepungua kwa kias kikubwa..... nilibaki nimeshika tama kwa mshangao...

Ni muhimu kwa kauli kama hizi zikawa na uthibitisho kwa kuwa kupungua kwa bei ya dawa haina uhusiano na kushuka kwa huduma za afya hasa dawa na vifaa tiba. Ambacho kimebadilika ni bei na sio kiasi, maana kushuka kwa bei ya dawa kunaongeza kiasi cha manunuzi ya dawa kwa wakati na kwa wingi zaidi.

Kwakuwa kinachosababisha dawa kupanda bei si wafanyabiashara kuhitaji faida Pekee, bali ni gharama sana kuingiza na kutunza dawa hapa nchini, zaidi sana ikichangiwa na serikali kutokulipa suppliers wake kwa wakati... nikipata muda nitaeleza kwa urefu.

Suala hili ni mtambuka. Kilichosababisha bei ya dawa kupungua ni maamuzi ya Rais kuielekeza MSD kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji. Ni muhimu kujua kuwa kununua kwa wazalishaji kunapunguzo mlolongo wa bidhaa kubadilishana mikono na hivyo kuokoa gharama kwa kiasi kikubwa. Ni muhimu kutambua kuwa Serikali imeongeza bajeti na upatikanaji wa fedha za manunuzi ya dawa na hivyo suala la washitiri (suppliers) kulipwa kwa wakati limekuwa historia.

Akiwa Tanga Waziri Ummy anawaagiza wakuu wa wilaya wawashughulikie waganga wa mikoa na wilaya ambao hospitali zao zinakosa Follic Acid (Muhim sana kuzuia mama mja mzito kupata mtoto mwenye kichwa maji).... nimepatwa na butwaa zaidi.. kwa kuwa

1. Waganga wa mikoa/Wilaya hawajui hizo dawa watapata wapi, kwa kuwa kwanza wao si wazalishaji na kwa level waliyopo ni ngumu sana kujua dawa ikiadimika watapata wapi..
Kwa wasiofahamu, Waganga hawa kwa kushirikiana na Mfamasia wa mkoa/Wilaya wanapiga simu MSD, wakikosa wanaenda kwa msambazaji wa karibu, wakikosa wanapiga simu Dar, wakikosa huko hawana ujanja tena.

Ni muhimu tukaacha siasa na kuangalia hoja ya msingi, je wewe ulitaka Waziri awaambiaje waganga wa mikoa/Wilaya? Ni jukumu la Waganga wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha dawa zinapatikana kwa namna yoyote ile. Hayo ambayo umependekeza hayakufanyika, yaani kuagiza kutoka MSD au soko huria! Ni muhimu kwa wataalam wetu kutoa taarifa badala ya kusubiri Mhe. Waziri kutoa maagizo ndipo watekeleze. Kwa mfano kwa nini waganga wakuu walisubiri mpaka Waziri aseme ndipo waanze kuhangaika? Ilitakiwa wajue hali hiyo mapema sana.

2. Huko Wilayani na Mikoani hakuna Vendor yupo tayari kuuza huko dawa kwa sababu ya changamoto ya malipo...
Upeleke dawa wilayani .. labda mzigo wa milioni 20, then margin labda ilikuwa 10% uje kulipwa zaidi ya miezi sita au mwaka mzima, inflation rate ya TSH ni 3% kila mwezi, kuna faida au hasara?

Nafikiri ulichokiandika hakina utafiti wa kutosha. Inawezekana kabisa unaongelea taarifa za nyuma. Kwa sasa washitiri wanalipwa kwa wakati. Ni muhimu kuwa na takwimu sahihi ya suala hili ili kujua na kutambua kuwa hali imebadilika.

3. TFDA walishazuia zamani sana Dawa za Kopo.
Hizo Fefol zilizokuwa zinauzwa huko hospitali za mikoa/Wilaya siku hizi hazipo sokoni.. kuna blister pack ambayo ni ghali .. may be 3000 kutoka kwa wholesaler wa Kariakoo... Hadi kufika huko wilayani itakuwa bei gani?

Ili la FEFOL ni mtambuka, maana dawa hizi zinapatikana MSD kwa bei nafuu. Hata hivyo, kama dawa hizi zitanunuliwa kwa njia ya kawaida bila msongo, bei yake ni ya kawaida. Ni muhimu kutambua kuwa TFDA wamezuia dawa za kopo ili kulinda afya za wananchi.

4. Dawa za kuongeza damu zimeadimika sana nchini
Kampuni kubwa za kutengeneza dawa za kuongeza damu, zinaona kama ni product isiyo na faida, hivyo nyingi hazizalishi kwa wingi kama ilivyokuwa kwa zile za kopo hapo nyuma.. nitafafanua na kutoa mifano ikilazimu


Katika huduma za afya, kuna njia mbili za kuhudumia wagonjwa. Kwanza ni kutumia dawa ili kutibu na pili ni lishe bora ili kuzuia kabisa. Inaonekana hoja yako ni kutaka TFDA warejee maamuzi yao ili kuruhusu dawa za kopo. Lakini hili litakuwa kwa faida ya nani? MSD kwa sawa wameongezewa uwezo wa kununua na hivyo wazalishaji wataongeza upatikanaji kutumia tenda za MSD ambazo zinakuwa za jumla.

5. Bajeti ya W/Mkoa kununua dawa ni ndogo mno kulinganisha na mahitaji.. hivyo wananchi wataendelea kukosa tu dawa kama hawataambiwa ukweli.


Ukweli ni kuwa, serikali imeongeza bajeti ya dawa katika mwaka wa fedha 2016/17 na hivyo suala la upatikanaji wa dawa linaendelea kuwa historia. Ni muhimu kuishi katika majira haya badala ya kutumia takwimu za tulikotoka ambazo zimebadilika.


Sasa ukweli ni Upi.

Kwanza bei za dawa na vifaa tiba sio bei rahis kama wananchi wanavyotaka kuaminishwa
Hizo Amoxyclav za elfu nne, zilikuwepo toka zamani.. labda ni hao msd wenyewe kwenye manunuzi yao.... Kwa taarifa tu ni kuwa Amoxycalv zipo za hiyo elf nne had elf 30 kwa molecule hiyo hiyo (Nadhan hizo hata wazri ndizo anazotumia)
Hep B bei ni 11500-20,000 (Pungufu unaongea)
Je wananchi watapata ahueni?

Nafikiri hapa huna hoja, bei ya amoxyclav imepungua kutoka shilling 9,800 hadi shillingi 4,000. Suala ni kwamba kwa sasa msd si wametaarifu umma kuwa wananunua bidhaa zao kwa wazalishaji moja kwa moja. Tambua kuwa hiyo inanunuliwa 4,000 ina sifa kama ile ya kwanza ya shilingi 9,800. Pia uelewe kuwa hizo za bei kubwa ni zile ambazo MSD ilikuwa inapigwa sana na hili linajulikana aisee.

Hapana , gharama za matibabu kwa wananchi wa kawaida hazipo OPD, zipo kwa mgonjwa anapolazwa au anapopata Ajali au Magonjwa Makubwa na ya kudumu kama Kisukari/Figo/Cancer

Kwa faida kidogo tu, ukipata tatizo kwenye figo ukahitaji kusafishwa(Dialysis) si chini ya laki 6 kwa mara moja.. na utahitaji kufanyiwa mara kwa mara.

Dawa ya cancer mfano Avastin Inj si chini ya Mil. na utahitaji kudungwa sindano zaidi ya moja

Kisukari wewe ni maisha yako yote.. na dawa zake si chini ya sh800 kwa kidonge.

Presha nayo vile vile.


Naona sasa umehamia kwenye matibabu, lakini napenda kukujulisha kuwa dawa za Cancer zote zimepungua bei kwa zaidi ya asilimia 40 baada ya MSD kuanza kununua moja kwa moja kwa wazalishaji na kuondoa middle men.


Pia, ni muhimu ujue kuwa taarifa MSD iliyotoa ilikuwa na lengo la kuwafungua macho wananchi jinsi ambavyo wafanyabiashara wanaongeza bei na kuwaumiza hao wananchi wanaougua.


MSD imeanza safari ya kununua kwa wazalishaji na ni busara kuipa muda na kupima matokeo baada ya mwaka mmoja. Tusubiri angalau tuone matokea ya hatua yao hiyo ambayo ni nzuri.


Suluhisho.

Kwa wananchi wa kawaida hakuna namna yeyote ya maana zaidi ya kuwa na bima ya Afya.. iwe NHIF/ au private.. CHF ni uchuro... achaneni nayo kwa kuwa mwisho wako wa kutibiwa ni hospitali ya wilaya ambako napo dawa hakuna, na limit ya matibabu ni kubwa sana ukilinganisha na NHIF


Nafikiri ni muhimu ukatambua kuwa Serikali imedhamiria kuondoa kero za upatikanaji wa dawa nchi nzima. Tembelea sasa hospitali za wilaya na utoe taarifa ni wapi ulipokosa dawa. Ni muhimu kutumia takwimu sahihi badala ya mihemko ambayo haijengi sana.


Wananchi wanaopiga makofi kama mazuzu kushangilia bei za dawa wasizozalisha/ au wasiojua hata zinatoka wapi na ubora upi.. bima ya Afya ndie mkombozi wao Pekee....

Nilidhani ingekuwa busara, Mh. Ummy, akaelekeza nguvu zake kwenye kuwekeza kwenye bima ya Afya na namna gani bora kuwafikia wananchi walio wengi (Sio ile ya CHF ).. kutoka mili 3 waliopo sasa....
Hata kujiunga kwa lazima kama kweli wanataka mapinduzi ya kweli ya sekta ya Afya hapa nchini


Wazo ulilolitoa ni zuri, lakini ni muhimu kutambua mchango mkubwa alioufanya Waziri wa Afya katika kuhakikisha ongezeko la fedha za dawa na hivyo kupunguza makali ya upatikanaji wa dawa nchini.


Hata sasa hiyo unayoiona kama mkombozi yaani NHIF na CHF inaendelea kufanyiwa maboresho makubwa ikiwemo dira ya kuelekea Universal Health Coverage

Napenda pia utambue chombo pekee cha kutathmini ubora wa dawa ni TFDA na dawa zote MSD inayosambaza zinapitia chini ya mamlaka hiyo.


Waziri ana bima yake, wala hatakaa alie shida ya dawa, ila kwa mwenendo wa malipo wa NHIF nae kuna siku atalia, japo kilio cha kwenye V8 hakina machozi.


Nitarejea kuelezea zaidi masoko ya dawa na namna viwanda vinavyotengeneza dawa zenye faida...
Kifupi tu, dawa hizi za level ya wilaya makampuni mengi ya maana yalisha achana nazo maana haziwasaidii kulipa tafiti na kupata faida...
Tutoke huko kama taifa...
Waziri Ummy njoo na mpango mzuri wa bima ya Afya kwa kila nyumba(si CHF) nitashiriki kuuboresha ..... Huo ndio ukweli mchungu unaotakiwa kila mwananchi aujue.


Kutokana na utafiti niliofanya ni vizuri ukatambua kuwa mwarobaini wa upatikanaji wa dawa umekwisha patikana ambao ni kuongeza bajeti ya dawa na kuhakikisha mfumo wa bima ya afya unaboreshwa jambo ambalo Wizara ya Afya inalifanya kwa sasa.Nashauri nawe ufanye utafiti kama wangu, kisha jenga hoja kwa kutumia taarifa sahihi na si mhemko.Tuwaache MSD wafanye kazi
 
3. TFDA walishazuia zamani sana Dawa za Kopo.
Hizo Fefol zilizokuwa zinauzwa huko hospitali za mikoa/Wilaya siku hizi hazipo sokoni.. kuna blister pack ambayo ni ghali .. may be 3000 kutoka kwa wholesaler wa Kariakoo... Hadi kufika huko wilayani itakuwa bei gani?
Mkuu kwa nini dawa ya kopo imezuiwa!!?

Kwa mtazamo tu dawa ya kopo itakuwa cheap kuliko ya blister pack by far ..... unaweza kutufafanulia hizo sababu za TFDA!!?
 
Kutokana na utafiti niliofanya ni vizuri ukatambua kuwa mwarobaini wa upatikanaji wa dawa umekwisha patikana ambao ni kuongeza bajeti ya dawa na kuhakikisha mfumo wa bima ya afya unaboreshwa jambo ambalo Wizara ya Afya inalifanya kwa sasa.Nashauri nawe ufanye utafiti kama wangu, kisha jenga hoja kwa kutumia taarifa sahihi na si mhemko.Tuwaache MSD wafanye kazi
Kuboreshwa maana yake nini mkuu?

Bajeti imeongezwa kutoka shng ngap hadi ngapi?
Unajua ukubwa wa mahitaji ya dawa nchini kulinganisha na bajeti kwa miaka angalao mitatu iliyopita mkuu....
Mihemko unayo wewe, nipe facts
 
Mkuu kwa nini dawa ya kopo imezuiwa!!?

Kwa mtazamo tu dawa ya kopo itakuwa cheap kuliko ya blister pack by far ..... unaweza kutufafanulia hizo sababu za TFDA!!?
Mkuu issue kubwa ilikuwa hygene na Expire date
Maana mfanyabiashara wa reja reja anazifungua alafu ana re pack upya.... Sasa huwezi jua zime expire lini na wala usafi wake hauelewwki
Ilikuwa sababu ya msingi kwa kweli...

Wanasiasa wetu walivyo waongo hata haya hamuwezi ambiwa kwa usahihi
 
Kuboreshwa maana yake nini mkuu?

Bajeti imeongezwa kutoka shng ngap hadi ngapi?
Unajua ukubwa wa mahitaji ya dawa nchini kulinganisha na bajeti kwa miaka angalao mitatu iliyopita mkuu....
Mihemko unayo wewe, nipe facts

Mkuu kwa ufafanuzi ni kwamba Bajeti imeongezeka kutoka

Tshs. Bilioni 30 - 2015/2016

Tshs. Bilioni 251 – 2016/2017

Tshs. Bilioni 269 – 2017/2018
 
Mkuu kwa ufafanuzi ni kwamba Bajeti imeongezeka kutoka

Tshs. Bilioni 30 - 2015/2016

Tshs. Bilioni 251 – 2016/2017

Tshs. Bilioni 269 – 2017/2018
Sawa mkuu, demand ya dawa nchi nzima ni USD 400M kwa mwaka....
Kwanini wananchi wasisaidiwe kujiunga NHIF badala ya kuendelea kukomaa na bei za dawa ambazo hatutengenezi?
 
Back
Top Bottom