Sakata la Dawa Nchini; Waziri Ummy Mwalimu waambie wananchi Ukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Dawa Nchini; Waziri Ummy Mwalimu waambie wananchi Ukweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mirisho pm, Jul 18, 2017.

 1. mirisho pm

  mirisho pm JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 2,483
  Likes Received: 3,306
  Trophy Points: 280
  Umofia kwenu wakuu.

  Toka sakata la bei za dawa na kuonesha kuwa kwa kuwa serikali imeamua kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, basi huduma za afya , hasa dawa na vifaa tiba zimepungua kwa kias kikubwa..... nilibaki nimeshika tama kwa mshangao...

  Kwakuwa kinachosababisha dawa kupanda bei si wafanyabiashara kuhitaji faida Pekee, bali ni gharama sana kuingiza na kutunza dawa hapa nchini, zaidi sana ikichangiwa na serikali kutokulipa suppliers wake kwa wakati... nikipata muda nitaeleza kwa urefu.

  Leo Akiwa Tanga Waziri Ummy anawaagiza wakuu wa wilaya wawashughulikie waganga wa mikoa na wilaya ambao hospitali zao zinakosa Follic Acid (Muhim sana kuzuia mama mja mzito kupata mtoto mwenye kichwa maji).... nimepatwa na butwaa zaidi.. kwa kuwa

  1. Waganga wa mikoa/Wilaya hawajui hizo dawa watapata wapi, kwa kuwa kwanza wao si wazalishaji na kwa level waliyopo ni ngumu sana kujua dawa ikiadimika watapata wapi..
  Kwa wasiofahamu, Waganga hawa kwa kushirikiana na Mfamasia wa mkoa/Wilaya wanapiga simu MSD, wakikosa wanaenda kwa msambazaji wa karibu, wakikosa wanapiga simu Dar, wakikosa huko hawana ujanja tena.

  2. Huko Wilayani na Mikoani hakuna Vendor yupo tayari kuuza huko dawa kwa sababu ya changamoto ya malipo...
  Upeleke dawa wilayani .. labda mzigo wa milioni 20, then margin labda ilikuwa 10% uje kulipwa zaidi ya miezi sita au mwaka mzima, inflation rate ya TSH ni 3% kila mwezi, kuna faida au hasara?

  3. TFDA walishazuia zamani sana Dawa za Kopo.
  Hizo Fefol zilizokuwa zinauzwa huko hospitali za mikoa/Wilaya siku hizi hazipo sokoni.. kuna blister pack ambayo ni ghali .. may be 3000 kutoka kwa wholesaler wa Kariakoo... Hadi kufika huko wilayani itakuwa bei gani?

  4. Dawa za kuongeza damu zimeadimika sana nchini
  Kampuni kubwa za kutengeneza dawa za kuongeza damu, zinaona kama ni product isiyo na faida, hivyo nyingi hazizalishi kwa wingi kama ilivyokuwa kwa zile za kopo hapo nyuma.. nitafafanua na kutoa mifano ikilazimu

  5. Bajeti ya W/Mkoa kununua dawa ni ndogo mno kulinganisha na mahitaji.. hivyo wananchi wataendelea kukosa tu dawa kama hawataambiwa ukweli.  Sasa ukweli ni Upi.

  Kwanza bei za dawa na vifaa tiba sio bei rahis kama wananchi wanavyotaka kuaminishwa
  Hizo Amoxyclav za elfu nne, zilikuwepo toka zamani.. labda ni hao msd wenyewe kwenye manunuzi yao.... Kwa taarifa tu ni kuwa Amoxycalv zipo za hiyo elf nne had elf 30 kwa molecule hiyo hiyo (Nadhan hizo hata wazri ndizo anazotumia)
  Hep B bei ni 11500-20,000 (Pungufu unaongea)
  Je wananchi watapata ahueni?
  Hapana , gharama za matibabu kwa wananchi wa kawaida hazipo OPD, zipo kwa mgonjwa anapolazwa au anapopata Ajali au Magonjwa Makubwa na ya kudumu kama Kisukari/Figo/Cancer

  Kwa faida kidogo tu, ukipata tatizo kwenye figo ukahitaji kusafishwa(Dialysis) si chini ya laki 6 kwa mara moja.. na utahitaji kufanyiwa mara kwa mara.

  Dawa ya cancer mfano Avastin Inj si chini ya Mil. na utahitaji kudungwa sindano zaidi ya moja

  Kisukari wewe ni maisha yako yote.. na dawa zake si chini ya sh800 kwa kidonge.

  Presha nayo vile vile.

  Suluhisho.

  Kwa wananchi wa kawaida hakuna namna yeyote ya maana zaidi ya kuwa na bima ya Afya.. iwe NHIF/ au private.. CHF ni uchuro... achaneni nayo kwa kuwa mwisho wako wa kutibiwa ni hospitali ya wilaya ambako napo dawa hakuna, na limit ya matibabu ni kubwa sana ukilinganisha na NHIF


  Wananchi wanaopiga makofi kama mazuzu kushangilia bei za dawa wasizozalisha/ au wasiojua hata zinatoka wapi na ubora upi.. bima ya Afya ndie mkombozi wao Pekee....

  Nilidhani ingekuwa busara, Mh. Ummy, akaelekeza nguvu zake kwenye kuwekeza kwenye bima ya Afya na namna gani bora kuwafikia wananchi walio wengi (Sio ile ya CHF ).. kutoka mili 3 waliopo sasa....
  Hata kujiunga kwa lazima kama kweli wanataka mapinduzi ya kweli ya sekta ya Afya hapa nchini

  Waziri ana bima yake, wala hatakaa alie shida ya dawa, ila kwa mwenendo wa malipo wa NHIF nae kuna siku atalia, japo kilio cha kwenye V8 hakina machozi.


  Nitarejea kuelezea zaidi masoko ya dawa na namna viwanda vinavyotengeneza dawa zenye faida...
  Kifupi tu, dawa hizi za level ya wilaya makampuni mengi ya maana yalisha achana nazo maana haziwasaidii kulipa tafiti na kupata faida...
  Tutoke huko kama taifa...
  Waziri Ummy njoo na mpango mzuri wa bima ya Afya kwa kila nyumba(si CHF) nitashiriki kuuboresha ..... Huo ndio ukweli mchungu unaotakiwa kila mwananchi aujue.
   
 2. Ushimen

  Ushimen JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 12,837
  Likes Received: 12,822
  Trophy Points: 280
  Duhh..
   
 3. Michael Bosco

  Michael Bosco Member

  #3
  Jul 18, 2017
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  safi sana mkuu
   
 4. zee Don

  zee Don JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 31, 2016
  Messages: 474
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 80
  Twaweza walishamaliza

  sent from my iPhone 6
   
 5. bruno twemanye

  bruno twemanye JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2017
  Joined: May 18, 2015
  Messages: 804
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 80
  Post 2225,, leo umepiga kati kati ya kidonda,,, nahis utakuwa dmo,, ahasante kwa ujumbe mzuri

  Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
   
 6. Mwifwa

  Mwifwa JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 3, 2017
  Messages: 14,953
  Likes Received: 36,571
  Trophy Points: 280
  Shukrani kwa Ufafanuzi mkuu
   
 7. mrangi

  mrangi JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 19, 2014
  Messages: 22,009
  Likes Received: 9,295
  Trophy Points: 280
  Hali ni mbaya!

  Ova
   
 8. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2017
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,178
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Point, hiyo augmentin ya buku 3 sijawahi kuiona!!!
   
 9. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2017
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hakuna tofauti na HALIMA MDEE alivyotoa tamko la kupinga bei ya mafuta kushuka,.......
  Serikali imeshatangaza bei ya dawa kushuka... Watu wengine hawataki bei zishuke.. HIVI MNATUTAKIA NINI JAMANI???
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Anatafuta Kiki kwa pikipiki.....amekurupuka mno sikuamini kama atasema aliyoyasema!! Amewapa ma DC upuuzi wa kufanya!! Kama hana dawa mganga mkuu....awekwe selo masaa 48 hajui alichokitengeneza!! Amedanganya wananchi kwa bajeti asiyoku nayo!!! Hiyo dawa moja tu ndio imuweke mtu ndani!! Najua chama cha madaktari wengi wataamua kuachia ngazi alete ma Dr wake watakaonunua Toka mifukoni!! Wana siasa wanaharibu nchi sasa!! Nasubiri sana nione wakiwekw ndani na baada hapo alete dawa Toka mshahara wake!!
   
 11. Rohombaya

  Rohombaya JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2017
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 8,263
  Likes Received: 3,100
  Trophy Points: 280
  Dah.... Kuna dili za watu zimeyeyuka ....

  Sent from my Osborne II using JamiiForums Mobile App
   
 12. mirisho pm

  mirisho pm JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 2,483
  Likes Received: 3,306
  Trophy Points: 280
  Bei zipi hizo mkuu?
  Hivi mnafikiri dawa za binadam ni sawa na sukari au Unga?
  Hapa unaongelea dawa tofauti zaidi ya aina elfu 5000 na vifaa tiba elfu moja na mia tano...
  Sasa zinashuka vipi wakati sisi hatuzalish dawa wala hatufanyi tafiti za kutengeneza Dawa?
   
 13. B

  BARRY JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Kama una dawa zako zilete sokoni MSD Wanunue.
  Sasa unalazimisha watu wasiamini chief kama folic acid ziwe bei rahisi?
   
 14. mirisho pm

  mirisho pm JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 2,483
  Likes Received: 3,306
  Trophy Points: 280
  Nimeeleza tatizo la Afya nchini halipo kwenye bei ya dawa
  Tatizo lilo kwenye uhakika wa kumudu gharama za matibabu kwa muda mrefu....
  Dawa bei rahisi nani kasema?
   
 15. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2017
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,566
  Likes Received: 16,535
  Trophy Points: 280
  Dawa nzuri ya Malaria ni kati ya 19,000 na 20,000 nyingine hizi za China ambazo hata kwa Tz 1500 unapata utazinywa mpaka utoke kiwanda cha dawa maana malaria haistuki
   
 16. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2017
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,566
  Likes Received: 16,535
  Trophy Points: 280
  Anaongelea zile za China au zile panadol za mafungu ambazo hata 20 waweza kunywa na maumivu yako pale pale
   
 17. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,439
  Likes Received: 10,645
  Trophy Points: 280
  Mkuu mleta mada nakubaliana na wewe katika hitimisho...kwamba ni lazima waziri apambane kutekeleza Ilani ya CCM yaani Universal coverage ya health Insuarance.Kumbuka kuna ugumu wa kuanza direct na jamii nzima kujiunga na NHIF Vs CHF.

  Wakati wa kampeni za uchaguzi niliwahi kuhoji wagombea akiwemo mama Anna Mghwira juu ya uelewa na maoni yao kuhusu compulsory health insuarance ingawa hawakuweza kulijibu(REJEA MJADALA WA TWAWEZA UCHAGUZI 2015)

  Kuhusu kushuka kwa dawa hilo halina ubishi kwani hadi bei elekezi zimeshatoka.Unachotaka kukitetea ni lugha ya wafanyabiashara tu...mara ooo gharama za uingizaji na blah blah nyingine...

  Katika suluhisho lako ningefurahi kama ungeongelea uwepo na uwekezaji katika viwanda vya dawa na vifaa tiba...hili ni eneo muhimu ambalo litapunguza gharama na ukiritimba wa kupatikana kwa dawa na pia ni eneo lenye ajira na faida ya kutosha.

  Ningependa ujiulize kwa nini hadi leo R/L na NS zinatoka Uganda ?Ningependa kusikia maoni yako kwa muktadha huu.

  Tatizo letu/lenu wataalamu hamuongelei mada nyeti katika afya na ndio maana wanasiasa wanakosa ya kuongelea kuhusu afya na wanabaki na matusi na dhihaka kuhusu ukosefu wa dawa na vifaa tiba.

  Tatizo lenu maDMOs na hata RMOs hamuongei katika vile vikao vyenu mnavyokutana...mkiwa kule mnachat watsapp na kupiga soga.

  Leo hii ukiingia Group la watsapp la ninyi DMOs/RMOs au wafamasia huwezi kulitofautisha na kundi la watsapp la wapiga singeli wa Tandale..wote ni mipicha ya wahenga tu.

  Kuhusu kauli ya ummy...iko very specific na sioni kama kuna upotoshaji unless muanze kuipotosha na kuwatishia wananchi kama ilivyo kawaida ya barvichaa.

  Kama unahisi huwezi kuitekeleza kaa pembeni aingie anayeweza...This is how the new Government runs things...
   
 18. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,439
  Likes Received: 10,645
  Trophy Points: 280
  Unaongelea dawa gani?
   
 19. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2017
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,566
  Likes Received: 16,535
  Trophy Points: 280
  Naongelea Artiquine
   
 20. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,439
  Likes Received: 10,645
  Trophy Points: 280
  Kwa nini uende kwenye artequin wakati ALU ipo ?
   
Loading...