Sakata la Dangote kaa la moto

Sakata la Dangote kaa la moto

Angalau hivi tuviwanda tudogo na tuchache tulivyo navyo hebu tusianze kuvikwamisha jamaniiiiiii. Duh ivi hii nchi ikoje???
 

SIKU moja baada ya Kiwanda cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara kuripotiwa kwamba kimesitisha uzalishaji, watu mbalimbali wakiwamo, wanasiasa, wachumi na wachambuzi wameibuka na kuishangaa Serikali namna inavyoshughulikia suala hilo.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT -Wazalendo) alisema suala la Dangote halikupaswa kufikia hatua hiyo kwani linatoa picha mbaya kwa wawekezaji waliopo na wanaotarajiwa kuja nchini.

Alisema kama Serikali inataka kuendelea na ajenda yake ya maendeleo ya viwanda ni lazima iboreshe namna yake ya ushirikiana na wawekezaji.

“Ukitazama kwa umakini utaona Dangote anakomeshwa kwa sababu ya hisia kuwa kuna wanasiasa wa awamu ya nne wanaubia naye, mawazo ya husda na chuki ndiyo yanayoongoza uamuzi wa baadhi ya watu serikalini, haifai kabisa, yanayotokea ni sawa na mtu ambaye wakati wa baridi anachoma moto nyumba yake ili aote moto.

“Serikali iache utoto, ishughulike na suala hili ili uzalishaji uendelee, lakini pia isikilize kilio cha wenye viwanda kuhusu gharama za uzalishaji kwa sababu ni kubwa mno, ruzuku kwa wazalishaji ni muhimu ili kuzalisha ajira isibishane kwa sababu ya ubishi, ” alisema Zitto.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Dk. Dalali Kafumu, amesema anashangazwa na hali tete inayojengeka kati ya Serikali na kiwanda hicho.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Dk. Kafumu alisema mvutano huo unaweza kuathiri taswira ya uwekezaji nchini na kuiomba Serikali ikae na mwekezaji huyo ili kumaliza tofauti zao.

Dk. Kafumu ambaye ni Mbunge wa Igunga (CCM) alikuwa akitoa maoni yake binafsi, ambapo ameonekana kuguswa na sakata hilo na kusema kuwa haoni busara za Serikali katika kumaliza mzozo huo zaidi ya ubabe.

Alisema kamati yake haijui chochote kuhusiana na mzozo huo na kueleza kuwa amezungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, akutane na kamati yake ili wabunge watoe ushauri wao kunusuru kiwanda hicho.

“Kwa maoni yangu binafsi, kwa namna tunavyoona kwenye vyombo vya habari, hapa kunatatizo, Dangote ni mwekezaji mkubwa suala hili linahitaji utulivu katika kulishughulikia.

“Inavyoonekana wakati mwekezaji huyu anakuja, kulikuwa na makubaliano na Serikali iliyopita labda masuala ya misamaha, masuala ya kodi, bei nafuu ya gesi na mengine.

“Sasa leo kumwambia tu usitumie makaa ya nje lazima utumie ya ndani, sawa inawezekana lakini mnajuaje kama huyu mtu ana mikataba na huko anakotoa hayo makaa?

“Dangote ni mwekezaji mkubwa, ana viwanda vingine huko duniani akifunga kiwanda chake hasara itakuwa ya kwetu. Serikali hii imejielekeza kwenye uchumi wa viwanda, leo unaposikia msuguano kama huu unapata shida kuelewa inakuwaje?,” alihoji.

Kafumu aliendelea kusema. “Mawaziri wanasema Serikali haipaswi kulaumiwa isipokuwa Dangote mwenyewe, wanasema alipewa kibali cha kuvuta gesi hakuvuta, tujiulize kwanini hakuvuta?

“Mara hakusaini mkataba wa kununua makaa ya mawe, ujiulize kwa nini hakusaini? Serikali ikae na Dangote wazungumze, kwa namna hii ni kama Serikali inafunga urafiki na mwekezaji huyu, jambo ambalo si zuri,” alisema Dk Kafumu.

Waziri Kivuli

Naye Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara, Anthony Komu alisema anasikitishwa na mwenendo wa sakata la Dangote, kwani linapaswa kushughulikiwa haraka ili kulinda maslahi mapana ya Taifa.

“Tuna tatizo kubwa juu ya ukweli wa jambo hili kutoka serikalini, kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, Serikali imekuwa ‘difensive’ mno, nadhani kwa hali hii hatuwezi kwenda kabisa. Siku zote tunaambiwa mambo yanakwenda vizuri sasa iweje tushuhudie hali hii.

“Kwanza Watanzania wengi watapoteza ajira, unafuu wa upatikanaji wa saruji utapotea kama zamani, ulipaji kodi utashuka, bei ya saruji itapanda mara dufu… haya yote ni mambo ya msingi ambayo yanapaswa kuangaliwa kwa kina,”alisema Komu.

Profesa Semboja

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) Profesa Hajji Semboja alisema katika kipindi hiki ambacho serikali iko kwenye mchakato wa kuanzisha viwanda, wanapaswa kushirikiana na wawekezaji wanaokuja nchini akiwamo Dangote na kuangalia matatizo yanayojitokeza na kuyafanyia kazi.

“Kiwanda hicho ni kikubwa ambacho kimezalisha ajira na saruji ambayo inauzwa kwa gharama nafuu hata mwananchi wa kawaida anaweza, hivyo serikali wanapaswa kukaa pamoja na kuangalia tofauti zilizopo na kuzifanyia kazi.

TPDC

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba alisema taarifa zilizotolewa na uongozi wa Dangote juzi hazina ukweli wowote.

“Kama TPDC tunapenda kukanusha taarifa zinazoenezwa na Kampuni ya Dangote pamoja na washirika wake kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kudai kuwa tumeshindwa kukiuzia gesi asilia kwa bei rahisi na kwamba ndiyo moja ya sababu ya kusimamisha uzalishaji wake,” alisema.

Alisema TPDC hufuata kanuni na utaratibu wa kupanga bei ya gesi asilia kulingana na aina ya mteja na kwamba wateja wamegawanyika makundi tofauti kama vile wateja wa viwandani, majumbani, magari, pamoja na wazalishaji umeme.

Alisema bei elekezi ambayo inapendekezwa na TPDC ni lazima iridhiwe na ipitishwe na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ndipo ianze kutumika na si mtu binafsi kujipangia bei yake.

Alisema TPDC hufuata kanuni na utaratibu wa kupanga bei ya gesi asilia kulingana na aina ya mteja na kwamba wateja wamegawanyika kufuatia makundi tofauti kama vile wateja wa viwandani , majumbani, magari, pamoja na wauzalishaji umeme.

“Dangote kama mtumiaji wa viwandani amekuwa na mazungumzo ya muda mrefu na TPDC kuhusu bei ya gesi asilia , ambapo kiwanda chake kimeomba kupewa gesi kwa bei ambayo hapa kwetu ni kidogo, kiasi hicho cha bei ndicho kinacholipwa kwenye kununulia gesi ghafi kutoka kisimani.

Akifafanua zaidi, Kaimu Mkurugenzi huyo wa TPDC alisema Dangote alikuwa anataka auziwe gesi hiyo kwa Dola za Marekani 4.7.5 na baadaye akakataa akitaka ishuke zaidi ingawa bei iliyopo kwa sasa ni Dola za Marekani 5.1.4 kwa kipimo cha energy jambo ambalo alisema halitawezekana.

“Dangonte amekuwa akibadilika badilika ambapo alianza na Dola milioni 2 akaja 4 na hii ya mwisho alitaka iwe hiyo ya Dola za Marekani 4.7.5 na bei hizi zinaitwa Dola chini ya kipimo ambapo kitaalamu inajulikana kama MMBTU.

Kuhusiana na utumiaji wa makaa ya mawe ambayo yanazalishwa hapa nchini, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi John Shija alisema mkakati wa serikali ni kuhakikisha viwanda vyote vinavyozalisha saruiji nchini vitumie makaa ya mawe yanayozalishwa na Mgodi wa Ngaka uliopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

Lengo la serikali kufanya hivyo ni kulinda mgodi huo ambao unatija kwa Watanzania wote na tayari baadhi ya viwanda vinavyozalisha saruji hapa nchini vimeshaingia mkataba na mgodi huo isipokuwa Dangote.

“Lakini mpaka sasa upande wa kiwanda cha Dangote wako kimya hawajasema chochote kuhusiana na hili, hivyo tutaangalia ni hatua gani zaidi za kuchukua iwapo tutakosa ufumbuzi wa baadhi ya viwanda kutotumia makaa ya mawe yanayozalishwa hapa nchini,” alisema.

Kuhusu ubora wa makaa hayo, alisema kila kiwanda kina aina yake ya matumizi na kusema kuwa mgodi wa Ngaka una maabara ambayo inatumika kupima makaa hayo kwa ubora unaostahili kinyume na inavyoelezwa kuwa hayafai.

Utajiri wa Dangote

Kinara huyo wa utajiri barani Afrika mwenye umri wa miaka 58 anashika nafasi ya 51 duniani akiwa na Dola za Marekani bilioni 15.4 nyuma ya James Simons mwenye utajiri 15.5 bilioni.

Dangote amejipatia ukwasi huo kupitia uwekezaji katika uzalishaji wa saruji, sukari na maua ambapo uwekezaji wake wa hivi karibuni aliufanya katika nchi za Cameroon, Ethiopia, Zambia, nyumbani kwao Nigeria and na hapa Tanzania.

Pia amewekeza katika nchi za Benin, Senegal, Ghana, Afrika Kusini na Togo, huku kampuni yake ikizalisha mara 30 zaidi ya kipimo cha tani za metriki kwa mwaka na akitegemea kuzalisha mara mbili ya hapo ifikapo 2018.

Chanzo: Mtanzania
Wapiga dili!!!
 
Naona huo ndio mwisho wako wa kufikiri
Hakuna namna ya kufanya ukishindwa terms.Serikali haibembelezi mtu wala kumbeba MTU kisa ni mwekezaji.fuata taratibu zilizowekwa fullstop.
 
Nauliza tu uwezo anao au ni mkwara tu ili ashinikize matakwa yake ? Na kama anao huo uwezo ni nani atalipa gharama ya uwekezaji wote? Ikumbukwe hiki ni moja kati ya Viwanda vyake vikubwa, sasa Je ana uwezo kupoteza hiyo hela au ndiyo tujiandae kwa Mapinduzi ya Serikali yetu kupindiliwa?
Ni kweli ametumia pesa nyingi kuwekeza lakini kama hakuna tija, aendelee kupoteza zaidi?

Hawezi kukiacha tu bali anaweza kukiuza, atakayenunua atakuja na mizania mpya kama vile mikataba mipya ya wafanyakazi, mikubaliano mapya na serikali, na bei mpya za saruji, n.k.
 
Nauliza tu uwezo anao au ni mkwara tu ili ashinikize matakwa yake ? Na kama anao huo uwezo ni nani atalipa gharama ya uwekezaji wote? Ikumbukwe hiki ni moja kati ya Viwanda vyake vikubwa, sasa Je ana uwezo kupoteza hiyo hela au ndiyo tujiandae kwa Mapinduzi ya Serikali yetu kupindiliwa?
Ni kweli ametumia pesa nyingi kuwekeza lakini kama hakuna tija, aendelee kupoteza zaidi?

Hawezi kukiacha tu bali anaweza kukiuza, atakayenunua atakuja na mizania mpya kama vile mikataba mipya ya wafanyakazi, mikubaliano mapya na serikali, na bei mpya za saruji, n.k.
 
amuuzie bakhresa au rostam ndio wanaweza kuwekeza bongo
 
SOSY MUONGO na MWIJAGE nawaona wakichezea ugali wao,let us wait.......!!!!!
 
Pamoja na hayo yote.Hizi kambi mbili moja iliyoko ndani ya serikali ya Magufuli na Kambi ya Pili iliyokuwa katika serikali ya awamu ya nne WALIONUNUA HISA nyingi ndo TATIZO.

Kama wananchi hatutakubali hizi kambi ZITUHARIBIE uchumi wetu wa viwanda! Katika mtazamo wa kindani. KUNA BEHIND the scenes FORCES/ Msukumo ULIOJIFICHA unaoipa Dangote Cement KIBURI na kutaka KUi Blackmail serikali kwa kuupindisha mkono kwa nguvu ili serikali isikie MAUMIVU na iseme YAISHE.


Dangote Cement can't dictate to the government terms and conditions as per their demands. Kuna MKONO MKUBWA nyuma ya hii SAGA/Jambo na ndio huo unaoipa KIBURI kampuni hii.Hilo ndo watanzania tulijadili na tujiulize.Ni MKONO wa AKINA nani??
Magufuli ASILINYAMAZIE!!!
Kwa taarifa yako Dunia inaongozwa na biashara siyo viwanda.
Ndio maana mnalipa capacity charges kwa IPTL bila kupata hata unit moja ya umeme hiyo inaitwa biashara.
Serikali imepatwa ugonjwa wa kichaa
 
Nauliza tu uwezo anao au ni mkwara tu ili ashinikize matakwa yake ? Na kama anao huo uwezo ni nani atalipa gharama ya uwekezaji wote? Ikumbukwe hiki ni moja kati ya Viwanda vyake vikubwa, sasa Je ana uwezo kupoteza hiyo hela au ndiyo tujiandae kwa Mapinduzi ya Serikali yetu kupindiliwa?
Mkuu mbona una mawazo ya kitoto.
Kiwanda syo zege, ati kukitoa lazima ulivunje!
Kiwanda ni mashine ambazo huweza kufunguliwa, tena chote wakati wowote.
Kama Dangote kaweka mitambo ya thamani ya US$500 mil, kwani atakosa US$100 mil kuking'oa chote kukipeleka kwingine?
 
Kwan atafunga milele...anafunga kwa miaka 9 akija rais mwingune anayeelewa mambo ya uwekezaji wataongea terms upya atafungua
Haha..kwani ana shida gani? Km anaweza hamisha hasara mlipe watanzania. Kiwanda kilijengwa kimakosa kwa papara za ccm na wapinzani km akina zzk kwa kujifanya ni mwenzao ktk imani.Sasa huyu nae anataka rekebisha kw akufanya makosa.CCM imejaa uozo,imefanya nchi shamba la bibi kila mwenye wenge anaweza fanya apendalo bila upinzani,madhara awachie watanzania wabebe.
 
Nauliza tu uwezo anao au ni mkwara tu ili ashinikize matakwa yake ? Na kama anao huo uwezo ni nani atalipa gharama ya uwekezaji wote? Ikumbukwe hiki ni moja kati ya Viwanda vyake vikubwa, sasa Je ana uwezo kupoteza hiyo hela au ndiyo tujiandae kwa Mapinduzi ya Serikali yetu kupindiliwa?
Wewe unafikiri kuendesha kiwanda kikubwa kama kile sawa na kuendesha mradi wenu wa magazeti ya UHURU ,hata kama hamuuzi na hamlipi watu mishara zaidi ya miezi zita bado mtaendelea na biashara!

Umewaza kitoto sana! Punguani wa head wewe!
 
Wewe unafikiri kuendesha kiwanda kikubwa kama kile sawa na kuendesha mradi wenu wa magazeti ya UHURU ,hata kama hamuuzi na hamlipi watu mishara zaidi ya miezi zita bado mtaendelea na biashara!

Umewaza kitoto sana! Punguani wa head wewe!
mkuu hao ni wajamaa ni wajinga duniani kote hawan kitu chenye faida, ni propaganda full time. Wapo tayari kupiga rangi na matangazo kibao, halafu wafanyakazi 10,000. wanazalisha gari mbili kwa mwezi. Kisha wanalia kuhujumiwa na mabeberu. Dangote anataka efficient production ili aweze bei nzuri na y akiushindani sokoni.CCM wanataka ugumu ili auze ghali n akulinda maviwanda yao waliyoyavuruga na kunyonya hela ktk jitihada za kubaki madarakani.
 
kuna Kabul apo.

gadaffii......40BL Mzee alitumia kwa uchaguzi

Dangote ni Chenga ya okocha l azima.kiuno kicheze tusubiri
 
Hivi kati ya Dangote na hao wanaochimba madini yetu ni nani mwekezaji wa faida hasa kwa nchi kama hii ya kwetu?
 
Kama anahitaji nafuu zaidi ya nchi inavyoweza kutoa, na kwenyewe kuna tatizo.

Leo hii kuna watu kibao, wengine wamo humu, wamekuwa wakilalamika sana kuwa serikali ni wapole sana wanapodeal na wawekezaji. Kwamba wawekezaji wananufaika zaidi kuliko nchi. Sasa serikali imejipanga ili nchi ifaidike hao hao wanalalamika.

Dangote anahitajika sana Tanzania na ni muhimu sana kwa uchumi wetu. Naye anatuhitaji sana. Hivyo, lazima kuwe na win win situation.
Watanzania ni watu wa ajabu sana, Huwa hata hawajiulizi kwa nini cement ilikuwa inatoka pakistan na kufika Tanzania kwa bei ya chini!! "Keep you production cost low then you can export and get Forex money" Sasa tatizo tuna rasilimali nyingi ila hatuna faida nazo!! Wachumi wetu wanasaidia nini taifa?
 
Utajiri wa Dangote USD 15.5 bn. Kumbe Trump na masifa yote yale hagusi kwa Alhaji Aliko Dangote.

Mkuu Hiyo ni GDP ya Tanzania kwa mwaka mzima....yaani Aliko Dangote anaweza inunua Tanzania nzima,watu na vilivyomo kwa muda wa mwaka mzima,na watu wasifanye kazi kwa muda wa mwaka mzima kabisa...

Aliko Dangote akisimama na Magufuli ana haki ya kumuita JPM "bwana mdogo".

Aisee tatizo serikali inakosa heshima kwa watu,no matter who the person is,treat him/her with respect....Ni upumbavu kudhani serikali hii ina akili kupita watu wengine na they can just push anybody around as they wish...

This is business,hafagiliwi mtu,hesabu za Dangote au serikali hazijakaa vizuri basi terminatia mbali....shida ni hoja za serikali sasa,vituko vitupu yaani...yaani ukimwangalia huyo "Mwijage" sasa,anaongea utafikiri yupo kwenye kamkutano ka kampeni huko Misenyi ndani....hajui analolijua...ujinga ujinga tu.

Na huyu Profesa Muhongo....jezzuz christ....eti "wanaweka watu wa kati wa gesi na gypsum tunataka wafanye wenyewe"....

Dangote is a cement factory and NOT a mining or power generation company dummy....ndio maana hayo wanapewa suppliers...dangote ni kuzalisha cement tu... sijui ujinga wamesomea wapi...maajabu!
 
Nauliza tu uwezo anao au ni mkwara tu ili ashinikize matakwa yake ? Na kama anao huo uwezo ni nani atalipa gharama ya uwekezaji wote? Ikumbukwe hiki ni moja kati ya Viwanda vyake vikubwa, sasa Je ana uwezo kupoteza hiyo hela au ndiyo tujiandae kwa Mapinduzi ya Serikali yetu kupindiliwa?

Huo uchochozi sasa!
Yaani mtu kufunga Biashara yake kunahusiana vipi na hayo?
 
Mtoa Mada Kwa Swali Hili.
Kweli Watanzania wengi ni Villaza.

Biashara siku zote kama Haikulipi Unafunga na yeye Dangote ndiyo Mwenyewe Kiwanda Akiamua Kufunga Hakuna wa Kumzuia.
 
Back
Top Bottom